Ufafanuzi wa kilichotokea Uchaguzi Meya Mwanza...

manispaa nayo huwa inachagua meyA
. umesahau hata jerry slaa ni meya wa ilala

mkuuu usimshangae huyo ni aina ya wanachama wa magamba waliopo hivi sasa,hajui hata meya anaongoza manispaa wakati jerry slaa wanamwita mstahiki meya kwa kuongoza manispaa ya ilala,halafu eti naye anajiita GREAT THINKER mh ama kweli nyinyiem inachangia kufifisha ubongo wa wanachama wake na kuwapunguzia uwezo wa kufikiri.
 
..nadhani hii ni aibu kwa CUF.

..kwamba CUF wamekuwa kikwazo kwa mageuzi ya kisiasa Tanzania.

kibaraka hawezi kuwa kikwazo cha mageuzi. Si muda mrefu wananchi wenye akili zao watatambua nani yuko upande wao Na nani anawasaliti. mpaka sasa wananchi waliowengi wameshatambua CUF ni CCM B. CUF bara ilikwisha kufa, kidogo karata ya Udini inayochezwa Na CCM kwa baati mbaya imempa uhai kidogo CUF Lakini inammaliza mme-CCM. CCM walidhani kueneza siasa za udini ingeweza kudhoofisha CDM. Sasa ndio maana unaona mme kazidisha mapenzi kwa mke akidhani Huu unyumba ndio utamnusuru 2015!
 
Wewe ndi mshamba umekalia uzanziari wenu huko na Jussa wenu aliyewahi kusema mlipoteza jimbo kwa ajili lilikuwa na wakristo wengi
Acha sias zetu wabara tuzijadili huku huku bara nyie endeleeni na fungate salama

kwani huyo mtoa mada alikua anazungumzia siasa za bara? Mbona mashirikiano kati ya cuf na ccm yako zanzibar? Inakuaje yeye anazungumzia na wewe humkatazi kuzungumzia mambo ya zanzibar wakati yeye mbara?

Pamoja na hayo mimi nina haki ya kuzungumzia siasa za popote pale duniani ispokua haki ya kugombea kuchaguliwa kuwa mbunge inaishia ndani ya mipaka ya tanzania.

Kama vyama vya siasa vimesajiliwa tanzania nina haki yakugombea popote pale tanzania hata huko kwenu arusha kwenye wachaga. Mbona hujamkataza halima mdee na john mnyika kuja kugombea majimbo yaliyoko ndani ya mkoa wa dsm ambao kimsingi ni mkoa ambao hauko bara bali pwani.

Ukitaka kuleta ubaguzi inabidi uanze kuwambia wachaga wahame maeneo yote ya ukanda wa pwani kwanza kuanzia dsm, tanga, kibaha, lindi, mtwara etc.

Jibu hoja zangu za juu huko kuhusu nchi ambazo zimeunda serikali za mseto wacha woga au ndio nyie muliowapiga mawe viongozi wa cuf arusha kwa woga wa kupambana na hoja? Je na sisi tuwashughulikie viongozi wenu wakija kwetu? Je hiyo ndio demokrasia? Munahisi hatuwezi? Tumieni akili kila mtu ana haki ya kutoa mawazo, kufanya mkutano na kuzungumzia siasa popote pale.
 
siasa za Tanzania bado zina "sisi" ni chama tawala na "wao" ni wapinzani. Mbaya zaidi wapiga kura kule vijijini hawajui haki na wajibu wao kiasi cha kutosha, ndio sababu napenda sana M4C inavyoshambulia vijijini huku ikiwafundisha wananchi kuwawajibisha watendaji wao wakiwamo madiwani, wabunge na watumishi wa serikali. Vipimo viwili-uzoefu na muda- vitatupa jibu kuanzia 2014
 
Wewe ndi mshamba umekalia uzanziari wenu huko na Jussa wenu aliyewahi kusema mlipoteza jimbo kwa ajili lilikuwa na wakristo wengi
Acha sias zetu wabara tuzijadili huku huku bara nyie endeleeni na fungate salama

muasisi wa chadema mzee mtei amewahi kunukuliwa akisema kua tume ya mabadiliko ya katiba ina waislam wengi kuliko wakristo. Je hi kauli inatafauti gani na kauli ya jusa? Wote 2 jusa na mtei sikubaliani na kauli zao hizo cha kushangaza hakuna hata mmoja kati yao ambae ameomba radhi kwa kuali yake. Ila naendelea kumuamini jusa kua mtetezi wa wazanzibar ingawa hataki kuomba radhi kwa kauli hiyo.
 
kushinda kwa uhuni jamaa wanashangilia ama kweli ndungu zetu wamezeeka hata hawajitambui kuwa wapo karne ya ngapi sahiz
 
Nilikuwa nasubiria kwa hamu tangia asubuhi post za wana cdm kuanza kujitetea baada yakupigwa dafrau hili la uchaguzi wa ccm , sasa ndio zinakuja. Na nashangaa mleta mada hii hajui kuwa meya ni wa Jiji la mwanza, ilemela ni manispaa itachagua mwenyekiti wa manispaa na sio meya.
Cdm kubalini kushindwa uchemfu mmeufanya wenyewe na maamuzi ya kamati kuu yasiyo zingatia maslahi ya wana mwanza kwa kuwafukuza madiwani walio chaguliwa na wananchi, madhara yame mmeyaona.

Hakuna cheo cha mwenyekiti wa manispaa katika mfumo wetu wa halmashauri ndugu, umekitoa wapi cheo hicho hacha kukurupuka kupost uongo.
Mfumo wetu wa uchaguzi haujakaa vizuri hususani kwenye kipengele cha ulazima wa kupitishwa na chama cha siasa kilichosajiliwa ili uweze ugombea nafasi ya uongozi wa kuchaguliwa na wananchi, naungana na Mchungaji Mtikila kuhusiana na suala la mgombea binafsi na pia nishauri katiba yetu mpya iruhusu mgombea binafsi na pia iwapo mtu atagombea kupitia chama akifukuzwa uanachama kwenye hicho chama aendelee kuwatumikia wananchi kama vile alikuwa mgombea binafsi
 
Nimejiuliza hili swali sina majibu ya uhakika.
CUF na CCM wamekuwa na Umoja usioelezeka kwenye masuala mbalimbali ya Utawala wa Taifa hili. Kimsingi maamuzi yao yamekuwa yakiwa kwenye Jihad kuu ya kupingana na CHADEMA kwa nguvu zote.
Sera za CHADEMA ziko tofauti sana na CUF na CCM. Kitendo cha Vyama hivi viwili CUF na CCM kuungana kwenye Maamuzi Muhimu ya kitaifa inaonyesha mkanganyiko mkubwa kwenye Demokrasia. Haijulikani bado kama CUF ni chama cha Upinzani au ni Chama Dada cha CCM. CUF imeungana na CCM kuipiga vita CHADEMA popote nwenye ngazi mbali mbali.

Nimejiuliza hivi haya wanayofanya ni kwa faida za nani?.

kwa faida ya ndoa na mapenzi yao
 
... After Election ,October 2015, mapungufu ya CDM kushindwa uchaguzi na rafu za CCM kushindwa zitaletwa tena hapa jamvini! What goes around,comes around!
 
Geniusbrain badili jina kwani meya ni wa masispaa au jiji mwenyekiti ni halmashauri,acha kutumia jina pasipo kulitendea haki!
 
Nilikuwa nasubiria kwa hamu tangia asubuhi post za wana cdm kuanza kujitetea baada yakupigwa dafrau hili la uchaguzi wa ccm , sasa ndio zinakuja. Na nashangaa mleta mada hii hajui kuwa meya ni wa Jiji la mwanza, ilemela ni manispaa itachagua mwenyekiti wa manispaa na sio meya. Cdm kubalini kushindwa uchemfu mmeufanya wenyewe na maamuzi ya kamati kuu yasiyo zingatia maslahi ya wana mwanza kwa kuwafukuza madiwani walio chaguliwa na wananchi, madhara yame mmeyaona.
Unaweza ukawa na mameya lakini wachafu na hawawajibiki kwa umma, je hapo utazingatia umeya au uadilifu? Jamaa kachambua vizuri sana. Ni CDM kuongeza idadi ya madiwani katika uchaguzi wa 2015, sio bora madiwani bali madiwani bora. Issue ya umeya itakuja automatic kama ilivyokuwa mwanzo. Umeya bila uadilifu ni mbaya kuliko haya yaliyotokea.
 
Ningewapongeza CCM kushida kiti hiki cha umeya kama wangekuwa wameboresha maisha ya watanzania kiasi cha hao waliowapigia kura kuona uhalali wa kufanya hivyo. Lakini kama wamepata umeya kwa ujanja ujanja wa kugawa madiwani n.k bado nakuwa mgumu kuwapongeza.
 
Hakuna cha kujivunia japo kisiasa nchi imetikisika lakini chadema tutasonga mbele ,wananchi tutawaelezea mwanzo mwisho ujambazi na umafia wa CCm waliofanya
 
Baada ya kuzigawa hizo halmashauri, madiwani wa viti maalum nao uwiano wao uangaliwe. Ilemela CDM wana madiwani 6 dhidi ya 3 wa CCM. Lakini vyama hivyo kila kimoja kina madiwani 2 wa viti maalum Nyamagana na Ilemela. It's senseless.
 
Mwanzo wa CDM kuwa imara.
1.Kauli za zitto
2.Kupoteza umeya mwanza
Mtake msitake tatizo si Mh zitto kutanganza kuwania urais 2015 laaa.Tatizo kuwa Mh ZITTO alikuwa hana cha kwa waambia watu walioudhulia mkutano huwo.Swali langu je walioandaa mkutano ndo lilikuwa lengo la kumwalika zitto pale.? Amini na usiamini Mh ZITTO anakwenda kama kinyonga.Kauli hizi zinaweza kuwa zinamsaidia au azimsaidiii huko twendako. Nanukuu msemo wa Marehemu BA,WA TAIFA JK.(Nyumba isipokuwa na msingi IMARA ikikumbwa na dhoruba itapata nyufa zinaweza kuwa kubwa au kidogo) Fikiri
 
Nimejiuliza hili swali sina majibu ya uhakika.
CUF na CCM wamekuwa na Umoja usioelezeka kwenye masuala mbalimbali ya Utawala wa Taifa hili. Kimsingi maamuzi yao yamekuwa yakiwa kwenye Jihad kuu ya kupingana na CHADEMA kwa nguvu zote.
Sera za CHADEMA ziko tofauti sana na CUF na CCM. Kitendo cha Vyama hivi viwili CUF na CCM kuungana kwenye Maamuzi Muhimu ya kitaifa inaonyesha mkanganyiko mkubwa kwenye Demokrasia. Haijulikani bado kama CUF ni chama cha Upinzani au ni Chama Dada cha CCM. CUF imeungana na CCM kuipiga vita CHADEMA popote nwenye ngazi mbali mbali.

Nimejiuliza hivi haya wanayofanya ni kwa faida za nani?.

Mkuu hata cdm tuna matatizo hayo hayo. Kuna wakati tunaacha kumshambulia ccm tunamshambulia cuf. Kwa ufahamu wako kulikuwa na haja gani kupeleka m4c lindi na Mtwara wakati already ni ngome ya cuf? Kama kuungana ni dhambi mbona cdm na ccm waliungana kigoma ya zitto kumpata mwenyekiti wa halmashauri
 


Tatizo nini?je ni kutoeleweka sawasawa kwa vugu vugu la M4C -chadema kwa upande mmoja na V4C- cuf na kueleweka sawasawa kwa vuvuzela la NAPE la vua gwanda vaa uzalendo????tafakari kisha toa maoni yatakayoisaida chadema na upinzani kwa ujumla mbele ya safari,waswahili wanasema inakua ni rahisi sana kusimama kama utaanguka na kukubali umeanguka kuliko ukiwa umeanguka lakini hukubali kwamba umeanguka,maana yake utaendelea kubali hapo hapo chini ukiamini bado umesimama kumbe upo chini unagalagala sakafuni.
 
Back
Top Bottom