Sasa adui wa Taifa la Tanzania si ujinga bali ni upumbavu

Kiboko ya Jiwe

JF-Expert Member
Apr 7, 2020
12,712
36,171
UPUMBAVU ni hali ya mtu au watu waliopata elimu lakini wameshindwa kuitumia kujikomboa wao wenyewe au kuikomboa jamii yao katika adha , dhiki, shida au aina yoyote ya mkwamo.

MPUMBAVU, ni mtu alitebahatika kupata elimu lakini kwa makusudi kabisa au kwa kutokujua hawezi kuitumia elimu yake kuikomboa jamii yake au hawezi kujikomboa kutoka katika mkwamo wa kifikra, kiuchumi n.k.

Kama Mkurugenzi ambaye ni mtumishi wa umma na hajafungamana na chama chochote anakubali kuacha ofisi na kuhudhuria mkutano wa katibu mwenezi wa chama Ili akaulizwe maswali ya kuabishwa, je, huyo Mkurugenzi hapaswi kuitwa mpumbavu?

Kama Mkurugenzi anakuwa mpumbavu je watumishi wa chini yake ambao kawaajiri wataondokana na upumbavu?

Kimamlaka Mkurugenzi wa wilaya ndiye mwajiri wa watumishi katibu wote wa Halmashauri ya wilaya husika.

Akija katibu mwenezi wa chama Mkurugenzi na maafisa wa wilaya wote wanaacha ofisi kwenda kujibu maswali ya katibu mwenezi.

Kama nchi hili jambo halitoshi kuthibitisha kuwa wasomi na viongozi ni wapumbavu?
 
Kama nchi hili jambo halitoshi kuthibitisha kuwa wasomi na viongozi ni wapumbavu?.
Ndege wanaofanana huruka pamoja...

Tunashuhudia upumbavu kiwango cha hamira kwenye nchi hii
 
Moyo wangu unabubujika damu nikiwaza hatma ya taifa hili
Miaka michache ijayo tutakuwa koloni la ama taifa la kiafrika, kiarabu au mashariki ya mbali.

Hali ya taifa inachosha sana. Vijana wengi hawana ufahamu wa mambo ya kawaida sana na ni graduates wa vyuo vikuu. Na ndio tegemeo la kesho.

Graduate anaona kulijua taifa lake ni ushamba. Ila ujanja ni kujua toleo jipya la iphone, vazi jipya, usajili wa klabu fulani au trend ya celebrit mmoja ya ajabu ajabu.
 
Graduate ukimuuliza mambo ya manara atakupa a to z.
The same graduate anadhani Songea, Sumbawanga, Moshi na Musoma ni mikoa.
 
UPUMBAVU ni hali ya mtu au watu waliopata elimu lakini wameshindwa kuitumia kujikomboa wao wenyewe au kuikomboa jamii yao katika adha , dhiki, shida au aina yoyote ya mkwamo.

MPUMBAVU, ni mtu alitebahatika kupata elimu lakini kwa makusudi kabisa au kwa kutokujua hawezi kuitumia elimu yake kuikomboa jamii yake au hawezi kujikomboa kutoka katika mkwamo wa kifikra, kiuchumi n.k.

Kama Mkurugenzi ambaye ni mtumishi wa umma na hajafungamana na chama chochote anakubali kuacha ofisi na kuhudhuria mkutano wa katibu mwenezi wa chama Ili akaulizwe maswali ya kuabishwa, je, huyo Mkurugenzi hapaswi kuitwa mpumbavu?
Kama Mkurugenzi anakuwa mpumbavu je watumishi wa chini yake ambao kawaajiri wataondokana na upumbavu?
Kimamlaka Mkurugenzi wa wilaya ndiye mwajiri wa watumishi katibu wote wa Halmashauri ya wilaya husika.
Akija katibu mwenezi wa chama Mkurugenzi na maafisa wa wilaya wote wanaacha ofisi kwenda kujibu maswali ya katibu mwenezi.
Kama nchi hili jambo halitoshi kuthibitisha kuwa wasomi na viongozi ni wapumbavu?.
Wapumbavu ni wengi kuliko werevu
 
Back
Top Bottom