Mwenyekiti wenu namaanisha JK.
Suala la Lowassa kutajwa mwembeyanga lilishajadiliwa na Mjadala kufungwa. Alishaeleza hausiki kwa anayohusishwa, akaeleza nani anahusika kwa Jina na kusema mkitaka nendeni mahakamani. Kimya.
Leo hii badala ya kumpeleka mtu huyu mahakamani, mnahangaika kuzuia mikutano ya hadhara ya ukawa, mnazuia Bunge kuonekana live, mnatafutana uchawi ndani ya chama kwa usaliti. Kwenu huo ndio Mbadala wa kumfungulia mashitaka kwa ufisadi na kumfunga jela. Watanzania wa Leo sio wa 1967.
Wanajua kinachoendelea, ndio maana wakamchagua kwa Kura nyingi kabla ya chama chenu kufanya njama ya kutungua matokeo angani kupitia wataalam mliowaleta na kuwaweka Mayfair plaza, mlimani city estate, double tree nk.
Pona ya ccm kwa sasa ni Rais magufuli kuendelea kuonekana kama sio sehemu ya wahafidhina wa ccm. The more you delay "kumpa" nafasi ya uenyekiti, hivyo ndivyo mnasukuma mbele mpasuko wa CCM. Mpasuko haukwepeki. CCM ya baada ya Mwalimu ni CCM ya kilaghai na ujanja ujanja. Tuombe uzima kushuhudia tukio hilo la kihistoria.