Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa!

Ufisadi wa Blandina Nyoni huu hapa!

Huyu mama ndiye alikuwa mhasibu mkuu wa serikali. Ina maana wakati huo pia alifanya madudu yote haya au wakati wa mkapa system ilikuwa ngumu kidogo. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza.

Nikisoma tuhuma zote hizi, hata kama alifanya nusu ya haya yaliyoandikwa, nadhani huyu mama ni wa kuhurumiwa zaidi. Nadhani ni mgonjwa, huwezi ukawa na akili sawa ukafanya anayoyafanya. Watu huuma na kupuliza ili usimhisi vibaya sasa yeye utemi utemi. Sidhani kama anaweza akachomoka. Maana mkuu wa kaya kasema makatibu wakuu wote sasa wachunguzwe, nadhani hata yeye ameshtuka na kushangaa.
 
Wanajamii kwani hamjui nani alikuwa anampa kiburi jamani? Baba yetu kambeba sana swaiba Nyoni, kwani hamshangai mbona yeye hakuwahi kuongea chochote kabisa kuhusu sakata la madaktari? hakutaka aguswe lakini maji yalifika shingoni. Hivi watanzania tutakuwa wapole mpaka lini??? au hadi Yesu arudi maana hapo wizarani kama waliona huo ufisadi lakini wakavumilia tu vipi na sehemu nyingine tusizozijua??? Hospitali hazina vifaa, wagojwa wa operation wanashonwa nyuzi za ovyo matumbo yanawafumuka, hivi mbona viongozi wetu hawana huruma jamani! kwakuwa wao wanajua wakiumwa wanaenda nje sisi tunaowapa kura ndio tunateseka, jamani tuamkeni kutetea haki zetu. wanakula kodi zetu bila mafanikio yoyote.
 
Huyu mama ndiye alikuwa mhasibu mkuu wa serikali. Ina maana wakati huo pia alifanya madudu yote haya au wakati wa mkapa system ilikuwa ngumu kidogo. Haya ndiyo maswali ya kujiuliza.

Nikisoma tuhuma zote hizi, hata kama alifanya nusu ya haya yaliyoandikwa, nadhani huyu mama ni wa kuhurumiwa zaidi. Nadhani ni mgonjwa, huwezi ukawa na akili sawa ukafanya anayoyafanya. Watu huuma na kupuliza ili usimhisi vibaya sasa yeye utemi utemi. Sidhani kama anaweza akachomoka. Maana mkuu wa kaya kasema makatibu wakuu wote sasa wachunguzwe, nadhani hata yeye ameshtuka na kushangaa.
Tuna safari ndefu sana!
 
Mfumo mzima ni mbovu, wamezoea kuiba! Zamani walikuwa wanaiba usiku ila sa hivi wanachukua mchana kweupe.

Ukistaajabu ya musa utayaona ya filaun
i. Mimi nawaangalia tu.
 
Kama nilivyohaidi, nimeendelea kuwasiliana na watumishi wa Wizara ya Afya na wa Wizara ya Maliasili na Utalii kuhusu Ufisadi wa Blandina Nyoni. Yafuatayo ni baadhi ya vitendo vya Ufisadi vya Mama huyu ambaye kwa wengine wanamuona kama mchapa kazi hodari asiyekuwa na doa na anaezuia mianya ya wizi:-

1. Amekuwa akijilipa mshahara wa ziada kupitia Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi (NACP) wakati tayari serikali inamlipa mshahara wa ngazi ya Commissioner kupita Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)


2. Ametengua utaratibu rasmi wa kila Idara ya Wizara ya Afya kuwa na afisa manunuzi wake badala yake ame centralize kwake mwenyewe. Kwa maana hiyo, manunuzi yote ya Wizara anamlazimisha (Comand) Mkurugenzi wa Kitengo cha Manunuzi kumpa kazi zote ndugu yake anaeitwa Donatha Koko.

3. Amekuwa akicomand wizara kununua uniform za madereva, suti za sikukuu (Sabasaba na Nanenane) na Maua kutoka Mariedo bila kushindanisha na muuzaji mwingine kinyume na kanuni za manunuzi.

4. Katika mikutano yote inayofanyika Wizarani, amekuwa akicomand kampuni ya Kaliula Catering Services kupewa tenda ya kulisha chakula washiriki tangu alipotua Wizarani kama Katibu Mkuu.

5. Miezi mitatu iliyopita aliiteua kampuni ya Soft tech ambayo yeye ni mbia kwenda kukagua Accounts System ya Muhimbili kinyume na kanuni za kikaguzi kwa kuwa tayari ana ‘Conflict of Interest'

6. Amekuwa akiongoza Wizara kwa kutumia Informers ambao kazi yao kubwa ni kumpelekea habari nani anasema nini na nani anasema nini kuhusu yeye binafsi na uongozi wake. Informers wake wakuu ni Elias Mkumbo ambaye ni dereva na Donatha Koko ambeye ni ndugu yake wa damu damu na ni afisa ugavi wa wizara

7. Amemkopesha gari la serikali aina ya Suzuki Informer wake Elias Mkumbo (dereva) ambae kimsingi hastahili kukopeshwa gari kutokana na cheo chake. Kwa dereva wa serikali, anachoruhusiwa kukopa ni Baiskeli, Piki piki na Piki piki ya miguu mitatu (Bajaj)

8. Amenunua vingamuzi vya magari (Vehicle Security and Fuel control system) vibovu kwa ajili ya magari manne kwa shilingi 1.3 Billion bila kufuata taratibu za manunuzi kwa kucomand Single source procurement kutoka kampuni moja yenye makao yake huko Israel. Manunuzi haya yamefanyika wakati Hospitali nchini zikiwa hazina dawa, Interns doctors hawajalipwa mishahara yao, watumishi wake wakidai fedha za likizo, uhamisho na vyuo vingi vya afya vilivyo chini yake vikiwa na madeni lukuki.

9. Mwishoni mwa mwaka wa fedha 2009/2010 alihamisha kiasi cha Shilingi 1,968,475,931 mali ya Wizara ya Afya kwenda National Institute for Medical Research (NIMR) bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizi zilikuja kuhojiwa na CAG katika ripoti yake ya serikali kuu ya mwaka 2009/2010

10. Mwishoni mwa mwaka huo huo wa fedha alihamisha kiasi cha Shilingi 3,083,400,000 mali ya Wizara ya Afya kwenda Health Sector Development Project bila kibali cha hazina kwa matumizi yasiyojulikana. Fedha hizo pia zilihojiwa na CAG.

11. Amelikosesha Taifa kupata fedha za Mfuko wa dunia mzunguko wa 11 (Global Fund Round 11) kwa kupitia Mradi wa Taifa wa kudhibiti Malaria Nchini (NMCP) kwa kushindwa kutumia fedha zote zilizotolewa na mfuko huo katika mizinguko ya nyuma. Kwa kifupi ni kwamba Global Fund hawatoi pesa wakiona una Significant unspent balances.

12. Amekuwa akizuia uhamisho wa Chief Accountant (Bi Helen Saria Mwakipunda), Chief Internal Auditor (Bi Anna Joseph Mhere) na Director of Adminstration and Personnel (Bi Tabu Chando) kwa kile anachodai wanamsaidia katika utendaji wa Wizara. Amezua barua za uhamisho za Chief Accountant mara mbili, Chief Internal Auditor mara moja na Director of Administration and Personnnel mara moja. Ukweli ni kwamba amekuwa akizua uhamisho wa wakurugenzi hawa kwa sababu ni watu waoga na wamekuwa wakikubali chochote anachosema hata kama kinavunja kanunu na taratibu za serikali mfano katika maeneo ya Manunuzi.

Kwa nini Chief Accountant (Hellen Saria Mwakipunda) na Chief Internal Auditor (Anna Joseph Mhere) wanamuogopa kama Mungu Blandina Nyoni? Ni hivi: Hellen Mwakipunda, alikua Junior staff kwa Nyoni, kipindi hicho Nyoni ni Mhasibu mkuu wa Serikali. Blandina Nyoni ndiye aliye mpandisha cheo Mwakipunda na kuwa Chief Accountant, kipindi hicho hata CPA hakuwa nayo. Anna Mhere alipata u-CIA akiwa na Advance Diploma in Accountancy - ADA tu. Ili swala lilikuwa linawashangaza watu wengi sana. Sasa kwa inferiority complex walizokuwa nazo hawa wakina mama, ni lazima wamuabudu Blandina Nyoni.

13. Amemuhamisha aliyekuwa Kaimu wa Kitecho cha Ugavi Mzee Funga kwenda Hospitali ya Mirembe Dodoma kwa kukataa kununua Uniforms, suti na Maua kutoka kwa Mariedo kwa sababu alihoji ni kwa nini Mariedo watoe huduma wakiwa hawana Mkataba na hawajashindanishwa na wauzaji wengine.

14. Amekuwa akihama hama na dereva wake toka Hazina alipokuwa Muhasibu Mkuu wa serikali hadi Wizara ya Maliasili na Utalii kama Katibu Mkuu. Pia amehama na dereva huyo huyo kutoka Maliasili hadi Wizara ya Afya kinyume na taratibu na kanuni za Utumishi wa umma ambazo haziruhusu kiongozi au mtendaji yeyote wa serikali kuhama na dereva au / na secretary

15. Hamsalimii Naibu wake Waziri Bi Lucy Nkya kutokana na Naibu huyo kugoma kupangiwa dereva ambaye ni Informer wake. Hadi leo hii hamsalimii hata wakikutana kwenye kordo. Kinachowazungumzisha ni madokezo tu.

16. Alikuwa na uhusiano mbaya na Naibu Waziri wake aliyeondoka Bi Aisha Kigoda kwa sababu ambazo hazijulikani. Kama ilivyo kwa Lucy Nkya nae pia walikuwa hawasalimiani.

17. Akiwa Wizara ya Maliasili na Utalii, aligombana na Waziri wake Bi Shamsa Mwangunga na wakawa hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

18. Alipokuwa Mhasibu Mkuu wa Serikali alikuwa anateua ndugu zake na watu anaofahamiana nao na kuwapa vyeo vya u Chief Accountants na Chief Internal auditors bila kuwa na sifa kamili ya kupewa vyeo hivyo. Mfano kuhold CPA (T) na Masters.

19. Amesababisha kushuka kwa morali ya utumishi kwa Wafanyakazi wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii. Hivi sasa ndiyo Wizara inayoongoza kwa kuwa na watumishi wengi walioamua kwenda likizo ya masomo ili kuepuka manyanyaso yake.

20. Ameanzisha utaratibu ndani ya Wizara ya Afya wa kupokea Excheque kutoka hazina na anazihold bila kufanya distribution kwenye idara zake. Kutokana na utaratibu wake huu anafanya malipo kwa kutegemea mahitaji yanavyojitokeza. Utaratibu huu ni kinyume na kanuni za hazina za matumizi ya fedha za umma.

21. Ikitokea kazi za Construction na maintanance anacomand tenda ipewe kwa Mzenzi Contractors Ltd. Alishinikisha Mzenzi ajenge ofisi za Wizara zilizopo Dodoma na akafanikiwa, baadae alishinikiza Mzenzi ajenge jengo banda la Maonyesho la Wizara kwa ajili ya Nane nane lilipo Dodoma na akafanikiwa na alishinikiza Mzenzi apewe tenda ya kufanya small maintanance wizarani kwenye ofisi yake, Ofisi ya Waziri na Naibu Waziri kwa ajili ya kuweka tiles na kuboresha vyoo na akafanikiwa.

22. Katika section ya Matibabu ya nje amejenga Network na Hospitali za India ambazo zinapelekewa wagonjwa kuibill wizara inflated invoice prices.

23. Amechukua mashine za kusafishia figo akishirikiana na Dk Linda Ezekiel pamoja na reagent na filter wakazipeleka Msasani kwenye Hospitali yao ambayo Blandina Nyoni ana shares.

24. Amejenga banda la maonyesho ya sikukuu ya nane nane kwa kutumia fedha za NIMR kwa Shilingi 1.5 billion. Lakini banda lenyewe lililopo pale Nane nane Dodoma ukiliangalia tu kwa haraka haraka kwa macho thamani yake haizidi hata million 400.

25. Ameingiza robo tatu ya vifaa bandia vya vipimo vya Ukimwi kutoka Korea Kusini.

26. Ameingiza kinyemela bila kufuata taratibu za Manunuzi kampuni ya kufanya usafi ndani ya Hospitali ya Taifa Muhimbili.

27. Ameshinikiza kampuni ya Jambo Concept Tanzania Limited kupewa tenda namba ME/007/2009-10/HQ/G/191 kwa ajili ya Printing and Placing of Billboards with TB/TBHIV bila kufuata taratibu za manunuzi. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada hii orodha

28. Blandina Nyoni akishirikiana na Dr Deo Mtasiwa wamecheza mchezo mchafu katika tenda ya ununuzi wa Bajaj kama ilivyoratibiwa na Wizara ya Miundombinu kupitia tenda namba ME/015/2009 - 2010/S/06. Katika tenda hiyo bajaj moja ilinunuliwa kwa US$ 8,400. Kwa maelezo zaidi juu hii tenda soma maelezo kutoka kwa 'someone' kama nilivyoyaatach hapa chini baada ya orodha hii.

29. Ametengua uteuzi wa Dr Mtimba kama Mkurugenzi Msaidizi na kumuhamishia Damu Salama Tabora na badala yake amemkaimisha Dr Budeba kwa miaka miwili mfululizo bila kumthibitisha kushika nafasi hiyo kinyume na taratibu za utumishi. Anafanya hivyo kwa sababu Dr Mtima hana urafiki naye.

30. Ametengua uteuzi wa Dr Sawe ambaye angeenda India kuwapokea Wagonjwa na badala yake kamteua Dr Goroka ambaye kiudugu ni mtu na Mama yake. Hivi sasa kampeleka Dr Ngoka ambaye ni family friend wake pia.

31. Ametengua uteuzi wa Dr Sawa anayesimamia uandikishaji / usajili wa Hospitali binafsi na kumpatia Mtoto wa Balozi Lusinde ambaye ni rafiki yake na walisoma nae High School Kilakala mmoja akiwa Form V mwingine akiwa Form VI

32. Ametengua uteuzi wa Dr Muhame ambaye alikuwa Msajili wa tiba asilia na kumpatia Dr Naomi ambaye ni Mama Mdogo wake. Yaani yeye na Blandina ni mtu na mtoto wa binamu.


33. Yeye ndiye chanzo cha masahibu yaliyowakabili Watanzania kwa kukosa huduma ya afya kwa zaidi ya Wiki mbili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kitendo chake cha kutaka kulipiza kisasi kwa Intern Doctors kwa kuwahamishia Mikoani pale walipodai haki zao ambazo ni stahili zao halali



Uchunguzi wa hizi tuhuma zilizowasilishwa na Mwana JF assuredly4 naendelea kufuatilia ili nipate majina kamali ya hao ndugu zake hatimae tuweze kuingiza kwenye Orodha yetu.

Note: Orodha itaendelea kuongezwa kadri tunavyozidi kupata data kwa watu walio karibu na Wizara na Muhimbili

From 'someone'


Ndugu yangu Tumbiri, TISS (UWT) wameshakufanyia uchunguzi, file lako wanalo na wameshakujua wewe ni nani. Wamenidokeza kuwa wewe ni mtumishi wa Wizara ya Afya, so kaa mkao wa kula siku yeyote wanakuletea kipira.
 
kila kukicha kituko kipya cha ufisadi kitasikika.
spare the bullet,spoil the nation.
 
TAKUKURU pia mkachunguze ni kwa vipi hawa mapacha wawili (nyoni na mtasiwa), walichukua magari ya wizara na kuyapaki majumbani mwao kwa shughuli za home, kama vile kwenda sokoni, saluni etc...
Nyoni alikuwa na landcruiser na volvo, mtasiwa alikuwa na landcruiser.
Haya magari yote yalikuwa mapya, na yalikuwa na namba za DFP.
Mkitaka full information, kamuulizeni mkuu wa kitengo cha transport mtapata majibu.
 
Tatizo la mfumo mzima wa utawala kuanzia very top. Blandina kama Blandina anajua maadili ya kazi yanakataza kufanya anayofanya, lkn anafanya hayo kwa kutegemea kuwa some1 aliyepo juu sana atamlinda. Yeye ameonekana, hizo wizara nyingine je? Taasisi nyingine za serikali? Wanalindwa hawa, inatubidi kuanzia juu sana.
 
Mkuu MD25 endelea kumwaga data usiogope kwa vile inaonekana wakuu wanapita humu na naamini TISS wamepunguziwa kazi kwa vile maeneo ya kuanzia yote wanayo. Tuwaunge mkono akina Dr Ulimboka ambao wame scrifice professions zao na kazi zao kwa ajili ya kulitetea taifa letu.
Kuna TISS bongo au wala mshahara wa bure tu??
 
Ndugu yangu Tumbiri, TISS (UWT) wameshakufanyia uchunguzi, file lako wanalo na wameshakujua wewe ni nani. Wamenidokeza kuwa wewe ni mtumishi wa Wizara ya Afya, so kaa mkao wa kula siku yeyote wanakuletea kipira.

acha kumtisha uchunguzi wa nini

msiingie jf kwa kutumia computer za maofisini kuleta habari moto

na wewe ulieandika hapa unaenda chini
 
Tatizo la mfumo mzima wa utawala kuanzia very top. Blandina kama Blandina anajua maadili ya kazi yanakataza kufanya anayofanya, lkn anafanya hayo kwa kutegemea kuwa some1 aliyepo juu sana atamlinda. Yeye ameonekana, hizo wizara nyingine je? Taasisi nyingine za serikali? Wanalindwa hawa, inatubidi kuanzia juu sana.
Huko juu ndio wapi mzee? Unaogopa kupataja? Hapa unatumia ID feki still unaogopa?
 
Ndugu yangu Tumbiri, TISS (UWT) wameshakufanyia uchunguzi, file lako wanalo na wameshakujua wewe ni nani. Wamenidokeza kuwa wewe ni mtumishi wa Wizara ya Afya, so kaa mkao wa kula siku yeyote wanakuletea kipira.

Haha ha ha ha! Nakushangaa sana kwa kutotambua kwamba Mimi ni mfanyakazi wa TISS. Nilikuwepo Afya mwaka uliopita kwa kazi hii baada ya kuimaliza kazi yangu nimehamishiwa Wizara nyingine kwa kazi kama hii. Pole sana!

 
Mkuu unapaswa kujua kwamba hapa JF unatakiwa ulete habari ukiwa umejiandaa vizuri na ushahidi. Tena ushahidi ambao si wa kubabaisha. Sasa kama tungesema toka awali kwamba Blandina Nyoni ni Fisadi bila hata kutoa ushahidi ni nani angetuelewa? Orodha ya matukio hapo juu ni matokeo ya kazi ya uchunguzi wa muda mrefu. Huwezi ukapata huo ushahidi kwa siku moja alafu ukauleta hapa JF. Kama huamini emu jaribu hata wewe mwenyewe kufuatilia Ufisadi wa mtu yeyote Serikali uone kama utaupata kwa siku moja alafu uubandike hapa. Ni bahati mbaya sana kwamba ushahidi hii ulipatikana complete wakati mgomo wa madaktari nao ukiwa in Progress. Sasa hapa huwezi ukasema kwamba ninaongozwa na matukio bali may be mwenzetu ndiye uliechotwa na hayo matukio. Tafakari!

Na kwa taarifa yako, Madaktari walishamwandikia Rais barua juu ya utawala mbovu wa Blandina Nyoni tangu mwaka 2010 na walitaka aondolewe. Kibaya zaidi Rais Kikwete badala ya kufanyia kazi ile barua alimuita Nyoni Ikulu akaanza kumueleza juu ya hiyo barua. Blandina Nyoni alivyorudi Wizarani akaanza kuwatukana Madaktari kwamba hakuna daktari Mwanaume Wizarani na kwamba kama waliona ana mapungufua kwa nini wasimwambie hadi waandike barua kwa Rais? Then akajitamba wataona sasa kama atafanywa chochote! Kwa hiyo kama ni hatua zilishachukuliwa toka zamani bila kuzaa matunda! TAFAKARI!
Kikwete oyeee! Kikwete juuuuu!
Ipeni kura CCm ipeni kura ahaaa!
 
Mpaka awabanie posho ndo mnafunguka????????we should be eyes open all the time wakuu!
 
Ndugu yangu Tumbiri, TISS (UWT) wameshakufanyia uchunguzi, file lako wanalo na wameshakujua wewe ni nani. Wamenidokeza kuwa wewe ni mtumishi wa Wizara ya Afya, so kaa mkao wa kula siku yeyote wanakuletea kipira.
Kama TISS wanafanya kazi kwa maslahi ya mtu mmoja basi taifa hakuna.
 
Haha ha ha ha! Nakushangaa sana kwa kutotambua kwamba Mimi ni mfanyakazi wa TISS. Nilikuwepo Afya mwaka uliopita kwa kazi hii baada ya kuimaliza kazi yangu nimehamishiwa Wizara nyingine kwa kazi kama hii. Pole sana!


A double agent, commonly abbreviated referral of double secret agent, is a counterintelligence term used to designate an employee of a secret service or organization, whose primary aim is to spy on the target organization, but who in fact is a member of that same target organization oneself. They are often used in local, national and international businesses. Most commercial organizations may formally delay the movement from one organization to another competitor after a defined time limit upon formally resigning from the official organization.
Double agentry may be practiced by spies of the target organization who infiltrate the controlling organization, or may result from the turning (switching sides) of previously loyal agents of the controlling organization by the target; the threat of execution is the most common method of turning a captured agent (working for an intelligence service) into a double agent (working for a foreign intelligence service) or a double agent into a re-doubled agent. It is unlike a defector, who is not considered an agent as agents are in place to function for an intelligence service and defectors are not, but some consider that defectors in place are agents until they have defected.
Double agents are often used to transmit disinformation or to identify other agents as part of counter-espionage operations. They are often very trusted by the controlling organization since the target organization will give them true, but useless, information to pass along.
 
Back
Top Bottom