Ufisadi wa Lowassa wakumbushiwa bungeni

BungelaKatiba2014tz

JF-Expert Member
Feb 18, 2014
1,231
648
Hali hiyo ilitokea jana bungeni mjini hapa, baada ya baadhi ya wabunge wa CCM kuwapiga vijembe wenzao wanaotoka Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kutokana na kumteua kuwa mgombea urais na kumuunga mkono katika Uuhaguzi mkuu uliopita.
Hata hivyo, kutajwa kwa Lowassa ndani ya bunge na kuibua mjadala, nusura kusababishe vurugu hivyo kumlazimu spika wa Bunge, Job Ndugai, kuahirisha kikao mpaka jana jioni.

Vienne hivyo viliibuliwa na Mbunge wa Madaba (CCM), Joseph Mhagama, alipokuwa akichangia Mpango wa Pili wa Maendeleo ya Taifa wa mwaka 2015/16 hadi 2020/21.
Mbunge huyo alisema uchumi wa Tanzania utaimarika ikiwa serikali itawekeza kikamilifu katika viwanda, lakini akajikuta anatoka kwenye hoja na kuanza kuwashambulia wapinzani akidai wanapinga utaratibu wa Serikali ya Awamu ya Tano wa kutumbua majipu.

Mhagama alisema anawashangaa wapinzani kwa kuwa vigeugeu, akidai wanawaunga mkono mafisadi ilhali kipindi cha nyuma sera kuu ya upinzani ilikuwa kupambana na ufisadi.

Wakati akiendelea kuchangia, Mbunge wa Tarime Vijijini (Chadema), John Heche, alisimama na kuomba kutoa taarifa ambayo alieleza kuwa upinzani haupingi utumbuaji majipu.

Heche alisema upinzani unaunga mkopo utaratibu huo na kufafanua kuwa hata sababu za kutumbuliwa kwa aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe, ziliwahi kuelezwa bungeni na aliyekuwa Mbunge wa Nyamagana, Hezekiah Wenje.
Heche alikwenda mbali zaidi kwa kueleza kuwa majipu yanayotumbuliwa yalitengenezwa na CCM na kwamba Mhagama ni sehemu ya majipu hayo.

Baada ya taarifa hiyo, Mhagama alikataa kuipokea baada ya kuuulizwa na Spika wa Bunge, Job Ndugai, akisisitiza kuwa hawezi kupokea taarifa ya wapinzani ambao walileta taarifa bungeni kuwa Lowassa ni fisadi, lakini wakampitisha kugombea urais.
Siwezi kuipokea taarifa hiyo kwa sababu wapinzani hawa hawa walioleta taarifa hapa bungeni na kutuaminisha Lowassa ni fisadi, mwaka jana walimkumbatia na kumpa nafasi ya kugombea urais,alisema Mhagama, huku wabunge wa CCM wakishangilia kwa kupiga makofi.

Baada ya kuona hali inaelekea kuchafuka bungeni, Spika (Ndugai) aliasitisha kikao hicho cha tatu cha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 hadi saa 11:00 jioni.
Katika hatua nyingine, Mbunge wa Busega (CCM), Dk. Raphael Chegeni, naye aliwapiga vijembe wapinzani wakati akichangia mpango huo akieleza kufurahishwa na uamuzi wa kuzuia matangazo ya moja kwa moja ya Bunge hilo. Chegeni alidai kuwa wapinzani sasa hawana ujanja kutokana na kuzuiwa kwa matangazo ya moja kwa moja ya Bunge. "Hata vijembe hapa bungeni sasa vimepungua kwa sababu hakuna anayeona kule. Tujengane hapa kwa hoja na si mbwembwe ambazo hazina faida kwa wananchi," alisema.
 
ha ha ha

wabunge wale ambao kuropoka sana ndio kuliwafanya waonekane wanajua kazi, ili hali majimbo yao hayana huduma bora za jamii imekula kwao

wakafanye kazi

as for Lowassa; kuna mtu anabisha kuwa sio fisadi??? LOWASA NI FISADI, wengine ni kikwete, ridhwani, Mbowe, niendelee??
 
Wakati unabwabaja hapa mafisadi jitahidi na ushahidi uwe nao zakuambiwa changanya na zako.
 
ha ha ha

wabunge wale ambao kuropoka sana ndio kuliwafanya waonekane wanajua kazi, ili hali majimbo yao hayana huduma bora za jamii imekula kwao

wakafanye kazi

as for Lowassa; kuna mtu anabisha kuwa sio fisadi??? LOWASA NI FISADI, wengine ni kikwete, ridhwani, Mbowe, niendelee??
Tatizo lako linajulikana sio la kwako tu bali la kifamilia na ukoo kwani vichwa vyenu sio wazima na wengi wenu mna ma file hosp. za wendawazimu. na ukiendelea kutaja utajikuta unataja jina lako kwa sababu hizo hizo za kiwenda wazimu.
 
Lazima iume unajua

yaani kukuambia Lowassa ni fisadi na ulikuwa unapiga deki barabarani na kuzungusha mikono .....baadae akili zilipokurudia na ukagundua uliingizwa shimoni lazima iume

pole mkuu, shika bandeji hii hapa, badnika juu ya nilipokuchoma sindano

Lowassa ni fisadi
 
Kusema ukweli kabisa mpaka leo bado nashindwa....kuwa wapinzani walitumia gani cha kufikiria hadi wakamuona kuwa Lowasa anafaa kugombea uraisi kupitia umoja ambao hapo mwanzo alikuwa akiupinga kwa nguvu zake zote...........

Mbowe alipata wapi ujasiri wa kumpendekeza LOWASA kuwa mgombea wa UKAWA hali ya kuwa anajua kuwa ni fisadi na badala yake anatuambia kuwa mwenye ushahidi atangulie mahakamani......??

SIDHANI KAMA UKAWA KUPITIA CHADEMA WALIKUWA KATIKA HALI YA KAWAIDA KIAKILI WAKATI WANAYAPENDEKEZA HAYO.......
 
ha ha ha

wabunge wale ambao kuropoka sana ndio kuliwafanya waonekane wanajua kazi, ili hali majimbo yao hayana huduma bora za jamii imekula kwao

wakafanye kazi

as for Lowassa; kuna mtu anabisha kuwa sio fisadi??? LOWASA NI FISADI, wengine ni kikwete, ridhwani, Mbowe, niendelee??
Nini kinazuia fisadi asichukuliwe hatua za kisheria?Hebu acheni porojo zenu!
 
Kusema ukweli kabisa mpaka leo bado nashindwa....kuwa wapinzani walitumia gani cha kufikiria hadi wakamuona kuwa Lowasa anafaa kugombea uraisi kupitia umoja ambao hapo mwanzo alikuwa akiupinga kwa nguvu zake zote...........

Mbowe alipata wapi ujasiri wa kumpendekeza LOWASA kuwa mgombea wa UKAWA hali ya kuwa anajua kuwa ni fisadi na badala yake anatuambia kuwa mwenye ushahidi atangulie mahakamani......??

SIDHANI KAMA UKAWA KUPITIA CHADEMA WALIKUWA KATIKA HALI YA KAWAIDA KIAKILI WAKATI WANAYAPENDEKEZA HAYO.......
Mkubwa huku ninakoishi tunaitwa WONGA!!!!!!!!!!!!
 
Kwa nini msishangae jinsi tume ya uchaguzi chini ya Lubuva waliyoyatenda wakati wa kujumlisha na kutangaza matokeo na mfano hai ni kwenye Jimbo la january makamba ambako waliopiga kura kumchagua Rais walikuwa mara 2 zaidi ya waliopiga kura kuchagua mbunge,na vipi kuhusu yale magunia ya kura feki yaliyokuwa yametapakaa nchi nzima yenye kura za Magufuli yalikuwa ya nini kama UKAWA walikuwa wamekosea kumteua Lowasa kugombea Urais kupitia umoja huo?
 
ha ha ha

wabunge wale ambao kuropoka sana ndio kuliwafanya waonekane wanajua kazi, ili hali majimbo yao hayana huduma bora za jamii imekula kwao

wakafanye kazi

as for Lowassa; kuna mtu anabisha kuwa sio fisadi??? LOWASA NI FISADI, wengine ni kikwete, ridhwani, Mbowe, niendelee??
mbowe ?/
 
Dah CCM wamepindua meza,wanamtumia Lowassa kama fimbo ya kuwachapia wapinzani, bora Dr Slaa amejiweka kando na hii fedheha Mbowe hivi ulifikiria nini kumfanya Lowassa kuwa mgombea wa CHADEMA? Ona sasa mmebanwa kwenye angle,hamshambulii tena kama tulivyowazowea,mmegeuka kuwa watu wa kujihami dhidi ya mashambulizi ya CCM.
 
Kusema ukweli kabisa mpaka leo bado nashindwa....kuwa wapinzani walitumia gani cha kufikiria hadi wakamuona kuwa Lowasa anafaa kugombea uraisi kupitia umoja ambao hapo mwanzo alikuwa akiupinga kwa nguvu zake zote...........

Mbowe alipata wapi ujasiri wa kumpendekeza LOWASA kuwa mgombea wa UKAWA hali ya kuwa anajua kuwa ni fisadi na badala yake anatuambia kuwa mwenye ushahidi atangulie mahakamani......??

SIDHANI KAMA UKAWA KUPITIA CHADEMA WALIKUWA KATIKA HALI YA KAWAIDA KIAKILI WAKATI WANAYAPENDEKEZA HAYO.......
Huo ujasiri ulikuwa wa kibiashara na maslah kwa baadhi yao ndomana wengine walikikimbia hicho chama
 
Kwa nini msishangae jinsi tume ya uchaguzi chini ya Lubuva waliyoyatenda wakati wa kujumlisha na kutangaza matokeo na mfano hai ni kwenye Jimbo la january makamba ambako waliopiga kura kumchagua Rais walikuwa mara 2 zaidi ya waliopiga kura kuchagua mbunge,na vipi kuhusu yale magunia ya kura feki yaliyokuwa yametapakaa nchi nzima yenye kura za Magufuli yalikuwa ya nini kama UKAWA walikuwa wamekosea kumteua Lowasa kugombea Urais kupitia umoja huo?
Mkuu inawezekana kabisa Lowasa kuwa alishinda kiti cha uraisi na kuwa uwezekano huo kwenye uchaguzi ujao kama anaweza akashinda kwa kuwa ni mwanasiasa mwenye ngome imara na mitandao iliyotapakaa kila mahali na hata ndani ya serikali.....mshangao ni jinsi gani CHADEMA waliwaza kumpitisha Lowasa.....mtu walikuwa wakisema kiwa hafai hata kuwa mjumbe wa nyumba kumi.....kwa kusema kuwa ushahidi wa ufisadi wa Lowasa wanao na leo wanatuambia kuwa mwenye ushahidi aende mahakamani....??
 
Dah CCM wamepindua meza,wanamtumia Lowassa kama fimbo ya kuwachapia wapinzani, bora Dr Slaa amejiweka kando na hii fedheha Mbowe hivi ulifikiria nini kumfanya Lowassa kuwa mgombea wa CHADEMA? Ona sasa mmebanwa kwenye angle,hamshambulii tena kama tulivyowazowea,mmegeuka kuwa watu wa kujihami dhidi ya mashambulizi ya CCM.
matokeo hujayaona ya lowasa kuwa mgombea? au unajitia upofu ?
 
Back
Top Bottom