Ufisadi NHIF

Anonymous

Senior Member
Feb 3, 2006
125
316
Tunaandika tukitambua kwa kufanya hivi tunahatarisha ajira zetu, lakini tunasukuma tukiamini kuwa ustawi wa taifa unatangulia mbele ya ajiri zetu. Sisi ni wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(National Health Insurance Fund-NHIF) tunachukua hatua hii baada ya kuwa tumepoteza imani na watendaji wakuu wa wizara ya Afya, Bodi inayosimamia Mfuko, Uongozi wa Juu Mfuko chini ya Mkurugenzi Bwana Emmanuel Dotto Bundala Humba ambao ndie kiini na mhimili wa ufisadi katika mfuko.

Baada ya kuwa tumejitahidi kuwasalisha hoja zetu kwa kufuata mikondo inayoeleweka pasipo hatua zozote kuchukuliwa tunalazimika leo kuwasilisha kwenu tukitambua juhudi zenu adhimu na za kizalendo katika kulisafisha taifa dhidi ya makucha yetu. Kwa msukumo huo tunawasilisha rasmi hoja zetu kwa viongozi wa CHADEMA kama taasisi pekee yenye dhamira sahihi katika kulisafisha taifa(hapa tunatambua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndio mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kusimamia mahesabu ya Mashirika ya umma) pamoja na magezeti ya Mwanahalisi na Tanzania Daima ambayo kwa mtazamo wetu ndio magazeti pekee yenye ujasiri wa kutosha katika kuanika uozo katika jamii na taasisi za umma. Pia Tovoti ya Jambo Forum ambayo inaendelea kutoa mchango mkubwa kwa taifa katika vita dhidi ya ufisadi na ujenzi wa demokrasia nchini. Tunatanguliza shukran zetu kwa hatua mtakazo zichukua katika hili.

1. Mgongano wa Kimaslahi na "Hongo" kwa viongozi wa Bodi na Wizara ya Afya
Bwana Humba ni mjanja na mwepesi katika kuweka mitego kwa viongozi wanaopaswa kusimamia utendaji wake. Uongozi wa Bodi uliopita uliwahi kupokea malalamiko ya wafanyakazi juu ya "ukatili" na Minenendo mibaya ya bwana Humba. Bodi iliamua kuunda tume ya uchunguzi chini ya mwenyekiti wa bodi wakati huo Professa Msimbichaka na Makamu wake ndugu Rutazamba.

Kamati hii iliibua matumaini kwa wagfanyakazi wakijua hatimae kilio chao kitasikika. Ghafla bwana Humba aliamua kuambatana na Mwenyekiti wa Bodi kwenda china kuhudhuria mkutano. Waliporudi kamati ya uchunguzi ilikufa na Bwana Humba akanza kutoa vitisho kwa wafanyakazi kwamba alipokuwa China alielezwa na mwenyekiti wa Bodi(Professa Msimbichaka) kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi akiwaondoa "atafanikiwa" sana katika shughuli zake.

Pia aliendeleza tabia ya kutoa upendeleo kwa mwenyekiti wa bodi katka kuhakikisha yote anayopanga yanapitishwa na bodi. Kuna kipindi alilazimisha mfuko kulipa gharama za matibabu ya ndugu wa mwenyekiti wa bodi iliyomaliza mda wake(Professa Msimbichaka) aliekuwa ametibiwa katika hospitali ya St. Bernard iliyopo Kariakoo ihali tayari mkataba ulikuwa umevunjwa baina ya mfuko na hospitali hiyo. "Upendeleo" wa aina hii hudhoofisha sana uwezo wa kiutendaji wa bodi.

Bwana Humba amendeleza utamaduni mbaya wa "kununua" viongozi wa Bodi na tayari mwenyekiti mpya wa bodi amaenasa katika mtego kwani binti yake ameajiriwa katika mfuko huu jambo ambalo linadhibiti uwezo wake wa kusimamia utendaji wa mkurugenzi na wa shirika kwa maana anajaribu kulinda fadhila aliyopewa kwa mtoto wake kupewa ajira.

Kama vile haitoshi mtoto wa kaka yake na katibu wa wizara ya afya nae ameajiriwa katika mfuko huu. Itakumbukwa kuwa katibu mkuu wa afya kwa wadhifa wake alikuwa ni mjumbe mwenye ushwawishi mkubwa katika bodi ya mfuko wa bima ya afya. Kwa sasa mjumbe wa bodi toka wizara ya afya ni mkurugenzi wa mipnago wa wizara hiyo ambae kimlaka yupo chini ya katibu mkuu wa widhara na baadhi ya mikutano katibu huudhuria, hali hii inamuhakikishiwa "ulinzi" bwana Humba katika wizara ya afya.

2.Kupindisha taratibu maksudi kwa maslahi Binafsi​

Mara nyingi bwana Humba amekuwa akikataa kuudhinisha malipo kwa wafanyakazi pale wanapokuwa wamepata matibabu katika vituo vya afya ua hopsitali ambazo hazijasaliwa na mfuko kwa maelezo kuwa ni nje ya utaratibu. Jambo la kushangaza ni kuwa mara mke wa wa Mkurugenzi alipopata matitizo ya mguu, alilazwa MOI(kitengo cha mifupa Muhimbili) wakati ambapo MOI hajaingia mkataba na Mfuko. Mfuko ulilipa kiasi kikubwa cha fedha kugharamia matibabu ya mke wa mkurugenzi.

Cha ajabu zaidi ni kuwa hivi majuzi mke wa mkurugenzi alipelekwa India kwa ajili ya matibabu na kugharamiwa na Mfuko. Safari hii iligharimu Mfuko kiasi cha shilingi 25,764,000. Itakumbukwa kuwa Mfuko haujaanza kugharamia matibabu nje ya nchi, mkurugenzi kwa kujitetea alisema kwamba ampewa kibali na wizara ya afya!

Cha kujiuliza ni wanachama wangapi wa mfuko wanapata fadhila hizi? Ikubukwe kuwa sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko na wanchangiaji wakubwa ni walimu je wao wanaweza kupelekwa nje kwa matibabu? Cha kusikitisha ni kuwa haya yanatokea wakati ambapo raisi wa chama cha walimu ni mjumbe wa bodi.

Pia katika maonyesho ya sabasaba jumla ya shilingi 23,033,000 zilitoweka, yani haizkutolea maelezo yoyote katika ripoti. "Uwizi" huu ulifanyika chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Sabasaba Bwana Raphael Mwamoto. Rafiki mkubwa wa Mkurugenzi. Uwizi huu ulibainishwa na mkaguzi wa ndani lakini habari zilipofikishwa kwa mkurugenzi hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Utendaji wa bwana Mwamoto ni wa kutilia shaka tangu alipoajiriwa katika mazingira ya kutatanisha. Hakuweza kufaulu katika kipindi cha majaribio(Propabation) lakini katika hali ya kustaabisha mkurugenzi aliaamua kumbadilisha idara. Bwana Mwamoto alikuwa mwalimu katika chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM) kabla ya kuletwa na mkurugenzi katika mfuko wa bima ya afya, inasemekana hajaacha rekodi nzuri IFM. Mara nyingi wafanyakazi wanapojaribu kumchunguza na kumuwajibishwa hutishiwa kwa maelezo kuwa yeye ni afisa wa usalama wa taifa!

3.Ufujaji wa fedha​

Kiasi kikubwa cha fedha huwa kinapotea katika miradi mbalimbali ya shirika. Uwizi mkubwa upo katika kununua mfumo wa PREMIA ambao ulipaswa kubuniwa katika kusaidia uharakishaji wa malipo ya madai. Mfumo huu ulinunuliwa India. katika mkataba ulionekana utagharimu dola za kimerekani laki nne(400,000), hii ilikuwa mwaka 2005. Lakini cha kushangaza zimetumika zaidi ya shilingi milioni 700 katika manunuzi na mpaka leo mfumo huu(sytem) bado haujaanza kufanya kazi mpaka sasa. Ukipita katika ofisi za kanda utakuta wanatumia mfumo wa kawaida kulipa mahospitali.

Gharama za jumla za kuleta mfumo huu hewa zinazidi Bilioni moja ukujumlisha gharama za maandalizi, kuzunguka mikoani kutoa elimu kwa watoa huduma, matangazo katika vyombo vya habari na uzinduzi uliofanywa kwa kishindo kwa kuwakaribisha viongozi kutoka wizara ya Afya.

Cha kujiulizwa ni kwanini bodi inashindwa kuwawajibisha viongozi wa shirika kwa hasara kubwa kama hii? Uwizi huu unatokea ihali kuna malamiko makubwa toka kwa wanachama juu ya huduma mbaya za Mfuko. Hii ni sehemu ndogo tu ya ufisadi katika Mfuko wa bima ya Afya. Uchunguzi toka taasisi huru unaeweza kuibua mengi sana katika maeneo ya fedha, ukiukwaji wa taratibu na ajira holela zizizofuata taratibu za ajira.

4. Huduma Mbovu za Mfuko​

Uongozi wa sasa wa Mfuko umeshindwa kabisa kubuni mikakati ya kuimarisha huduma kwa wateja wake. Mfano sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko huu ni walimu, wanapokwenda katika mahospitali au vituo vya afya katika maeneo yao na kukosa dawa, hulazimika kutumia fedha zao kununua dawa na Mfuko hukataa kuwafidia ghrama za mananuzi ya dawa ihali kila mwezi hukatwa katika mishahara yao kwa ajili ya mfuko. Haya yanatokea wakati Mfuko umekuwa mwepesi katika kutoa michango mikubwa katika shughulizi za hisani kama michezo!

Pia Kuna usumbufu mkubwa sana katika kutengeneza vitambulisho vya wanachama. Uongozi wa Humba hujitetea kuwa wao bado ni wachanga, yaani ni miaka saba ya uchanga! Itachukua miaka mingapi kwa Mfuko huu kukua chini ya uongozi wa Mfuko huu?

Katika hali ya kukosa mwelekeo ya kiongozi Mkurugenzi amaahaidi kujenga Hospitali Dodoma na Dar es salaam kwa kile anachokiita "centre of execelence". Pia Mfuko umetoa shilingi milioni 225 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya amana na mwananyamala! Hizi "centre of execelence" wanamjengea nani wakati wanachama wa Mfuko wako vijijini? Haya yanatokea wakati Raisi wa chama cha Walimu(CWT) bwana Mukoba na mwakilishi wa wafanyakazi wa serekali (TUGHE) bwana kiwenge ni wakumbe wa bodi! Ni kwanini wanashindwa kutetea maslahi ya wale wanaowawakilisha? Wanapumbambazwa na nini?

Kuna hitaji la lazima kuchukua hatua za haraka katika kuunusuru mfuku muhimu katika ustwi wa wafanyakazi. Tutaendelea kuwataarifu zaidi juu ya ufisadi unaoendelea katika taasisi hii muhimu katika ustawi wa wananchi hasa wenye kioato kidigo.

5.Dharau na Mienendo isiyokubalika katika jamii​

Mkurugenzi mkuu wa bima ya Afya moja ya Taasisi nyeti sana nchini ni mtu mwenye tabia ya majigambo, vitisho na dharahau. Mwenendo wake huu amewahi kuudhihirisha nje ya ofisi na kuupa fursa umma kutambua tabia halisi ya kiongozi mkuu wa shirika muhimu katika taifa. Itakumbukwa amewahi kumtukana na kumnyanyapaa nesi mmoja wa hospitali ya Hindu mandal(sasa marehemu) aliekuwa muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Alifanya hivyo baada ya kuwa amekataliwa kupewa huduma kupitia mfuko wa bima ya afya kwa kuwa hakwenda na kitambulisho chake. Huu ni utaratibu wa kawaida katika uendeshaji wa mfuko.

Marehemu kwa kutambua muongozo na taratibu za mfuko alimkatalia mkurugenzi kwa kuwa alikuwa amekiuka utaratibu, mkurugenzi alijaribu kumtisha kwa kutumia wadhifa wake na kwamba atahakikisha anafukuzwa kazi, baada ya marehemu kuwa na msimamo pamoja na vitisho vya mkurugezi ndipo bwana Humba alipoanza kutukana matusi na kumskashifu marehemu kutokana na hali yale ya kiafya hali iliyopelekea marehemu kupata shinikizo liliochukua maisha yake masaa machache badae. Habari hii iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini ghafla ikapotea katika namna ya kushangaza. Upo uwezekano alihonga ndungu wa marehemu na baadhi ya vyombo vya habari ili kudhibiti taarifa zaidi kutoka na pengine kuchukuliwa hatua za kisheria. Kadhia kama hizi sehemu ya kazi kwa wafanyakazi wa NHIF. Hatuamini kama hizi ni tabia stahili kwa mtu mwenye dhamana ya kuongoza shirika la bima ya Afya nchini.
 
nakumbuka hizi ishu za ulaji NHIF, POWER BREAKFAST clouds fm walizipigia kelele sana wale watoto.
 
Umenigusa sana mtu wa NHIF kwa mada hii, huu mfuko umetunyanyasa sana. Tulilalamika sana na hakuna aliyetusikia, hadi wengine tukaacha kazi huko, sasa hivi tunajitegemea kivingine. Nawasifu NSSF kwa kuja na mpango wao wa bima ya Afya, lakini bado kwa bahati mbaya sana haiwasaidii waalimu walioajiriwa na serikali kuchagua kati ya NHIF na hiyo SHIB itolewayo na NSSF. Suluhisho mojawapo lingekuwa kwa serikali kuruhusu makampuni mengi ya bima kutoa huduma hii, na kumruhusu mfanyakazi kuchagua kampuni anayotaka. Hali ya sasa hivi ni ufisadi na uzandiki mtupu, maana ukishaajiriwa na serikali unakatwa mchango wa bima ya afya bila hiari yako. Na bora mtu angekatwa basi hiyo hela japo kwa lazima lakini akafaidika! Watu wanazidi kunyanyasika, hela anakatwa kila mwezi na bado huduma ni mbovu sana.
 
Mkuu wa NHIF,

Heshima mbele kaka, umekuja JF kwenye the right place mkuu, tena kwa bahati njema ya Mungu, hapa niko na kiongozi mmoja mzito sana wa sasa wa serikali yetu, kwa hiyo nimei-print na kumkabidhi hii article yako kama ilivyo,
majibu yanakuja!

Ahsante Mkuu!
 
Ngoja tuombe wakuu waiweke hii kwenye Sticky maana naona kuna vichwa vitauma wiki hii... hivi kuna kitu chochote tunachoweza kukifanya vizuri, kwa ubora, na kwa wakati muafaka?
 
Hakuna Mkuu Hapa Mi Hata Sijui Mbona Watu Kila Wanapoweka Wanaaribu,,,nini Tatizo Inawezekana Wana Mapepo Hawa Aiwezekani Kila Sehemu Ttcl ,,,atcl,,,,huku Tena...haya Mod Usiitoe Hii Watu Waone Pesa Zao Zinavyoliwa....
 
mtu analeta mchezo kwenye sehemu muhimu kama Afya!
tukitaka kuondoa huu uoza uliopo, itabidi kwanza tuhakikishe viongozi wa serikali kuu na mashirika yote ya umma, wanatolewa. ...na tunaanza upya!
 
to be honest wala sijui nani alileta hili zimwi la bima ya afya, na kwa nini watu wan'gang'anizwe kutibiwa bima ya afya? mabavu, mabavu yasiyo na msingi? wanakatwa pesa nyingi na hata panadol hupati. Kamshahara kenyewe hako ka serikali halafu unaendelea kuslash na mabima ya God Knows what.
Ah inatia hasira.
 
Hivi ni nani ametuloga siye watanzania,Huyu Mzee hata mie nilianza kuata wasiwasi naye kuhusu utendaji wake,Niliwahi kukutaa naye wakati akiagiza gari lake La Range Rover aina ya vogue..

Nikamuuliza wewe unafanya kazi wapi aaniambia yuko Bima ya Afya.Baada ya kufatilia kwa ukaribu nikagundua siyo kwamba ana aari moja tu la kifahari.

ana VX na utitiri wa magari,sasa Hizi pesa amezipataje??Serikali yangu inalipa mshahara na psho kubwa kiasi hicho.Nasikia kuna mtoto wa Mramba pi pale naye ni FISADI mkuu.Wakati tukifikiria kuhusu hatua zipi zichukuliwe kuhusu BIMA ya afya.

Tusilifute shirika hili sababu watanzania wengi watapoteza ajira.la msingi ni kung'oa watu wote wa ovyo na kuhakiksha kuna viongozi wanaolinda maslahi ya taifa na kuwajari wafanyakazi.hivi hawa watu wanaoitwa watu wa Usalama kazi yao ni nini hasa??kufanya ufisadi na kulindwa??No way..We need soe changes here.Naomba kuunga hoja Mkurugenzi huyu afukuzwe kazi ili apishe uchunguzi na akipatikana na hati aungiliwe mbali.
 
Ufisadi uko kila shirika la serikali. Tunashukuru kwamba siku hizi watanzania wameamka wanaanika wazi ufisadi. Sasa ni kwenda mbele tu. Mafisadi watakosa pa kujificha. Mambo yao yote hadharani!!!
 
mimi nafikiri kwanza kabisa tuishukuru JF.hapa ndipo kimbilio la wanyonge wanapokuja kupaza sauti zao mbele ya umma wa watanzania.Haya mambo yalikuwepo toka enzi na enzi ila ilikuwa ni vigumu kwa watu kuyazungumza kinagaubaga kwa bahati nzuri muda umefika tutaona mengi na kusikia mengi.tatizo lilikuwa ni wakati na sasa si tatizo tena,huu ni wakati wa kupata moja baada ya jingine ndio maana watu wapo hapa kila siku bila kukosekana wa habari moto moto
 
Tanzania hakuna sehemu iliyosafi hata moja kila sehemu imeoza na inashindana na nyingine kwa uozo, ndo maana tunahitaji kiongozi ambaye hatajari sentiment za watu kwani ataumiza wengi sana wakiwemo ndugu zake.
 
Hii sasa kali yaani huyu HUmba kiboko....analeta mchezo kwenye afyaa.naomba MMJ pamoja na F.MARSHAL na member wote wa JF mmeliona hili tulishughulikie kabla halijawa sugu....atapandikiza vifisadi vidogo vitakavyo mrithi.
 
Mie nitatafuta business Card yake na nitawapa Namba yake Mmpigie
 
NHIF Staff,

Tunashukuru kwa taarifa. Ni Watanzania wachache ambao watakuwa wamefanikiwa kupata nafasi ya kusoma makala haya hasa ukichukulia level ya Teknolojia ya nchi yetu.

Na huu mfuko, kwa asilimia kubwa nadhani umelenga Watanzania wafanyakazi wa serikali wenye kipato cha kawaida ambao zaidi ya asilia 90% hawana "access" na mtandao.

Niliukuwa natoa wito kwa vyombo husika (Makamanda wa Chama Mbadala, Mwanahalisi, Mtanzania Daima) wafanye uchunguzi wa kina kupata undani wa hili jambo na baada ya hapo waliweke wazi ili kila Mtanzania ajue ni jinsi gani tunavyoishi kunufaisha wachache.

"Ni sauti zetu ambazo zitatukomboa katika hili Janga"
 
3.Ufujaji wa fedha
Kiasi kikubwa cha fedha huwa kinapotea katika miradi mbalimbali ya shirika. Uwizi mkubwa upo katika kununua mfumo wa PREMIA ambao ulipaswa kubuniwa katika kusaidia uharakishaji wa malipo ya madai. Mfumo huu ulinunuliwa India. katika mkataba ulionekana utagharimu dola za kimerekani laki nne(400,000), hii ilikuwa mwaka 2005. Lakini cha kushangaza zimetumika zaidi ya shilingi milioni 700 katika manunuzi na mpaka leo mfumo huu(sytem) bado haujaanza kufanya kazi mpaka sasa. Ukipita katika ofisi za kanda utakuta wanatumia mfumo wa kawaida kulipa mahospitali.

Bw Emanuel Humba akiwa kwenye kikao kule Zambia mwaka 2005, August alitoa paper kuhusu NHIF, na nukuu kama ifuatavyo:

"Computerization
The Fund has managed to computerize most of its functions including linking its head office with zones under a wide area network (WAN). This move relieved the Fund from carrying out its duties manually. In 2004-2005 the Fund managed to procure software for claims management and accounting system (PREMIA) to hasten claims processing and to detect the incidence of fraud."

Mara baada ya paper, nilikuwa very surprised na mfumo wao wa computer!! Maana nilikuwa nafahamu mazingira ya nyumbani (yaani computerization in Govt institution!!) Sasa leo hii 2008, kumbe bado NHIF wanatumia makaratasi kuprocess malipo kwenye ofisi zao za Kanda!! yaani ina maana Bw Humba alikuwa anapiga "kamba" kule Zambia?!!!
 
Tunaandika tukitambua kwa kufanya hivi tunahatarisha ajira zetu, lakini tunasukuma tukiamini kuwa ustawi wa taifa unatangulia mbele ya ajiri zetu. Sisi ni wafanyakazi wa Mfuko wa Bima ya Afya(National Health Insurance Fund-NHIF) tunachukua hatua hii baada ya kuwa tumepoteza imani na watendaji wakuu wa wizara ya Afya, Bodi inayosimamia Mfuko, Uongozi wa Juu Mfuko chini ya Mkurugenzi Bwana Emmanuel Dotto Bundala Humba ambao ndie kiini na mhimili wa ufisadi katika mfuko.

Baada ya kuwa tumejitahidi kuwasalisha hoja zetu kwa kufuata mikondo inayoeleweka pasipo hatua zozote kuchukuliwa tunalazimika leo kuwasilisha kwenu tukitambua juhudi zenu adhimu na za kizalendo katika kulisafisha taifa dhidi ya makucha yetu. Kwa msukumo huo tunawasilisha rasmi hoja zetu kwa viongozi wa CHADEMA kama taasisi pekee yenye dhamira sahihi katika kulisafisha taifa(hapa tunatambua kuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA ndio mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya kusimamia mahesabu ya Mashirika ya umma) pamoja na magezeti ya Mwanahalisi na Tanzania Daima ambayo kwa mtazamo wetu ndio magazeti pekee yenye ujasiri wa kutosha katika kuanika uozo katika jamii na taasisi za umma. Pia Tovoti ya Jambo Forum ambayo inaendelea kutoa mchango mkubwa kwa taifa katika vita dhidi ya ufisadi na ujenzi wa demokrasia nchini. Tunatanguliza shukran zetu kwa hatua mtakazo zichukua katika hili.

1. Mgongano wa Kimaslahi na “Hongo” kwa viongozi wa Bodi na Wizara ya Afya
Bwana Humba ni mjanja na mwepesi katika kuweka mitego kwa viongozi wanaopaswa kusimamia utendaji wake. Uongozi wa Bodi uliopita uliwahi kupokea malalamiko ya wafanyakazi juu ya “ukatili” na Minenendo mibaya ya bwana Humba. Bodi iliamua kuunda tume ya uchunguzi chini ya mwenyekiti wa bodi wakati huo Professa Msimbichaka na Makamu wake ndugu Rutazamba.

Kamati hii iliibua matumaini kwa wagfanyakazi wakijua hatimae kilio chao kitasikika. Ghafla bwana Humba aliamua kuambatana na Mwenyekiti wa Bodi kwenda china kuhudhuria mkutano. Waliporudi kamati ya uchunguzi ilikufa na Bwana Humba akanza kutoa vitisho kwa wafanyakazi kwamba alipokuwa China alielezwa na mwenyekiti wa Bodi(Professa Msimbichaka) kuwa kuna baadhi ya wafanyakazi akiwaondoa “atafanikiwa” sana katika shughuli zake.

Pia aliendeleza tabia ya kutoa upendeleo kwa mwenyekiti wa bodi katka kuhakikisha yote anayopanga yanapitishwa na bodi. Kuna kipindi alilazimisha mfuko kulipa gharama za matibabu ya ndugu wa mwenyekiti wa bodi iliyomaliza mda wake(Professa Msimbichaka) aliekuwa ametibiwa katika hospitali ya St. Bernard iliyopo Kariakoo ihali tayari mkataba ulikuwa umevunjwa baina ya mfuko na hospitali hiyo. “Upendeleo” wa aina hii hudhoofisha sana uwezo wa kiutendaji wa bodi.

Bwana Humba amendeleza utamaduni mbaya wa “kununua” viongozi wa Bodi na tayari mwenyekiti mpya wa bodi amaenasa katika mtego kwani binti yake ameajiriwa katika mfuko huu jambo ambalo linadhibiti uwezo wake wa kusimamia utendaji wa mkurugenzi na wa shirika kwa maana anajaribu kulinda fadhila aliyopewa kwa mtoto wake kupewa ajira.

Kama vile haitoshi mtoto wa kaka yake na katibu wa wizara ya afya nae ameajiriwa katika mfuko huu. Itakumbukwa kuwa katibu mkuu wa afya kwa wadhifa wake alikuwa ni mjumbe mwenye ushwawishi mkubwa katika bodi ya mfuko wa bima ya afya. Kwa sasa mjumbe wa bodi toka wizara ya afya ni mkurugenzi wa mipnago wa wizara hiyo ambae kimlaka yupo chini ya katibu mkuu wa widhara na baadhi ya mikutano katibu huudhuria, hali hii inamuhakikishiwa “ulinzi” bwana Humba katika wizara ya afya.

2.Kupindisha taratibu maksudi kwa maslahi Binafsi​

Mara nyingi bwana Humba amekuwa akikataa kuudhinisha malipo kwa wafanyakazi pale wanapokuwa wamepata matibabu katika vituo vya afya ua hopsitali ambazo hazijasaliwa na mfuko kwa maelezo kuwa ni nje ya utaratibu. Jambo la kushangaza ni kuwa mara mke wa wa Mkurugenzi alipopata matitizo ya mguu, alilazwa MOI(kitengo cha mifupa Muhimbili) wakati ambapo MOI hajaingia mkataba na Mfuko. Mfuko ulilipa kiasi kikubwa cha fedha kugharamia matibabu ya mke wa mkurugenzi.

Cha ajabu zaidi ni kuwa hivi majuzi mke wa mkurugenzi alipelekwa India kwa ajili ya matibabu na kugharamiwa na Mfuko. Safari hii iligharimu Mfuko kiasi cha shilingi 25,764,000. Itakumbukwa kuwa Mfuko haujaanza kugharamia matibabu nje ya nchi, mkurugenzi kwa kujitetea alisema kwamba ampewa kibali na wizara ya afya!

Cha kujiuliza ni wanachama wangapi wa mfuko wanapata fadhila hizi? Ikubukwe kuwa sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko na wanchangiaji wakubwa ni walimu je wao wanaweza kupelekwa nje kwa matibabu? Cha kusikitisha ni kuwa haya yanatokea wakati ambapo raisi wa chama cha walimu ni mjumbe wa bodi.

Pia katika maonyesho ya sabasaba jumla ya shilingi 23,033,000 zilitoweka, yani haizkutolea maelezo yoyote katika ripoti. “Uwizi” huu ulifanyika chini ya usimamizi wa Mwenyekiti wa Sabasaba Bwana Raphael Mwamoto. Rafiki mkubwa wa Mkurugenzi. Uwizi huu ulibainishwa na mkaguzi wa ndani lakini habari zilipofikishwa kwa mkurugenzi hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.
Utendaji wa bwana Mwamoto ni wa kutilia shaka tangu alipoajiriwa katika mazingira ya kutatanisha. Hakuweza kufaulu katika kipindi cha majaribio(Propabation) lakini katika hali ya kustaabisha mkurugenzi aliaamua kumbadilisha idara. Bwana Mwamoto alikuwa mwalimu katika chuo cha usimamizi wa Fedha(IFM) kabla ya kuletwa na mkurugenzi katika mfuko wa bima ya afya, inasemekana hajaacha rekodi nzuri IFM. Mara nyingi wafanyakazi wanapojaribu kumchunguza na kumuwajibishwa hutishiwa kwa maelezo kuwa yeye ni afisa wa usalama wa taifa!

3.Ufujaji wa fedha​

Kiasi kikubwa cha fedha huwa kinapotea katika miradi mbalimbali ya shirika. Uwizi mkubwa upo katika kununua mfumo wa PREMIA ambao ulipaswa kubuniwa katika kusaidia uharakishaji wa malipo ya madai. Mfumo huu ulinunuliwa India. katika mkataba ulionekana utagharimu dola za kimerekani laki nne(400,000), hii ilikuwa mwaka 2005. Lakini cha kushangaza zimetumika zaidi ya shilingi milioni 700 katika manunuzi na mpaka leo mfumo huu(sytem) bado haujaanza kufanya kazi mpaka sasa. Ukipita katika ofisi za kanda utakuta wanatumia mfumo wa kawaida kulipa mahospitali.

Gharama za jumla za kuleta mfumo huu hewa zinazidi Bilioni moja ukujumlisha gharama za maandalizi, kuzunguka mikoani kutoa elimu kwa watoa huduma, matangazo katika vyombo vya habari na uzinduzi uliofanywa kwa kishindo kwa kuwakaribisha viongozi kutoka wizara ya Afya.

Cha kujiulizwa ni kwanini bodi inashindwa kuwawajibisha viongozi wa shirika kwa hasara kubwa kama hii? Uwizi huu unatokea ihali kuna malamiko makubwa toka kwa wanachama juu ya huduma mbaya za Mfuko. Hii ni sehemu ndogo tu ya ufisadi katika Mfuko wa bima ya Afya. Uchunguzi toka taasisi huru unaeweza kuibua mengi sana katika maeneo ya fedha, ukiukwaji wa taratibu na ajira holela zizizofuata taratibu za ajira.

4. Huduma Mbovu za Mfuko​

Uongozi wa sasa wa Mfuko umeshindwa kabisa kubuni mikakati ya kuimarisha huduma kwa wateja wake. Mfano sehemu kubwa ya wanachama wa mfuko huu ni walimu, wanapokwenda katika mahospitali au vituo vya afya katika maeneo yao na kukosa dawa, hulazimika kutumia fedha zao kununua dawa na Mfuko hukataa kuwafidia ghrama za mananuzi ya dawa ihali kila mwezi hukatwa katika mishahara yao kwa ajili ya mfuko. Haya yanatokea wakati Mfuko umekuwa mwepesi katika kutoa michango mikubwa katika shughulizi za hisani kama michezo!

Pia Kuna usumbufu mkubwa sana katika kutengeneza vitambulisho vya wanachama. Uongozi wa Humba hujitetea kuwa wao bado ni wachanga, yaani ni miaka saba ya uchanga! Itachukua miaka mingapi kwa Mfuko huu kukua chini ya uongozi wa Mfuko huu?

Katika hali ya kukosa mwelekeo ya kiongozi Mkurugenzi amaahaidi kujenga Hospitali Dodoma na Dar es salaam kwa kile anachokiita “centre of execelence”. Pia Mfuko umetoa shilingi milioni 225 kwa ajili ya ukarabati wa hospitali ya amana na mwananyamala! Hizi “centre of execelence” wanamjengea nani wakati wanachama wa Mfuko wako vijijini? Haya yanatokea wakati Raisi wa chama cha Walimu(CWT) bwana Mukoba na mwakilishi wa wafanyakazi wa serekali (TUGHE) bwana kiwenge ni wakumbe wa bodi! Ni kwanini wanashindwa kutetea maslahi ya wale wanaowawakilisha? Wanapumbambazwa na nini?

Kuna hitaji la lazima kuchukua hatua za haraka katika kuunusuru mfuku muhimu katika ustwi wa wafanyakazi. Tutaendelea kuwataarifu zaidi juu ya ufisadi unaoendelea katika taasisi hii muhimu katika ustawi wa wananchi hasa wenye kioato kidigo.

5.Dharau na Mienendo isiyokubalika katika jamii​

Mkurugenzi mkuu wa bima ya Afya moja ya Taasisi nyeti sana nchini ni mtu mwenye tabia ya majigambo, vitisho na dharahau. Mwenendo wake huu amewahi kuudhihirisha nje ya ofisi na kuupa fursa umma kutambua tabia halisi ya kiongozi mkuu wa shirika muhimu katika taifa. Itakumbukwa amewahi kumtukana na kumnyanyapaa nesi mmoja wa hospitali ya Hindu mandal(sasa marehemu) aliekuwa muathirika wa ugonjwa wa UKIMWI. Alifanya hivyo baada ya kuwa amekataliwa kupewa huduma kupitia mfuko wa bima ya afya kwa kuwa hakwenda na kitambulisho chake. Huu ni utaratibu wa kawaida katika uendeshaji wa mfuko.

Marehemu kwa kutambua muongozo na taratibu za mfuko alimkatalia mkurugenzi kwa kuwa alikuwa amekiuka utaratibu, mkurugenzi alijaribu kumtisha kwa kutumia wadhifa wake na kwamba atahakikisha anafukuzwa kazi, baada ya marehemu kuwa na msimamo pamoja na vitisho vya mkurugezi ndipo bwana Humba alipoanza kutukana matusi na kumskashifu marehemu kutokana na hali yale ya kiafya hali iliyopelekea marehemu kupata shinikizo liliochukua maisha yake masaa machache badae. Habari hii iliripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari lakini ghafla ikapotea katika namna ya kushangaza. Upo uwezekano alihonga ndungu wa marehemu na baadhi ya vyombo vya habari ili kudhibiti taarifa zaidi kutoka na pengine kuchukuliwa hatua za kisheria. Kadhia kama hizi sehemu ya kazi kwa wafanyakazi wa NHIF. Hatuamini kama hizi ni tabia stahili kwa mtu mwenye dhamana ya kuongoza shirika la bima ya Afya nchini.

Haaaghhhhh!

Yaani nimechoka kabisa hapa!
 
Sasa kama kila kukicha yanatokea mambo haya ya ajabu sana na ukiangalia sana ufisadi mwingi ambao tumepata au kuelezea katika JF yametokea Dar na inatisha.Jamani, je na huko mikoani? tukazipata mbona itakuwa ya Dar ni tone la maji katika bahari.

Mimi nimefikiria nimeona tunahitaji JF Radio ambayo ni powerful ikasikika pande zote za nchi yetu tukufu halafu tunahitaji waandishi wa habari ambao wenye guts kama yule mtoto aliyekuwa EATV i think her name is Carol.Tunahitaji watu kama yule jamaa Bob Woodward na kashfa ya watergate.

Ukingalia internet haijafikia huko vijijini na watu wengi hawajui ufisadi unaoendelea katika nchi yetu na ndio hawa wapiga kura na ndio hawa majina yao mengi ni bin CCM or binti CCM...wanabidi wajulishwe yule baba yao ana wa betray.

TUISAFISHE NCHI YETU NIA TUNAYO,NJIA TUNAZO na UWEZO TUNAO.....MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom