Naomba ushauri wenu kuhusu biashara ya ufugaji wa kuku wa mayai

Da'Vinci

JF-Expert Member
Dec 1, 2016
35,690
106,827
Habari, wataalam na wenye uzoefu wa jambo hili naombeni muongozo katika jambo langu hili.

Ili kujikwamua na ufukara uliokithiri Nilitaman kufanya biashara ya ufagaji.. Nilionelea nifanye ufagaji wa kuku wa mayai. But sijawah kufanya hii kitu uzoefu nilionao ni wa kuhudumia kuku wetu wale tunaofuga nyumbani so kwa kiasi naelewa kuku wanavyotia stress.

Nilitaka ninunue eneo kuanzia 1 hector and above kisha ndio nifanyie hapo shughuli hizo za ufugaji.....
  • So Ningependa kujuzwa vitu vya kuzingatia katika kuchagua eneo la kufanya ufugaji huo.
  • Je biashara hii inalipa au ndio pasua kichwa?
So maelezo yenu ndio yatanipelekea kufanya Viability and feasibility analysis yangu.

Karibu wajuzi wa mambo mnipe mawazo. Yaani naanza from scratch naweza sema sijui lolote kwenye biashara hii.

Nimesoma soma threads humu, kutazama video YouTube na kufuatilia fb swala hili. Natumaini GT wa JF mtanijuza zaid.
 
Biashara ya kuku wa mayai sio mbaya katika uwekezaji, ila ushauri wangu Anza na kuku wachache kwanza hata kama una mtaji mkubwa, Hawa sio kuku wa nyama kuwalisha Hawa viumbe mpaka waanze kutaga inachukua miezi mpaka 6, Hawa wajomba hawalali kazi Yao kubwa iliyowaleta hapa duniani ni kupiga msosi, na gharama za vyakula vyao na vitamin na dawa za kuwachanganyia kwenye maji zimepanda pia.... Kwa hiyo unaweza kukimbilia kuwafuga wengi badae ikawa mtihani katika kuwafuga.

Nimeona watu wengi wakiwauza kabla hawajataga baada ya kushindwa kuwahudumia mpaka mwisho.

Tahadhari nyingine tafuta sehem au namna umeme uwe wa uhakika Hawa kuku umeme ukikatika ni wajinga sana watatafuta Kona Moja watarundikana na kulaliana kesho unaweza Kuta hata 50 wamekufa kwa kulaliwa na wenzao, sehemu iwe tulivu, kwenye paa lao akitokea hata mtoto mtundu akarusha jiwe watalaliana sehemu Moja kwa hofu na watakufa wengine.

Uwe na roho ngumu kidogo, kuna kaupepo ka ugonjwa kakipita wao kufa hata 30 Kila siku sio jambo la ajabu sana, lakini Mungu akisaidia inalipa maana wakianza kutaga unaongeza na mke wa pili kabisa😃😃

Nimeona nikupe baadhi ya changamoto chache wengine wataleta mengine
 
Hongera mkuu kwa uthubutu.

Najua huku kuna threads nyingi za ufugaji wa layers, lakini ngoja nitoe na mimi hints chache;

1. Initial capital investment lazima uwe nayo kwa angalau kuku mpaka waanze kutaga. Uwe na uhakika wa operating costs kama kununua vifaranga, chakula, chanjo, matibabu, usimamizi etc. Layers wanataga kuanzia miezi 5. So ukumbuke hapa hautaingiza hata shing kumi.

2. Anza kidogo kidogo (mfano vifaranga 100 tu), then uendelee ku expand kadri unavyo pata exprience ili kupunguza risk ya kupata hasara kwa mkupuo. Mambo ya pdf na Youtube utumie kama inspiration tu.

3. Hata kama utamwachia mtu asimamie make sure mwanzoni unashiriki kwa 100% na baadae unakua unafuatilia on a daily basis. Never trust mtu yeyote.

4. At the same time unaweka nguvu kwenye uwekezaji, fanya utafiti na ufahamu wateja wako ni akina nani. Tengeneza connections kadri siku zinaenda. Hii ni muhimu sana.

5. Kuwa na mshauri/mtaalam aliyebobea kwenye ufugaji ili kuwa mshauri hususani kuboresha uzalishaji na matibabu.

6. Lazima ujue machimbo ya vyakula vya kuku bei nafuu maana gharama za ufugaji wa kuku wa mayai zaidi ya 80% ni chakula na virutubisho. Tengeneza chakula chako mwenyewe utakachowalisha, achana na kununua mifuko, utapata hasara

7. Take your time uongeze ujuzi katika mbinu za ufugaji hususani ulishaji, uchanganyaji wa chakula, magonjwa na dalili, chanjo zao etc. Hii itakusaidia wewe binafsi kama mwekezaji kwenye business hii.

Ngoja niishie hapa, wajuzi wengine waongeze.
 
Kama una uwezo wakuchukua hector moja. Huwezi washindwa kuku wa mayai. Ila lazma uwe na mtaalamu. Ambaye si ww. Atayekua shambani muda wte na vijana hata wawili.
Mkuu niumepanga katika hili zoezi nishiriki mwenyewe pia kwa asilimia 120% sitaki ufugaji wa kupiga simu. Pia nilitaka nipate japo heka 2-5 ambapo humo naweza kufanya shughuli zingine za kilimo.

Japo sijui kulima ila nitajulia huko huko. Huko nilitamani niwekw mbuzi na mifugo mingine kama. Oink oink
 
Mkuu niumepanga katika hili zoezi nishiriki mwenyewe pia kwa asilimia 120% sitaki ufugaji wa kupiga simu. Pia nilitaka nipate japo heka 2-5 ambapo humo naweza kufanya shughuli zingine za kilimo.
Japo sijui kulima ila nitajulia huko huko. Huko nilitamani niwekw mbuzi na mifugo mingine kama. Oink oink
Ulipotaja hector nikatamani nikwambie weka nguruwe tu.
Ila kama kweli utakua shambani usiogope sijui magonjwa.
Fuga makuku hayo. Mapambano tu.
 
mkuu soma kwa makini comment no 09 amepiga mle mle

cha kuongezea hapo usitegemee chakula cha kununua pekee vyakula vingine tengeneza wewe mwenyewe maana katika ufugaji wa kuku chakula ndo mziki ulipo kwa eneo hilo ukiwa nalo hakikisha mchicha unao,chinise nk vilevile kama upatikanaji wa maji utakuwa mzuri fanya kuozesha kinyesi chao kwa ajiri ya funza wadudu hao wana protein za kutosha

hakikisha kiangazi unatengeneza hydroponic folder zitakupunguzia sana gharama.

usisahau kutupa mrejesho
 
Biashara ya kuku wa mayai sio mbaya katika uwekezaji, ila ushauri wangu Anza na kuku wachache kwanza hata kama una mtaji mkubwa, Hawa sio kuku wa nyama kuwalisha Hawa viumbe mpaka waanze kutaga inachukua miezi mpaka 6, Hawa wajomba hawalali kazi Yao kubwa iliyowaleta hapa duniani ni kupiga msosi, na gharama za vyakula vyao na vitamin na dawa za kuwachanganyia kwenye maji zimepanda pia.... Kwa io unaweza kukimbilia kuwafuga wengi badae ikawa mtihani katika kuwafuga



Nimeona watu wengi wakiwauza kabla hawajataga baada ya kushindwa kuwahudumia mpaka mwisho


Tahadhari nyingine tafuta sehem au namna umeme uwe wa uhakika Hawa kuku umeme ukikatika ni wajinga sana watatafuta Kona Moja watarundikana na kulaliana kesho unaweza Kuta hata 50 wamekufa kwa kulaliwa na wenzao, sehemu iwe tulivu, kwenye paa lao akitokea hata mtoto mtundu akarusha jiwe watalaliana sehemu Moja kwa hofu na watakufa wengine


Uwe na roho ngumu kidogo, Kuna kaupepo ka ugonjwa kakipita wao kufa hata 30 Kila siku sio jambo la ajabu sana, lakini Mungu akisaidia inalipa maana wakianza kutaga unaongeza na mke wa pili kabisa😃😃


Nimeona nikupe baadhi ya changamoto chache wengine wataleta mengine
Ahsante kwa maelezo yako. Kuku maybe 500 nianze nao au ww una shauri wangapi?
 
Back
Top Bottom