Ujue undani wa ugonjwa Degedege unavyoshabihiana na ‘mbia’ Kifafa

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Kuna maradhi Degedege na Kifafa, huwa yanawaingiza Watoto na watu wazima katika hatari, yakionekana kwa sura tofauti, kulingana na hali ya mgonjwa.

Kuna kundi la wanajamii wanaunganisha na ushirikina. Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Watoto Hospitali ya Rufani Mkoa Temeke, Salha Ally, anataja Degedege ni dalili ya mvurugano katika ufanyaji kazi wa seli za ubongo (neurons) zinazowasiliana kwa njia kama mtiririko wa umeme.
degedege1 ED.jpg
Anasema, iwapo inatokea tofauti yoyote katika ufanyaji kazi wa seli hizo za ubongo, zinakosa mtiririko huo wa asili na kusababisha Degedege.

Dk. Salha anafafanua sababu zinazochangia; ikianza na kuwapo jeraha katika ubongo, linalokuwa sababu, hasa mtoto anapozaliwa.

Pia, anasema Degedege inahusishwa na mabadiliko ya muda mfupi katika ubongo kama vile joto kali, matumizi ya dawa za kulevya, viwango vya juu vya sukari na sodiamu katika damu, hata kuwapo uvimbe katika ubongo.

Suala la saratani ya ubongo, matatizo ya ini na figo (matatizo ya kimetaboliki) kama vile ugonjwa wa kukojoa kiwango kikubwa zaidi, hasa aina fulani ya tindikali ya amino, kwa watoto umri chini ya mwaka mmoja.
degedege-ulyclinic.jpg
Degedege la Homa;
Dk. Salha anataja inawatokea kila mara watoto, akiitaja inatibika na kupona kirahisi, kuliko nyinginezo. Pia, inatajwa inaweza kuashiria hatari ya maambukizi ya bakteria mwilini (sepsis) au katika ubongo wa mtoto.

Anafafanua, Degedege hiyo inasababishwa na magonjwa kama vile malaria, mashambulizi ya vimelea katika njia ya hewa, maambukizi kupitia chakula, vilevile maambukizi kwenye mkojo (UTI).

Dk. Salha anasema inawapata wenye umri kati ya miezi 6 mpaka miaka mitano, huku walio na umri miezi 14 mpaka 18, ndio wanaoongoza kuathirika.

Anasema tafiti zinaendelea kuchambua uhusiano kati ya homa kali na Degedege, ingawa baadhi ya wanasayansi wanahusisha na sababu za kijenetiki.

Kunatajwa Degedege lingine linalohusu kupanda ghafla joto mwilini kufikia sentigredi 39 au zaidi, ikidumu chini ya dakika 15, mtoto anatawaliwa na kizunguzungu. Hiyo hutokea wastani mara moja kwa saa 24 na haisababishi jeraha la kudumu katika ubongo.

Degedege la homa lisilo rahisi; hilo linadumu kwa zaidi ya dakika 15, ikihusisha sehemu za mwili wa mtoto na inatokea zaidi ya mara moja katika saa 24, ikiwa na uwezekano mkubwa kusababisha kifafa, siku za baadaye.

Degedege lisilo na homa; hiyo haiambatani na homa za kila mara, ila inaashiria kuwapo tatizo katika ubongo, ikisababishwa na mtiririko mkali wa mawasiliano kati ya seli za ubongo kuwa na kasi kubwa. Huwa na tabia ya kujirudia.

Dk. Salha anashauri, mgonjwa kupimwa kiwango cha madini mwilini hasa sodiamu, sukari, au sumu. Ikitokea mara mbili au zaidi kwa saa 24, ni ishara ya ujio wa kifafa.

Degedege la upande mmoja mwilini; hujitokeza kwa kuhusisha sehemu ya ubongo na ishara ya sehemu tu ya mwili inaonyesha dalili zake.

Aina hiyo hutokea kwa namna mbili; mtoto anaweza kupoteza fahamu asijue kinachomtokea, pasipo kupoteza fahamu.

Vilevile kuna wakati inakuwa vigumu kutambua aina hiyo ya Degedege, kwa sababu huchukua muda mfupi, wastani sekunde 10 hadi 20 na kuna wakati mtoto anaweza kuongea, wakati Degedege inaendelea.

Hapo huhusisha kucheza misuli usoni, shingo au sehemu za mikono hata mzazi asitambue. Ili kutofautisha na michezo, Degedege inapoanza, mtoto hawezi kuizuia mpaka imalizike, hata kama mzazi utamwambia aache.

Degedege mwili mzima; Sehemu kubwa ya ubongo huathirika na matokeo mwili wote, kuonyesha dalili anaumwa akipoteza fahamu.

Dk. Salha anaieleza kwa namna mbili; Degedege potevu, ambayo ni nadra kwa mtoto chini ya miaka mitano, zaidi ikiwahusisha wasichana na haidumu zaidi ya dakika moja.

Mgonjwa huwa hafahamu, bali anaduwaa asifanye chochote kwa sekunde kadhaa, kabla ya kurudiwa na fahamu akaendelea na shughuli zake za awali na humtokea mtoto mara nyingi kwa siku, ila nguvu ya misuli haipotei.

Degedege ya kifafa; ni zaidi kwa watoto na inakuwa na kiashiria cha muda mfupi kabla ya kuanza. Mtaalamu anasema, kuna viashiria vinatofautiana kati ya mtoto mmoja na mwingine, ikijenga hisia kitu kinatembea mwilini, kichefuchefu, harufu, kichwa na tumbo kuuma, kuhisi woga na mabadiliko ya ladha mdomoni.

Watoto wenye Degedege, wanakuwa na viashiria vinavyowapata na inakuwa rahisi kwao kukimbia, kuliko salama kabla ya Degedege kuanza.

Madhara yalivyo, mtoto anapopoteza fahamu, wengine hutoa sauti na kugeuza macho au kuchezesha misuli ya mwili mzima ikikamaa.

Wakati Degedege kwa mtoto, anaweza kuung’ata ulimi, kukojoa na wakati mwingine haja kubwa. Baada ya Degedege, mhusika anadumu na hali hiyo kwa dakika kadhaa, anabaki katika usingizi, takribani nusu saa au zaidi.

Degedege la wachanga; inatajwa kuwapata zaidi wenye umri chini ya siku 28, kwa sababu mbalimbali kama maambukizi ya vimelea vya magonjwa, matatizo ya kimaumbile na sumu mwilini.

Mara nyingi wanakuwa kama wanatafuna kitu, wakati mwingine macho kuyaelekeza upande mmoja bila ya kuyachezesha huku wakiwa wamekakamaa, pia wanaweza kuchezesha miguu kama wanaendesha baiskeli, vilevile kujionyesha kwa kubadilika rangi, au kutopumua kwa muda.

Degedege linalodumu; ina hiyo inatajwa ni hatari zaidi na Degedege humpata mtoto kwa zaidi ya dakika 30, pasipo fahamu zake.

Dalili za Degedege huonekana katika sehemu tofauti mwilini, ikihusisha sehemu mojawapo mwilini, kwenye misuli ya upande kucheza, kukakamaa au inaweza kuhusisha mwili wote.

Pia, inatajwa kuambatana na kupotea fahamu kwa mtoto. Kuna baadhi ni ngumu kutambua inapotokea na Degedege hutofautiana, kutegemea na umri wa mtoto.

Mtoto anapoteza fahamu, akiwa katika hisia kama za woga na hofu isiyoelezeka, ikijenga furaha iliyopitiliza au kicheko kisicho na maelezo.

"Ni ugonjwa unaofanana na Degedege. Kifafa kinasababishwa na seli katika mishipa ya fahamu kwenye ubongo zinazotoa umeme, mwingi kuliko kawaida, kwenda kwenye misuli na sehemu zingine za mwili.

"Hiyo inatajwa kusababisha mtu kupata dalili kama za kuishiwa nguvu, kichwa kuuma sana, kuchanganyikiwa, mwili kukamaa na hata kupoteza fahamu.

"Dk. Salha anasema ugonjwa chanzo chake kikuu hakifahamiki, ila kuna sababu kama urithi kifamilia; ajali inayodhuru mishipa ya fahamu; kuugua muda mrefu mfumo wa ubongo ukapoteza uwezo; uvimbe kwenye ubongo, kiharusi, pia magonjwa ya uzeeni.

"Aina za kifafa, zinatajwa ni ya mtu anakakamaa mwili mzima na akipoteza fahamu, kutoa povu au kupata hajakubwa na ndogo bila kujitambua.

"Pia, kuna ambayo mgonjwa hapotezi fahamu wala hakakamai, bali anapatwa na hali fulani ya bumbuwazi kwa dakika kadhaa, kizunguzungu na kichwa kuuma.


Chanzo: IPP
 
Back
Top Bottom