Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza...

sasa kama chadema wanakuza demokrasia, kwa nini mlalamike kushindwa wakati baadhi ya kura mmejipunguzia wenyewe kwa kutimua madiwani....mimi naamini sababu ilikua moja tu... "Chadema tumeshindwa uchaguzi sababu ya mgogoro na baadhi ya madiwani wetu" hizo zingine mbwembwe tu.

Bado hujamuelewa mtoa mada pointi yake. Anasema CDM haiwezi kulea mafisadi kwa kisingizio cha kutaka umeya. na hapo hapo CDM yataka haki na utaratibu uliowekwa ufuatwe katika chaguzi, hata kama kitashindwa!

Kweli CCM mna vichwa vya nazi!
 
Duuuu cdm mshaniharibia week end yangu...naianza vibayaaaaaa, dawa ni kumlimboka tu huyo mkurugenzi wa mza! Hivi viongozi wetu mlipowatimua hao madiwani hamkujua kuna uchaguzi wa umeya?

Hapana, hapana, hapana.
Sina hakika kama cdm ingechelea kuwafukuza wale waliowaona ni wasaliti eti kusubiria kushinda umeya.
Kwa kufanya hivyo ni kuwa sambamba na kile tunachokiona kwenye chama tawala na kuwagwaya mafisadi'eti wataiangusha serikali wakifukuzwa. Hakika, cdm itaendelea kushinda kwa nguvu za wananchi bila shinikizo wala mbinu, nashauri cdm watumie muda na resources walizo nazo kuangalia mbele baada ya tafakuri zao. Siasa za hv kiulimwengu zimekuwa outdated, wale watumiazo ndio huleta machafuko duniani kote.
Cdm ijikite na elimu ya uraia. Ya nini meya mwenye back up ya madiwani, na sio wapiga kura?!
 
hata hivyo ccm wangeshinda. sababu ccm walitakiwa wawe na kula 10 dhidi ya 9 wa chadema. je huyo diwani wa Ilemela asingekuja chadema wangeshinda?. bila shaka wangelingana kura ambapo mkurugenzi ambaye ni msimamizi wa uchaguzi ingemlazimu kupiga kura na angeipigia ccm bila shaka. Tukubali tu kwamba chadema tumeshindwa. Tujipange upya kimafia zaidi. mia

mkuu uko sawa kabisa. Tukubali kabisa kushindwa kwa chadema asilimia kubwa kunachangiwa na chedema wenyewe... Wakati ccm walienda kwa hesabu sisi tulienda kwa huruma kutoka cuf na kwa bahati itokee ccm.!
 
Hapana, hapana, hapana.
Sina hakika kama cdm ingechelea kuwafukuza wale waliowaona ni wasaliti eti kusubiria kushinda umeya.
Kwa kufanya hivyo ni kuwa sambamba na kile tunachokiona kwenye chama tawala na kuwagwaya mafisadi'eti wataiangusha serikali wakifukuzwa. Hakika, cdm itaendelea kushinda kwa nguvu za wananchi bila shinikizo wala mbinu, nashauri cdm watumie muda na resources walizo nazo kuangalia mbele baada ya tafakuri zao. Siasa za hv kiulimwengu zimekuwa outdated, wale watumiazo ndio huleta machafuko duniani kote.
Cdm ijikite na elimu ya uraia. Ya nini meya mwenye back up ya madiwani, na sio wapiga kura?!

Mkuu, itawachukua CCM 1000 years kuelewa hicho unachokisema. CDM wajikite katika umma, na siyom small clique ya madiwani ambao wanaweza kuwa manipulated. Na CCM wanajua fika matokeo ya uchaguzi wa umeya umngekuwa vipi iwapo wananchi ndiyo wangepiga kura. Imefikia hatua kwamba CCM sasa inaanza kuogopa nguvu ya umma, na ndiyo maana inajihusisha zaidi na siasa za proxy.
 
Bado hujamuelewa mtoa mada pointi yake. Anasema CDM haiwezi kulea mafisadi kwa kisi
ngizio cha kutaka umeya. na hapo hapo CDM yataka haki na utaratibu uliowekwa ufuatwe katika chaguzi, hata kama kitashindwa!

Kweli CCM mna vichwa vya nazi!

sasa kama chadema haiwezi kulea ufisadi ili kushinda umeya. Kwanini ishiriki uchaguzi wenye ukiukwaji mkubwa wa taratibu za uchguzi, kwa nini wasigome kabla ya uchaguzi.?
 
Cuf na ccm ni mtu na mke wake, mipango yao yote wanapanga wanapopumnzika kitandani. Waacheni waendelee na unafiki wao.
 
Kushindwa kwa CHADEMA katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Mwanza hakukunisikitisha. Nimefarijika sana. Kwanza,ni kuona chamani kuna mshikamano. Kura zote nane za CHADEMA zimebaki chamani. Pili, kushindwa kumedhihirisha uimara wa chama hicho katika kusimamia maadili na nidhamu chamani BILA YA KUOGOPA MADHARA YA KISIASA KAMA haya. Tatu,CHADEMA imeonesha jinsi isivyopikika chungu kimoja na CUF. Nilitaka kushangaa! Hongereni sana CHADEMA...
 
CDM wameona ni bora waache uchaguzi ufanyike halafu ndiyo waende mahakamani. Yaani ni lazima process ikamilike in full kwanza ili wawe na kitu concrete cha kukipigana nacho. That's how CDM works!

Mkuu unachoongea ni upuuzi wa hali ya juu sana,eti unasubiri mwizi akuibie ili uende polisi wakati huo unauwezo wa kumdhibiti mwizi asikuibie ili usiende polisi,je unajua kitakachotokea ukifika polisi.??
 
..nadhani hii ni aibu kwa CUF.

..kwamba CUF wamekuwa kikwazo kwa mageuzi ya kisiasa Tanzania.
 
Naunga mkono hoja kwani kufuga nyoka ndani kisa umayer ingekuwa kosa kubwa!

Big up cdm!
 
Kushindwa kwa CHADEMA katika uchaguzi wa Meya wa jiji la Mwanza hakukunisikitisha. Nimefarijika sana. Kwanza,ni kuona chamani kuna mshikamano. Kura zote nane za CHADEMA zimebaki chamani. Pili, kushindwa kumedhihirisha uimara wa chama hicho katika kusimamia maadili na nidhamu chamani BILA YA KUOGOPA MADHARA YA KISIASA KAMA haya. Tatu,CHADEMA imeonesha jinsi isivyopikika chungu kimoja na CUF. Nilitaka kushangaa! Hongereni sana CHADEMA...

utumbo wakati mwingine hauliki eti eee !!!!!!!!
 
ni wakati wa kubadilisha huu utaratibu wa kumpata meya kutoka huu mfumo wa kupigiwa kura na madiwani, iwe meya achaguliwe na wananchi sababu mfumo wa sasa umeweka maslahi ya chama mbele, pia huu mfumo si wa kidemokrasia kwasababu diwani analazimika kumpigia mtu wa chama chake hata kama ni mbovu

Hapo umenena hizi siasa za umeya wa majiji zihusishe wananchi!
 
Uko pamoja na mimi mkuu, matokeo ya nyamagana nilitegemea yatakuwa hivyo, Chagulani pia amedhihirisha rangi yake halisi!
Big up sana!
 
Mkuu unachoongea ni upuuzi wa hali ya juu sana,eti unasubiri mwizi akuibie ili uende polisi wakati huo unauwezo wa kumdhibiti mwizi asikuibie ili usiende polisi,je unajua kitakachotokea ukifika polisi.??

CCM wametuzidi kete, wanatumia serikali yao kupindisha sheria na kucheza rafu
 
Back
Top Bottom