GUSSIE
JF-Expert Member
- Dec 2, 2014
- 3,866
- 11,100
Yanayoendelea kwa vijana wetu Wasomi na ambao sio Wasomi huwezi kutofautisha kitu Katika kundi hili. Hoja za matusi na kutukana ndio njia pekee ya hawa vijana, Wanaamini upande mmoja wa habari
Yawezekana ni makosa yetu wazazi kuwajaza watu ujinga na wao kuyaamini kama yalivyo bila kufikiria au kujiridhisha
Mambo yafuatayo yameonyesha aina ya watu na vijana tulionao hapa JF :
Mosi, Hoja za kuendeleza gesi na maamuzi ya kutafuta wanasheria wa nje kwa ushauri, Vijana wamejazwa upepo kuwa wao wanaweza kazi hii ya sheria za kimataifa kwa kusoma soma sheria za International law pale Udsm na Udom, Wamekaa wanakula popcorn hawaelewi kuwa serikali inalipa madeni mengi kwa kudharau sheria za kimataifa, Ushauri wa kipuuzi wa wanasheria wa ndani kuwa tunaweza serikali imeishia kulipa hasara na medeni
Pili, Hoja za Bandari ya Bagamoyo, Wengi wamejazwa upepo bandari haifai,Wachina wanatupiga. Ukiwauliza wewe unafahamu mkataba wake anajibu nilimsikia Rais na Waziri. Leo hii mtu anaweza sema tutaajiri vijana 100,000 serikalini na vijana wanapiga makofi, Ukiuliza ajira zitatoka wapi kwa pesa ipi hakuna majibu, Mtu haelewi hata maana ya kina cha bandari bali utasikia aaha kule Bagamoyo si kwa Mzee JK ndio maana wanajenga bandari, Ukimuuliza sasa ulitaka JK azaliwe Dodoma
Tatu, Hoja za Freeman Mbowe na kesi inayoendelea huko mahakamani, Utasikia Leo shahidi amegalagazwa vibaya sana, Tangu lini shahidi akagalagazwa? Shahidi anaeleza alichokiona Yeye na kukishuhudia, Maswali anayoulizwa nje ya yale aliyoyasema na kuyaandika hayamuhusu,Jaji anajenga msingi kwa alichokisema shahidi, Maswali ya kuwa una degree ngapi? Una wake wangapi? Unamfahamu Tundu Lisu? Uliona watu wakibeba petrol na magogo?. Haya yote inategemea kama shahidi aliyasema kama hakuyasema ni kupoteza muda kumuuliza, Maswali nje ya context ya alichokisema na kukiandika shahidi ndio vijana wanashabikia huku wakiwa na Tecno na itel za wachina wasiowataka kujenga bandari ya Bagamoyo
Hoja ya Ridhwani Kikwete kuwa naibu Waziri, Utasikia aaha yule Ridhwani hafai kabisa, Ukiuliza lini Ridhwani amewahi kuwa Waziri na akakosea hakuna Jibu lolote, Lipi baya alilofanya Ridhwani utasikia aahaa nchi sasa imerudishwa kwa wapigaji, amepiga pesa gani hakuna majibu, Kumbe wanaumia kwanini mtoto wa fulani kawa Waziri, Kwanini uumie mtoto wa Mo Dewji kuwa tajiri kama Baba yake ulitaka avae kandambili zilizoshonwa shonwa
Hoja za Spika Ndugai kujiudhuru na chama chake cha ccm, Utasikia Spika ameonewa na Rais ana nguvu zaidi. Je unafahamu taratibu za ndani za ccm kanuni na maadili ambayo chama kilimpendekeza Ndugai kuwa Spika, Utasikia sifahamu, Ndani ya ccm mtu anawajibika kwa chama chake kwanza halafu ndio anawajibika kwenye nafasi yako uliyopewa, Hata Rais Samia anawajibika kwenye chama kwanza halafu kama Rais, Chama ndio kimekupa nguvu na sio cheo, Ndugai alivunja maadili na kanuni za chama kilichompendekeza awe Spika kwa kushindwa kujizuia kutofautisha nafasi akiwa Bungeni na nje ya Bunge
Vijana ambao wanategemea akili za watu wengine wawafikirie kwa niaba yao, Hao ni vijana mfu