Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 1,900
- 944
MBUNGE TAUHIDA NYIMBO - TUFIKIE WAKATI MTU KUTOKA BARA AENDE KUWA RAIS ZANZIBAR
"Ufike wakati tutamani kuona mtu kutoka bara na kwenda kuwa Rais wa Zanzibar tuipelekeni Tanzania huko itikadi za kisiasa tusiivunje Tanzania kwani upande wetu ndiyo umoja wetu" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi
"Maamuzi yanayotolewa ni kwa maslahi ya nchi na si kwa maslahi ya mtu, haiwezekani zaidi ya wabunge 300 tuone kitu kinachofanyika ni cha hovyo na tukakiridhia hicho kitu hakiwezekani abadani" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi
"Makubaliano haya hayana chembe ya shaka, Watanzania ifike wakati tuamke tujue hizi kelele zinatoka wapi, hakuna vita kubwa kubwa duniani kama ya vita vya uchumi" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi
"Kuna maeneo na vipengele vilikuwa na vihisia kwamba haviko sawa lakini niwatake Watanzania waondoe hofu serikali yao iko makini na viongozi wao wako makini ripoti zote zimepitiwa" - Mhe. Tauhida Cassian Gallos, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi.