Ufahamu wa kuzidiwa kwa CCM, ni kama wanatoa buriani kwa wananchi

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,946
3,820
Bado kuwaachia mashehe wa Kiislamu tu, sasa tunaona CCM wanajitahidi kuweka na kuziba au kutia viraka sehemu zao,mara walimu, mara pembejeo, mara afya, mara 'ishuwarensi'. Yaani wanahangaika na kurusha madaluga vibaya sana. Walikuwa wapi tokea tupate Uhuru, walikuwa wapi miaka mitano iliyopita?

Hivi ni nani kawakurupusha, je ni wapinzani? Hapana ni wananchi; wananchi wameamka na wanatamka waziwazi sio kuwa hawampendi Magufuli, hapana wanampenda sana ila mahali alipo wananchi hawapo. Wananchi hawaitaki CCM hata kuiona, wameteseka wanaendelea kuteseka na haitokaa sawa milele hata mashehe na mapadire wanapokuwepo CCM huwa na roho mbaya sana ni hatari.

CCM imepoteza muelekeo, hili halitaki tochi kuliona. Sasa sasa ni wakati muafaka CCM inaondoka mdomo wazi.

Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali
Kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili

Kwaheli CCM, ni kweli umetoka mbali
 
Sema wanakaa kimabavu walishakataliwa zamani na walala hoi labda wanasubiri vyombo vingine viwakatae,unajua kwa sasa CCM ni kama wavamizi au tuseme himaya flani hivi imehodhi sehemu nyeti za nchi kama tujuavyo wameiteka Tume ya uchaguzi kabla hata uchaguzi bado.Tukitaka tusitake tume ya Uchaguzi imetekwa na ccm.
 
Ukweli ni kwamba ccm ni genge la walaji wanaotumia nafasi zao kujinufaisha bila kufanya chochote cha maendeleo kwa taifa, tuwapumzishe.
 
Mkuu umeandika vizuri kipindi flani niliwai andika hum kwamba jpm agombee 2020 pitia upinzani ,na awaachie ccm chama Chao wasemacho kina wenyewe ,ila may be sikueleweka, ila hoja ilikua watu wameichoka ccm, barikiwa Sana mkuu
 
Ukweli ni kwamba ccm ni genge la walaji wanaotumia nafasi zao kujinufaisha bila kufanya chochote cha maendeleo kwa taifa, tuwapumzishe.

Ndani ya hilo genge la walaji kuna wahujumu uchumi, mafisadi, majangili, wachawi, waganga wa kienyeji, wachungaji feki, wanafiki, wachumia tumbo, nk.

Kuna ulazima wa kuliondoa hili genge la wa walaji haraka iwezekanavyo. Kwa njia yoyote ile.
 
Back
Top Bottom