Ufahamu mradi mkubwa wa umeme wa Rufiji

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
UFAHAMU MRADI WA ’STRIEGLER'S GORGE

Mradi wa umeme wa ‘’STRIEGLER'S GORGE’’ uliasisiwa na marehemu baba wa Taifa Mwl Julius Nyerere miaka 1970. Mwalimu Nyerere alianzisha wazo la kujenga mradi huu mkubwa ili kuondoa tatizo la umeme nchini lakini pia ili kuongeza tija ya uzalishaji viwandani. Ni miaka zaidi ya 40 sasa toka tafiti ya kuzalisha umeme katika maporomoko ya mto rufiji maarufu kama "Strigler's Gorge" kufanyika.

Wapo waandishi ambao wamejaribu kuzungumza kinagaubaga juu ya historia fupi ya asili ya jina la Strigle’s Gorge wakihusisha na mambo mengi. Kwa mujibu wa Kitabu cha Tanzania The Limits to Development from Above, ambacho kimeandikwa na Kjell Havnevik, kimeainisha kuwa asili ya jina hilo ni kutokana na tukio la mwaka 1907, ambapo Stiegler alikanyagwa kanyagwa na tembo hadi kufariki dunia. Wao wanadai kuwa Stiegler akiwa mawindoni katika pori hilo alikanyagwa na tembo hadi kufariki na mwili wake kukutwa kwenye maporomoko yam to huo.

Hata hivyo, vyanzo vingine vinadai kuwa, Stiegler hakuuawa na tembo, bali alianguka kwa bahati mbaya ndani ya bonde hilo na kupoteza maisha.Kwa ujumla simulizi ya kifo cha Stiegler katika eneo hilo la maporomoko ya maji ya Mto Rufiji ndiyo iliyozaa jina Stiegler’s Gorge.Mtandao wa Kimataifa wa Africantourer unaelezea Bonde la Stiegler’s Gorge kuwa linafanana kwa ukaribu na lile la Canyon la nchini Marekani.Africantourer unatanabahisha kuwa, Stiegler’s Gorge ni sehemu ya Mto Rufiji ndani ya Pori la Akiba la Selous. Eneo hilo linatajwa kama ‘mpalio mwembamba’ wenye urefu wa kilomita 8, upana wa mita 50 na kina kutoka kilele chake cha maji ni mita 100.

Mradi huu ambao unajengwa katika maporomoko ya mto Rufiji ndani ya hifadhi ya Selous ulikuwa ukipingwa na baadhi ya taasisi zinazoshughulika na hifadhi za mazingira,ekolojia,utamaduni na wanyama pori hasa WWF na hata UNESCO.Hoja kubwa waliyokuwa wakitoa wadau hawa wa mazingira na uhifadhi na hata wanaekolojia ni kuwa endapo Tanzania itatekeleza mradi huu mkubwa wa umeme basi mambo yafuatayo yanaweza kutokea.
Kwanza walidai mradi huu utapelekea kukauka kwa vyanzo vya maji ndani ya mto rufiji ambayo hutegemewa na wanyama kwenye pori hilo na nje ya pori hilo hivyo kuathiri sekta ya utalii.

Pia wanadai mradi huu utapelekea kupungua kwa rutuba katika ardhi na mazingira ya delta ya mto rufiji hivyo kuathiri kilimo.

Wadau hao wa mazingira na ekolojia walidai pia mradi huu utasababisha kupungua kwa samaki hasa wale aina ya "Kambakochi" na wengine wanaopatikana eneo hili hivyo kuathiri maisha ya wananchi wengi wanaopakana na eneo hili.

Pia walidai mradi huu utapelekea mmomonyoko mkubwa wa ardhi ambao ni hatari kwa mazingira ya eneo hilo.
Lakini tafiti zingine zilizofanyika duniani zimeonyesha kuzalisha umeme kwa njia ya maji ni salama zaidi kwani kutasaidia kutunza mazingira, lakini pia kuna faida kiuchumi kwetu kwa kuwa unatumia gharama kidogo kuliko kuzalisha umeme kwa njia nyingine yeyote ile.

Utafiti uliofanywa miaka ya sabini na mwanzoni mwa miaka ya themanini (1978-1980) na Shirika la Kuendeleza Bonde la Mto Rufiji (RUBADA ) kwa kushirikiana na kampuni ya kigeni ya M/s Norplan/Hafslund, ulionyesha kuwa mradi wa Stiegler’s Gorge una uwezo mkubwa wa kuzalisha umeme mwingi wa maji (hydro-power) zaidi ya umeme ambao Tanzania inahitaji.Matokeo ya utafiti huo pia yalionyesha kuwa mpalio wa Stiegler’s Gorge una uwezo wa kuhimili mitambo mitatu mikubwa ya kuzalisha umeme.

Mh Rais Magufuli baada ya kuzingatia mambo mengi hasa faida za mradi huu ndipo aliamua kufanya maamzi sahihi ambayo watangulizi wake wote hawakuweza kufanya. Mh Rais alifanya maamzi haya baada ya kuona mradi huu ukitekelezwa utazalisha umeme megawatt zaidi ya 2100 yaani umeme mwingi kuliko tulio nao sasa. Umeme huu unakuja kumbeba zaidi mtanzania wa chini ambaye alikuwa akinunua umeme kwa bei kubwa. Kukamilika kwa mradi huu maana yake Tanzania itaizidi Kenya ambaye ni kinara wa kuzalisha umeme Afrika mashariki akizalisha megawati zaidi ya 2250 huku raia wake asilimia 64.5% wakipata huduma hii kwa uhakika.

Kwa mfano ukizalisha umeme kwa njia ya maji kila uniti moja itagharimu kiasi cha shilingi 36 wakati kuzalisha umeme kwa njia nyingine gharama huwa juu zaidi. Kwa mfano, umeme wa nyuklia kila uniti moja inagharimu shilingi 65,umeme wa jua na upepo kila uniti moja hugharimu shilingi 103.05,umeme wa makaa ya mawe kila uniti moja hugharimu shilingi 118,umeme wa gesi kila uniti moja hugharimu shilingi 147 na umeme ghari zaidi ni ule wa mafuta ambapo kila uniti moja ugharimu shilingi 426 . Hapa kwa logic tu ya kawaida utaona namna mradi huu mkubwa utakavyotusaidia.

Katika tafiti zilivyofanyika hivi karibuni Tanzania ni miongoni mwa nchi zinazozalisha umeme kwa gharama kubwa sana kwa uniti moja ukilinganisha na nchi nyingine.Kwa mfano, Tanzania hutumia dola za marekani senti 10.7 kwa uniti moja huku nchi nyingine mfano Misri 4.6,Afrika Kusini 7.4,Ethiopia 2.4, na India 6.8.

Leo hii linapotajwa jina la Stiegler’s Gorge, fikra za Watanzania zinajielekeza kwenye faida moja tu ambayo ni ukombozi wa uchumi wa taifa hili.Faida hiyo si nyingine, bali ni nishati ya umeme. Kama ambavyo Rais Dk. John Magufuli amekuwa na shauku ya kutengeneza bwawa la maji kwenye bonde hilo, ambalo litakuwa na uwezo wa kuzalisha megawati 2,100 za umeme.Kusudio hilo si geni, bali ni mwendelezo wa kutimiza dhamira ambayo aliiweka Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, takribani miongo minne iliyopita.

Mwali Nyerere alikuwa na wazo la kujenga bwawa la umeme katika eneo hilo ili kusaidia nchi kupata umeme wa kutosha.

Stiegler’s Gorge, ambayo kwa mujibu wa taarifa ya satellite inapatikana umbali wa kilomita 185 kutoka jijini Dar es Salaam, kwa sasa inaangaliwa kama kitovu kitarajiwa cha kuimarisha mzizi mkuu wa uchumi wa nchi huko tuendako.Kama mradi huo utakamilika utazalisha umeme maradufu ya unaozalishwa sasa na mazingira hayo yatasaidia kupatikana umeme wa uhakika kwa nchi nzima.Kwa muktadha huo, dhamira ya sasa ya Rais Magufuli inakusudia kuwapo kwa nishati ya umeme inayojitosheleza ili kukidhi dira ya Serikali ya kujenga uchumi wa viwanda ambao ni mhimili mkubwa wa lengo la nchi kuingia kwenye mfumo wa uchumi wa kati kwa nchi.Katika kutimiza dhamira ya mradi wa uzalishaji mkubwa wa umeme kutoka kwenye Bonde la Stiegler’s Gorge, Rais Magufuli amesisitiza umuhimu wa kujenga bwawa la kuzalisha umeme kwenye eneo la Stiegler’s Gorge.

Pamoja na hayo lakini pia mradi huu hadi kukamilika kwake pia utaleta faida nyingi. Kwa mfano Waziri Kalemani akiwakabidhi wakandarasi aliwahi kusema faida zifuatazo ambazo pia zitatokana na mradi huu.
Dk. Kalemani alitaja manufaa ya mradi huo ikiwamo kuifanya nchi kuwa na umeme wa uhakika na wa kutosha utakaosaidia maendeleo ya uchumi wa viwanda na maendeleo endelevu ya wananchi.Hii ni kwa kuwa umeme utakuwa upo kwenye chanzo kikubwa na cha uhakika huku umeme unaozalishwa ukiwa ni mwingi wa kuwatosha watanzania wote na kuuzwa nje.

Mbali na hiyo, alisema pia nchi itakuwa na maji ya uhakika kwa kilimo cha umwagiliaji, hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao na ufugaji katika eneo lililo chini ya eneo la mradi wa maporomoko ya Mto Rufiji. Kwa msingi huu, pia Umeme wa maji ni rafiki wa mazingira na utapunguza ukataji wa miti na kutunza mazingira yetu na itaokoa miti inayokatwa kwa ajili ya kuni na mkaa kwa watu kutumia umeme...Tani milioni 2.3 za mkaa kwa mwaka zitatumia miti milioni 30 hivyo basi uwepo wa mradi huu utasaidia kupunguza ukataji wa miti.Hivi sasa kila siku kunavunwa hekta 583 ya miti kwa mwaka, eneo la selou lina ukubwa wa hekta mil.5 hivyo kwa ukataji huu wa miti baada ya miaka kumi na tano tu, selou inaweza kupotea.

“Kuboresha shughuli za utalii katika Pori la Akiba la Selous kwa kuwapo mazingira mazuri ya ustawi wa wanyama pori kutokana na uhakika wa maji wakati wote ya bwawa litakalotokana na ujenzi wa mradi.
“Kuongeza mapato ya nchi kutokana na kustawi kwa shughuli za kitalii katika eneo la mradi. Kuvutia uwekezaji katika sekta ya viwanda na sekta mbalimbali za uchumi kutokana na kuwepo kwa umeme wa uhakika na wa bei nafuu hivyo kupunguza tatizo la ajira.

“Kupunguza athari za mafuriko ya Mto Rufiji kwa wakazi waliopo maeneo ya Rufiji chini hadi delta ya Mto Rufiji na kuongeza pato la taifa na lishe kutokana na mazao ya uvuvi,” alisema Dk. Kalemani.

Kwa mukutadha huu tunaona namna mradi huu ulivyo na matokeo makubwa hasa matokeo chanya kwa nchi yetu. Tanzania tunapotaka kuwa na nchi ya viwanda tunahitaji umeme wa hakika na kwa mradi huu unaoisha miaka michache ijayo utatupatia faida kubwa. Kwa mradi huu Mh Rais anaandika historia kubwa ambayo itamfanya akumbukwe vizazi na vizazi.
 
Una matatizo mangi unahiitaji msaada mkubwa sana

kila kheri...

Jibu hoja mzee acha kugeuka mganga wa kufanyia diagnosis watu online na kuwapa majibu yao hapo hapo!

Umeme wa gas ya Mtwara ni half price,output ya umeme ni mara tatu ya Stiglers,eneo dogo sana linatumika,uchafuzi wa mazingira ni zero!

What are Stigler’s numbers?

Eneo la uchafuzi?ni the whole Tanzanian coastal delta karibu half ya Tanzania nzima!

Maji sio reliable kama gas!

Gharama za ujenzi ni mara mbili ya Gas plant!

Maarifa has never been a good strength of Jiwe!

Maarifa,maarifa,maarifa!
 
Back
Top Bottom