Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Dickson Ng'hily, Sep 28, 2012.

 1. Dickson Ng'hily

  Dickson Ng'hily Verified User

  #1
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  CCM wameshindishwa na mbinu za kisiasa amabzo uhalali wake kisheria linabaki kuwa suala la wanasheria wanaojua taratiu zikoje.

  Baada ya mgawanyo wa h/shauri ya jiji na kuwa na h/shauri ya jiji inayoundwa na jimbo la Nyamagana na halmashauri ya ilemela inayondwa na jimbo la ilemela mwezi Julai mwaka huu mgawanyo wa madiwai ulikuwa hivi kwa nyamagana

  Chadema -wa kata 5, viti ,maalum 2. mbunge mmoja, jumla wanakuwa 8
  CCM - wa kata 6, viti maalum 1 jumla wanakuwa 7
  Cuf - wa kata 1, viti maalum 1

  Ilemela

  Chadema -- wak kata 6, viti maalum 2 mbunge 1 jumla wanakuwa 9
  CCM - wa kata 3, viti maalum 2 na mbunge 1 (wa viti maalum) jumla wanakuwa 6
  CUF - MBUNGE WA viti maalum 1

  Kilchotokea kwenye uchaguzi ni CCM kuhamisha diwani mmoja wa viti maalum (kwa barua ya CCM kwenda kwa mkurugenzi wa jiji ya tarehe 14, Septemba, 2012) na mbunge wa viti maalum toka Ilemela kuja nyamagana na hivyo kuongeza idadi ya kura zao kuwa 9, wakati huo huo Chadema walishakuwa hawaihehabu kura ya Diwani wa Igoma Chagulani ambaye wamemfukuza uanachama akalejeshewa na mahakama wao wanapugukiwa na kura 1 zao zinabaki 7 , aliyepungua Chadema akiwapigia CCM wanakuwa na kura 10 dhid ya 7 za Chadema.

  Lakini pia CUF walishakubaliana na chadema kuungana mkono, kwa hiyo kwa kura 2 za CUF Chadema wangekuwa na kura 9, lakini inaonekana ama mwana Chadema mmoja kapigia CCM au CUF mmoja kapigia CCM na kufanya matokeo ya kuwa kuwa 11 kwa CCM dhidi ya nane za Chadema.

  Hiyo ndiyo hali halisi ya jinsi mahesau ya kura yalivyochezwa, kama kuna uhalali katika mchakato huo au la ni suala la wataalamu wa masuala haya kutujuza.

  Hayo yakiendelea uchaguzi wa Meya wa Ilemela meahirshwa katika mazingira tata, baada ya Mkurugeni kusoma Amri ya Mahakama iliyopewa tafsiri na mwanasheria wa jiji kuwa inakifanya kikao hicho kuahirishwa kwa kuwa Diwani wa Chadema Matata (pia alifukuzwa uanachama pamoja na wa igoma na anaendelea na udiwani kwa amri ya makahama) kuleta pia barua ya kutaka atambuliwe kaa mgombea.

  Ukazuka ubishi kidogo juu ya hoja ya mgombea kuteuliwa na chama, mkurugenzi wa jiji akasema hiyo siyo sheria ni mwogozo, na kwa kuwa sheria na mwongozo zikigongana sheria ndiyo inatamalaki hatakia aingie katka mgogoro wa tafsiri ya sheria, akaahirisha kikao bila hata madiwani kujadili hoja hiyo.

  Kwa mujibu wa mwanasheria wa wa Chadema, pingamizi hilo lilikuwa linawarejeshea haki yao ya uanachama na hivyo kuendelea na udiwani wao, na kutaka matata asizuiliwe kuendelea na mchakato wa kuomba umeya, Kwa hiyo matata ameomba lakini hakuteuliwa na chama na mahakama haiwezi kuwalazmisha chama wateue mgombea kwa amri ya mahakama, anadhani ni uhuni tu na njama za kisiasa zimefanyika kuahirisha uchaguzi huo.
  Nadhani kidogo piacha itaeleweka kwa wanjamvi juu ya nini hasa kimetokea.

  SOURCE: Kamnada Deus Bugaywa-Mchambuzi Raia Mwema

  Ushuhuda wa aliyekuwa eneo la tukio:

   
 2. m

  mjanja1 Member

  #2
  Sep 28, 2012
  Joined: May 11, 2010
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sahihisho: habari yapaswa kuwa KAFU +CCM waibwaga CDM Nyamagana.

  last week RAIMWEMA liliandika.....


  HUKU kikiwa na mvutano wa ndani na madiwani wake wawili kiliowafuta uanachama, Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kinakabiliwa na mtihani mzito katika kutetea nafasi Meya wa Jiji la Mwanza dhidi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu.
  Uchaguzi huo unaofanyika baada ya kugawanywa kwa Halmashauri ya Jiji la Mwanza na kuunda Halmashauri ya Jiji na Manispaa ya Ilemela unatarajiwa kuwa na mvuto wa aina yake katika siasa za Mwanza, ukitiwa chachu na hatua ya CHADEMA kuwafukuza uanachama madiwani wake ambao kwa namna fulani wanaweza kuathiri matokeo ya uchaguzi huo.

  Wakati CHADEMA wana uhakika wa kutwaa nafasi ya meya na naibu wake katika Manispaa ya Ilemela ambako pamoja na kumvua uanachama Diwani wa Kitangiri, Henry Matata, bado idadi ya madiwani wake ni wanane akiwamo mbunge wao dhidi ya madiwani sita wa CCM na mbunge wa viti maalumu mmoja wa CUF, shughuli pevu itakuwa katika halmashuri ya Jiji la Mwanza ambapo CUF ndiyo wenye turufu ya kuamua nani anakuwa meya.
  Kwa upande wa Halmashauri mpya ya Jiji la Mwanza, inayoundwa ndani ya mipaka ya Jimbo la Uchaguzi la Nyamagana, awali kabla ya CHADEMA kumvua uanachama Diwani wa Kata ya Igoma, Adam Chagulani, kilikuwa na wajumbe wanane sawa na CCM ambacho pia kilikuwa na idadi hiyo ya wajumbe wa Baraza la Madiwani, ambapo sasa baada ya Chagulani kuvuliwa uanachama CHADEMA kinabaki na wajumbe saba.

  Hata hivyo bado turufu ya nani anakuwa Meya wa Jiji hilo bado iko mikononi mwa CUF ambao wana wajumbe wawili ndani ya baraza hilo, ambao wakiamua kuunga mkono upande wowote huo ndio utaibuka na ushindi katika kinyang'anyiro hicho.

  kabla ya chagulani Nyamagana
  CCM=8 CDM=8 CUF=3

  baada ya Chagulani na ndoa ya CUF+ CCM=11

  so hata kama huyo chagulani angekuwepo bila kula za CUF CDM wangeishia kula 8 tu. na hamna ambalo lingebadilika

  ujanja wa CCM uliazianza baada ya kugawanya JIJI kuwa na Nyamagana na Ilemela kupitia waziri mikuu ambaye ni CCM. so turufu ikabaki kwa CUF ambao ni maswahiba na wenza wao (unabisha haupo TZ!)

  kabla ya kugawa jiji
  ccm=15
  cdm=19
  cuf=3

  so piga ua CDM ingeshinda mwanza! wanaakili sana lakini wanashau kuwa hata kama unaakili watu wakichoka hauwezi badili watu! so kina chagulani walitumika kuharibu hali ya hewa hili watu wasiojua ukweli wanaone chadema si chama cha maana, arafu uchaguzi wa meya urudiwe ili CCM washindwe. Sasa najiuliza Chagulani na mwenzako mmefurahi nini?
   
 3. F

  Froida JF-Expert Member

  #3
  Sep 28, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Dickson ahsante kwa kutuelewesha nadhani uitishwe mkutano wa wananchi waelezwe huo umafia halafu wao wataamua kama huyo mkurugenzi aliyemfuta wenje kugombea anastahili kuendelea kukaa Mwanza au plan B yao ni kutaka kununua tena baadhi ya madiwani/diwani hakuna kukata tamaa ni kutafuta namna nyingine ya kuhakikisha haki inatendeka hata kama kuna vibaraka na mapandikizi inauma kweli
   
 4. J

  Jenifa JF-Expert Member

  #4
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 603
  Likes Received: 193
  Trophy Points: 60
  mijitu mingine upumbavu mwingi utamdanganya nani
   
 5. C

  Concrete JF-Expert Member

  #5
  Sep 28, 2012
  Joined: Mar 12, 2011
  Messages: 3,607
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Mkuu wewe umeeleka vema sana,

  ila hapo mwanzo wa mahesabu yako unamaanisha Ilemela au Mwanza(Nyamagana)?
   
 6. Narubongo

  Narubongo JF-Expert Member

  #6
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,922
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 135
  ni wakati wa kubadilisha huu utaratibu wa kumpata meya kutoka huu mfumo wa kupigiwa kura na madiwani, iwe meya achaguliwe na wananchi sababu mfumo wa sasa umeweka maslahi ya chama mbele, pia huu mfumo si wa kidemokrasia kwasababu diwani analazimika kumpigia mtu wa chama chake hata kama ni mbovu
   
 7. r

  raymg JF-Expert Member

  #7
  Sep 28, 2012
  Joined: Jun 30, 2012
  Messages: 845
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Huyo diwan viti maalumu Ilemela kwa nn apigie kura Nyamagana? Je hili hawakulitambua wapiga kura hao?
   
 8. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #8
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Nilikuwa nasubiria kwa hamu tangia asubuhi post za wana cdm kuanza kujitetea baada yakupigwa dafrau hili la uchaguzi wa ccm , sasa ndio zinakuja. Na nashangaa mleta mada hii hajui kuwa meya ni wa Jiji la mwanza, ilemela ni manispaa itachagua mwenyekiti wa manispaa na sio meya. Cdm kubalini kushindwa uchemfu mmeufanya wenyewe na maamuzi ya kamati kuu yasiyo zingatia maslahi ya wana mwanza kwa kuwafukuza madiwani walio chaguliwa na wananchi, madhara yame mmeyaona.
   
 9. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #9
  Sep 28, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,809
  Likes Received: 1,129
  Trophy Points: 280
  Mfu siku zote haachi kutapatapa.
  Wasiosoma ni chakula cha wasomi.
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi kwa nini CCM haiwezi kushinda kihalali hadi ifanye uhuni, umafia, ghilba, maguvu etc etc? Ni last kick opf the horse? Wanataka kuleta vita baada ya kuanza kukataliwa kila mahali?

  Hivi yale ya Arusha yakitokea Mza, nani ataalaumiwa?


  Huyo Mkurugenzi ni kipenzi cha CCM, maana alianza kwa kumuengua Wenje na kupitisha lau, lakini halki ikajitokeza na kumuumbua huyo Mkurugenzi na CCM yake.
   
 11. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #11
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Asante sana mkuu nimekuwa nikitafuta habari hizi tangu mchana lakini wengi wanaleta porojo tu...
   
 12. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #12
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135


  Nenda kasome sheria, viti maalum hawana mipaka ya majimbo inategemea chama watamuidhinisha jimbo gani
   
 13. b

  blueray JF-Expert Member

  #13
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 15, 2012
  Messages: 2,219
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ni mbinu chafu na za kihuni ambazo mastermind wake ni chama cha magamba. Mbinu chafu hazidumu, nguvu ya umma itatawala. haki unaweza kuichelewesha tu huwezi kuizuia!
   
 14. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #14
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Lol! CCM uharamia kila mahali! jamani CCM hivi hamwezi kabisa kugombea bila haya mambo yenu ya kisanii tu, kwa kuwa mna nguvu za dola?

  Katika Katiba mpya tunatala mameya na wenyeviti wa halmashauri wachaguliwe na wapiga kura direct, na siyo madiwani wachache ambao ni rahisi kwa maharamia wa CCM kuwaghilibu kwa pesa.
   
 15. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #15
  Sep 28, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0


  Nilijua 100 percent kwamba lazima CCM watafanya umafia tu. Vinginevyo hawaiwezi nguvu ya umma.
   
 16. mgen

  mgen JF-Expert Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 15,194
  Likes Received: 1,914
  Trophy Points: 280
  Dawa ya hii kitu ni M4C kuwapiga kwa knock out na sio points kwenye chaguzi zote!
   
 17. Ronal Reagan

  Ronal Reagan JF-Expert Member

  #17
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,745
  Likes Received: 1,459
  Trophy Points: 280
  Asante Dickson,

  Ndio hasara na gharama za baadhi ya sheria mbovu ambazo watawala wanazitumia kuhalalisha kukosa kwao ridhaa na uhalali wa kutawala.

  Lazima tujifunze kutokana na hii mianya ya kimafia. Mimi siamini huu mchakato wa sasa utatupa katiba mpya na inayohitajika. Itakuwa mpya kwamba imeandikwa miaka hii lakini contents zake nina mashaka makubwa sana nayo.

  Karibuni wataalam wa sheria mtujuze way foward
   
 18. GeniusBrain

  GeniusBrain JF-Expert Member

  #18
  Sep 28, 2012
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 4,321
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135

  Vipi msuba wa Leo wa wapi wa musoma -tarime, mererani , au wapi?
   
 19. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #19
  Sep 28, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Kwa Mbunge wa viti maalum haina tatizo kwasababu yuko ndani ya mkoa huo huko kwa ninavyojua maana huwa ni wabunge wa mkoa siyo jimbo...lakini kwa diwani naona wamebaka kama walivyofanya Arusha..
   
 20. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #20
  Sep 28, 2012
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  Aisee inanipa nguvu sana ya kulikomboa taifa langu mikononi mwa Dhalimu CCM,
   
Loading...