Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa!

Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa!

Kuna ushahidi au kupaka watu matope pasi na sababu mpate umaarufu?

mkuu, mleta mada amenukuu maneno ya mbunge aliyekuwa anaongea bungeni, hakutaka kuweka wazi lakini alipoombwa kuweka wazi ndio akaitaja hiyo hospitali ya aga khan, si jambo la kupuuzwa limesemwa sana
 
ni maelezo ya mbunge wa viti maalum magdalena sakaya bungeni...kweli inasikitisha sana...katibu mkuu wa wizara anaondoa vifaa muhimu vya tiba kwenye hospitali ya umma na kuvipeleka kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya dili...hatimaye anayelaumiwa ni serikali na rais kumbe ni wasaliti wachache wenye njaa zao...kwa taarifa ya magdalena sakaya blandina nyoni akamatwe na polisi na kisha afikishwe mahakamani

watanzania mnaosoma hii thread msisahau kinana naye anatuhumiwa kuchukua mashine za kufulia za hospitali ya mount meru na kupeleka kwenye drakilina ya mdogo wake.polisi wa arusha mpo?
 
Kwa CCM nijambo la kwaida kwani kila mtu anakula kutokana na office yake. Kwao hilo sio kosa na hakuna wakumfunga paka kengele.

mkuu kwani yule mama ana kadi ya ccm?? msiwe mnaingiza chuki kwenye mambo ya msingi, tujadili hili suala jinsi lilivyo kwa manufaa ya watanzania
 
Kama ni kweli wala Nyoni asilaumiwe... Kuna watu chungu nzima waliotakiwa kulisemea hilo kabla ya kufika kwa wanasiasa... Hii ni nchi yetu sote, tusisubiri wanasiasa hata mambo yanayohusu uhai wetu...

kweli mkuu, ila kwa kuwa limesemwa na mwanasiasa, tushinikize hatua stahiki zichukuliwe dhidi ya wahusika hawa hasa blandina nyoni
 
Hawa wabunge wengine kazi yao kuropoka tu ili kuwachafua wenzao; haingii akilini kuwa katibu mkuu anaweza kuhamisha CT-SCAN toka Muhumbili na kuipeleka Aga khan hospital kwa misingi gani? After all Aga Khan hospital wanayo SC-Scan yao hata kabla ya Muhimbili!!! Huyu mbunge alete ushahidi wa hayo anayoyasema badala ya kusema mambo yasiyokuwa na maana ili mradi nae asikike kuwa kazungumza bungeni!!

hili ni zito, usiseme wanaropoka, si kawaida mtu wa hadhi ya mbunge akaibuka na neno zito kama hili kama hana ushahidi. ww mfuate mwambie akupe ushahidi, akishindwa ndipo utuambie maneno haya.
 
Aga khan hospitals ni taasisi yenye heshima na hadhi ambayo isingekubali kitu kama hicho kifanyike; ingefaa ielezwe ni kwa mazingira gani CT-Scan iliondolewa Muhimbili na kupelekwa huko. Hiki chombo kinachozungumziwa sio chombo kama bilauli ni chombo chenye gharama kubwa kiasi kwamba hakiwezi kuondolewa mahala kimchezomchezo!! Huyu mbunge inawezekana kabisa hajui hata hiyo CT-Scan ikoje lakini kwa fitina za kijiweni kaenda kubwabwaja bungeni ili nae asikike!!
 
mkuu kwani yule mama ana kadi ya ccm?? msiwe mnaingiza chuki kwenye mambo ya msingi, tujadili hili suala jinsi lilivyo kwa manufaa ya watanzania

Ni CCM DAMU NDIO MANA SERIKALI INAMLEA. Kama serikali ingekua makini ingeshamchukulia hatua mapema lakini mwisho wasiku katoka wizara ya afya then wakampa ulaji mwingine TRA.
 
hili ni zito, usiseme wanaropoka, si kawaida mtu wa hadhi ya mbunge akaibuka na neno zito kama hili kama hana ushahidi. ww mfuate mwambie akupe ushahidi, akishindwa ndipo utuambie maneno haya.

Mara nyingi tu wabunge wanaropoka mambo ambayo wakiambiwa wathibitishe wanashindwa!! Muhimbili kuna Mkurugenzi Mkuu , je ilikuwaje akakubali mpaka kitendea kazi muhimu kama hiki kiondolewe toka hospitalini kwake na kipelekwe hospiali ya Aga khan? Sio hivyo tu; Muhimbili kama taasisi ina bodi yake ambayo ina oversight functions ambazo ni pamoja na kuangalia mali za shirika , je walibariki uhamishaji wa kifaa hicho kama ni kweli?
 
Huyo mbunge aliyesema hivyo ni wa chadema nini? Maana Msigwa disease inaweza kuwaathiri wabunge wenzake pia.
 
Ni maelezo ya mbunge wa viti maalum magdalena sakaya bungeni...kweli inasikitisha sana...katibu mkuu wa wizara anaondoa vifaa muhimu vya tiba kwenye hospitali ya umma na kuvipeleka kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya dili...hatimaye anayelaumiwa ni serikali na rais kumbe ni wasaliti wachache wenye njaa zao...kwa taarifa ya magdalena sakaya blandina nyoni akamatwe na polisi na kisha afikishwe mahakamani
Sio kila Litamkwalo ni habari
 
Hawa wabunge wengine kazi yao kuropoka tu ili kuwachafua wenzao; haingii akilini kuwa katibu mkuu anaweza kuhamisha CT-SCAN toka Muhumbili na kuipeleka Aga khan hospital kwa misingi gani? After all Aga Khan hospital wanayo SC-Scan yao hata kabla ya Muhimbili!!! Huyu mbunge alete ushahidi wa hayo anayoyasema badala ya kusema mambo yasiyokuwa na maana ili mradi nae asikike kuwa kazungumza bungeni!!
Mie nafikiri tufikie mahali itungwe sheria inayoruhusu kuwashitaki wabunge wanaotuhumu watu ambao hawako ndani ya bunge ili haya majungu yapungue.
 
Mara nyingi tu wabunge wanaropoka mambo ambayo wakiambiwa wathibitishe wanashindwa!! Muhimbili kuna Mkurugenzi Mkuu , je ilikuwaje akakubali mpaka kitendea kazi muhimu kama hiki kiondolewe toka hospitalini kwake na kipelekwe hospiali ya Aga khan? Sio hivyo tu; Muhimbili kama taasisi ina bodi yake ambayo ina oversight functions ambazo ni pamoja na kuangalia mali za shirika , je walibariki uhamishaji wa kifaa hicho kama ni kweli?

hivi unajua hata mzabuni wa kutunza bustani za muhimbili alipelekwa na mama huyu wakayi muhimbili wana bodi ya zabuni ya kwao hata Mhe. Pinda alilisema hili katika vikao na madaktari? unajua mkurugenzi wake aliteuliwa na huyu mama kwa mintarafu yenye mashaka mengi kwani awamu za awali alikataliwa na Bodi?je unajua nn alifanya kuhakikisha mkurugenzi muhimbili anakuwa yule anayemtaka yy hata kama sifa zingine hakuwa nazo? mm sipo upande wowote ila haya yalisemwa na kwa vielelezo, mtafute tumbiri atakupa data
 
Look here kamanda, Pinda mwenyewe ndio aliyemishandle suala zima la wizara ya Afya mbona la Jairo aliyekuwa nae KM alimgoja Kikwete.! Kama bodi inashindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria huwezi kumlaumu katibu mkuu wa wizara husika. Kumbuka bodi ya Muhimbili haiko answerable kwa katibu mkuu wa wizara ya Afya!! Sina haja ya kuntafuta Tumbili kwa hilo kwani ni common sense na liko wazi!!
 
Hawa wabunge wengine kazi yao kuropoka tu ili kuwachafua wenzao; haingii akilini kuwa katibu mkuu anaweza kuhamisha CT-SCAN toka Muhumbili na kuipeleka Aga khan hospital kwa misingi gani? After all Aga Khan hospital wanayo SC-Scan yao hata kabla ya Muhimbili!!! Huyu mbunge alete ushahidi wa hayo anayoyasema badala ya kusema mambo yasiyokuwa na maana ili mradi nae asikike kuwa kazungumza bungeni!!

Kwani ushahidi wa epa haukua ushahidi?
 
Ni maelezo ya mbunge wa viti maalum magdalena sakaya bungeni...kweli inasikitisha sana...katibu mkuu wa wizara anaondoa vifaa muhimu vya tiba kwenye hospitali ya umma na kuvipeleka kwenye hospitali binafsi kwa ajili ya dili...hatimaye anayelaumiwa ni serikali na rais kumbe ni wasaliti wachache wenye njaa zao...kwa taarifa ya magdalena sakaya blandina nyoni akamatwe na polisi na kisha afikishwe mahakamani

Mara zote serikali ndiyo yenye makosa hapo..
Jiulize;
1. Amewajibishwaje hata leo kwa kufanya hayo?
2. Je sasa ambapo imekuwa bayana atafanyiwa nini?

Thats right...serikali hii ni ya kiswahiba.
 
Look here kamanda, Pinda mwenyewe ndio aliyemishandle suala zima la wizara ya Afya mbona la Jairo aliyekuwa nae KM alimgoja Kikwete.! Kama bodi inashindwa kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa sheria huwezi kumlaumu katibu mkuu wa wizara husika. Kumbuka bodi ya Muhimbili haiko answerable kwa katibu mkuu wa wizara ya Afya!! Sina haja ya kuntafuta Tumbili kwa hilo kwani ni common sense na liko wazi!!

mm na ww hatuna haja ya kubishana, ila kumbuka uwepo wa bodi yoyote anayekubali na kupeleka mapendekezo ya majina ya wajumbe wa bodi kwa waziri ni katibu mkuu, uko uwezekano wa bodi kuwa obidient kwake hata kama inaona anayofanya ni kinyume cha sheria ili kulipa fadhila. pinda inawezekana alimishandle lakini huenda iliokana na yy kutoambiwa ukweli wa suala zima la mgomo wa madaktari. mie nadhani tuiachie serikali ifanye lile inaona inafaa kwani ni serikali sikivu
 
hawa wabunge wengine kazi yao kuropoka tu ili kuwachafua wenzao; haingii akilini kuwa katibu mkuu anaweza kuhamisha ct-scan toka muhumbili na kuipeleka aga khan hospital kwa misingi gani? After all aga khan hospital wanayo sc-scan yao hata kabla ya muhimbili!!! Huyu mbunge alete ushahidi wa hayo anayoyasema badala ya kusema mambo yasiyokuwa na maana ili mradi nae asikike kuwa kazungumza bungeni!!

hata mhe sakaya akileta ushahidi utafinyangwa tu uonekane si mali kit.ya epa?ya richmond?unasahau sera za magamba za kulindana mzee?ya rada nani amekamatwa?tuhuma za wizi wa kuiba mashine ya hospitali huko arusha?na,,,,,na......na.......na.....na.......tutafika tu mungu yuko nasi.
 
tanzania bana...serekali imejeuka taasisi ya wahuni flani hivi ambao ni marafiki
 
Back
Top Bottom