Ufisadi ndani ya Mlimani City Project

zacha

JF-Expert Member
Feb 28, 2009
1,189
1,828
Jamani wadanganyika wenzangu kwa info nilizozipata kutoka kwa wachunguzi wa mambo kuhusu mkataba wa mwarabu wa Mlimani City na Chuo Kikuuu...

Habari zinasema yule mwarabu kapewa kile kiwanja ajenge na afanyie biashara kwa muda wa miaka 50 bila kulipia kodi yoyote........ halafu baada ya muda huo ndo majengo na kila kitu vinakuwa chini ya chuo... Ebu tuangalie hii kitu jinsi ilivyokaa..

Ni nani atakaye faidi katika huu mkataba?

=====
2017 updates:

Ripoti ya CAG: Mkataba wa Mlimani City na Chuo Kikuu cha UDSM ni wizi mtupu
 
Mhh nasikia Olenaiko na Mshana ukitaka kuwagusa babaya ongelea hilo deal la Mliman city ni kweli ina kashfa kubwa mno
 
Yeah ni kweli hili swala lipo tena wazi we fikiria nyumba au majengo yale unafikiri yatadumu baada ya miaka 50?
Kweli miTanzania ndivyo tulivyo
 
Hilo swala niliwahi kulisikia wakati niko pale Mlimani nasoma (muda umepita kidogo) kwa hiyo naanza kuamini kuwa kuna ukweli ndani yake. Baada ya Miaka 50, wanajuaje kama wadanganyika bado watakuwa wanahitaji bidha zinazopatikana pale Mlimani City??
 
huu ni uupuuzi usio kuwa na maana kwani hata mimi nilivyoambiwa nimeumia sana hadi kufikia hatua ya kuileta hapa. Jamaa anapata faida sana ukizingatia na zile nyumba alizojenga pale pembeni ambazo kupanga kwenye hizo nyumba ni lazima uonyeshe Bank Statement kwanza so haziko pale kuwasaidia wadaganyika walalahoi ........

Dah! Imeniuma sana na tena sana........... ila tutafika tuu
 
Ukweli ni kwamba, jamaa atakuwa analipa kodi kwa chuo, lkn haijafahamika ni kiasi gani. na baada ya miaka hamsini ndiyo majengo yatakuwa mali ya chuo.

Ninavyofahamu mimi kwa standard ya nyumba zetu nyingi, advised life span ya majengo yetu ni kati ya miaka 30 na 40 (civil engineers wanaweza kutusaidia).

Kama ni kweli, basi nadhani chuo kitakuwa kimekabidhiwa kazi ya kuyabomoa na si kumiliki.
 
Ninavyofahamu mimi kwa standard ya nyumba zetu nyingi, advised life span ya majengo yetu ni kati ya miaka 30 na 40 (civil engineers wanaweza kutusaidia).
Hata likidumu miaka hiyo 30 litakuwa limeshapitwa na wakati hivyo litakuwa halilipi tena
 
Hii ishu ya mlimani city ni ya ukweli kabisa wabostwana hao wamepewa 50 years ndio yawe ya chuo na ujengaji wake kwa sisi wa wataalam wa civil miaka 50 hayawezi kufika lazima yawe magofu.

Sasa inabidi tuwe macho wadanganyika na huu mradi
 
Wakati mwingine tunaweza tukaanza kujadili kitu bila hata ya kuwa na ushahidi ambao ni msingi wa majadiliano.

Aliyosema zacha hapo juu ni kama umbea wa mtaani tu. Kwa sababu angeweka mkataba hapo au angetueleza kama ameuona na vipengele ni vya kijinga basi tungemuelewa. Lakini mie sidhani kama dons wana ujinga wa kiasi cha kuingia mkataba wa miaka hamsini bila rent wala any benefit to the university.

Mie kwangu ni logic ndio ina apply zaidi kuliko kuanza kuongelea mambo mabaya wakati mazuri yamejaa. Ujenzi wa dual carriage ya Sam Nujoma pamoja na upanuzi wa daraja la Ubungo ni kwa sababu ya mradi wa mlimani city.

Tunatarajia kuona upanuzi wa barabara inayopita rose garden kwa sababu ya mradi wa Dar village. Sometimes tuongelee mazuri kidogo
 
Ile project ni ya kihuni na waliosaini mkataba nao ni wahuni tu. Ningewaita mafisadi.. lakini sasa tunatakiwa ku move on, kwani hata wale tuliowaita mafisadi hakuna hata mmoja amesekwa gerezani.

Lile eneo la mlimani ambako ipo Milimani City ni eneo lililo kuwa wazi kwa miaka yote.. ni eneo bikira kabisa kabla ya kuletwa ile project. Hakuna hata jengo la maana pale... ni ma godown matupu yale. hayatofautiani chochote na yale yaliyopo pale kwenye kiwanda cha zamani cha fishnet karibu na kiwanda cha Urafiki.

Sehemu yote ile ametandaza magodown badala ya kujenga majengo yanayokwenda juu ile kuleta maana ya matumizi safi ya ardhi na pia maana halisi ya shopping mall.

Nadhani hata may fair plaza ni project ya manufaa zaidi kuliko ile ya Mlimani city.

Aliyesaini na kuingia mkataba, mmiliki wa ile mlimani city na wote wanaodhani kuwa ile ni project ya manufaa kwa watanzania ni wahuni watupu.

Na hata vile vijengo vilivyopo barabara ya sam Nujoma mbele kidogo ya mlimani city kuelekea Ubungo, vile vya mama Anna mkapa nao ni uhuni mtupu. kwanini wajenge vijumba vidogo vodogo wakati kuna uwezekano wa kutumia nafasi vizuri na kujenga majengo yanayokwenda juu ili kuleta matumizi bora ya eneo na nafasi.

Ni masikitiko makubwa ninayo kwa project hizi mbili... ni uhuni mtupu!!!!!
 
jamani wadanganyika wenzangu kwa info nilizozipata kutoka kwa wachunguzi wa mambo kuhusu mkataba wa mwarabu wa mlimani city na chuo kikuuu...

Habari zinasema yule mwarabu kapewa kile kiwanja ajenge na afanyie biashara kwa muda wa miaka 50 bila kulipia kodi yoyote........ Halafu baada ya muda huo ndo majengo na kila kitu vinakuwa chini ya chuo... Ebu tuangalie hii kitu jinsi ilivyokaa..

Ni nani atakaye faidi katika huu mkataba?
wimbo wa taifa la mafisadi...hiki ni kibwagizo au korasi ya saba
 
Huu mkataba wa kifisadi, Hapo ndio utatambua prof. au wasomi wa kitanzania tuna kasoro kama si umbumbu

Huu mkataba ulisainiwa wakati Prof. Luhanga akiwa mkuu wa chuo na ulileta mvutano pale chuoni wakati huo kwa kipengele hiki cha miaka 50 ya mkataba bila kulipa chochote.

Nakumbuka UDASA ikiwa chini ya marehemu Prof. Chachage waliweka pingamizi na issue ilifika mahakani sijui maamuzi ya mahakama yalikuwaje.
 
Nataka nikubaliane kidogo na Kaka Mdogo..lazima unapoleta hoja uwe na data ili hata anayechangia asichangie kishabiki tuuu.

Naikumbuka project ya Mlimani city hata kabla mkataba wake haujasainiwa. Aliyekuwa msimamizi wa ile project alikuwa ni Dr, Chungu wa UDSM wakati huo akitufundisha Enterprenuer akawa anatuhadithia kuhusu huu mradi..nobody could beilve it coming true...but it is now there...ukitaka kujua mafanikio yake ni mengi sana.. na kusema kwamba ule mkataba ni wa kifisadi inakubidi ujue biashara za real estate zaivyofanya kazi..there is win-win situation..na unaposema yale majengo baada ya hiyo miaka 50 yatakuwa magofu...unajua mabweni ya UDSM yana umri gani..na pia ile project bado inaendelea..

Ila kuhusu effective use of the land kama anavyosema bwana Mundu ni kweli..pale kuna kosa..originally yale majengo yalikuwa yawe ni ghorofa angalau moja hata watakaokumbuka ile michoro ya kwanza kabisa ilikuwa inaonyesha hivyo na hata engineer aliyefanya EIA (environment impact assesment) namjua kuna siku alisema hivyo...sasa kinachotokea i dont know...

Kuhusu zile nyumba za mama Anna Mkapa pale kuna bomu na utapeli mkubwa sana, mama Anna alilazimika kuzifanya ziwe za yatima baada ya ishu kufumuka..kwa plan ile hata mtoto wa darasa la kwanza hawezi kuamini kwamba zile nyumba zilikuwa za watoto yatima...yule mama hana roho nzuri kiasi hiko..ukiangalia vizuri hata plan ya finishing aliibadilisha badae..kaangalie madilisha...ilikuwa yawe ya vioo lakini mwisho ikapigwa nyavu ya kawaida tu...labda nae tutaangalia huko baadae itakuwaje na ana mkataba gani na serikali kuhusu ile ardhi but it is a completely a waste...

SIKU ZOTE NCHI ITALIWA NA WAJANJA...
 
Mtazamowangu usilinganishe yale majengo ya mlimanicity na mabweni ya chuo yaliyojengwa na Mwizrael.

Yale majengo ya mlimani city yanajengwa kitapeli kabisa !! Ni temporaly buildings zile. Nenda kaangalie material anayotumia lile jengo analojenga pembeni pale sasa hivi.

1. Anatumia mabati sehemu kubwa ukutani. Hii ina maana ameshafanya study kwamba for 20 yrs itakuwa maximum lazima yataanza kuoza mabati yale na kufikia hiyo 50 yrs yenu hamtabaki na kitu.

2. Pili kwa kuona pale wana eneo kubwa basi wameamua kujenga mijengo ya godown ambayo ni cheap bila kujali land value!! Pamoja na kujenga lile la kwanza godown nilitegemea uongozi wa chuo uliojaa wasomi, Maprofessor wa majengo , Civil building, Land valuers, n.k wanaojua jinzi ardhi ya dar ilivyoadimu basi wasingemruhusu aendeleze ujenzi kama huo tena sehemu ya pili. Lakini wamemwacha anachojenga ule upande wa pili ni uchafu zaidi ya ule wa kwanza.

3. Yale maeneo ya Chuo kikuu yalitengwa na wataalamu enzi hizo wakisaidiwa na Mwingereza kwa manufaa ya chuo, na yalikuwa na lengo la kwamba yatasaidia ukuaji wa chuo na upanuaji wa chuo. Nilitegemea kama ni investment wangewekeza kujenga Student villages ambazo zingesaidia wanafunzi wanalala Manzese warudi maeneo ya pamoja. Na hizo student villages zingesaidia sana kwa vyuo vyote vilivyopo Dar.

Hivi ni kweli hawa waliofanya maamuzi hawapiti maeneo ya vyuo vikuu vya nje wakaona vinavyokuwa na maeneo makubwa na yanatumika kwa manufaa ya vyuo siyo kuingia miradi ya kijinga kama hiyo isiyo na manufaa kwa taifa.
 
Jamani ebu tutoe comment za kina-tukiwa na full information. hata watu wakatembelea pale au kuwaulzia NOREMCO staff, au Prof.Msambichaka aliyekuwa consultant.

please!
 
Mhh nasikia Olenaiko na Mshana ukitaka kuwagusa babaya ongelea hilo deal la Mliman city ni kweli ina kashfa kubwa mno

Jamani wadanganyika wenzangu kwa info nilizozipata kutoka kwa wachunguzi wa mambo kuhusu mkataba wa mwarabu wa Mlimani City na Chuo Kikuuu...

Habari zinasema yule mwarabu kapewa kile kiwanja ajenge na afanyie biashara kwa muda wa miaka 50 bila kulipia kodi yoyote........ halafu baada ya muda huo ndo majengo na kila kitu vinakuwa chini ya chuo... Ebu tuangalie hii kitu jinsi ilivyokaa..

Ni nani atakaye faidi katika huu mkataba?


mhhhh mbona sielewi ?
hebu fafanua..mwarabu gani? toka nchi gani? kampuni gani?kaletwa Tanzania na nani? au partner wake Tanzania ni nani?

Kinachoniboa pale ni inconsistency ya umeme wao hasa upande wa film theatres zilizojaa PANYA, sound system yao ni mbovu, na films zinazoonyeshwa pale ni za zamani ambazo ziko kwenye DVD ..in short those guys are a bunch of jockers!!! nataka nitazame STAR TREK basi mpaka leo hawajui wataileta nini


Hii ishu ya mlimani city ni ya ukweli kabisa wabostwana hao wamepewa 50 years ndio yawe ya chuo na ujengaji wake kwa sisi wa wataalam wa civil miaka 50 hayawezi kufika lazima yawe magofu. Sasa inabidi tuwe macho wadanganyika na huu mradi

mara waarabu...mara wabotswana...which is which?
 
Last edited:
Jamani ebu tutoe comment za kina-tukiwa na full information. hata watu wakatembelea pale au kuwaulzia NOREMCO staff, au Prof.Msambichaka aliyekuwa consultant.

please!


Hivi hawa na NORCONSULT kitu kimoja? if so then mmoja wao alikuwa na kashfa ya rushwa na serikali imepewa ripoti na jamaa wa WORLD BANK lakini madudu yaliomo humo ndani hiyo ripoti haiwezi kuwekwa public...kisa? wakubwa wametajwa
 
Dawa ni kumwaga hiyo lease agreement ya MLIMANI CITY humu kisha tutajua maana hapa tunazungumzia speculation tuuu bas!

anyway umezungumzia designs za majengo na kusema ukweli mimi nadhani yale ma jengo ni mabovu kwa kuyatazama usoni infact they look more like a hospital than anything else..huo ndio upande wa aesthetics overall naweza kusema kuwa in short hawa jamaa wa Mlimani city wanatueletea upuuzi wa Matalan, Lidl, Netto, Toys ’R’ Us, drive-through KFC and McDonald’s, and retail park in the land all rolled in one na matokeo yake ndio haya

itabidi nianzishe thread maalum ya kuwachambua ma consultants wetu na majengo waliosimamia
 
Back
Top Bottom