Mbunge Tauhida akabidhi Vifaa vya Ofisi Shule za Kijitoupele na Bububu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,898
943
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mjini Magharibi (UWT) amefanya ziara na ametembelea Shule ya Msingi Kijitoupele na Shule ya Sekondari Bububu kwaajili ya kugawa vifaa mbalimbali vya Ofisi katika shule hizo zilizopo Mfenesini.

Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo ameambatana na viongozi mbalimbali wa UWT Wilaya na UWT Mkoa akiwemo Mwenyekiti na Katibu UWT Mkoa na Wilaya na Madiwani wa Wilaya ya Dimani na Mfenesi katika kukabidhi vifaa vya Ofisi mashuleni.

Vifaa vya Ofisi alivyokabidhi Mbunge Tauhida ni pamoja na Kompyuta, Madaftari, Peni, Vitabu, Karatasi (Rimu Paper) kwaajili ya matumizi ya Ofisi Shuleni Kijitoupele na Bububu ambavyo vimepokelewa Mwalimu Mkuu wa Shule katika shule alipotembelea.

Akizungumza baada ya kukabidhi vifaa hivyo Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo amesema kuwa lengo la kukabidhi vifaa ni ili kuwasaidia kuboresha sekta ya Elimu mashuleni hususani matumizi ya TEHAMA.

Kwa upande wao Walimu Wakuu na Walimu wengine walihudhuria hafla ya makabidhiano ya vifaa vya Ofisi mashuleni wamemshukuru Mbunge tauhida Cassian Gallos Nyimbo na kumuomba aendelee kuwa na moyo huo huo wa kuziwezesha shule vifaa vya kujifunzia

Mhe. Tauhida Cassian Gallos Nyimbo ameahidi na kusema kuwa Elimu ni kipaumbele muhimu sana kwa watoto ambao ni Taifa la kesho hivyo hataacha kuwasaidia kama Kiongozi anayewajibika katika kushiriki kutatua changamoto katika sekta ya Elimu.

WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.23(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.18.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.12(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.16(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.20.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.23.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.25.jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.24(1).jpeg
WhatsApp Image 2023-07-21 at 15.47.18.jpeg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom