Ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara

thisisboman1

Member
Feb 11, 2019
5
10
Nmeanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara.

VIJANA WENZANGU, Niwatoe hofu na kuwatia moyo ufugaji wa kuku wa kienyeji utakupa matokeo makubwa kupanda kiuchumi, kwa kuzingatia ufugaji wenye tija.

Mimi nafuga mradi unajiendesha nimezingatia eneo la uwekezaji na namna Bora ya kuepusha magonjwa kwenye mifugo nazingatia chanjo, usafi, ukaribu na kuwasoma vilivyo kuku hii imenisaidia malezi mazuri kiujumla na biashara kuleta faida.

NIMEWEZAJE KUMUDU HILI?
1. Tetea hutaga mayai, Huwa nahakikisha lazima Kila mwaka uzalishaji uongezeke, nilianza na kuuza trei moja Kila siku (MAYAI KIENYEJI) 500x30=15000 pili nilihakikisha Kila mwezi natotolesha vifaranga 50 kupitia tetea 5 tu kwa maana sikuwa na uwezo wa kununua INCUBATOR

2.Ukiachana na faida ya mayai kwa trei pia Huwa napiga hesabu ya tetea ambao Wamepunguza uwezo wa kutaga naingiza sokoni hapo ni baada ya kunizalishia mayai kwa miezi kati ya 6-8 hapa nachanganya na majogoo yaliyoanza kuwika makadilio wa miezi 6 kumbuka kwenye kutotolesha napata kuku mchanganyiko jogoo na tetea ndiyo maana lazima nipate majogoo pia ya kuuza hapa pia ni faida

3. NIKAZIE HAPA KWANGU MIMI KUKU WA KIENYEJI NI FAIDA TU, Hii ni kwasababu wanajitafutia chakula nawapa pumba kidogo kwa mwezi Tsh 9000 na eneo ninalofugia lipo mbali na makazi ya watu nikiwa na maana kwamba na takribani ekari na nusu, pia pembeni yangu walio nizunguka hawaendelezi Maeneo yao HIVYO ni fursa kupitia kuku ambao pia hunisaidia kuingiza pesa na kununua Maeneo mengine ya jirani hapa napata faida ya kuongeza eneo na kujiimarisha kiuzalishaji.

HIVYO NDIVYO NILIVYOANZA NAKUTIA MOYO NA WEWE, PITIA PICHA HAPO CHINI ZINAZOONYESHA NILIVYOANZA.

KWENYE PICHA UTAKUTANA NA BANDA LA KUKU LA MIFUKO (VIROBA) NDIYO NILILOANZIA KUFUGIA UTALIONA VIZURI NA NDANI PIA NIMEJENGA MWENYEWE KWA MITI, MIFUKO, KAMBA NA MISUMARI KIDOGO.

IMG_20230811_141108_203.jpg
 
Nami natafuta maarifa hasa ya ujenzi wa mabanda Bora nianze November hii ufugaji wa kuku wa kienyeji...
 
bado ni mapema sana kushangilia. Unaposema kuna faida tuambie kuku wako huchukua muda gani hadi kufikia kutaga na jogoo wako huchukua muda gani hadi kufikia kuuzwa. Ukiingiza suala la muda kwenye hicho unachokiita faida utagundua ni unaishi na kuku siyo kufuga kibiashara
 
Nmeanzisha mradi wa ufugaji wa kuku wa kienyeji kibiashara.

VIJANA WENZANGU, Niwatoe hofu na kuwatia moyo ufugaji wa kuku wa kienyeji utakupa matokeo makubwa kupanda kiuchumi, kwa kuzingatia ufugaji wenye tija.

Mimi nafuga mradi unajiendesha nimezingatia eneo la uwekezaji na namna Bora ya kuepusha magonjwa kwenye mifugo nazingatia chanjo, usafi, ukaribu na kuwasoma vilivyo kuku hii imenisaidia malezi mazuri kiujumla na biashara kuleta faida.

NIMEWEZAJE KUMUDU HILI?
1. Tetea hutaga mayai, Huwa nahakikisha lazima Kila mwaka uzalishaji uongezeke, nilianza na kuuza trei moja Kila siku (MAYAI KIENYEJI) 500x30=15000 pili nilihakikisha Kila mwezi natotolesha vifaranga 50 kupitia tetea 5 tu kwa maana sikuwa na uwezo wa kununua INCUBATOR

2.Ukiachana na faida ya mayai kwa trei pia Huwa napiga hesabu ya tetea ambao Wamepunguza uwezo wa kutaga naingiza sokoni hapo ni baada ya kunizalishia mayai kwa miezi kati ya 6-8 hapa nachanganya na majogoo yaliyoanza kuwika makadilio wa miezi 6 kumbuka kwenye kutotolesha napata kuku mchanganyiko jogoo na tetea ndiyo maana lazima nipate majogoo pia ya kuuza hapa pia ni faida

3. NIKAZIE HAPA KWANGU MIMI KUKU WA KIENYEJI NI FAIDA TU, Hii ni kwasababu wanajitafutia chakula nawapa pumba kidogo kwa mwezi Tsh 9000 na eneo ninalofugia lipo mbali na makazi ya watu nikiwa na maana kwamba na takribani ekari na nusu, pia pembeni yangu walio nizunguka hawaendelezi Maeneo yao HIVYO ni fursa kupitia kuku ambao pia hunisaidia kuingiza pesa na kununua Maeneo mengine ya jirani hapa napata faida ya kuongeza eneo na kujiimarisha kiuzalishaji.

HIVYO NDIVYO NILIVYOANZA NAKUTIA MOYO NA WEWE, PITIA PICHA HAPO CHINI ZINAZOONYESHA NILIVYOANZA.

KWENYE PICHA UTAKUTANA NA BANDA LA KUKU LA MIFUKO (VIROBA) NDIYO NILILOANZIA KUFUGIA UTALIONA VIZURI NA NDANI PIA NIMEJENGA MWENYEWE KWA MITI, MIFUKO, KAMBA NA MISUMARI KIDOGO.

View attachment 2715726
Upo maeneo ya wap mkuu pwan au
 
Kila mwezi unatotolesha vifaranga 50 kwa kuku wa 5 ..? Ukisema kila mwezi unamaanisha nini
Yai la kuku wa kienyeji linakuwa feasible kutotolea kabla ya kufika siku 14 na kuku anaanza kuantamia walau kufika siku ya 21 so mayai yenye uwezo mzuri wa kutotolewa n almost 7 na hapo tumeassume kuku kataga siku zote had siku anataka kuatamia

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kwanza nipende kusema mimi nafuga kienjeyi pure kwa ajili ya biashara ya mayai lakini na Sasso ambao nawatoa kila baada ya mezi 2.5 mpaka 3 kwa ajili ya nyama. Kuku wa kienyeji mpaka aanze kutaga inahitaji umlishe kwa takribani miezi 5.5 mpaka 6. Nina maswali machache kwa ajili ya ufahamu.

1. Unataka kuuza kuku kwa ajili ya nyama au unauza mayai tu au vyote?

2. Unajua gharama za ulishaji kwa kilo kwa kuku? Hili ni muhimu sana.

3. Soko lako likoje? Target unalenga kuwauzia watu gani haswa?

4. Una mtaji wa kukuwezesha kuwahudumia kuku wako kwa kipindi chote mpaka waanze kuleta faida? (Chakula, chanjo, upanuzi wa banda etc).

5. Kwa idadi ya kuku mpaka waanze kuingia kwenye mzunguko wa kupata mzunguko wa hela, lini utaweza ku break even? (Gharama za kuwalisha kuku kuweza kutoka kwenye mauzo ya kuku/mayai na wewe kupata faida?

6. Una technical capability ya ufugaji angalau ufahamu wa chanjo, magonjwa, aina ya chakula kwa kila stage ya kuku kukua? Hii ni muhimu sana

7. Msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za ufugaji kuku kuna mtu specific au ni wewe mwenyewe? Hii wafugaji wengi wanakwama hususani kwenye kuangalia progress ya maendeleo ya kuku na uncertainities zinazoambatana na ufugaji.

Mwisho huu uzi uendelee kutupa updates ili iwe inspirations na pia wengine kujifunza.
 
hakunaga ufugaji wa kuku wa kienyeji kibihashara......labda uwalishe udongo cyo vyakula vyenye ratio nzuri

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app

3. NIKAZIE HAPA KWANGU MIMI KUKU WA KIENYEJI NI FAIDA TU, Hii ni kwasababu wanajitafutia chakula nawapa pumba kidogo kwa mwezi Tsh 9000 na eneo ninalofugia lipo mbali na makazi ya watu nikiwa na maana kwamba na takribani ekari na nusu
 
Ukitaka fuga achana na kuku wa kienyeji kamili, jikite kwenye chotara ie kuchi, sasso, kuroiler etc

Aina hiyo una uhakika ndani ya miezi 6 umeuza mara 2 zaidi maana wanakuwa wakubwa
 
Kwanza nipende kusema mimi nafuga kienjeyi pure kwa ajili ya biashara ya mayai lakini na Sasso ambao nawatoa kila baada ya mezi 2.5 mpaka 3 kwa ajili ya nyama. Kuku wa kienyeji mpaka aanze kutaga inahitaji umlishe kwa takribani miezi 5.5 mpaka 6. Nina maswali machache kwa ajili ya ufahamu.

1. Unataka kuuza kuku kwa ajili ya nyama au unauza mayai tu au vyote?

2. Unajua gharama za ulishaji kwa kilo kwa kuku? Hili ni muhimu sana.

3. Soko lako likoje? Target unalenga kuwauzia watu gani haswa?

4. Una mtaji wa kukuwezesha kuwahudumia kuku wako kwa kipindi chote mpaka waanze kuleta faida? (Chakula, chanjo, upanuzi wa banda etc).

5. Kwa idadi ya kuku mpaka waanze kuingia kwenye mzunguko wa kupata mzunguko wa hela, lini utaweza ku break even? (Gharama za kuwalisha kuku kuweza kutoka kwenye mauzo ya kuku/mayai na wewe kupata faida?

6. Una technical capability ya ufugaji angalau ufahamu wa chanjo, magonjwa, aina ya chakula kwa kila stage ya kuku kukua? Hii ni muhimu sana

7. Msimamizi mkuu wa shughuli za kila siku za ufugaji kuku kuna mtu specific au ni wewe mwenyewe? Hii wafugaji wengi wanakwama hususani kwenye kuangalia progress ya maendeleo ya kuku na uncertainities zinazoambatana na ufugaji.

Mwisho huu uzi uendelee kutupa updates ili iwe inspirations na pia wengine kujifunza.
Mkuu umeongea kitaalam sana
Mimi nimefuga kuku wote kienyeji na chotara ntatumia namba zaidi make hazidanganyi

Mfano ukinunua kifaranga cha chotara wa mwezi 4500/
Gharama za chakula kama kweli uwabanii utatumia 7000/ kwa kuku mmoja hadi anafikisha miezi mitano ambayo vitabu vya wajasiliamari vinasema wanaanza kutaga wakati hii inategemea hali ya hewa uliyopo, genetic makeup ya kuku na factors kibao so max ni miezi sita kuku anatakiwa aanze kutaga
kama kwenye banda una majogoo unaweza kuyapunguza wakifika miezi minne na hapo inategemea kg zao na location max 15000
Hii mitetea inayotaga assume hipo 100 so atleat kwa siku 75% wanatakiwa watage assume bei ya trey kwa jumla ni 12000/ wakiwa at the peak na baada ya mwezi mzima wa kutaga watahitaji week tatu za kupumzika na kufanya utagaji kushuka hadi 20%
At 20% itabidi uanze kutoa faida yako uliyoitengeneza kwa miezi miwili kuwarudisha kwenye peak....so inakuwa ni circle fulani hivi ambayo utakuja kutoboa
NB kuna kuku tasa wao hawatagi

Ukitaka kuijua hii ni biashara kichaa weka records, weka chakula kulingana na idadi ya kuku na kwa bei uliyonunua utajua kila kuku anakugharim kiasi gani kwa siku.

Fun enough kuku akishafika miezi sita ni nguma kuongeza kilo so no matter utamlisha kiasi gani bei yako sokoni itabiki almost vilevile so ni hasara kuzidi kumtunza.

Kwa kuku wa kienyeji hao ukitaka kupata faida watoe vijiji wauze mjini wakiwa wakubwa cyo kuwafuga utakonda

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Kama hujui ungekaa kimya mkuu. Labda kama unapigia na hesabu za ujenzi wa banda. Ila kiukweli hawa kuku wanafaida sana kwanza kwa kuwauza pia mayai.
Sijakataa wana faida tena nzuri tu

Hila by fact
Imagine una mitetea 100 ya kienyeji inataga na unailisha ratio nzuri tu ya dukani na baada ya siku 22 ya utagaji mitetea 70 inahitaji kuatamia mayai kama ilivyo nature yao.

Usipo wapa wayai itabidi uwafungie week moja plus wanakula bure hili waanze kutaga baada ya week 2, utabaki na mitetea 30 nao siku si nyingi watataka kuatamia, so wanakula bure kipindi chote, ikitokea umewapa mayai siku 21 you dont sell eggs mradi umesimama mpaka watotoe.

Na ukiwanyanganya vifaranga baada ya kutotoa you wait for a week hile wa-regain kuanza kutaga na hapa utatumia protein nying kweny ratio which is very expensive na ukizumbaa ni week 2 plus.

Na ikitokea unatumia incubator inakuwa vice versa ya nilichokiandika hapo juu.

Na kama unawafuga kwa ajili ya kuuza nyama...vifaranga wa kuku kienyeji wale wenye mwili mkubwa wa mwezi ni 5000 kutokana na ugumu na upatikanaji wa mayai yake.
Ukimlisha vizuri plus madawa, maji, usimamizi nk utatumia 7000/+ kwa kuku mmoja hadi wanafika miezi sita; total ni 13000/ ukimpleka sokoni utajua utamuuza sh ngapi kulingana na location na madalali

Na ukisema unaingia singida ndanindani ukachkua kuku wako wa kienyeji na ukaja kuwauza sokoni ina maana hizo risk zote hapo juu unamwachia mkulima kazi n kutafta soko

Sijaandika hivi kumkatisha mtu tamaa, hila nahitaji vijana tujue agribusiness ilivyo tusifate mkumbo kufanya kitu kwa passion ni sawa hila kama hakikupi hela dahhh ni kupoteza mda

Sent from my SM-A207F using JamiiForums mobile app
 
Habari za jioni wadau...naombeni tupeane tips ufugaji kuku wa kuku wa kienyeji ...naombeni mawazo yenu ,na experience...pia kati ya kuku wa kienyeji na kuku wa kizungu ni kuku wapi ambao Wana soko zaidi na Bei za kuuzia sokoni zikoje pia na running cost yake ikoje
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom