Ufisadi wa kutisha wa Bernard Membe

Ufisadi wa kutisha wa Bernard Membe

Hivi wana sheria wanaweza kunikosoa lakini Kama wananchi mna ushahidi mkiwa na group yenu ya wana sheria wapenda nchi hamuwezi kumpeleka mahakamani kiongozi kwa kutumia vibaya Mali za umma/ wizi kama huu au mpaka jamhuri/ mwendesha mashtaka/ takukuru wachukue hatua ? kwa kweli hii suala la kulaumua membe sijui nani nchi za mbele huko inaweza kusaidia Hapa inabidi tufanye kitu
 
Waliojenga uchafu huu wamedhalisha fani nzima ya uhandisi.
 
Yaani kampuni ni ya Shemeji,lakini anayetuhumiwa ni Membe?

Siasa zetu zitakua za kijinga sana kwa staili hii.

Nadhani hapa ni gutter politics ndani ya chama chao tu.Mafisadi wanataka kila mtu aonekane kuwa anafanana nao.
Ben Emmanuel Masanche ni kama msimamizi tu hiyo kampuni ni ya familia ya mkewe na inawakilisha initials zao D ni Dorcas....watu wa TPA wanasema hata hiyo tender haikufuata taratibu kampuni haikuwa na vifaa na wataalamu wa kutosha lakini kwa shinikizo la bwana mkubwa kampuni ilipata kazi tena collectively magati mawili Mbamba Bay na Kigoma na kote imeharibu vibaya
 
Lowasa ndiyo jembe mkuu. kwanza ni binadamu makini anayejua kutubu dhambi kwa Mungu wake na mchapa kazi haswa sio huyu anayetembea kwenye kivuli cha mwenzake aliyechokwa.

...mkuu' watandanyika wanataka rais anayevutia kwa sura, mrembo na mtanashati "handsome" ili akauze sura ulimwenguni (ulaya na kwingine)' rais wa wadanganyika anatakiwa awe na mvuto ili wakati anatembeza kapu la kuombea mikopo sura yake iwe inakubalika kwa wengi, tuliyenaye...!
 
Wanajamvi kumekuwa na upotoshaji wa makusudi kwenye siasa za Tanzania kumuhusu ndg Benard Membe, waziri wa mambo ya nje na ambaye anatajwa kwenye mbio za kusaka ukuu wa nchi kuwa ni msafi na asiye na doa.

Ukweli ni kwamba huyu hana tofauti na wenzake huko kwenye chama chao,huyu bwana ameitia nchi hii kwenye hasara kubwa kwa makusudi ama kwa malengo anayoyajua yeye.

Akiitumia kampuni ya ujenzi ya shemeji yake Emmanuel Masanche iitwayo MODSPAN bwana huyu alichukua kandarasi ya ujenzi wa gati katika bandari ya Mbamba Bay huko Ruvuma na Kigoma lakini kilichofanyika ni usanii wa hali ya juu kwani gati la Mbamba Bay halikidhi viwango na liliamriwa kubomolewa na kujengwa upya.

Ajabu ni kwamba hasara hii ni ya serikali kwa sababu MODSPAN imelipwa fedha zote na kandarasi imepewa tena kampuni ya kichina kubomoa gati hilo na kulijenga upya huku MODSPAN ikiachwa kwa amani kabisa na haijachukuliwa hatua zozote kisheria kisa kazi ilikuwa ya bwana mkubwa MEMBE.

Hivi huyu anaitakia mema hii nchi kweli ndg zangu.....shime wananchi CCM ni kama ukoo wa panya hakuna aliye msafi huko tuwaondoe

View attachment 149045View attachment 149045

Pichani ni sehemu ya gati hilo la mbamba bay ambalo linavunjwa ili kujengwa upya.

umesikika na una stahili kupuuzika
 
Yaani kampuni ni ya Shemeji,lakini anayetuhumiwa ni Membe?

Siasa zetu zitakua za kijinga sana kwa staili hii.

Nadhani hapa ni gutter politics ndani ya chama chao tu.Mafisadi wanataka kila mtu aonekane kuwa anafanana nao.


Hii statement angekuwa kaitoa Zitto @Zito ahahahha CCM Oyeee.
 
Last edited by a moderator:
Yaelekea kuna wanaokerwa kuona kwamba kuna watu CCM ambao hawana scandal za ufisadi. Mada hii inadhihirisha hili. Ifike wakati tupongeze wasiokuwa wafisadi na kukemea wafisadi badala ya kuwatafutia ufisadi wa kuchongesha na kuupost. Ati failure ya shemeji lawama anapewa Membe! Nahisi aliyebandika bandiko hili anajaribu ku neutralize impact ya bodaboda kupigwa marufuku mjini.
 
Membe ameingiaje hapo,Je Membe ana hisa kwenye hiyo kampuni? Je Membe aliingiza mkono kwenye upatikanaji wa hyo tenda?
Kama aliweka mkono wake kwenye zabuni ndo tuanze kumjadili bwana Membe.
 
Weka vielelezo vya mkataba

dah yaani we bure kabisa mkataba mie niutoe wapi? kampuni ikifanya mradi mahali inatambulika nimeleta nilichokishuhudia mambo ya mikataba kawaulize TPA
 
Yaelekea kuna wanaokerwa kuona kwamba kuna watu CCM ambao hawana scandal za ufisadi. Mada hii inadhihirisha hili. Ifike wakati tupongeze wasiokuwa wafisadi na kukemea wafisadi badala ya kuwatafutia ufisadi wa kuchongesha na kuupost. Ati failure ya shemeji lawama anapewa Membe! Nahisi aliyebandika bandiko hili anajaribu ku neutralize impact ya bodaboda kupigwa marufuku mjini.

Hii post ni ya ajabu mno kupata kusomwa na mm!
Membe HANA haki ya kuwa na shemeji?Shemeji wa Membe HANA haki ya kushinda zabuni?Kama shemeji wangu kaharibu basi ina maana na mm nimeharibu?

Is this not a real gutter politics?
 
Mkuu hii ni tetesi au fact? Acha kumchafua Membe usije ukaingia kwenye list ya watakaopata matatizo akiingia Ikulu.

Kwa hiyo Sirikali imeidhinisha mafungu mara mbili kufanya ujenzi wa gati hiyo hiyo? tena ndani ya muda mfupi?

Maswali ni mengi kwako kuliko majawabu hebu weka full document kabla hatujadeclare huu kuwa umbea

Hilo la kuidhinisha malipo mara mbili kwa mradi mmoja ndio staili ya magamba ya kuibia wananchi; mbona hata mradi wa barabara ya Bagamoyo mpaka Msata ulilipwa mara mbili baada ya wajanja wa Bagamoyo kuzikomba fedha wakishirikiana na contractors wa Korea!!!! Magamba ndio zao hizo.
 
Back
Top Bottom