Ufugaji wa Kuku aina ya Kuchi na masoko yake ndani na nje ya Tanzania

Mkuu kuna Jamaa alikataa milioni 3 hajauza jogoo la kuchi maeneo Ya kigamboni. Wahindi Na. Waarabu ndio wanapeda Kununua Sana hii Aina Ya kuku.lkn kuna faida kwani Hata kifaranga tu cha mwezi ni elfu 50.na yake ni elfu 15 moja
Hii haina tofauti na thamani fikirivu za sarafu za zamani. Kuna wakati nikiwa mdogo nilikuwa naona watu wanatafuta sarafu za zamani enzi za mkoloni kwa taarifa eti wataziuza kwa fedha nyingi zisizo na idadi. Kifaranga shs 50,000 na yai shs 15,000? Mimi naona kama kuna kundi la watu wanadanganya wenzao. Sioni uhalisia zaidi ya matarajio tu.
 
Hii ni lugha biashara tu. Ununue kuku wa uzito maximum kilo 3.5 kwa shs 200,000/=? Kwa ajili ya nini, nyama au mapambo? Mimi simuelewi huyu bwana


Sikiliza. Wewe umeshaninua. Sasa hivi na Wewe unatafuta wa kumuuzia. Kama utampata mwenye mawazo uliyokuwa nayo wakati ule unanunua, unaweza kuuza. Ila ktk hali halisi hiyo siyo biashara endelevu. Ni kubahatisha watu wasiyojielewa. Ninunie kuku shs 200,000/= kwa sababu gani hasa. Nyama nzuri, mapambo au bondia wa maonyesho ya mapambano? Mimi siwaelewi. Naona kama mlipoteza hela zenu kwa maneno ya kuambiwa. Samahani lakini huenda nimetumia lugha kali kuonyesha hisia yangu

Au anatoa na maziwa

nahisi hao kuku ni kwa ajili ya ufahari maana kama kuku huwez hata muuzia jirani yako kwa ajili ya kitoweo ni wa nini ,haya twende upande wa nyama ina vitu gani vinayoifanya nyama yake iwe special mpaka huyo kuku awe laki 2,Nina uhakika nyama yake INA ladha ya kuku wa kawaida japo utajisifu nimekula kuchi bwana ,naomba unielimishe basi au ni kwa ajili ya soko LA nje
 
Kutokana na ongezeko la maswali ya wadau wengi juu ya ufugaji wa kuku aina hii, tumeonelea ni vema tukauweka mjadala huu vema kuweza kuwasaidia wafugaji na wanunuaji wa vifaranga/kuku wa aina hii.

Kuku aina ya KUCHI, ni wale ambao wanawauza kwa shilingi 200,000 hadi zaidi kwa kuku mmoja. Pamoja na kuwa kuku hawa wanaonekana kama wa kawaida, lakini si kama kuku wale tunaowafahamu; mbegu (breed) aina hii ya kuku huwa ni nadra sana kupatikana katika soko.

Ni kuku wakubwa kwa umbo, warefu na wenye kusimama mgongo ukiwa wima.

attachment.php


Kuchi wana manyoya machache mwilini hasa kifuani, wana mdomo mfupi na panga/vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa kilo 3.5 na mitetea kilo 2.

Mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gramu 45. Kuku hawa wanapatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.

Kuku hawa ni wazuri kwa nyama.

attachment.php


VIDEO toka Kenya:

KSHS 1 zidisha mara 20 kupata TSHS.

Nilipoona heading ya Uzi na I'd kuwa ni JF Nilitarajia makubwa sana!

Sasa hayo masoko ya nje na ndani uliyoyataja kwenye heading yako Wapi!?
 
Ukishangaa ya Musa unaona ya filauni
Kuna wajinga wasioelewa maana hawapaswi kuombiwa maana
Xaxa unaambiwa wanauzwa laki 2
Unatoa povu umelazimishwa kama ghali kamalizie bar iyo laki 2 zenu
 
Kuku wa kroiler ana kilo 3.5 anauzwa 25,000/= alafu kuchi kilo 3.5 anauzwa 200,000/=. What is so special with kuchi? Nyama yao ina virutubisho zaidi ya kuku wengine?
kununua kuchi kwa zaidi ya bei ya soko ni ulimbukeni. kuchi hutumika sana kwenye michezo ya kupiganisha kuku, wapemba, wahindi na waarabu wanawatumia sana hawa. nanwatu huwekeza pesa zao kwenye haya mapambano. kwaiyo kama akikuta una kuchi mzuri, na yeye akajiridhishankuwa kupitia uyo kuku anaweza akaendeleza ubabe kwenye mapambano na akajipatia pesa, atamnunua uyo kuchi hata kwa laki tano.....ila kama unalenga kumuuzia mswahili akamle nyama, utasubiri sana kumuuza kwa iyo bei.

na hata wapemba wenyewe, wanaweza kumnunua mmoja tu kati ya mia, maana si kila mtu ana interest nanhuo mchezo
 
Mmhh hiyo Bei ni yako .Inaonekana hujui unachokiandika.

Sema kuku hawa hasa majogoo ni maarufu kwa kupigana na wanapunzi ya hatari na ujasili anaweza kimbiza hata mtu au mnyama.

lakini kwa bei sikubali nawe asilani.
 
Kuku wa laki2, hiyo michezo ya kupigana mpaka waje kununua sio leo

Sent from My GooglePixel using JamiiForums mobile app
 
Cascos si nilikwambia nikuuzie yule kuku kwa laki na nusu ukakomaa laki na ishirini? Unaona bei zake?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom