TENGEFU
Senior Member
- Jan 25, 2017
- 138
- 206
Masheikh wa uamsho waliofanya matendo yenye viashiria vyote vya ugaidi wanaachiwa huru lakini raia mwema ambaye kosa lake ni kutamka tamka “katiba Mpya” anakamatwa na kuuziwa kesi ya Masheikh wa Uamsho. Ugaidi wa Mbowe ni mkubwa kiasi gani ukilinganisha na Masheikh walioachiwa huru.
Mtu anajiuliza kama kweli tuko serious na kupambana na ugaidi, tunawaachiaje masheikh wa Uamsho halafu tunamkamata mbowe ambaye hata hajawahi mmwagia mtu hata maji?
Viongozi wa Tanzania mjue watanzania wanaona na wanajua kuchambua mambo kwa kina na mapana. Kilichozuiwa ni kongamano la Katiba, hivyo tunataka kujua hili lina uhusiano gani na ugaidi?.
Kama kuongelea Katiba mpya tungetegemea pia Jaji Warioba aunganishwe kwenye kesi ya Mbowe; lakini pia kwa muktaza huo walioshiriki Bunge la katiba nao wote ni magaidi.
Lazima ijulikane kuwa watanzania waliomwomba Mungu katika kipindi cha awamu ya Tano bado wako magotini wakimlilia Mungu. Kuna kila dalili kuwa viongozi wetu huingia madarakani na macho na masikio lakini wakianza tu kukalia kiti wanakuwa vipofu na viziwi na mara nyingi hufiisha hisia zao kwa kuhakikisha keki iliyoko mezani haipati hata vumbi.
Ifike mahali viongozi waendelee kujua uongozi ni koti na wasipolivua Mungu atawavua. Na pia viongozi wa Tanzania wajue Mungu hajawaacha Watanzania bali anawajaribu watu mbalimbali kama wanaweza kuwaongoza kwa haki na akiona watu wake wanaumia basi anatumia uungu wake kufanya kazi yake.
Kama kumkamata Mbowe ni amri toka juu basi tumeshaingia chaka hata kabla ya miezi sita ya uongozi wa awamu ya Sita.
Kutaka kuongoza nchi bila challenge ni kujidanganya maana hata wazazi katika familia zao hupata changamoto nyingi toka kwa family Members haswa Watoto lakini husikii wazazi wakiwabambikia Watoto wao kesi. Rais chukulia nchi kama familia ambayo usitegemee smooth leadership.