JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,202
- 5,007
Kutokana na ongezeko la maswali ya wadau wengi juu ya ufugaji wa kuku aina hii, tumeonelea ni vema tukauweka mjadala huu vema kuweza kuwasaidia wafugaji na wanunuaji wa vifaranga/kuku wa aina hii.
Kuku aina ya KUCHI, ni wale ambao wanawauza kwa shilingi 200,000 hadi zaidi kwa kuku mmoja. Pamoja na kuwa kuku hawa wanaonekana kama wa kawaida, lakini si kama kuku wale tunaowafahamu; mbegu (breed) aina hii ya kuku huwa ni nadra sana kupatikana katika soko.
Ni kuku wakubwa kwa umbo, warefu na wenye kusimama mgongo ukiwa wima.
Kuchi wana manyoya machache mwilini hasa kifuani, wana mdomo mfupi na panga/vilemba vyao ni vidogo. Majogoo huwa na wastani wa uzito wa kilo 3.5 na mitetea kilo 2.
Mayai ya kuchi yana uzito wa wastani wa gramu 45. Kuku hawa wanapatikana kwa wingi maeneo ya Mwanza, Shinyanga, Tabora na Zanzibar.
Kuku hawa ni wazuri kwa nyama.
VIDEO toka Kenya:
KSHS 1 zidisha mara 20 kupata TSHS.

Attachments
Last edited by a moderator: