UFISADI Kila Kona: Baraka za CCM KINGA ya Ufisadi BoT na Viongozi Mafisadi

Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,873
1,894
Baraka za CCM kinga ya ufisadi Benki Kuu

Lula wa Ndali-Mwananzela Januari, 16, 2008

HIVI nikikuuliza ndugu msomaji ni mbunge gani wa CCM ambaye jina lake linaweza kukujia mara moja kichwani, ambaye alisimama mwaka jana na kuonekana mtetezi wa wananchi, rasilimali zao na haki zao, utanitajia nani? Nina hakika hutaweza kunitajia.

Hata hivyo nikikuuliza ni mbunge gani wa upinzani ambaye kwa mwaka jana alionekana ni mtetezi wa wananchi, raslimali zao na haki zao utanitajia nani? Bila shaka utawataja Zitto na Dk. Slaa.

Jibu hilo labda halikuwa mbali sana na halikuwa na ugumu wowote kwani rekodi zao zinaonekana wazi na watu wanayajua majina yao kama vile ya watoto wao.

Hata hivyo swali ambalo limenisumbua mimi binafsi hasa baada ya Ballali kuvuliwa ugavana (na kuachwa bado kwenye utumishi wa serikali) ni kuwa inawezekanaje kati ya wabunge 320, wabunge kama 40 waonekane na nguvu zaidi kuliko wabunge 271 wa chama tawala?

Ni kwa nini kati ya wabunge 271 ambao ndio wana uwezo wote wa kufanya lolote watakalo wawe butu na goigoi na kuzidiwa nguvu na watu wasio na serikali na wasio na nguvu yoyote ile zaidi ya ile ya hoja?

Tukiiweka hoja hii kati ya CCM na CHADEMA tu (TLP, CUF, na NCCR-Mageuzi mniwie radhi), inakuwaje wabunge 11 wa CHADEMA wawe na nguvu ya kutetemesha serikali hadi kulazimisha milingoti itikisike ukilinganisha na wabunge 271 wa chama tawala wanaocheua rangi ya kijana na kumeza rangi ya njano?

Nauliza hivyo kwa sababu kuanguka kwa Ballali, na uchunguzi uliofanyika Benki Kuu na kusababisha hatua kali kuchukuliwa na Rais haukutokana na shinikizo ndani ya CCM au wabunge wake bali uliletwa na wapinzani! Mwaka jana ilikuwa kama vile Bunge letu ni la wapinzani.

Jambo jingine ambalo linanisumbua katika sakata hilo lote ni kuwa iliwezekana vipi Gavana Ballali na makampuni ya kifisadi kuweza kuchota fedha kama njugu na kujigawia kama kugawiana kashata huku CCM na wabunge wake wakiendelea kutanua na kuimba nyimbo za “CCM Idumu”?

Ndugu zangu, ninachoweza kusema bila ya shaka yoyote lile ni kuwa ufisadi wa Benki Kuu ambao matokeo yake ndiyo tumeyaona siku hizi chache zilizopita na bila ya shaka tutaona zaidi mbeleni umetokana, umeendelea, na umesabishwa na baraka za dhati za Chama cha Mapinduzi.

Kwa wale wanaokumbuka watagundua kuwa kashfa na tetesi za usifadi Benki Kuu hazikuanza mwaka 2005/2006 kama serikali ya CCM inavyotutaka tuamini, bali imeanza karibu muongo mmoja uliopita kabla yake. Wafuatiliaji wa mambo ya siasa watakumbuka kuwa kati ya vitu vilivyosababisha Mrema kutimuliwa uwaziri na hatimaye kujitoa CCM ilikuwa ni sakata la upotevu wa mabilioni ya shilingi toka Benki hiyo kuu kwa mtindo huo huo wa kutumia makampuni hewa.

Mrema alipojitolea kuwaambia wananchi serikali ya CCM chini ya Rais Ally Hassan Mwinyi wakamuita yeye (Mrema) kichaa na ya kuwa hakuwa “mwajibikaji wa pamoja”.

Leo hii, siri za benki kuu zinapoonekana wazi ndipo Watanzania tunajua ni nani alikuwa kichaa kweli kweli. Kumbe aliyoyasema Mrema akiwa ndani ya CCM yalikuwa na ukweli mkubwa kwani ndio maana Rais Kikwete leo hii hajathubutu kuchunguza Benki hiyo Kuu kwa miaka kama 15 iliyopita na kututuliza, akaamua kuchagua miezi michache tu ya msimu wa 2005/2006!

Hata hivyo, baraka hizi za CCM ambazo zimechangia ufisadi mkubwa Benki Kuu zimetokana na wabunge wa CCM kuwa watetezi wa Chama chao na serikali yao na siyo wafuatiliaji na wasimamizi wa serikali hiyo. Wakati wapinzani wanataka iundwe kamati teule ya Bunge, wabunge wetu wa CCM wakapigwa mkwara na matokeo yake wakagwaya na kusababisha Dk. Slaa, mtetezi wa wananchi, kuondoa hoja yake hiyo.

Nilibahatika kupata nakala ya hoja ambayo Dk. Slaa alikuwa ailete Bungeni mwaka jana, na wapendwa wasomaji, kama yaliyomo humo yangesemwa Bungeni, basi ya Buzwagi yangeonekana “mtoto”. Katika hoja yake hiyo kulikuwa na maswali muhimu na ya msingi kuhusu utendaji wa Bunge na jinsi gani Bunge “liliingizwa” mjini katika kupokea ripoti kuhusu Benki Kuu.

Kama hilo halitoshi, wabunge wa CCM walikuwa ndio watetezi wa ufisadi huu kwa kukaa kwao kimya kwa zaidi ya miaka minane sasa ambapo watu wamekuwa wakilalamikia ufisadi Benki Kuu. Hakuna Mbunge hata mmoja wa CCM aliyekuwa na ujasiri wa kumnyooshea Ballali kidole hadharani au makampuni yaliyohusika na badala yake wote walikuwa wanazungumzia pembeni!

Ndiyo maana wananchi walikiona kitendo cha wapinzani pale Mwembe Yanga Temeke kuzungumzia na kutaja majina ya wahusika wa ufisadi kuwa ni kitendo cha kijasiri na kishujaa. Kama waliopewa dhamana ya kutawala wameshindwa kufanya hivyo, basi, wengine wana haki ya kuonesha jinsi nchi inavyoweza kutawaliwa.

Wabunge wa CCM ni waoga tena waoga wa kutupwa. Wanaogopa Kamati Kuu na lile jinamizi la “Nidhamu ya Chama”. Wanagwaya na kutetemeka wakiitwa mbele ya dubwasha hilo na hawawezi kuthubutu kuzungumza kwa uhuru wote Bungeni na badala yake kutetemeka huku wakijiumauma meno.

Mfano mzuri wa wabunge wa namna hii ni yule Mbunge wa Kwela Bw. Chrisant Majiyatanga Mzindakaya. Mwezi Novemba mwaka 2001 aliyekuwa Waziri wa Biashara na Viwanda Bw. Idi Simba alijiuzulu baada ya hoja nzito ya Bw. Mzindakaya kuhusu utoaji wa vibali vya kuingiza sukari ulivyokuwa umejaa utata na ulivyokuwa kinyume na maslahi ya Taifa. Kutokana na hoja yake hiyo Kamati ya Bunge iliundwa na masaa machache kabla ya ripoti ya Kamati hiyo kuanza kujadiliwa Bungeni, Bw. Idi Simba akajiuzulu.

Jambo hilo lilimpa sifa ya mtetezi wa wanyonge Bw. Mzindakaya na akaonekana ndani ya CCM kama ni Mbunge machachari. Hivyo katika sakata hili la Benki Kuu siku aliposimama kutetea wengi wetu tulitarajia na tulisubiri kwa hamu kusikia atasema nini. Kumbe tusichokijua kilikuwa ni kama usiku wa giza kwani Bw. Mzindaka ni mmoja ya watu walionufaika kwa namna moja au nyingine na yale yanayoendelea Benki Kuu.

Katika utetezi wake wa Benki Kuu, Bw. Mzindakaya alisema mambo mawili ambayo ni muhimu kuyaangalia moja baada ya jingine. Kwanza, alikanusha kuwa fedha zilizopotea Benki Kuu siyo bilioni 200 kama ilivyodaiwa na wapinzani. Alisema hivi, “nazungumza kwa mamlaka kwani nimefanya uchunguzi wangu, fedha zilizopotea ni bilioni 131 na siyo bilioni 200 kama walivyodai wapinzani”.

Cha kushangaza ni kuwa baada ya uchunguzi wa Ernst and Young na kutumia mamilioni ya fedha kwenda hadi Ulaya na kwingineko kutafuta ukweli wa fedha zilizochotwa, tunaambiwa kuwa zilizopotea ni bilioni 133 tu! Karibu sawa kabisa na fedha alizodai Bw. Mzindakaya.

Maswali ya kujiuliza ni kuwa kama Mzindakaya aliweza kufanya “uchunguzi” wake na akaweza kupata hesabu hizo kiurahisi namna hiyo (siku kadhaa tu tangu wapinzani waseme Bungeni) kulikuwa na ulazima gani wa kutafuta kampuni ya nje kufanya uchunguzi mwingine? Kama jibu CCM walikuwa nalo kwanini kutufanyia mazingaombwe ya uchunguzi na kutufanya tuwe na kiroho juu kumbe wenzetu majibu walikuwa nayo tangu mwezi wa sita mwaka jana!

Lakini jambo la pili ambalo limenishtua ni kuwa kama huyo aliyewahi kuwa mtetezi wa wanyonge aliweza kukaa kimya na kudai kuwa “Benki Kuu yetu ni safi na ni moja kati ya Benki Kuu 10 bora barani Afrika” ni kitu gani kilimfanya akubali na kuufumbia macho wizi huu wa mabilioni ya fedha badala ya kupigia kelele kama alivyopigia kelele sakata la sukari? Wakati mmoja akihojiwa kule Uingereza Bw. Mzindakaya alisema kuwa aliamua kuja na hoja hiyo hadharani baada ya Waziri Simba kuweka “pamba masikioni” na kutokukubali makosa.

Hata hivyo, siwezi kusema ni Mzindakaya peke yake ambaye ametoa baraka za ufisadi wa BoT. Wengi tunakumbuka jinsi Waziri wa Fedha Bi. Meghji alivyojaribu kutetea ujenzi wa minara pacha ya Benki Kuu alipoulizwa swali la mtego na Mhe. Siraju Kaboyoga. Jinsi Bi. Meghji alivyojiuma uma meno ndivyo wengi tulipoona kuwa kuna kitu kinafichwa.

Katika mojawapo ya magazeti ya jana imeripotiwa kuwa Bi. Meghji na yeye ameamua kumtosa Ballali kwa madai kuwa yeye Ballali alimpotosha Meghji. Ninavyoona sasa hivi ni kuwa Bi. Meghji na wenzake bila ya shaka wameona kuwa sakata zima la BoT linamuelemea Ballali hivyo wote sasa wanataka kumbebesha madhambi yao yote huku wao wenyewe wakikaa pembeni kuchekelea.

Kinachoonekana sasa ni jaribio dhaifu la kumfanya Ballali ndio hasidi na hasimu mkuu Tanzania ambaye ndiye kilele cha ufisadi nchini. Ni wao wanajaribu kutuonesha Ballali kama shetani mwenye mapembe na wao serikali na CCM ndio malaika wazuri ambao hawakufanya makosa yoyote yale.

Bahati mbaya gia yao hiyo ya “reverse” tumeishtukia kwani tunatambua kuwa Ballali hakujipachika ugavana na kwa miaka minane aliyokaa kwenye kiti hicho hakuwa amejifunga pingu na mnyonyoro asitoke! Ni wao CCM na serikali yao waliomuingiza hapo, ni wao waliomtetea na sasa hivi kwa vile wameshamtumia kwa kadiri wanavyotaka wameamua kumtema kama makapi ya miwa! Ndiyo wamemfyonza na kumnyonya utamu wote na sasa wameamua kumtupa nje ya mji akanyagwe na wapita njia!

Hata hivyo hilo ni jaribio dhaifu kwa sababu Watanzania waliokuwa wanaamini kila serikali inasema wameanza kuamka. Mazingaombwe yao ya kitoto na hoja zao zisizo na kichwa wala mguu zimeanza kuonekana wazi. Wanaweza kuvificha vichwa vyao kama mbuni mchangani wakidai hawaonekani!

Tunawaona na tunawatambua, siyo tu tunawaona na kuwatambua bali tumedhamiria kuwang'amua na kuwaumbua mpaka watakapojua kuwa wao hawana lao tena kwani kumekucha, Tanzania mpya iko njiani na mwangaza wake umeanza kuangaza kama mapambazuko!

Wabunge wa CCM na chama chao ambao walitoa baraka za ufisadi na kusababisha mabilioni ya fedha kutoweka katika benki yetu kuu ni lazima wajulikane kama washirika wa ufisadi. Wabunge wa CCM walioshindwa kumuwajibisha Gavana, Waziri na watendaji wengine na wale wote ambao walipitia hesabu za BoT na kuzipa baraka zake, wote ni washirika wa ufisadi. Hawastahili tena kutuambia mambo ya rushwa na ufisadi kwani tumewaona walivyoshughulikia suala la Benki Kuu.

Wabunge wengine waliotusikitisha zaidi ni wale wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi. Ndugu zetu hawa waliangalia mahesabu aliyoangalia Mzindakaya na ambayo baadaye yakaangaliwa na Ernst & Young, lakini wakaja na kusema mahesabu hayo yalikuwa safi! Hii ni tofauti na Kamati ya kina Mwakyembe ambao walipoangalia mambo ya nishati wakakuta kuna tatizo kwenye mkataba wa Richmond na wakapigia kelele hadi kamati ikaundwa. Hawa wa Fedha na Uchumi wakaamua kuisafisha BoT! Ambacho hatukuambiwa ni kuwa mmoja wa wajumbe mtoto wake ni mfanyakazi BoT!

Kamati hiyo, ikiongozwa na Mbunge wa Handeni (CCM), Dk Abdallah Kigoda, akisaidiwa na kijana msomi, Adam Kighoma Malima, ambaye ni Mbunge wa Mkuranga kupitia CCM, iliweka hadharani kwamba hesabu za BoT za mwaka 2005/2006 ni safi, hesabu ambazo leo hii tumeambiwa kwamba katika akaunti moja tu zimepotea zaidi ya Shilingi bilioni 133 na Gavana akang’olewa.

Aibu tupu. Yaani kwa kifupi wao hawakuona ka-kampuni hata kamoja kalikochota hata senti moja, halafu miezi chini ya sita baadaye tunaambiwa tumeibiwa! Ama kweli sisi si Watanzania tena bali ni Wadanganyika!

Itakuwa ni kichekesho na ni tusi kwa akili za Watanzania kama wabunge wengi wa CCM wataendelea kuchaguliwa na wananchi. Kama itatokea wananchi wa jimbo lolote wakamchagua mbunge wa CCM wajue kabisa wanachagua mtu ambaye hawezi kutetea maslahi ya Taifa. Hadi hivi sasa hakuna mbunge yeyote wa CCM ambaye anaweza kuwa mtetezi wa kweli wa wananchi. Wote wamenaswa kwenye mtego walioutega wenyewe.

CCM ni zimwi litujualo, linatula na kutubakisha kidogo ili lipate nafasi ya kututafuna tena. Limekula Buzwagi likabakisha, likala kwenye rada likabakisha, likala kwenye dege la Rais likabakisha, likala Meremeta, likala Mwananchi Gold, likala Deep Green, likala Tangold, likala Kiwira na kubakisha, na sasa tumegundua kuwa limekuwa likila Benki Kuu na kubakisha kidogo ili lile tena! Kuendelea kufumba macho kuwa siku moja litaacha kula ni kujidangaya, njaa yake haitakoma na kiu yake haizimuliwi kwa maji wala kwa togwa!

Dawa yao ni moja na nilazima wanyweshwe hata kwa kuzibwa pua - kuwanyima viti vya kura. Binafsi naamini mahali bora pa kuanzia ni kwenye uchaguzi wa Kiteto unaokuja mwezi ujao. Wananchi wa Kiteto lazima waoneshe mfano kwa Watanzania wengine kuwa CCM wanaweza kusimamisha mtu yeyote hata malaika wao, na wanaweza kuwaleta wapiga debe wa kila aina lakini jimbo hilo halirudishwi tena CCM.

CCM haistahili jimbo jingine hata moja la ziada kwani wanavyo viti 271 ambavyo wamevikalia kwa fahari na matunda yake hatuyaoni. Wananchi wa Kiteto na sehemu nyingine zitakazofanya uchaguzi mwaka huu hawana budi kutambua kuwa, yawezekana mgombea atakayesimamishwa na CCM ni mzuri na anapendwa, na inawezekana ni mtu ambaye wanamfahamu hata hivyo, suala hili siyo la kuhusu wagombea. Suala ni chama cha mgombea.

Katika hili, CCM ni chama kilichoshindwa kupambana na ufisadi na kilichozowea mazingaombwe ya ahadi. Leo hii tunafanyiwa mazingaombwe tunashangilia ati “hatimaye Rais afanya kweli”, “Ati Rais aanza vitu vyake”. ‘Udanganyika’ mwingine mbaya. Miaka 46 sasa bado wanaanza? Amkeni wana na mabinti wa taifa hili, onesho limekwisha yote ni mazingaombwe!

Tunataka vitu vya kweli. Ni bora tuwe na wabunge 50 wa upinzani wanaotetea nchi kuliko wabunge 280 wa CCM wanaotetea chama chao! Bora tukipe chama kingine mbunge huyo wa Kiteto kuliko kuwaongezea CCM mbunge wa ndoto!

Niandikie: lulawanzela@yahoo.co.uk
 
Kuna wakati huwa nakaribia kukata tamaa ila nikisoma maandishi ya vichwa makini kama hiki basi nafarijika kuwa kuna watanzania wanaweza kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji.

CCM ndio mhimili mkubwa wa matatizo yote hapa. Wabunge wa CCM wapo tu kama hawapo na wengi wao wamelala usingizi pono kama vile hawajui kinachoendelea. Wanaojaribu kusema kidogo wanaitwa kwenye vikao vya chama na mzee wa kasungura na ndege ya kupaa ya richmonduli na kufungwa midomo.

CCM inabidi waondolewe na wajengewe gereza lao la kiguantanamo kule ukara katikati ya ziwa victoria ili mzimu huu ututoke. Kama vijana nao (kina Lugaza) wameanza kuingia kwa kasi katika hii list ya kifisadi? kama watoto wa mafisadi Ridhiwani na January nao sasa ni part ya serikali hii ya kifisadi? Kama watoto wa wakubwa ndio wanajazwa BOT kulinda siri za kifisadi? Hii nchi inabidi kitu kikubwa sana kifanyike kuvunja hii circle.
 
Kuna wakati huwa nakaribia kukata tamaa ila nikisoma maandishi ya vichwa makini kama hiki basi nafarijika kuwa kuna watanzania wanaweza kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji.

I love words.. I sure do.. na hapa bi mdogo umenigusa kumoyo.. yaani hiyo simile yako hapo juu imenifanya ubongo utetemeke kwa furaha.. "kuona moto katikati ya ukungu mzito wa theluji".. it is so oxymoronic..
 
Dk. Slaa amtumia makombora Mzindakaya (Tanzania Daima)

na Peter Nyanje, Dodoma na Irene Mark

MSEMAJI Mkuu wa kambi ya upinzani bungeni, Dk. Willibrod Slaa, amemtumia makombora mazito Mbunge wa Kwela, Chrisant Mzindakaya (CCM), akimtuhumu kuwa ni miongoni mwa wabadhirifu wanaodaiwa kulisababisha taifa hasara ya sh bilioni 9.7.
Dk. Slaa, alisema Mzindakaya alisababisha hasara hiyo baada ya kushindwa kulipa mkopo kutoka Benki ya Standard Charted, uliokuwa umedhaminiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), shutuma ambazo Mzindakaya alizikanusha jana jioni, akisema hakudhaminiwa na BoT, bali Serikali Kuu ndiyo ilifanya hivyo.

Msemaji huyo wa kambi ya upinzani bungeni, alitoa makombora hayo jana wakati akijibu hotuba ya Waziri Mkuu kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha katika ofisi yake na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMA) kwa mwaka wa fedha 2007/08.

Alisema malipo ya mkopo huo yanatokana na mkopaji kushindwa kulipa deni na kwa mujibu wa sheria, mdhamini wake ambaye ni BoT kulazalimika kulipa fedha hizo. Mbali na Mzindakaya, makombora hayo pia alitupiwa Gavana wa BoT, Daudi Balali.

Alisema, utafiti wa kambi ya upinzani unaonyesha kuwa, mwaka 2004, Mzindakaya alichukua mkopo wa sh bilioni 9.7 kwa ajili ya shughuli zake binafsi kutoka Benki ya Standard Charter kupitia Kampuni ya SAAFI na kudhaminiwa na BoT ambapo Gavana wa BoT ndiye mhusika mkuu katika tuhuma hizo.

Dk. Slaa alibainisha kuwa, hivi sasa, baada ya miaka minne ya deni hilo kutolipwa, BoT kama mdhamini, imewajibika kuilipa Benki ya Standard Charter fedha zinazotokana na kodi za wananchi.

“Mheshimiwa Spika, fedha alizokopa mheshimiwa Mzindakaya miaka minne iliyopita, alitumia kwa maslahi binafsi, lakini sasa zinalipwa na wananchi kupitia kodi na tozo mbalimbali kwa vile benki hiyo ni mali ya taifa,” alisema Dk. Slaa.

Aidha, alieleza faraja ya kambi ya upinzani baada ya Waziri wa Fedha, Zakia Meghji, kukiri kufahamu taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu ubadhirifu mkubwa ndani ya BoT unaomgusa gavana, wafanyabiashara wengine, akiwemo mbunge huyo (Mzindakaya) kupitia kampuni anayomiliki.

Wakati akijibu hoja za Waziri Mkuu, Dk. Slaa mara kwa mara alikuwa akikatishwa na baadhi ya wabunge waliokuwa wakitaka ufafanuzi wa masuala yaliyozungumza ama kuthibitisha kauli alizokuwa akitoa.

Waliomkatisha Dk. Slaa ni Spika wa Bunge, Samuel Sitta, Waziri wa Miundombinu, Andrew Chenge, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika na mbunge, George Simbamwene.

Spika Sitta, alimuonya mara mbili Dk. Slaa, akimtaka kurejea kujibu hoja iliyokuwa mbele yake na si kuzumgumza masuala mengine na iwapo angeendelea kufanya hivyo angemzuia kuendelea.

Wakati Dk. Slaa anaendelea kuchangia hoja, Mzindakaya alionekana akituma ‘vinoti’ kwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa na Spika Sitta.

Baadaye, Spika alisema mbunge yeyote anaweza kutoa hoja kama ameguswa na suala lililozungumzwa na akasema kwamba Mzindakaya ameomba apewe dakika 15 kabla ya kuahirishwa kwa kikao cha bunge kutoa hoja binafsi.

Akiendelea kuchangia, Dk. Slaa, alisema wakati akichangia hoja ya BoT, Juni 20, mwaka huu, Mzindakaya alitoa tuhuma nzito dhidi ya wabunge kwamba wanatakiwa kufanya uchunguzi wa jambo watakalolisema bungeni na kwamba takwimu za kwenye mtandao (internet) zilizotolewa na Dk. Slaa, kuhusu taarifa za Benki Kuu hazina ushahidi, na si sahihi.

Dk. Slaa, alinukuu kauli ya Mzindakaya aliyotoa bungeni kuwa: “Kama kuna mambo mazito na ambayo mbunge angependa kuyasema, mimi nafikiri kuhutubia habari za Internet haitoshi kuwa ndio ushahidi sahihi, kwa sababu baadhi ya mambo tunayoyafahamu sisi wengine tumefayafanyia ‘research’ (uchunguzi)… kwanza takwimu si sahihi.

“Takwimu sio dola milioni 200, ni dola milioni 131, ndio takwimu sahihi. Pili, baadhi ya wafanyabiashara wanaweza wakatumia ujanja wa kuwatumia wabunge waje wawasemee mambo yao au tofauti zao katika biashara. Na jambo hili linahitaji kuliangalia… bahati nzuri habari hii naijua kutoka kwa mhusika mwenyewe…”
Mwisho wa kunukuu.

Dk. Slaa, alisema: “Mambo kadhaa yamejitokeza na kwa kuwa yamesemwa bungeni, basi ni vema nikayazungumzia pia bungeni… kwa mujibu wa kanuni za Bunge, kifungu cha 49(7), mbunge hatakiwi kuzungumzia jambo lolote ambalo yeye mwenyewe ana maslahi ya kifedha nalo, isipokuwa baada ya kutaja jinsi anavyohusika, na kiwango cha maslahi hayo.”

Alihoji sababu ya Mzindakaya, kujikanyaga pale anapokiri kuwa takwimu sahihi ni dola milioni 131 badala ya dola milioni 200 ambazo ailitaka serikali ithibitishe ukweli kuhusu ubadhirifu huo.

“Au Mheshimiwa Mzindakaya, anaona ni halali kuibwa kwa dola milioni 131 ila siyo dola milioni 200? Kama takwimu zake zinathibitisha upotevu huo, ni vipi Mzindakaya anayejulikana hodari wa kulipua mabomu hapa bungeni na mtetezi wa wanyonge, leo awageuke na kuwa msemaji wa serikali katika kumtetea Gavana wa BoT?

“Kwanini Mzindakaya hakutamka lolote kuhusu maslahi yake katika jambo hili? Amekiuka kanuni ya bunge,” alisema.

Aliongeza kwamba, Mzindakaya ameomba mkopo mwingine wa sh bilioni mbili (hakutaja kutoka benki gani), lakini ameomba kudhaminiwa na BoT na kusema kuwa, mkopo huo upo kwenye hatua ya kujadiliwa.

Alisema, hatua ya kujadiliwa kwa ombi la Mzindakaya kunatoa nafasi kwa BoT ama kuidhinisha udhamini wake ama la.

“Mheshimiwa Spika, hapa ieleweke kuwa hatuzungumzii uhalali au vinginevyo wa mkopo wa Mheshimiwa Mzindakaya… tunazungumzia kukiukwa kwa kanuni ya Bunge na dhana anayotaka kujenga Mzindakaya, dhidi ya baadhi ya wabunge kwa wananchi, yote haya ni mambo mazito sana,” alisema Dk. Slaa.

Kauli ya Mzindakaya ilielekezwa kwa Dk. Slaa, kwa kuwa alinukuu taarifa ya Internet wakati akizungumza bungeni mwishoni mwa wiki na kwamba tafsiri ya Mzindakaya, inatoa dhana kuwa baadhi ya wabunge hawafanyi uchunguzi.

“Tafsiri ya Mzindakaya, inamaanisha kuwa baadhi ya wabunge ikiwemo mimi hatufanyi ‘research’ (utafiti) ila yeye tu ndiye anayefanya ‘research’. Hili ni tusi kwa Bunge na Watanzania waliotutuma tuwasemee, pia analenga kuupotosha umma kuwa, kuna wabunge wanaokurupuka na kusema mambo bila kufanyia utafiti.

“…Mheshimiwa Mzindakaya hajaeleza kwanini awe na mawazo hayo potofu, au kwa vile yeye ni tajiri na sisi wengine anadhani ni malofa, hivyo ni rahisi kuhongwa na kununuliwa?” alihoji Dk. Slaa na kuongeza.

“Lakini hata yeye utajiri mbona kaupata kwa fedha alizokopa kwa dhamana ya BoT, ambazo Watanzania wote matajiri na maskini sasa wanazilipa kwa kodi yao kupitia BoT?

“Tukisema Mzindakaya anasukumwa na fadhila aliyopewa na gavana kwa kumdhamini mkopo wake wa zaidi ya sh bilioni 9 na kulipiwa deni hilo halafu anataka gavana huyo huyo amdhamini tena mkopo wa sh bilioni mbili nyingine tutakuwa tumekosea?

“Kwa niaba ya kambi ya upinzani, nawaachia wananchi kutoa hukumu ya nani hafanyi utafiti kati yetu sisi na Mzindakaya anayelenga kuficha uozo wa ndani ya Benki Kuu… uzalendo hauna gharama, unahitaji dhamira safi,” alisema Dk. Slaa.

Alizungumzia pia suala la Kampuni ya Kagoda Agricultural Ltd, iliyosajiliwa Septemba 29, mwaka 2005 ambayo katika kipindi cha wiki nane ilipata fedha zaidi ya sh bilioni 30.8 kupitia External Service Debt Account na Benki Kuu, ambayo gavana ndiye msimamizi mkuu.

Alisema, taarifa hiyo inaonyesha kuwa mikataba tisa ilisainiwa kati ya Oktoba 18 na 19 mwaka 2005 na makampuni 12 ya nje chini ya mkataba na Kampuni ya Kagoda.

Aliongeza kuwa, ipo haja ya kufahamu undani wa kampuni hiyo na iwapo wamiliki wake waliorodheshwa kwenye daftari la BRELA, ama kuna vigogo nyuma yake.

Aidha, amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Jakaya Kikwete, katika kukabiliana na watumishi wabadhirifu, ili kupambana na vitendo vya rushwa.

Alisema, maswala hayo ni muhimu kwa mustakabali wa nchi yetu, na hivyo kambi ya upinzani inapenda kupata majibu ya kina na si majibu ya kisiasa ambayo hayana manufaa kwa taifa.

My Take:

a. Katika mazungumzo yake Bungeni Dr. Slaa hakudai mama Zakia hakujua kinachoendelea au kumhusisha na ufisadi na kwa hansard zinasema Bi. Meghji alikuwa anajua kuhusu tuhuma hizo na alikuwa anazifanyia kazi na lilikuwa ni jambo la faraja kwa kina Slaa. Sijaona bado ni wapi Meghji aliwakejeli kina Dr. Slaa au kusema BoT hakukuwa na matatizo!

b. C. Mzindakaya alipomsahihisha Dr. Slaa alisema kilichoopotea ni bilioni 131 na ukichukulia inflation si mbali na 133 zilizotangazwa na Ernst and Young. Sasa, kama Mzindakaya aliweza kupata data hizo ndani ya dakika chache, kwanini kuchunguza tena?

c. Kama Mzindakaya alijua ufisadi wa BoT na hakufanya lolote au hata kutaka tume iunde au kuibua bomu hilo kubwa kwanini na yeye asiunnganishwe katika msururu wanaotakiwa kujiuzulu. Kama Mbunge alijua umefanyika upotevu na yeye akaufumbia macho, na yeye ni mshirika wa ufisadi! Ajiuzulu!
 
Nakwambia huu mzimu wa wizi wa BOT utawasumbua sana wote wanaohusika na hii case hadi washangae.

Poor Mzee wa Mabomu mzindakaya naye kahusishwa big tyme na sasa yameanza kugonga chupi na kurudi!
 
Nimrod Mkono naye ni fisadi mwingine kwa kulipwa shilingi bilioni 8 wakati hakuna alichokifanya. Wote hawa wfilisiwe mali zao ili kuhakikisha ufisadi unatokomezwa kabisa Tanzania.
 
Dr Slaa sasa anatafuta balaa mizimu ya Sumbawanga haiogopi huyu?

Unapoamua kuwa mtetezi wa wanyonge na kuhakikisha haki inatendeka basi hata mizimu au hirizi haziogopwi.
 
Mzindakaya alifungua kiwanda kikubwa cha ku-process nyama huko Rukwa. JK alishiriki katika kukizindua na kumsifia ujasiariamali wake. Mkopo wa kufungua kiwanda hiki ulidhaminiwa na BOT. Isije ikawa ni hizi pesa zinazoongelewa hapa. Link hii inahitaji kufatiliwa.
 
Yup ndizo zenyewe kabisa na mengine mengi yakifuatia,.....
 
Huyu Dr. Slaa ni mwanaume kweli kweli. Mzindakaya hata biashara hajui, utamkopeshaji hizo bilioni karibu tisa? Sasa zote zimepotea na anaomba zingine, balaa tupu.

Mwanakijiji, nafikiri unamuelewa Dr. Slaa, yeye ni makini na anamfunga kengere mmoja mmoja. Siku ya Meghji ni Meghji, Mzindakaya ni Mzindakaya, itafika siku ya Mramba, Mkapa na wengine.

Anachokiongea hata mkulima wa Sumbawaga anaelewa.
 
Dotori:
Aliyezindua na kutoa misifa ni Benjamin; sio Kikwete.

Jaman, kuna swali alilouliza Mbunge na Meghji akakaaa kulijibu.

Pesa ya kjengea minara miwili BOT ilizitoa wapi? Isije ikawa ni pamoja na hizi tunazozipigia kelele humu!!
 
Kuna thread nilisema sana juu ya Mzindakaya na pesa hii . Alipewa in USD na wala si Tshs . Yeye Mkurugenzi , Mwanae Accountant na Mkewe Manager sasa hakuna kitu . Unadhani anaweza kuacha kuitetea BOT ? Nilisha wapa data hapa zifukueni mtaona hao this man alipata pesa hii na kupitia mikono ipi .
 
Kalamu, swali lilijibiwa japo kwa kujiuma uma kwa taarifa alizopewa. As a matter of fact, naamini lile jibu alilopewa akaja nalo baadaye alidanganywa tena na yeye akalidanganya Bunge. Ninayo hotuba ile kwenye podomatic kwenye archives unaweza kusikiliza..

Hakukataa kujibu, hakuwa na jibu kwani swali lilikuwa na mtego muhimu sana.
 
I have no idea wangu.. I just had to use it ili na mimi nionekane sikukimbia umande.. labda Pundit anaweza kutusaidia..
 
damn mafisadi,yaani watu wamejichotea mpaka unashindwa kuamini,kuanzia TRA,BOT,Wizarani ni ufisadi kwa kwenda mbele na hawana huruma sasa nimeamini chukua chako mapema wako in mission,lakini kidogo kidogo na watu kama hawa kina Slaa tutafika tuu na huyu mama Meghji asilete za kuleta maana wizi ulitokea akiwa ndio boss pale na hakufanya kitu zaidi ya kujidai sasa nilifanya this & that,na bila kina Slaa kulipua tusingejua chochote,huyu mama inawezekana hakuchukua kitu lakini aende tuu maana kazi imemshinda...wametuibia migodi na mikataba fake haikutosha sasa naona wameingilia mpaka account za nchi,ama kweli nchi imejaa mafisadi na lazima waondoke na walioiba lazima wazirudishe,lakini kazi moja tuu wananchi wanayoweza kufanya kuzuia haya mafisadi ni kuyapiga nje wakati wa uchaguzi la sivyo itakuwa kazi bure,lakini tume yetu ya uchaguzi nao ndio engineers wa wizi wa kura yaani sijui tutaponea wapi na haya mafisadi
 
Yaani nakuambia kama kungekuwa na maombi ya kumwomba Mungu afute generation nzima, ningekuwa wa kwanza kufunga siku arobaini au zaidi ili kizazi hiki cha mafisadi na watoto wao kipoteee kabisa na tuanze upya!

Grrrrrrrrrrrrrrrrr
 
Back
Top Bottom