Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Baraka za CCM kinga ya ufisadi Benki Kuu
Lula wa Ndali-Mwananzela Januari, 16, 2008
HIVI nikikuuliza ndugu msomaji ni mbunge gani wa CCM ambaye jina lake linaweza kukujia mara moja kichwani, ambaye alisimama mwaka jana na kuonekana mtetezi wa wananchi, rasilimali zao na haki zao, utanitajia nani? Nina hakika hutaweza kunitajia.
Hata hivyo nikikuuliza ni mbunge gani wa upinzani ambaye kwa mwaka jana alionekana ni mtetezi wa wananchi, raslimali zao na haki zao utanitajia nani? Bila shaka utawataja Zitto na Dk. Slaa.
Jibu hilo labda halikuwa mbali sana na halikuwa na ugumu wowote kwani rekodi zao zinaonekana wazi na watu wanayajua majina yao kama vile ya watoto wao.
Hata hivyo swali ambalo limenisumbua mimi binafsi hasa baada ya Ballali kuvuliwa ugavana (na kuachwa bado kwenye utumishi wa serikali) ni kuwa inawezekanaje kati ya wabunge 320, wabunge kama 40 waonekane na nguvu zaidi kuliko wabunge 271 wa chama tawala?
Ni kwa nini kati ya wabunge 271 ambao ndio wana uwezo wote wa kufanya lolote watakalo wawe butu na goigoi na kuzidiwa nguvu na watu wasio na serikali na wasio na nguvu yoyote ile zaidi ya ile ya hoja?
Tukiiweka hoja hii kati ya CCM na CHADEMA tu (TLP, CUF, na NCCR-Mageuzi mniwie radhi), inakuwaje wabunge 11 wa CHADEMA wawe na nguvu ya kutetemesha serikali hadi kulazimisha milingoti itikisike ukilinganisha na wabunge 271 wa chama tawala wanaocheua rangi ya kijana na kumeza rangi ya njano?
Nauliza hivyo kwa sababu kuanguka kwa Ballali, na uchunguzi uliofanyika Benki Kuu na kusababisha hatua kali kuchukuliwa na Rais haukutokana na shinikizo ndani ya CCM au wabunge wake bali uliletwa na wapinzani! Mwaka jana ilikuwa kama vile Bunge letu ni la wapinzani.
Jambo jingine ambalo linanisumbua katika sakata hilo lote ni kuwa iliwezekana vipi Gavana Ballali na makampuni ya kifisadi kuweza kuchota fedha kama njugu na kujigawia kama kugawiana kashata huku CCM na wabunge wake wakiendelea kutanua na kuimba nyimbo za CCM Idumu?
Ndugu zangu, ninachoweza kusema bila ya shaka yoyote lile ni kuwa ufisadi wa Benki Kuu ambao matokeo yake ndiyo tumeyaona siku hizi chache zilizopita na bila ya shaka tutaona zaidi mbeleni umetokana, umeendelea, na umesabishwa na baraka za dhati za Chama cha Mapinduzi.
Kwa wale wanaokumbuka watagundua kuwa kashfa na tetesi za usifadi Benki Kuu hazikuanza mwaka 2005/2006 kama serikali ya CCM inavyotutaka tuamini, bali imeanza karibu muongo mmoja uliopita kabla yake. Wafuatiliaji wa mambo ya siasa watakumbuka kuwa kati ya vitu vilivyosababisha Mrema kutimuliwa uwaziri na hatimaye kujitoa CCM ilikuwa ni sakata la upotevu wa mabilioni ya shilingi toka Benki hiyo kuu kwa mtindo huo huo wa kutumia makampuni hewa.
Mrema alipojitolea kuwaambia wananchi serikali ya CCM chini ya Rais Ally Hassan Mwinyi wakamuita yeye (Mrema) kichaa na ya kuwa hakuwa mwajibikaji wa pamoja.
Leo hii, siri za benki kuu zinapoonekana wazi ndipo Watanzania tunajua ni nani alikuwa kichaa kweli kweli. Kumbe aliyoyasema Mrema akiwa ndani ya CCM yalikuwa na ukweli mkubwa kwani ndio maana Rais Kikwete leo hii hajathubutu kuchunguza Benki hiyo Kuu kwa miaka kama 15 iliyopita na kututuliza, akaamua kuchagua miezi michache tu ya msimu wa 2005/2006!
Hata hivyo, baraka hizi za CCM ambazo zimechangia ufisadi mkubwa Benki Kuu zimetokana na wabunge wa CCM kuwa watetezi wa Chama chao na serikali yao na siyo wafuatiliaji na wasimamizi wa serikali hiyo. Wakati wapinzani wanataka iundwe kamati teule ya Bunge, wabunge wetu wa CCM wakapigwa mkwara na matokeo yake wakagwaya na kusababisha Dk. Slaa, mtetezi wa wananchi, kuondoa hoja yake hiyo.
Nilibahatika kupata nakala ya hoja ambayo Dk. Slaa alikuwa ailete Bungeni mwaka jana, na wapendwa wasomaji, kama yaliyomo humo yangesemwa Bungeni, basi ya Buzwagi yangeonekana mtoto. Katika hoja yake hiyo kulikuwa na maswali muhimu na ya msingi kuhusu utendaji wa Bunge na jinsi gani Bunge liliingizwa mjini katika kupokea ripoti kuhusu Benki Kuu.
Kama hilo halitoshi, wabunge wa CCM walikuwa ndio watetezi wa ufisadi huu kwa kukaa kwao kimya kwa zaidi ya miaka minane sasa ambapo watu wamekuwa wakilalamikia ufisadi Benki Kuu. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CCM aliyekuwa na ujasiri wa kumnyooshea Ballali kidole hadharani au makampuni yaliyohusika na badala yake wote walikuwa wanazungumzia pembeni!
Ndiyo maana wananchi walikiona kitendo cha wapinzani pale Mwembe Yanga Temeke kuzungumzia na kutaja majina ya wahusika wa ufisadi kuwa ni kitendo cha kijasiri na kishujaa. Kama waliopewa dhamana ya kutawala wameshindwa kufanya hivyo, basi, wengine wana haki ya kuonesha jinsi nchi inavyoweza kutawaliwa.
Wabunge wa CCM ni waoga tena waoga wa kutupwa. Wanaogopa Kamati Kuu na lile jinamizi la Nidhamu ya Chama. Wanagwaya na kutetemeka wakiitwa mbele ya dubwasha hilo na hawawezi kuthubutu kuzungumza kwa uhuru wote Bungeni na badala yake kutetemeka huku wakijiumauma meno.
Mfano mzuri wa wabunge wa namna hii ni yule Mbunge wa Kwela Bw. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya. Mwezi Novemba mwaka 2001 aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Bw. Idi Simba alijiuzulu baada ya hoja nzito ya Bw. Mzindakaya kuhusu utoaji wa vibali vya kuingiza sukari ulivyokuwa umejaa utata na ulivyokuwa kinyume na maslahi ya Taifa. Kutokana na hoja yake hiyo Kamati ya Bunge iliundwa na masaa machache kabla ya ripoti ya Kamati hiyo kuanza kujadiliwa Bungeni, Bw. Idi Simba akajiuzulu.
Jambo hilo lilimpa sifa ya mtetezi wa wanyonge Bw. Mzindakaya na akaonekana ndani ya CCM kama ni Mbunge machachari. Hivyo katika sakata hili la Benki Kuu siku aliposimama kutetea wengi wetu tulitarajia na tulisubiri kwa hamu kusikia atasema nini. Kumbe tusichokijua kilikuwa ni kama usiku wa giza kwani Bw. Mzindaka ni mmoja ya watu walionufaika kwa namna moja au nyingine na yale yanayoendelea Benki Kuu.
Katika utetezi wake wa Benki Kuu, Bw. Mzindakaya alisema mambo mawili ambayo ni muhimu kuyaangalia moja baada ya jingine. Kwanza, alikanusha kuwa fedha zilizopotea Benki Kuu siyo bilioni 200 kama ilivyodaiwa na wapinzani. Alisema hivi, nazungumza kwa mamlaka kwani nimefanya uchunguzi wangu, fedha zilizopotea ni bilioni 131 na siyo bilioni 200 kama walivyodai wapinzani.
Cha kushangaza ni kuwa baada ya uchunguzi wa Ernst and Young na kutumia mamilioni ya fedha kwenda hadi Ulaya na kwingineko kutafuta ukweli wa fedha zilizochotwa, tunaambiwa kuwa zilizopotea ni bilioni 133 tu! Karibu sawa kabisa na fedha alizodai Bw. Mzindakaya.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa kama Mzindakaya aliweza kufanya uchunguzi wake na akaweza kupata hesabu hizo kiurahisi namna hiyo (siku kadhaa tu tangu wapinzani waseme Bungeni) kulikuwa na ulazima gani wa kutafuta kampuni ya nje kufanya uchunguzi mwingine? Kama jibu CCM walikuwa nalo kwanini kutufanyia mazingaombwe ya uchunguzi na kutufanya tuwe na kiroho juu kumbe wenzetu majibu walikuwa nayo tangu mwezi wa sita mwaka jana!
Lakini jambo la pili ambalo limenishtua ni kuwa kama huyo aliyewahi kuwa mtetezi wa wanyonge aliweza kukaa kimya na kudai kuwa Benki Kuu yetu ni safi na ni moja kati ya Benki Kuu 10 bora barani Afrika ni kitu gani kilimfanya akubali na kuufumbia macho wizi huu wa mabilioni ya fedha badala ya kupigia kelele kama alivyopigia kelele sakata la sukari? Wakati mmoja akihojiwa kule Uingereza Bw. Mzindakaya alisema kuwa aliamua kuja na hoja hiyo hadharani baada ya Waziri Simba kuweka pamba masikioni na kutokukubali makosa.
Hata hivyo, siwezi kusema ni Mzindakaya peke yake ambaye ametoa baraka za ufisadi wa BoT. Wengi tunakumbuka jinsi Waziri wa Fedha Bi. Meghji alivyojaribu kutetea ujenzi wa minara pacha ya Benki Kuu alipoulizwa swali la mtego na Mhe. Siraju Kaboyoga. Jinsi Bi. Meghji alivyojiuma uma meno ndivyo wengi tulipoona kuwa kuna kitu kinafichwa.
Katika mojawapo ya magazeti ya jana imeripotiwa kuwa Bi. Meghji na yeye ameamua kumtosa Ballali kwa madai kuwa yeye Ballali alimpotosha Meghji. Ninavyoona sasa hivi ni kuwa Bi. Meghji na wenzake bila ya shaka wameona kuwa sakata zima la BoT linamuelemea Ballali hivyo wote sasa wanataka kumbebesha madhambi yao yote huku wao wenyewe wakikaa pembeni kuchekelea.
Kinachoonekana sasa ni jaribio dhaifu la kumfanya Ballali ndio hasidi na hasimu mkuu Tanzania ambaye ndiye kilele cha ufisadi nchini. Ni wao wanajaribu kutuonesha Ballali kama shetani mwenye mapembe na wao serikali na CCM ndio malaika wazuri ambao hawakufanya makosa yoyote yale.
Bahati mbaya gia yao hiyo ya reverse tumeishtukia kwani tunatambua kuwa Ballali hakujipachika ugavana na kwa miaka minane aliyokaa kwenye kiti hicho hakuwa amejifunga pingu na mnyonyoro asitoke! Ni wao CCM na serikali yao waliomuingiza hapo, ni wao waliomtetea na sasa hivi kwa vile wameshamtumia kwa kadiri wanavyotaka wameamua kumtema kama makapi ya miwa! Ndiyo wamemfyonza na kumnyonya utamu wote na sasa wameamua kumtupa nje ya mji akanyagwe na wapita njia!
Hata hivyo hilo ni jaribio dhaifu kwa sababu Watanzania waliokuwa wanaamini kila serikali inasema wameanza kuamka. Mazingaombwe yao ya kitoto na hoja zao zisizo na kichwa wala mguu zimeanza kuonekana wazi. Wanaweza kuvificha vichwa vyao kama mbuni mchangani wakidai hawaonekani!
Tunawaona na tunawatambua, siyo tu tunawaona na kuwatambua bali tumedhamiria kuwang'amua na kuwaumbua mpaka watakapojua kuwa wao hawana lao tena kwani kumekucha, Tanzania mpya iko njiani na mwangaza wake umeanza kuangaza kama mapambazuko!
Wabunge wa CCM na chama chao ambao walitoa baraka za ufisadi na kusababisha mabilioni ya fedha kutoweka katika benki yetu kuu ni lazima wajulikane kama washirika wa ufisadi. Wabunge wa CCM walioshindwa kumuwajibisha Gavana, Waziri na watendaji wengine na wale wote ambao walipitia hesabu za BoT na kuzipa baraka zake, wote ni washirika wa ufisadi. Hawastahili tena kutuambia mambo ya rushwa na ufisadi kwani tumewaona walivyoshughulikia suala la Benki Kuu.
Wabunge wengine waliotusikitisha zaidi ni wale wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi. Ndugu zetu hawa waliangalia mahesabu aliyoangalia Mzindakaya na ambayo baadaye yakaangaliwa na Ernst & Young, lakini wakaja na kusema mahesabu hayo yalikuwa safi! Hii ni tofauti na Kamati ya kina Mwakyembe ambao walipoangalia mambo ya nishati wakakuta kuna tatizo kwenye mkataba wa Richmond na wakapigia kelele hadi kamati ikaundwa. Hawa wa Fedha na Uchumi wakaamua kuisafisha BoT! Ambacho hatukuambiwa ni kuwa mmoja wa wajumbe mtoto wake ni mfanyakazi BoT!
Kamati hiyo, ikiongozwa na Mbunge wa Handeni (CCM), Dk Abdallah Kigoda, akisaidiwa na kijana msomi, Adam Kighoma Malima, ambaye ni Mbunge wa Mkuranga kupitia CCM, iliweka hadharani kwamba hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 ni safi, hesabu ambazo leo hii tumeambiwa kwamba katika akaunti moja tu zimepotea zaidi ya Shilingi bilioni 133 na Gavana akangolewa.
Aibu tupu. Yaani kwa kifupi wao hawakuona ka-kampuni hata kamoja kalikochota hata senti moja, halafu miezi chini ya sita baadaye tunaambiwa tumeibiwa! Ama kweli sisi si Watanzania tena bali ni Wadanganyika!
Itakuwa ni kichekesho na ni tusi kwa akili za Watanzania kama wabunge wengi wa CCM wataendelea kuchaguliwa na wananchi. Kama itatokea wananchi wa jimbo lolote wakamchagua mbunge wa CCM wajue kabisa wanachagua mtu ambaye hawezi kutetea maslahi ya Taifa. Hadi hivi sasa hakuna mbunge yeyote wa CCM ambaye anaweza kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi. Wote wamenaswa kwenye mtego walioutega wenyewe.
CCM ni zimwi litujualo, linatula na kutubakisha kidogo ili lipate nafasi ya kututafuna tena. Limekula Buzwagi likabakisha, likala kwenye rada likabakisha, likala kwenye dege la Rais likabakisha, likala Meremeta, likala Mwananchi Gold, likala Deep Green, likala Tangold, likala Kiwira na kubakisha, na sasa tumegundua kuwa limekuwa likila Benki Kuu na kubakisha kidogo ili lile tena! Kuendelea kufumba macho kuwa siku moja litaacha kula ni kujidangaya, njaa yake haitakoma na kiu yake haizimuliwi kwa maji wala kwa togwa!
Dawa yao ni moja na nilazima wanyweshwe hata kwa kuzibwa pua - kuwanyima viti vya kura. Binafsi naamini mahali bora pa kuanzia ni kwenye uchaguzi wa Kiteto unaokuja mwezi ujao. Wananchi wa Kiteto lazima waoneshe mfano kwa Watanzania wengine kuwa CCM wanaweza kusimamisha mtu yeyote hata malaika wao, na wanaweza kuwaleta wapiga debe wa kila aina lakini jimbo hilo halirudishwi tena CCM.
CCM haistahili jimbo jingine hata moja la ziada kwani wanavyo viti 271 ambavyo wamevikalia kwa fahari na matunda yake hatuyaoni. Wananchi wa Kiteto na sehemu nyingine zitakazofanya uchaguzi mwaka huu hawana budi kutambua kuwa, yawezekana mgombea atakayesimamishwa na CCM ni mzuri na anapendwa, na inawezekana ni mtu ambaye wanamfahamu hata hivyo, suala hili siyo la kuhusu wagombea. Suala ni chama cha mgombea.
Katika hili, CCM ni chama kilichoshindwa kupambana na ufisadi na kilichozowea mazingaombwe ya ahadi. Leo hii tunafanyiwa mazingaombwe tunashangilia ati hatimaye Rais afanya kweli, Ati Rais aanza vitu vyake. Udanganyika mwingine mbaya. Miaka 46 sasa bado wanaanza? Amkeni wana na mabinti wa taifa hili, onesho limekwisha yote ni mazingaombwe!
Tunataka vitu vya kweli. Ni bora tuwe na wabunge 50 wa upinzani wanaotetea nchi kuliko wabunge 280 wa CCM wanaotetea chama chao! Bora tukipe chama kingine mbunge huyo wa Kiteto kuliko kuwaongezea CCM mbunge wa ndoto!
Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk