Ufisadi wa Capt. Komba wa TOT Band (CCM) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi wa Capt. Komba wa TOT Band (CCM)

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Sep 16, 2008.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  UFISADI MPYA CC
  ---KAPTEN KOMBA ABEBESHWA TUHUMA
  --RIPOTI YAORODHESHA ULAJI MKUBWA WA ""tOT"
  --CCM YATHIBITISHA ,,KOMBA AKANA TUHUMA
  --ADAI NI CHUKI NA MAJUNGU
  ---KITAMBI CHOTE KUISHA???

  Mkurugenzi wa kikundi cha TOT kapten john komba anakabiliwa na tuhuma chafu za ubadhirifu wa mamilion kinachomilikiwa na chama cha mapinduzi
  tuhuma hizo zimeibuliwa baada ya ukaguzi wa mara kwa mara unaofanywa katika asasi zinazotolewa na chama cha mapinduzi..ukaguzi huo ulifanyika kuanzia machi 3 hadi 16 na baadaye apr 1 hadi 6..
  katika taarifa ya uchunguzi komba anadaiwa kutafuna zaidi ya sh milllioni 30...zaidi ya mishahara ya wafanyakazi wa tot miezi 15
  uchunguzi uliopata baraka za chama unaonyesha CCM ilitoa sh 37,442.923
  kwa ajili ya malimbikizo ya mishahara ya miezi 14 kuanzia agosti 2006 hadi aug 2007
  malipo ya awami ya kwanza yalifanyika kwa hati namba 056996 ya sh 18,532,458 na tar 21/12/2007 hati ya malipo namba 1343 ya sh18,910,465 ilisema tarifa ya uchunguzi,ukaguzi ulishtuka kuona majina ya watu waliosainishwa nakulipwa sh 6928298 kwa muda wa miezi miwili tu..watumishi waliulizwa na kukiri walipewa malimbikizom ya miezi miwili tu....
  """""''

  PIA VIONGOZI HAWA WANAHUSISHWA NA UDANGANYIFU WA KUWALIPA MAREHEMU WASIO WAASIS WA CHAMA JUMLA YA SH 27,3MILLIONI
  LAKINI BAADHI WALIOTAJWA KWENYE ORODHA WAMEKANA KULIPWA FEDHA ZOZOTE..KWA MUJIBU WA UCHUNGUZI LINAONYESHA JINA LA MAREHEMU NA JINA LA MRITHI NA KIASI ALICHOPEWA

  MAREHEMU :::GODFERY LUGENDO \
  MRITHI WAKE HAJI MWAMNTUMU ALISAINI MILLION 4,320,000

  MAREHEMU ::LEYLA HATIBU
  MRITHI :MONICA ROBERT ALISAINI SH MILLION 6,752,000

  MAREHEMU ::FRED MSHANA
  MRITHI::BENSON MSHANA ALISAINI 4,880,000

  MAREHEMU::HAMIMU HAMERA
  MRITHI::MWANAKOMBO AHMED ALISAINI 4,240,000

  MAREHEMU ::SALUM POOGWE
  MRITHI::NURU SALUM
  ALISAINI 7,200,000

  FEDHA ZOTE ZILIZOLIPWA KWA AJILI HIYO NI SH MILLION 27,000,000

  MADAI MENGINE ANAYOTUHUMIWA KOMBA NIKUWAPUNJA WAFANYAKAZI WA TO KWA KUWALIPA POSHO YA SH 20,000 WAKIWA NJE BADALA YA SH 40,000
  ZINAZOTOLEWA NA CHAMA
  TAARIFA INAONYESHA WAKISAFIRI KILASIKU NJE YA DAR VIONGOZI WANALIPWA SH 40,000 NA WALIOBAKI 30,000 WANAOKWENDA KUCHUKUA FEDHA HIZO NI AMA KAPT KOMBA AMGASPER TUMAINI..FEDDHA HIZI HUWA HAZIINGI KITABUNI WALA WASANII HAWARUHUSIWI KUSAINI SEHEMU YOYOTE ILISEMA TAARIFA
  UKIACHA HIZO KASHFA TAARIFA INASEMA KOMBA ANATUHUMIWA KUSAJILI GARI LA CCM KWA JINA LA ASASI YAKE IJULIKANAYO KAMA EDUCARE GIRLS...HE MUNGU WANGU??????????????????????
  PIA ALISAJILI GARI JIPYA LA CHAMA NISSAN CIVILLIAN MINI BUS TZT 8978 NA BAADAYE AKALIUZWA KA SH 2300,000 WAKATI ALINUNUA KWA SH 16,200,000
  PIA ANAKABILIWA KUUZA GARI LA CHAMA MITSUBISHI TZR 6056 KINYUME NA UTARATIBU NA UKAGUZI WA ANASEMA HAJASEMA ALIPATA KIASI GANAI NA ZILITUMIKAJE...TARRIFA NYINGINE INASEMA KABLA YA UCHAGUZI WA 2005 ALIPEWA NA CCM MAGARI 3 SCANIA LA KUVUTA TELA..ISUZU FORWARD NAMBA T488 AHD NA BASI DOGO T203 ABC..KUTOKANA NA TUHUMA HIZO IMEEPENDEKEZWA KUANZIA SASA MALIZOTE ZIWE CHINI YA MAJINA YA CCM.NA ZISAJILIWE NA JINA LA CCM NA KOMBA AREJESHE FEDHA ZOTE
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Arejeshe fedha zote walizopata kwa kuuza magari kinyume na taratibu na chama kiwachukulie hatua za kinidhamu.....kwa mujibu wa komba anadai lori ni lake.......kwa mujibuwa komba anadai tarifa hizo zimejaa chuki na umbea na unafiki anasubiri aletewe
   
 3. K

  Kipanga JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2008
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 679
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Hivi hawa CCM wametuona watz tuko usingizini nini?? Na sasa wanasubiri za EPA kwenye kampeni wagawane....Kumbe akina Misambano wanalia njaa fisadi anakamua kiroho mbaya...ama kweli ukishangaa ya musa utaona ya firauni...
   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2008
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Sera ya chana cha mafisadi mimi sishangai kitu hapo!! wako kwenye kutekeleza sera zao
   
 5. Lambardi

  Lambardi JF-Expert Member

  #5
  Sep 17, 2008
  Joined: Feb 7, 2008
  Messages: 10,306
  Likes Received: 5,594
  Trophy Points: 280
  sasa wanaumbuana wenyewe...tunasubiri nae Komba ajibu mapigo kwa kuwaanika wenzake wanaokula wote........mwaka huuu na badoo...2010 itakuwa isambe....
   
 6. WomanOfSubstance

  WomanOfSubstance JF-Expert Member

  #6
  Sep 17, 2008
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 5,465
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 0
  TUJIANDAE kuona wizi kila kona...mradi kuna precedent on how to deal with embezzlers and thiefs basi cha kuogopa nini tena? Kila mtu anajitahidi kubugia akiwa mezani mwake tena kwa spidi ya ajabu!
   
 7. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #7
  Sep 17, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  Watanzania nawaambia wote mnaosoma hii jf kama mungu ataendelea kutupa uhai ccm ya sasa hivi siyo itakayokuwa 2010...amini watu wengi watakimbia na wengine kuona hakuna haja tena ya kuwa na chama ..na labda kwa ajili ya uzee wanashindwa kukimbia nchi

  mungu tushike mkono
   
 8. BabaDesi

  BabaDesi JF-Expert Member

  #8
  Sep 17, 2008
  Joined: Jun 30, 2007
  Messages: 2,793
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  ...Kunakuja tume hapo kuchunguza!
   
 9. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #9
  Sep 17, 2008
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Waache wamalizane wenyewe kwa wenyewe sasa. Ila kama fedha zilizotumika kutoa malipo ni za EPA hapo itabidi tumshikie bango Komba.
   
 10. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #10
  Sep 17, 2008
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Mhhhhhhh! Kwa Chama Cha Mafisadi sishangai sana. Kuna jipya hapa??? Kwani wakubwa zake waliokula nyingi zaidi ya hizi wamechukuliwa hatua gani? Kuna jambo hap!!!!! Wewe sikilizia uchaguzi 2010. Ndo maandalizi yameanza hivyo!!!!!

  Katika kesi hiyo aunganishwe na mkewe kwa kuanzisha SACCOs na kupewa hela za JK Fund wakajichukulia kiulani. Wanachama wa SACCOs ya Mbezi Beach wamefungua kesi na CRDB wamefungua kesi. Tehe tehe. Wife ni tapeli namba moja!!!!

  Zile shule Mbweni Coletha Memorial na Kamuzu Banda ni majeruhi. Za usanii hizo. Kachunguze matokeo ya mitihani hasa pale ambapo mwaka huo paper haijavuja. Sijui wizara ya Elimu inafanya ukaguzi kweli.

  Ila wabongo wengi wanaishi kwa maisha ya usanii. Elimu kushoto but mbwembwe na kutumia briefcase za headed papers zote nyeti na mihuri mbele.

  Komba afanyiwe uchunguzi wa ndani. Ila hatutaki mambo ya kuunda tume maana hazina jipya zaidi ya kumaliza pesa za walipa kodi through poshos.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Sep 17, 2008
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,061
  Likes Received: 5,552
  Trophy Points: 280
  ...Kunakuja tume hapo kuchunguza!  CHAIRMANI  MH ANDREW CHENGE MWENYEKITI WA TUME

  CCM NAKUPENDA DAIMA MMMMHHHH

  TANGANYIKA NTAKULILIA MILELE
   
 12. N

  NTIRU Member

  #12
  Sep 19, 2008
  Joined: Sep 20, 2007
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mnashangaa nini?? Komba ni mwana-Chama cha Mafisadi. Yeye ameamua kuchota ndani ya Chama chenyewe. Kwani kakosea nini? Si unajua tena wazungu husema "charity begins at home". Hongera sana Big Komba!! Hilo limwili la tembo ungelipataje kama si kujichukulia ndani ya "system?" Ungeenda EPA ungelaaniwa bure. Sasa ndani kwa ndani kwa kuwachapa wanenguaji wa TOT ... 40,000/- kwa 20,000/-. Wanenguaji wote wale, ukale wapi!! Mhh!!! Kazi ipo.
   
 13. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #13
  Sep 19, 2008
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 104
  Trophy Points: 145
  Nambari one eheeeeee nambari one ni CCM......tieni tieni tieni pemba na unguja nambari one ni CCM........Kigoma twende...Iringa twende....Nambari one ni CCM........
  Saizi akisimama hata kitovu hakioni anakunia pembeni si mchezo fweza tamu wajameni....
  Anakula naye kwa urefu wa kamba yake sijui mapapa mafisadi watamshughulikia au ndo hivyo tena..
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Sep 19, 2008
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Hivi kuna kiongozi/mbunge ye yote wa ccm ambaye ni safi walau kwa 25%? kama yupo nitajieni.
   
 15. M

  Mgelukila JF-Expert Member

  #15
  Jun 13, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 224
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wanamuziki wa TOT wanamdai mh. Komba na wako tayari kufikisha madai yao kwa mwenyekiti wa ccm taifa ili waweze kulipwa haki zao pamoja na kupatiwa studio kwa ajili ya kufanyia kazi zao waliyohaidiwa na Jk na kuelekeza lawama kwa Y. makamba kushiwa kutekeleza ahadi ya Jk na kuilaumu ccm kwa kuto wajali wamelalamika wakiongozwa na katibu wa kikundi hicho Gasper Tumaini
   
 16. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #16
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 730
  Trophy Points: 280
  Waambie wajitegemee, watoe alban zao wauze mitani kama wasanii wenzao.
   
 17. POMPO

  POMPO JF-Expert Member

  #17
  Jun 13, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 6,694
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Nepi hebu walipeni wasani mbona mnawatumia, ma mmestuka kuwa ni wapenz wa chadema?
   
 18. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #18
  Jun 13, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  ccm oyeeee!!
   
 19. Landala

  Landala JF-Expert Member

  #19
  Jun 13, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 938
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 45
  CCM wanawafanya wanamuziki wa TOT Kama kondom mtu huitumia akiisha maliza shida zake huitupa na hataki hata kuigusa,poleni sana wanamuziki wa TOT kwa kunyanyaswa na kunyimwa haki zenu na John Komba ambaye pia ameshindwa kuwalipa mishahara walimu wa shule yake ya Bakili Muluzi.
   
 20. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #20
  Jun 13, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  wakome
   
Loading...