Secret Star
JF-Expert Member
- Jul 1, 2011
- 1,708
- 1,553
Mzee umepiga kitabu loh!Constellation ya Virgo (au Mashuke) ni mkusanyiko wa nyota unaofananishwa na mwanamwali (Virgin). Kama uko Tanzania kwa sasa Virgo inajitokeza mashariki kuanzia saa moja usiku. Ikifika saa 6 na nusu usiku itakuwa utosini kwako. Kama uko sehemu nyingine duniani nitonye nitakueleza uangalie wapi.
Kwa hiyo kama unataka kujua blackhole yetu iko muelekeo gani, jua linapozama tu angalia mashariki ndipo ilipo au angalia straight up kwenye saa sita na nusu usiku. Wakati ukiiangalia hii constellation ya Virgo basi milkway galaxy yetu iko magharibi ya Virgo. Milkway galaxy huwezi kukosa kuiona (hasa usiku wa manane). Utaona nyota nyingi kama mtu amemwaga maziwa (hence milkway) huko angani.
Vitu vinavyomezwa na blackhole vinakuwa sehemu ya hiyo blackhole na inazidi kukua.