Kifafa kwa mtoto-msaada

TUKUYU88

Member
Jul 25, 2022
63
196
nina mtoto wangu ambaye anasumbuliwa na kifafa kila apatapo hom kali au sometime homa ya kawaida tu.

ilianza akiwa na miaka miwili. alivyofika miaka minne hali ni kama ilizidi kidogo. nilifanikiwa kuonana na daktari bingwa wa watoto ambaye alinishauri nianze kumpa dawa ya SODIUM VALPROATE mg 100 daily kwa muda wa mwaka mmoja. na endapo hatapata hali hiyo kwa muda huo hali itakuwa imetibitika.

nilifuata ushauri wake na mwaka jana mwezi wa kwanza (january 2022) alianza kutumia dawa mpaka january 2023. kwa muda wote huo ni kweli hakupata hiyo hali kabisa. shida imeanza tena mwezi huu wa pili ameanza tena kupata kifafa. kama mzazi naumia sana😭😭😭. naombeni msaada kwa mwenye ushauri wa namna ya kunisadia.

MUNGU awabariki wote watakaoguswa na tatizo langu
 
Rudi kwa daktar,jaribu kuchukua muda umuelezee history ya mtoto tangu akiwa tumbo ni ,alpozaliwa km kuna ajali zozote alizowahi kupata kwenye makuzi yake,kama kuna matumizi ya dawa ya muda mrefu n.k .Pole
 
ahsante. nimerud kwa daktari kanishauri kuendelea kutumia dawa alizokuwa anatumia. but ninachoogopa ni je atatumia dawa hizo mpaka lini?
 
Mapito ya mtoto ni mapito ya mzazi najua unavyoumia, maombi yangu kwa Mungu juu yako ni ipatikane tiba kwa mtoto wetu.
Naamini wataalamu watakupatia ufumbuzi.
 
Pole sana mkuu..
Nenda kwa neurosurgeon wamfanyie ct scan maybe na mri kuona source ya kifafa kwenye ubongo kama hakisababishwi na homa pekee.
Once again, pole
 
Pole sana
Najua yanayokusibu kama mzazi
Ila utapata ushauri wa kila aina mara utaambiwa ana uvimbe kwenye kichwa

Ila usikubali na hata kufikia maamuza ya operation mpaka upate Dr wa watoto tena mzoefu

Mkuu waganga wengi huwa wanafananisha magonjwa walioyasoma
Sasa unakuta anakuambia tumia dawa hizi miezi 6 au mwaka
Halafu unaenda kwa mwingine anakuambia tupa yote Anza na hizi
Usikate tamaa kupata ushauri kwa Dr tofauti
Mara watakuambia mtoto mwehu, mara kifafa cha tumbo, mara malaria sugu

Yaani kila mmoja na lake

Wakikuambia ni hernia usikubali haraka haraka tafuta ushauri sana kwa Dr maarufu wa watoto especially wazee ndio wana experience zaidi nionavyo mimi
Pole sana namuombea mtoto sana na nyie pia
 
Wewe mwenye mtt upo mkoa gani. Huo ugonjwa huwa hautibiwi hospital nikuambie labda. Nimekuuliza uko wapi Mana inatakiwa uwe karibu na nilipo. Huo Ni ugonjwa wa watoto unatokea huko haja kubwa Kama Kuna namna ya wanajikuna. Ujue hii sayansi ya wazungu imekuja kuharibu dawa zetu ili wapate Kodi.

Kama utaweza labda tuongee mie naweza nikakusaidia bila hata ya hela yako jamani.

Hizo dawa kwa jamii huwa wanazijua mno na easily available yaani miti unachuma tu sijui unachemsha unampatia. Hata mke wangu huwa namuona anawapa wanangu.

Yaani wale bacteria wa asili walioko mwilini wengine huwa wana grow abnormally sijui Kama iyo English utaielewa. Sijui ndio wengine wanaita mchango.
Yaani iyo hospital hupati dawa mpaka India uk USA France German s Korea and Japan .

Naweza hata nikakupa namba ya mke wangu anaweza akakuelekeza sio kuwa ndio kazi zetu ,Ila Ni sawa tu unasaidiwa Basi.

Nimekuuliza uko wapi Mana inaweza ikachemshwa wanangu wakainywa na mwanao akainywa ukiwa hapa hapa karibu
 
Pole mkuu kwa hiyo changamoto ya mtoto wako
Kama ni kifafa basi nakupa hii tafuta mmea flani unaota juu ya miti yaan haina mizizi ni juu kwa juu maarufu kama nguruka au ngurukila zipo aina 2 ila inayotibu ni ile yenye majani mapana siyo yenye majan madogo angalia alafu twanga loweka mfano ukiloweka asubhi atainywa mchana na ukiloweka mchana atainywa usiku hivyo ataitumia ndan ya sku 10 Mungu atamsaidia atapona ikiwa tofaut utarudi hapahapa
 
Naweza PATA hata picha yake mkuu? Ili niweze kuutafuta?
 
Wewe mwenye mtt upo mkoa gani. Huo ugonjwa huwa hautibiwi hospital nikuambie labda. Nimekuuliza uko wapi Mana inatakiwa uwe karibu na nilipo. Huo Ni ugonjwa wa watoto unatokea huko haja kubwa Kama Kuna namna ya wanajikuna. Ujue hii sayansi ya wazungu imekuja kuharibu dawa zetu ili wapate Kodi.

Kama utaweza labda tuongee mie naweza nikakusaidia bila hata ya hela yako jamani.

Hizo dawa kwa jamii huwa wanazijua mno na easily available yaani miti unachuma tu sijui unachemsha unampatia. Hata mke wangu huwa namuona anawapa wanangu.

Yaani wale bacteria wa asili walioko mwilini wengine huwa wana grow abnormally sijui Kama iyo English utaielewa. Sijui ndio wengine wanaita mchango.
Yaani iyo hospital hupati dawa mpaka India uk USA France German s Korea and Japan .

Naweza hata nikakupa namba ya mke wangu anaweza akakuelekeza sio kuwa ndio kazi zetu ,Ila Ni sawa tu unasaidiwa Basi.

Nimekuuliza uko wapi Mana inaweza ikachemshwa wanangu wakainywa na mwanao akainywa ukiwa hapa hapa karibu
Nipo mbeya mkuu. Wewe uko wap?
 
Nipo mbeya mkuu. Wewe uko wap?
Mbona ulipotea mno Sasa. Ama uliweka ukakimbia ama mtt alizidiwa.
Mie Niko mwanza naa iyi dawa ama miti itabidi itoke Tarime ndio home,naongea na mama anachuma majani ama miti fulani mkuu ambayo hata ukiwa unachunga nadhani mifugo inayala so ni rahisi ivyo tu.
 
Sorry mkuu nilikuwa kwenye mahangaiko tu ya hapa na pale. Nipo tayari hata kuifuata kiongozi Kwa sababu nataman Sana mwanangu apone hili tatizo
 
Ngoja Basi nipe namba yako naweza nikampatia mke wangu ama mama mzazi ataongea na wewe ili uniambie hizo dalili ahakikishe kabla ya wewe kusafiri. Mana wao ndio wanaojua. Sie nakumbuka tunapewaga tu madawa tunakunywa wababa wako shambani. So unajua anayelea vifaranga.
Namba yako pm ,useme muda gani uko POA ili uongee vizuri uwaambie dalili za mtt Ila najua Kama ndio wenyewe sema kuhakiki.
Kama Ni wenyewe Kama Hakuna Mambo mengi naweza nikakutumia kwa Basi Mana mie Niko hapa town nauli kwa hiace Ni 600 mpaka town na kurudi Ni 600 ndio gharama. Na huko gharama utawalipa ukiipokea. Ukishapokea utapata namna ya kumpa Ila Kama pia unapenda uje naye hapa ili tunywe wote hata wanangu wanainywa hakuna nouma. It's up to you
 
Back
Top Bottom