Uendeshaji wa boda boda na baiskeli kwa muda mrefu unapunguza nguvu za kiume; waendesha boda boda kuweni makini

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,899
3,201
UENDESHAJI WA BODA BODA NA BAISKELI KWA MUDA MREFU UNAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME; WAENDESHA BODA BODA KUWENI MAKINI.

Leo naenda kwenye mada moja kwa moja, maana hili ni suala nyeti sana.

Kwa sababu wengi huwa tunataka ushahidi, naomba kila mmoja atakayepita kwenye huu uzi, akafanye utafiti wake mwenyewe na ikipendeza, njoo uchangie kile ulichokigundua kwenye utafiti wako kuhusiana na hili janga kwa vijana ambalo linashadidiwa na watawala eti ni ajira mbadala kwa vijana wetu wakiwemo wahitimu wa VETA, vyuo vya kawaida na vyuo vikuu hapa nchini.

Nafanya hivi kwa kuzingatia kanuni ya asili, ambayo inatutaka kuwatendea wenzetu vile ambavyo sisi wenyewe tunataka kutendewa. Kwa ufupi, kila mmoja anapaswa kuvaa viatu vya mwenzake na kufikiri kama yeye ndo angekuwa kwenye nafasi ya huyo, angejisikiaje?!!

Vijana wengi chini ya umri wa miaka 45 ambao wamejihusisha na uendeshaji wa boda boda au baiskeli kwa muda wa kuanzia miezi 6 na kuendelea, wanasumbuliwa na tatizo la nguvu za kiume. Hii ina maana wengi wao humaliza (hufikia mshindo wa kwanza) kwa chini ya dakika 3! Na wengi wao, hawawezi kuendelea tena baada ya bao moja!!

Ongea na vijana wanaojihusisha na hii kazi ambao mna ukaribu sana, watakuthibitishia hili ninalokushirikisha.

Wengi siku hizi wamegeukia dawa za kuongeza nguvu za kiume, ambazo bahati mbaya ni kwamba kadri unavyozitumia, ndivyo unajenga utegemezi kwa dawa hizo, na itafikia hatua, pamoja na kuzitumia, bado hutaweza kufanya tendo kwa ufanisi!

Hapo katikati, sote tulisikia Mkuu wa nchi akisema, vijana wengi siku hizi hawana nguvu za kiume kwa sababu ya kutokula vizuri. Kwa maneno mengine wanakula vibaya. Hii kauli ina ukweli kwa kiasi kikubwa, lakini siyo sababu pekee ambayo hupelekea tatizo hili ambalo kwa kweli kama lilishawahi kukukumba utagundua huwa linasababisha fedheha kubwa sana. Mwenyewe ninayeandika hizi ni mhanga kwa hiyo ninaeleza kitu ambacho nina uzoefu nacho. Narudia tena kusema, unaweza kufanya utafiti pia, halafu utuletee mrejesho. Maana lengo la huu uzi ni kusaidiana na wala siyo kumlaumu mtu au watu fulani. Janga hili ni kubwa sana japo linakuwa "underrated".

Kwa hiyo vijana, fanyeni kila linalowezekana kuhakikisha mnatafuta kazi zingine na wala msiridhike na hiyo kazi ya bodaboda kama alivyowashauri Godbless Lema.

Godbless Lema, ana maoni mazuri sana kwa Watanzania kwa ujumla. Kitu ambacho anatakiwa akiache, ni kumsema tu vibaya Hayati JPM kwani ni kipenzi cha Watanzania wengi hasa wale ambao hawako kwenye mfumo wa kulamba asali wa awamu hii.

Nimalizie kwa kuwashauri vijana; msifanye kazi ya bodaboda kuwa kazi ya maisha, kwani mbali na kupunguza nguvu za kiume, lakini pia, inazo changamoto nyingi sana.
Mjumbe hauwawi.
Karibuni sana.
 
Kumbe boda boda wengi ni hawana nguvu kabisa?

Sasa kwa nini wanaharibu watoto wa shule hovyo hovyo?
Kuharibu ni kuharibu tu haijalishi wanaharibu kwa kiwango gani?!
Wengi wana hiyo shida, fuatilia utaligundua hili.
Sifa nyingine ya watu wenye upungufu wa nguvu za kiume ni hawajiamini. Ndiyo maana wanataka kila msichana watembee Naye wakitarajia kupata matokeo ya tofauti!
 
UENDESHAJI WA BODA BODA NA BAISKELI KWA MUDA MREFU UNAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME; WAENDESHA BODA BODA KUWENI MAKINI.


Karibuni sana.
Ingawa wanakabiliwa na tishio hilo lakkni cha ajabu ni kwamba, wanaongoza kwa kuwatafuna kimasihara pisi kali na zisizo kali

Wanaseviwa kama Bodaboda wangu 🤣🤣
 
Kama huna huna tu msizipe kesi boda wa baiskeli zetu
Mwisho mtasema
Kutembea kwa miguu kuna maliza nguvu za kiume

Kama huna huna tu
Umeongea ukweli. Kama huna, huna tu. Kuna watu wako vijijini huko miaka nenda wanaendesha baiskeli, na wana watoto kama simbilisi.

Kuna sababu nyingi zinazosababisha nguvu za kiume, na zimethibitishwa kitaalam. Na katika hizo sababu zote, sidhani kama hizi za mtoa mada zipo kwenye hilo kundi.
 
UENDESHAJI WA BODA BODA NA BAISKELI KWA MUDA MREFU UNAPUNGUZA NGUVU ZA KIUME; WAENDESHA BODA BODA KUWENI MAKINI.

Karibuni sana.
Chini ya dakika 3 inatosha sana!! Ukitaka mtoto hata sekunde mbili zinatosha.

Sasa kama mwenza wako anataka zaidi ya dakika 3 mwambie awasiliane na Punda, hata dakika moja ataiona ni nyingi
 
Umeongea ukweli. Kama huna, huna tu. Kuna watu wako vijijini huko miaka nenda wanaendesha baiskeli, na wana watoto kama simbilisi.

Kuna sababu nyingi zinazosababisha nguvu za kiume, na zimethibitishwa kitaalam. Na katika hizo sababu zote, sidhani kama hizi za mtoa mada zipo kwenye hilo kundi.
kwani nani alikuambia ukiwa na upungufu wa nguvu za kiume huwezi kuzalisha?
Ninachokiongelea na kukimaanisha ni kwamba, waendesha baiskeli na bodaboda wanakabiliwa na changamoto ya upungufu (siyo ukosefu) wa nguvu za kiume.
 
Back
Top Bottom