UFISADI: The Making Of IPTL

Mkuu FEMS,
Niongeze tu kuwa kuna wale ambao nao wanatamani kukaa kuume kwa wakubwa hao, kazi yao ni kusifia kila kitu ili mradi tu kinatendwa na wao. Wengine ni wale waliosahaulika, kisha wakapiga kelele kidogo lakini kwa kuwa wanafahamika wakaonywa na wengine wakaahidiwa mshikaki wa kasungura au wakapewa ufadhili na namna fulani, hawa nao wamekuwa bendera fuata upepo na hawako tayari kuwachambua maafisadi hawa kwani wanajulikana au wanaogopa kukatiwa mirija kama mwanzo.
 
Asante mkuu, lakini ukiangalia kwa makini sana utaona wazi kwamba kila kitu kinachohusu CCM kinapingwa vikali sana na wana JF walio wengi. Kuna ufuatiliaji wa hali ya juu wa mambo na matendo yanahusu CCM na Viongozi wake. Hata kama jambo ni zuri na lina faida lakini hapa litajadiliwa kwa mtazamo mbaya. Kwa mfano wana CCM kuweka mashada ya maua katika kaburi la aliyekuwa mwasisi wa chama hicho imekuwa nongwa hapa JF.
Nakubali kabisa kwamba kuna mambo mabaya yanayofanywa ama yaliyofanywa na baadhi ya wanachama wa CCM, lakini si vyema kuwahusisha wana CCM wote katika ubaya huo. Upotevu wa pesa za EPA umehusisha watu toka vyama tofauti ndani na nje ya Tanzania, lakini lawama zote ni mzigo wa CCM. Kukosoa ama kulaumu kwa ajili ya kufuata mkumbo si kitu chema. Kama huna uhakika na kitu ni bora na ni hekima sana kukaa kimya ili ujifunze.
Hakuna jambo lolote zuri lililofanywa ama linalofanywa na CCM limeandikwa hapa ila ni mabaya tupu na ni imani yangu 110% kwamba CCM haifanyi mabaya tu bali ina mambo mengi mazuri pia inayafanya. Shillingi haina upande mmoja tu ina pande mbili, na kama ina pande mmoja basi hiyo si pesa tena.


Mtambo
Mkuu heshima mbele kwako. Unaposema mazuri MENGI ya CCM na ya Serikali uwe unayataja, mimi nitakuwa wa kwanza kukuunga mkono. Kuna sekta ya afya, elimu, nishati, ulinzi na usalama, sayansi na teknolijia, utalii, miundo mbinu .........kuna sekta nyingi sana. Kkama wewe kuna mazuri unayaona na yanastahili kusifiwa kwenye sekta yoyote kati ya hizo weka hapa. Kuna member mmoja anajiita MTU mpaka leo hataki kujibu maswali aliyoulizwa kuhusu mazuri aliyosema yamefanya na serikali na CCM.
Lakini pia ukumbuke kuwa kuwa madarakani unatarajiwa kufanya mazuri, kwa hiyo it is natural kutomsifu mtu kwa kufanya mazuri kwa kuwa tunategemea afanye mazuri.
Ni sawa na kuwa Baba. Huwezi kumsifu baba kwa kwa kuhakikisha anaipatia familia yake chakula, hiyo ni kazi yake. Lakini akichemsha ni lazima apingwe dongo, kwa kushidnwa kazi aliyoitaka.
 
Mkuu Nyangumi,

Heshima mbele kaka, nimekusikia mkuu analysis yako nzito sana mkuu, tuendelee kumkoma nyani giladi!

Na ninaamini mkuu Mtambo, amekuelewa.
 
Najua hapa sio mahala pake ila nilikuwa naulizia ile article ya spika iliyokuwa ikionyesha matumizi mabovu ya ofisi yake naona imepotea ghafla ilikuwa na page kama saba ...can someone please tell me where I can find it
 
Mkuu FMES,

Kwa hakika, uchambuzi wako ni makini! Ni muhimu kuwepo na watu wa namna yenu kwenye JF, otherwise JF inaweza kuonekana kama kijiwe cha Walalamikaji na Wapinzani wa CCM.
 
Kwa hakika, uchambuzi wako ni makini! Ni muhimu kuwepo na watu wa namna yenu kwenye JF, otherwise JF inaweza kuonekana kama kijiwe cha Walalamikaji na Wapinzani wa CCM.

Ahsante mkuu, ukweli ni kwamba wengi hawaelewi kuwa bunge letu lina wabunge wengi wa CCM kuliko upinzani, na hakuna tatizo, sasa kwa nini kuwe na tatizo hapa JF kwa kuwa kuna wapinzani wengi kuliko CCM?

Tujifunze kabla ya kulalamiaka kuwa Zitto na Slaa, sio wabunge wa CCM, lakini hebu niambie kama kuna wabunge wanaofahamika na wananchi kuliko hao, I mean huwezi kuilazimsiha demokrasia iache itakuja yenyewe as long as kuna determination na the will kwenye taifa demokrasia itakuja tu,

hoja nzito na facts of the matter ndio siku zote zitaaamua mwelekeo na mwisho wa topics, regardless of idadi ya walioko kwenye any of the side of the ishu. I am not worried na idadi ya upande mmoja hapa JF, hapana ninaaamini hoja tu ndio muhimu na kuheshimiana.
 
Ahsante mkuu, ukweli ni kwamba wengi hawaelewi kuwa bunge letu lina wabunge wengi wa CCM kuliko upinzani, na hakuna tatizo, sasa kwa nini kuwe na tatizo hapa JF kwa kuwa kuna wapinzani wengi kuliko CCM?

Tujifunze kabla ya kulalamiaka kuwa Zitto na Slaa, sio wabunge wa CCM, lakini hebu niambie kama kuna wabunge wanaofahamika na wananchi kuliko hao, I mean huwezi kuilazimsiha demokrasia iache itakuja yenyewe as long as kuna determination na the will kwenye taifa demokrasia itakuja tu,

hoja nzito na facts of the matter ndio siku zote zitaaamua mwelekeo na mwisho wa topics, regardless of idadi ya walioko kwenye any of the side of the ishu. I am not worried na idadi ya upande mmoja hapa JF, hapana ninaaamini hoja tu ndio muhimu na kuheshimiana.



Turudi sasa kwenye hoja kwa nini JK mnadhani asihushwe na IPTL maana ndiyo mada iliyo mezani mengine ni mazungumzo baada ya hoja hii .Kivipi mleta hoja anataka tuache kunyoosha kidole kwa JK ?
 
Further evidence is brought to the London arbitrators to prove that IPTL involved systematic corruption. Patrick Rutabanzibwa has sworn an affidavit that James Rugemalira offered him $200,000 to support IPTL. Rugemalira left a package containing Shs 500,000 at Rutabanzibwa's home during Christmas 1994. Rutabanzibwa says he returned the package, at the time worth eight and a half months' salary, to Rugemalira. Rutabanzibwa's former assistant, Prosper Victus, also testified that he was offered a similar amount to keep key information from Rutabanzibwa. Victus also implicates Mary Ndosi (later Maria Kejo), the state attorney who endorsed the IPTL contract on behalf of the government: 'When she telephoned me, Mrs Ndosi said … that "we want you to help us get this power project approved" and then she reminded me that Mr Rugemalira would give me 100,000,000 Tanzanian Shillings if the IPTL project were approved. I was shocked to learn that Mrs Ndosi had apparently been corrupted by Mr. Rugemalira.' (Witness Statement, 19 April 2000, p. 3).
 
Countries like Tanzania will never be able to aspire to the rates of economic growth and social development achieved by countries like Malaysia in the absence of ruling élites whose rent-seeking strategies contribute to rather than subtract from the public good. It is one thing for politicians and bureaucrats to take a cut from a valid investment that generates significant employment, turns out useful products, and contributes to government revenue.[/

Ujumbe maridhawa huo.

MWK, hivi unafikiri tuko mbali..yaani we live in interesting times. Kifupi ni kwamba huu ni ulimwengu wa doti com kama wenyewe wanavyosema wadhungu. Kwa hiyo gone are the days of sweeping things under the carpet. Ukweli ni kwamba hali ni ngumu kwa sababu information siku hizi zinasambaa within seconds na huwezi jua nani katuma! Just brace kwamba itafika kipindi kwamba wananchi tutasema NO na watawala wakigoma tutashikana masharti!

Mugabe sasa ana haha na effect ya information..ingekuwa zamani, ahh mbona angekuwa ameshatangaza kwamba kashinda..lakini sasa info ziko wazi..nakwambia things are becoming hard for our watawala-which is a good news for wananchi!
 
Last edited by a moderator:
Countries like Tanzania will never be able to aspire to the rates of economic growth and social development achieved by countries like Malaysia in the absence of ruling élites whose rent-seeking strategies contribute to rather than subtract from the public good. It is one thing for politicians and bureaucrats to take a cut from a valid investment that generates significant employment, turns out useful products, and contributes to government revenue.

Ujumbe maridhawa huo.

MWK, hivi unafikiri tuko mbali..yaani we live in interesting times. Kifupi ni kwamba huu ni ulimwengu wa doti com kama wenyewe wanavyosema wadhungu. Kwa hiyo gone are the days of sweeping things under the carpet. Ukweli ni kwamba hali ni ngumu kwa sababu information siku hizi zinasambaa within seconds na huwezi jua nani katuma! Just brace kwamba itafika kipindi kwamba wananchi tutasema NO na watawala wakigoma tutashikana masharti!

Mugabe sasa ana haha na effect ya information..ingekuwa zamani, ahh mbona angekuwa ameshatangaza kwamba kashinda..lakini sasa info ziko wazi..nakwambia things are becoming hard for our watawala-which is a good news for wananchi!

Yaani wewe acha tu,

Nimesoma hii dosier na kujiuliza kama kusingekuwa na internet au JF in this effect sidhani kama haya yote ningeyajua?!
 
Last edited by a moderator:
Unajua mambo yanapowekwa hadharani namna hii ndo wajue kwamba kuna watu wana uchungu na ugwadu na nchi hii zaidi yao.

I have never seen such a dubious contract mbaya zaidi waliohusika wengi still wako madarakani.

Ivi kama sisi wenyewe hatuna uchungu na nchi yetu ivi nani atakuwa na uchungu nayo.

Inauma sana


Muulize JK what and how much was his cut ? We know better his on IPTL .Aseme tu
 
Yebo,

I am curious to know what role did CCM play part on this! Ikiwa inasemekana kuwa Kolimba alikwenda Malaysia kuchonga dili, should we start to examine IPTL the same way we are examining EPA?

Is it possible that IPTL deal was actually first CCM deal to create alternative source of income? Then came Rada, Ndege, Meremeta, Tangold, Minara ya BOT, EPA, Richmond and almost Mvua za Mfalme?

Smell fishy fishy ehh...?
 
IPTL: Those In Favour … Those Against
'Kama huu ndiyo ushirikiano wa nchi za kusini, bora ukoloni urudi.'
('If this is 'South-South co-operation', then colonialism is preferable.')
Julius K Nyerere commenting on IPTL

Inafanana na nani aliyesema juzi juzi hapa!!
 
Umefika wakati wa kuangalia mikataba yote iliyosainiwa, kwanini rugemalila hakushitakiwa kama katibu mkuu amekiri kupew rushwa na yeye, au na yeye wakati huo alikuwa juu ya sheria.
 
Mr. Ngurudoto, good day. Habari ya huko amerika?
Inaelekea wewe ni mmoja wa watoto wa hao vigogo, unayetanua ughaibuni kwa vijisenti vitokanavyo na wapinda mgongo wa nchi yako. Hongera, ungekuwa mzalendo wa kweli usingejisifia kuishi ukimbizini. Wewe ni mkimbizi kama wakimbizi wengine, kuna wakimbizi wa vita, siasa, njaa, hali ngumu ya maisha n.k.
Kukazia hoja yangu, ni wamarekani wangapi wanapanga foleni usiku na mchana katika balozi zetu huko kuomba viza za kuja kutafuta elimu, kazi au maisha afrika? Hebu kumbuka mlivyosoteshwa kwenye mistari mirefu kwenye ubalozi wa marekani, na kupigishwa kwata za nenda rudi ili kupata viza ya kwenda kuishi huko? Una tofauti gani na mrundi au mnyarwanda anayepanga foleni huko biharamuro?
Sasa ulichokikimbia huku wenzio wanapambana kukiondoa, hao ndio mashujaa wa kweli. Mwoga hata siku moja hawezi kuitwa shujaa. Mnaoishi ugenini kujifanya mnatafuta maisha bila kuimarisha nyumbani ni waoga. Tuachieni tulioamua kuikomboa nchi yetu kutoka kwenye hili janga tupambane.
Tulipambana kuondoa ukoloni sasa tunapambana kuondoa ufisadi.
Tafakari: Nchini marekani na nchi zote zilizoendelea ni aibu na kosa kubwa mtu kukwepa kodi, hapa nchini ni hao unaowatetea ndo wanaongoza kukwepa kodi. Labla utuambie katika vijisenti alivyonavyo Chenge, ni kiasi gani cha kodi amelipa kwa serikali? Je kuna chombo chochote cha serikali kimewahi kuhoji hilo? Na Viongozi mabilionea wengine je?
Utakataaje kwamba serikali inaungana na wahalifu?
Labda huko ulikokimbilia kunafanyika negotiations kati ya mwivi na mwenye mali kuhusu kurudisha mali iliyoibwa. Is that so? Huku kwetu ndivyo ilivyo, tena negotiations zinafanywa na AG, IGP na DG PCCB. Upo hapo? Halafu umekazana nyenyenye!!!!!
Hivi una habari kwamba wakati wewe na watoto wa vigogo wenzako, mnalipiwa starehe zenu kwa kodi za walala hoi huku, watoto wa hao walipa kodi hizo wamenyimwa hata fursa ya kukopeshwa tu pesa wanazotozwa baba zao ili waweze angalau kulipia ada tu za vyuo vikuu vya hapa nchini, huku sembe na maharage wakibangaiza wenyewe?
Wajua kwamba watoto wa shule za msingi wanafukuzwa kufanya mitihani kwa kukosa dola sents 3 ambayo ni shilingi mia tano. Najua unaogelea kwenye midola, lugha ya dola ndo utaielewa.
Una habari kwamba watoto wa Tanzania wanatembea kilomita 15 asubuhi 15 jioni kwenda na kurudi kazini kutafuta riziki kwa kukosa nauli ya basi? Katika hali hiyo unategemea tuongeze uzalishaji? Hivi wewe unayajua mateso ya nchi hii??? Ama!
Huna tofauti na kiongozi wetu mmoja wa juu ambaye aliulizwa swali na mtangazaji wa BBC kwamba licha ya utajiri mlionao kwanini watanzania watanzania ni masikini. Akajibu hata yeye anashangaa ni kwanini watanzania ni masikini. Halafu wanaposimama kuomba kura wanatoa ahadi nyingi za kuondoa umasikini. Nonsense, utaondoaje umasikini wakati hujui sababu za huo umasikini? Badala yake mnatoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo ambao ni trading concerns, hawazalishi ati, matokeo yake boosting inflation. Tufanye upembuzi yakinifu kwanza. Matatizo ya mtanzania yapo kwenye uzalishaji. Hatuzalishi au tunazalisha kwa ajili ya matumbo yetu tu, mnasema "visious cycle of poverty". Huo sio wimbo au theories za vitabuni kama mlivyozoea watoto wa vigogo, it is a real thing. Poverty eradication is not the matter of sitting at Ngurudoto enjoying food, drinks and fresh air, it means real hard working.
What if hiyo mipesa wanayospend kianasa ingenunua matrekta, harvesters n.k halafu yakakodishwa kwa wanavijiji, malipo yakafanywa wakati wa mavuno, tungeshindwa kuwa na surplus?
Je badala ya kujenga BOT, tungehodhi mgodi wa mererani kwa ubia kati ya serikali na wananchi, tungesimamia/ control bei ya vito au kiwango tunachozalisha refer OPEC tungeongea lugha gani leo?
Je Watswana ni bora kiakili kuliko sisi? Mbona nchi yao ni jangwa na wanategemea zaidi almasi lakini wako juu? Tena kwa taarifa yako, idadi ya wananchi wote wa botswana haipishani na wakazi wa Dar Es Salaam, lakini wako juuu.
Kwa mawazo ya kitumwa kama yako, nchi haiwezi kuendelea. Tunahitaji fikra za kimapunduzi.
Vyombo vya dola vimekuwa vikipambana zaidi na wapigania haki, ambao wamekuwa wakiitwa wachochezi mfano Jambo Forum n.k, lakini kwa hakika ni katika kulinda mafisadi.
Nadhani umefika wakati vyombo hivyo vifanyiwe mabadiliko makubwa kimuundo. Vyombo kama PCCB, Police Force, Mahakama n.k.
Tuwe na fikra mpya wananchi, ule wakati wa zidumu fikra umepita sasa, mtu apimwe kwa kazi na utu wake na si itikadi yake.
Mapambazo dhidi ya mafisadi yanaendelea!!!!!!
 
Haya naona mpambano umekua "KWA WANAOISHI NJE NA WANAOISHI NDANI"
Tuntufye,hivi kuna haja kweli ya kumchukia Mtanzania mwenzako kwa kuwa tu amepata nafasi ya kwenda nje ya nchi na kupata makazi huko? Na kwa fikira yangu ya darasa la sita inanifanya nigundue kuwa hii hatred hata siku moja haitaweza kujenga katika hili tulipiganialo humu ndani.
Nadhani Ngurdoto amekuja na Issues zake, kitu cha kumuomba ni tu atuletee facts ili tujue kwa hakika kama asemayo ni facts.Hear says na maneno yenye Hasira ndani yake hayawezi kutushawishi sisi wasomaji kuwa asemayo ni kweli.
Ngurdoto,kwa ushauri ni vema ukafanyaia kazi madai yako Kuhusu Kubenea na wengien uliowataja kisha ukaja ukatuambia kwa nini unaamini unayoyasema.
Si rahisi sana kuandika hoja na kukubalika kirahisi humu ndani.Inahitaji upeo na uwezo wa kukusanya vidhibitisho ili uaminike na watu kujenga confidence juu yako.

Ni hayo tu
 
amanigk,

....pamoja na melezo yako mazuri, nafikir alilofanya Ally ni kumueleza ukweli Ngurdoto na wala sio kwamba ana hatred na walio nje. Huyu Ngurdoto kuingia tu siku ya kwanza na kuanza kuita wanaJF washenzi.........is beyond what we expect kwa mtu mwenye akili timamu...........kama ulivyoeleza....yeye kama anazo facts basi atuwekee hapa halafu aone moto wa wanaJF utakavyokuwa.............

...........kwa taarifa yenu nyie msioijua JF....................hapa HAKOPESHWI MTU, hatumuangalii Nyani usoni...........ukichemka ni mawe tu............hapendwi mtu hapa.........na ukifanya vyema wana JF watakupa KUDOS unazostahili..................and thats why we have this saying "Kumkoma Nyani Giladi"
 
Richmond, Dowans sawa, bado IPTL

Tanzania Daima~Sauti ya Watu

HABARI iliyotawala kwenye vyombo vingi vya habari leo kuwa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), limevunja mkataba wa kununua umeme wa dharura kutoka kwa Kampuni ya Dowans, ni faraja kubwa kwa Watanzania.

Ni faraja kwani mkataba huo uliorithiwa kutoka kampuni nyingine tatanishi ya Richmond Development Company LLC, ulikuwa ukiligharimu taifa sh milioni 152 kila siku ambazo ni fedha za walipakodi.

Uamuzi wa kuvunjwa kwa mkataba huo ambao ulikuwa umalizike Septemba 5, mwakani, ulitangazwa jana mbele ya waandishi wa habari na Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Dk. Idris Rashidi.

Dk. Rashidi alisema TANESCO imechukua hatua hiyo ambayo utekelezaji wake unaanza Agosti mosi mwaka huu, kutokana na ushauri wa kitaalam uliotolewa na taasisi moja ya kisheria ya hapa nchini.

Alisema tayari TANESCO ilikuwa imeshachukua hatua ya kuitaarifu rasmi Dowans ambayo inalipwa wastani wa shilingi milioni 152 kwa siku kwa kuliuzia shirika hilo la umeme nchini sehemu ya nishati wanayozalisha inayofikia megawati 100.

Kwa mujibu wa Dk. Rashidi, uchunguzi uliofanywa na wataalam hao ulibaini kwamba, uhamishaji wa mkataba kutoka Kampuni ya Richmond Development Company LLC kwenda Dowans Holdings SA na hatimaye Dowans Tanzania haukuwa halali kwani ulikiuka msingi wa mkataba.

Aidha, Dk. Rashidi alisema wataalam hao ambao walifanya kazi hapa nchini na kupokea taarifa kutoka Texas nchini Marekani yaliko makao makuu ya Richmond na baadaye Costa Rica inakotokea Dowans Holdings SA, walibaini kwamba mkataba wa awali kati ya TANESCO na Richmond Development Company LLC ulikiuka Sheria ya Manunuzi (Public Procument ACT No. 21 of 2004).

Tunaunga mkono hatua hiyo ya serikali ingawa uamuzi huo umechelewa kwani umefikiwa huku tayari ukiwa umeacha athari kubwa kwa watumiaji wa nishati hiyo na kwa TANESCO yenyewe.

Uamuzi huo umechelewa kutokana na ukweli kwamba tayari kulishakuwa na ubabaishaji mkubwa ulioonyeshwa na Kampuni ya Richmond kabla ya kukabidhi madaraka yake kwa Dowans.

LLC iliingia mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura na TANESCO Juni 23 mwaka 2006 na mkataba huo ukahamishiwa Dowans Oktoba 10, mwaka huo huo kutokana na Richmond kushindwa kutimiza malengo ya msingi ya kuleta kwa muda mitambo hiyo ya kuzalisha umeme wa dharura, lakini bado ama kwa kujua au kwa kutokujua serikali iliikubali Dowans.

Hata hivyo, tunafikiri kuwa uamuzi wa kuvunja mkataba tu ambao umefanyika baada ya kubaini kwamba kulikuwa na udanganyifu ndani yake, hautoshi bila kuchukua hatua zaidi za kisheria na hata kudai fidia kwa kampuni hiyo.

Ukiachilia mbali ubabaishaji uliofanywa na Dowans hadi mkataba wake kuvunjwa, bado kuna kampuni zingine zinazozalisha umeme wa dharura na kuiuzia TANESCO kama IPTL, mikataba yake nayo ivunjwe.

IPTL inalipwa zaidi ya sh bilioni 3 kila mwezi, iwe inazalisha au haizalishi umeme. Hali hiyo imefanya bei ya nishati hiyo kuzidi kuwa kubwa na kuongeza mzigo wa gharama za maisha kwa Mtanzania wa kipato cha chini. Tunaupongeza uongozi wa TANESCO, na kuupa changamoto kuwa baada ya Richmond na Dowans, sasa iangalie IPTL.
 
IPTL sues Tanesco over ‘84bn/- debt’

FAUSTINE KAPAMA
Daily News;
Friday,July 04, 2008


The Independent Power Tanzania Limited (IPTL) has filed an application at the International Centre for Settlement of Investment Disputes (ICSID), demanding 84bn/- in unpaid capacity charges from the Tanzania Electric Supply Company (Tanesco).

In the application lodged last month in New York, IPTL is seeking interpretation of an Award given by the ICSID on June 22, 2001 in arbitration proceedings that were initiated by Tanesco against the company operating a 100MW power plant at Tegeta in Dar es Salaam.

Tanesco had sought either termination of the Power Purchase Agreement (PPA) signed by the two parties in 1995 or reduction of the tariffs. Under the agreement, Tanesco was obliged to make monthly capacity, energy, supplemental and penalty payments to IPTL.

However, since January last year, Tanesco stopped paying the capacity charges after discovering that IPTL had not injected equity payments since commencement of the project as a determining factor for capacity charge payments.

According to the application, the basis by Tanesco was premised on misinterpretation of the Award, requiring the country’s giant electricity firm to comply with its obligations under the agreement. The application stated that the monthly capacity payments Tanesco was ordered to make were based on the application of an agreed upon financial model, which was made part of the Award to determine the arbitration.

One of determinations that was made part and parcel of the Award and Financial Model was that the project was financed with 70 per cent debt and 30 per cent shareholders’ equity, facts which were made known to Tanesco during the arbitration.

“Yet, Tenesco now states that since IPTL accounts for its shareholders’ equity contribution as a shareholder loan to IPTL, Tanesco is not bound by the Award, but is free to re-calculate the capacity payments,” the statement said.

The IPTL, a joint venture company between VIP Engineering and Marketing Limited, a Tanzanian Engineering Company and Mechmar Corporation (Malaysia) Berhad, states that such facts were determined in the previous arbitration. It is, therefore, asking the ICSID to resolve the controversy as it has such jurisdiction and IPTL has taken all internal actions to authorize the filing of the application.

The filing of the applications comes a few months after the United States District Court, in April this year, refused to proceed with the hearing of the IPTL complaint, demanding 30bn/- from the Tanzanian government, for breach of Power Purchase Agreement. Judge Alvin Hellerstein, instead, stayed the case and ordered IPTL to go for arbitration first as per the agreement and gave them six months to file a report on the course of arbitration, failure of which the case would be dismissed with costs.
 
Back
Top Bottom