Ufisadi: Samaki huoza kuanzia kichwani

Ufisadi: Samaki huoza kuanzia kichwani

DoubleOSeven

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2008
Posts
661
Reaction score
145
Mojawapo ya kamba walizofungwa jirani zetu wa Kenya katika kampeni za uchaguzi mkuu uliompa Uhuru kiti cha urais ni pamoja na wapiga kura kuaminishwa ati wamchague Rais mwenye mihela yake ili nchi iondokane na tatizo la ufisadi uliokithiri.

Kinyume na matarajio yao, tatizo la ufisadi limebaki mtambuka. Kwa hiyo pamoja na mihela ile ya Mkulu, ufisadi umeendelea kubisha hodi hadi mlangoni kwake. Uozo umeanzia huko. Kibaya zaidi ni pale status-quo ya "corruption with impunity" inavyodumishwa. Watuhumiwa wanabadilishiwa lebo za ofisi. Leo huku kesho kule bila kuchukuliwa hatua stahiki.

Picha hii inajirudia katika nchi nyingi. Matokeo ya udhaifu huu ni dhahiri na imefikia pale watawala wanapofananishwa na Wakoloni. Kwa Afrika yetu tunao wakoloni weusi kwa vile wale wengine walikuwa Wazungu. Wale tunaowanyooshea vidole kama chanzo cha matatizo yanayolikumba bara la Africa hata leo hii, miaka 50 baadae.

Hapa kwetu, watuhumiwa mbalimbali wa kansa hii ya ufisadi wamejipanga kuwania utawala wa nchi yetu. Kama kwa jirani zetu, wanataka watuaminishe wao ni MATAJIRI, wanayo mihela yao na kwa hiyo aidha wamevimbiwa nazo au pia watatusaidia nasi tusionazo tuwe matajiri. Ati umasikini ni kitu kibaya sana. Ya kwamba ukimpa maskini uongozi atageuka kuwa fisadi na kwa hiyo hafai!
Hatuhitaji kuangalia mbali. Pale kwa jirani, uozo umeanzia kichwani. Matokeo yake mnayaona. Tusidanganyike!
 
Hata kama wakenya wanakabiliwa na hayo ya ufisadi lkn wako njema kuliko Tanzania...wanajitambua sana!
 
Sijakuelewa vizuri hii mada inahusu Katiba au Siasa??isije ikawa nimekosea mwenyewe kuingia hapa maana nimeona pameandikwa Jukwaa la Katiba afu nikafuangua kusoma nikaona ni mchuano wa urais na mihela duuu kweli tunatofautiana uelewa sijui wenzangu!!!

Ushauri mada yako peleka jukwaa la siasa!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom