Ufisadi tatizo kubwa kwa watawala afrika tukiamua unakwisha-rais paul kagame | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufisadi tatizo kubwa kwa watawala afrika tukiamua unakwisha-rais paul kagame

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Apr 28, 2011.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Waafrika habarini za saizi tena kwa mara nyingine tena twamshukuru mungu mwenyezi mjaza neema ndogondogo na kubwa nene na nyembamba fupi na ndefu kwa uhai wake kukupa nafasi tena kuwepo jamvini humu...yafuatayo ni mazungumzo ya mh rais wa rwanda paul kagame kuhusu ufisadi wa viongozi wetu baran afrika

  kwa mujibu wa shirika la transaparency international tawi la afrika masharki linasema rwanda ni nchi inayoongoza kwa mfano wa kuigwa katika mapambano dhidi ya ufisadi na rushwa ....ni ka ncho kadogo ambacho 1994 ilipata matatizo makubwa sana ya kukumbwa na mauwaji ya kimbari yaliyosababisha watu karibu milion moja na zaidi kufa ;kwa mujibu wa ripoti hiyo iitwayo teh east african bribery index 2010 linaonyesha nchi ya burundi kama mzizi unaoongoza kwa mlungula ktk ukand wa afrika mashariki.....ikiponzwa kwa mamlaka yake ya kukusanya kodi ambayo imeongoza kwa kudai rushwa ktk kundi la jumuia ya afrika mashariki

  burundi imechukua nafasi ya kenya kwa 36.7% na kufuatiwa na kenya 31.5% uganda 33% tanzania 28% na rwanda 6.6% kiwango kidogo sana kulinganisha na nchi jiran

  kwa nini kiwango cha rushwa rwanda kidogo??

  inaelezwa ni kutokana na sheria za serikali ya kagame kali za kupambana na vitendo vya rushwa miongoni mwa viongozi wake...kagame amekuwa mfano wa kuigwa kwa viongozi kwa nchi za kiafrika ambapo serikali imekuwa makini hasa katika kuwatumikiawananchi kwenye huduma za jamii baada ya kuharibiwa na vita

  rais kagame anakiri binafsi rushwa na ufisadi ni vita kali dhidi ya uongozi wa bara la afrika na ina garama kubwa sana kisiasa na ni hatari kwa usalama wa maisha ya viongozi wengi ktk nchi za afrika....akieleza sababu kubwa watu wanaohusika na ufisadi mkubwa wana mahusiano makubwa na maraisi wa afrika na hiyo ni sababu inayochangia vita kuwa ngumu

  kaamaa kiongozi mkuu ni lazima ifike sehemu ufanye maamuzi magumu kuwachukulia hatua za kisheria wenzako wanaojihusisha na ufisaadi ama rushwa ili uwe shujaa kwa wananchi wako na nchi yako kwa ujumla.. Au waendelee kushiriki vitendo hivyo ukiwa madarakani ili upate unafuu wa kisiasa na usishirikiane nao kwenye uongozi anasema rais kagame

  tangu niwe rais sijasikia mtu anasifia rushwa ama ufisadi lakini cha ajabu viongozi wa afirka wengi wanakabiliwa na ufisadi ama waoa ama marafiki waliokaribu nao na sijawahi kusikia hata siku moja mtu anawekwa ndani ama kulipa arama za uchafu aliofanya kutoka kwa viongozi wenzangu...na hili limewafanya hata mawaziri wa afrika sasa kujilimbikiza pesa kama awafi kesho na hivyo kusahau majukumu yao ni kuwatumikia wananchi

  rais kagame alitamka haya hivi majuzi wakati akiwa na viongozi wa eacyo a drc waliomtembelea kuhudhuria maazimisho ya miaka 17 ya mauwaji ya kimbari
  alisema pamoja na hatari iliopo ktk mapambano dhidi ya rushwa yeye kama kiongozi mkuu wa nchi ameamua kujitolea maisha yake kupambana na watu wote waliomdarakani wanaojishuugulisha na rushwa na kwamba hatokubali hata siku moja viongozi wake wajibufaishe kwa pesa za wananchi

  nasema siwezi kuwacha viongozi wajinufaishe kwa pesa za wanachi wangu ambao ni maskini hata siku moja...mimi siogopi kufa nimemwachia mungu maisha yangu na hili ndilo tatizo kubwa la viongozi wa afrika kuwaachia maisha yao watu wenye fedha zao alisema hon kagame
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Inashangaza kuona kila wakati afrika tunaomba msaada hadi ktk mambo madogo lakini wakati huo huo tuna rasilimali za kutosha hebu jiulize kwa nini tulishwe na fedha za walipa kodi wa nchi nyingine?? Na tutekeleze maendeleo yetu kwa garama za walipa kodi wa nje??

  Isitoshe hao wanaokupa misaada wanakupangia jinsi ya kuendesha mambo yenu ya ndani watakwambia sitaki hiki nataka hiki missada yenyewe shida tupu alisema hon kagame;hii si sawa lazima waafrika tubadilike tuachane na dhamana potofu hakuna aliezaliwa kwa ajili ya kuwa masikini alisema kagame

  hivi hadi usafi wa jiji unawaitaji wafadhali hii sio laana jamani haya n mambo yalio ndani ya uwezo wetu.....nilivyojua hilo niliwaambia wanyarwanda kwa hili hapan atuitaji wafadhili usafi wetu wenyewe tukaletewe magari ya taka na wachina wafinland wajapan hata kidogo.. Nikaweka ratiba ya usafi na kuwapa kazi kampuni za kusafisha miji ambazo mikataba nimesaini mwenye nikijua kuwaachia manispaa nitaleta mengine na leo hii mnaona matunda yake ama sivyo jamani........,akiwatoa nje na kuwapitisha kwenye barabara za kigali huku watu wakishangaa ...
   
 3. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #3
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  I like Kagame, i wish he would be the first presidend for the new EAC republic.......
   
 4. M

  Mugerezi JF-Expert Member

  #4
  Apr 28, 2011
  Joined: Mar 28, 2007
  Messages: 454
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Huyu rais japo naye alishiriki kwenye vita vilivyoleta mauaji lakini aliyoyafanya Rwanda niyakupigiwa mfano. Jamaa anastahili sifa.
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  maisha binafsi ya kagame:

  kuhusu maisha yangu binafsi yako kama biandamu wengine na kusema kuna mambo anayoyapenda kama michezo kusoma vitabu pamoja na kuwatembelea marafiki zake

  kwa bahati mbaya sijajaliwa kipaji cha kuimba kama kaka yangu museveni alietoa kibao cha you want another rap...lakini napenda kusikiliza muziki wakati wa mapumziko alisema hon kagame...

  wkati mwingine nahudhuria soka uwanja wa amahoro kama mtu wa kawaida na ninapofika pale jamaa zangu wanataka niende vip nisilipe kiingilio nawaambia naitaji risiti hela zangu na familia hizi..nawaambia nimekuja kama paul kagame na si rais kagame..basi naangalia na wenzangu kisha naondoka zangu alisema kagame
  pia ninapokuwa na nafasi na kwenda kuwatembelea marafiki zangu na jamaa zangu bila hata ya kuwapa taarifawanastukiaga napiga hodi wanashangaa basi nakaa nao naondoka in general napenda kuishi maisha ya kawaida najua nilipotoka sipendi kuumiza watu kama viongozi wengine.. Kwa hiyo hata nyinyi leo hii nimefurah sana kuwaona na nawahakikishia mkiniitajiwakati wote aijalishi ni shida gan tafadhali wasiliana na hizi namba utoshindwa kuniona ..unajua kuna viongozi wanaishi kama miungu mtu na hii si sawa hata mungu hapendi..tunaitaji kujua akuna aliezaliwa awe maskini ama tajiri so lazima tuishi kwa upendo na mwisho nawatakia kila la kheri vijana wenzangu watu wakaacheka hoi.....

  KUHUSU KUANZISHWA SHIRIKISHO LA AFRIKA MSHARIKI KAGAME ALISEMA KWA MTAZAMO WAKE ANGEPENDA KUANZISHWA HATA KESHO KWANI NDIO NJIA YA KUFIKSHA MAENDELEO YA HARAKA ..ALISEMA PAMOJA NA MTAZAMO WAKE HUO ANAITAJI KUSUBIRI HADI MAMBO YA MSINGI YATAKAPOPATIWA UFUMBUZIKABLA YA KUANZISHWA ALISEMA.. ANASEMA HATARI ILIOPO NI KUANZISHWA KWA SHIRIKISHO HILO BILA YA MAMBO YA MSINGI KUREKEBISHWA KWANZA KWANI KUKURUPUKA KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUMPA DOSI MGONJWA BILA KUFUATA VIPIMO VILIVYOPENDEKEZWA NA DAKTARI DOSI LAZIMA IMZURU MGONJWA....

  huyu ndio rais paul kagame wa rwanda hakika tungepata watu kama hawa wawili zaidi hili bara lingekuwa na adabu ya kuzaliwa...katika mambo muandishi anasema ameyafurahia ni kuwapa adabu wanaoiba serikalini.....akaelezwa kuna balozi aliiba ufaransa ajust small ammount wakapelekwa wakaguzi walipomfaxia data akaomba jamaa afunge vitu vyake aje na hao wakaguzi following day alipofika kigali aliishia kwenye karandinga na alikaa ndani miezi miwili alipoamua kufunguliwa mashtka na alikuwa mmoja wa marafiki wakubwa waliopigana nae ..

  ..............lingine alilofurahisha watu ni kitendo cha kurudisha magari yote y akifahari na kuwachukua viongozi wote kwenda kampuni ya toyota na kuwaambia mwenye kuchagua analotaka achague wakandikiana kukopeshwa na kupewa kiasi cha mafuta kadhaa kwa mwezi endapo umetumia yameisha unaambiwa kama anakuitaji safari zake utaweka mafuta kwa hela yako huyu ndie kagame...akiwaonyesha depo walipojaza hayo magari ambayo mengi amewagawia taasisi zinazosaidia watoto yatima na wanaoshugulika na mazingira rais kagame amesema mengine amepeleka kwenye balozi zake za karibu...waandishi walishangaa sana wakati wakiwa na mazungumzo baadhi ya mawaziri waliitwa wengine wakaingia na toyota korola wengine pickup za kubebea majani na kusema akika ifike wakati serikali ione uchungu wa hizi hela za wananchi wake....huku akisema sio kwamba sitaki kupanda shangingi la hasha hili million zaidi ya 100 kuna ndugu zangu awajui wanaamka wanaakuala wapi kwa nini nitumie gari ya anasa..imetosha viongozi wabadilike

  tunamtakia heri na fanaka mh kagame kwa kikosi kazi cha nguvu na mungu amsaidie labda watatokea watu kumuiga roho aliyonayo

  mungu ibariki afrika mungu ibariki rwanda na watu wake
   
 6. kichomiz

  kichomiz JF-Expert Member

  #6
  Apr 28, 2011
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 11,999
  Likes Received: 2,655
  Trophy Points: 280
  Kwa nini hakuzaliwa Tanzania?
   
 7. k

  kiloni JF-Expert Member

  #7
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 575
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  The first president of Eastern African Federation. He is worth it. He can fight the graft at large scale.
  My TZ president is DR WP SLAA.
  MY EA FEDERATION PRESIDENT PAUL KAGAME.
   
 8. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #8
  Apr 28, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,784
  Likes Received: 2,393
  Trophy Points: 280
  Mhhh kumbe hata ruangwa- LINDI kuna dhahabu?nimeona nipashe leo eti mtu mweupe anakuja kuichimba.naona watanzania tutahukumiwa na mungu kwa upendeleo maalumu mungu aliotubariki lakini tukawa wajinga wa kupindukia!
   
 9. M

  Marytina JF-Expert Member

  #9
  Apr 28, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Eti museveni alitaka kuwa rais wa kwanza wa east africa in case.

  Bora lisiwepo hilo EA IF NOT FOR KAGAME TO BE 1ST PREZDA

  bIG UP KAGAME
   
 10. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #10
  Apr 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  We acha tu, ukiwaza sana...unaanza kulia. Unyonge wetu na ujinga wetu umetumiwa na watawala walafisi/wabinafsi kujinufaisha "at the expenses of wananchi".Fikiria, nchi inaweza kulipa IPTL milioni 152 kwa siku kwa umeme ambao hata hivyo hauwatoshelezi watanzania wote milioni 52. Kwa kuwa hilo ni pato letu la ndani ni sawa na kupoteza wastani wa matumizi ya maendeleo ambayo nchi yaweza kumhudumia kila mtanzania kwa wastani wa tshs. 152/42=3.6milioni. kwa kila siku!!!!!!!!!!!!!! Leo unasema hatuna madawa? hatuwezi kutoa elimu bure ?? hatuwezi wasomesha watoto wetu chuo kikuu?? hatuna barabara?? Hatuwezi kulipa mishahara mizuri wafanya kazi wetu? Eti hatuna fedha!!!!!!!! Na hizi milioni 152 kila siku zinatoka wapi?? Huo ni ufisadi mradi mmoja tu!!!!!!!!!!!!!! Je, maeneo mengine?? Can you imagine jinsi watanzania na mali zao/mapato ya nchi ya ndani yamegeuzwa SHAMBA LA BIBI. Inauma sana, kila mtu akae imila na kwa pamoja tuchue hatua ya kufanya mageuzi ya ki makusudi.
   
 11. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #11
  Apr 28, 2011
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,441
  Likes Received: 5,693
  Trophy Points: 280
  Tuombe immigration wamfwatilie yawezekana alizaliwa kigoma tukapata bahati
   
Loading...