UDSM, MUHAS & UDOM Vinashika Nafasi Tatu za juu kwa Vyuo Vikuu Kumi Bora Tanzania

Annunaki

JF-Expert Member
Dec 30, 2021
1,911
3,171
Baada ya kufanya utafiti mdogo kuhusu vyuo kumi bora Tanzania, nimejiridhisha vya kutosha vyuo nitakavyo vitaja hapa ndivyo vyuo kumi bora kwasasa hapa Tanzania. Katika utafiti huu mdogo nimezingatia machapisho ya chuo husika kwenye international journals, tafiti za chuo husika, mchango wa chuo husika katika suala zima la maendeleo na vyanzo vikuu nane vinavyo toa orodha ya vyuo bora katika nchi mbali mbali na duniani kwa ujumla, ambavyo vyanzo hivyo ni www.webometric.com, www.TimesHigherEducation.com, www.AcademicRankingofWorldUniversities.com, www.Quacquarellisymonds.com, www.EduRank.com, www.ShanghaiRankingConsultancy, www.UniversityGru.com bila kuisahau TCU.

Kwasasa hapa Tanzania vyuo vifuatavyo ndivyo vyuo kumi bora

1. University of Dar es salaam(UDSM)- Acceptance 75%
1656682696531.jpg



2. Muhimbili University of Health and Allied Sciences(MUHAS)- Acceptance 68%

1656682735734.jpg


3. University of Dodoma (UDOM)- Acceptance 65%
1656681724353.jpeg


4. Sokoine University of Agriculture(SUA) - Acceptance 63%
1656681785046.jpeg


5. Ardhi University- Acceptance 58%
1656683026878.jpg


6. Mzumbe University- Acceptance 48%
1656681860650.jpeg


7. Nelson Mandela African Institution of Science and Technology- Acceptance 48%

1656681912048.jpeg


8. State University of Zanzibar-Acceptance 41%

1656681966561.jpeg


9. Hubert Kairuki Memorial University-Acceptance 36%
1656682793344.jpg


10.ST Joseph University of Tanzania- Acceptance 33%

1656682103263.jpeg




N.B
Katika kufanya upembuzi wangu huu, sijatumia chanzo kimoja ili kupata ranking hii, hapa nimetumia vyanzo nane vinavyojihusisha na ranking za vyuo vikuu kama nilivyozitaja huko juu.

Wanafunzi na wazazi hivi ndivyo vyuo vikuu vya hapa Tanzania ambavyo mwanafunzi/mtu anaweza kusoma na kutambulika ndani na nje ya nchi kirahisi.

Imeandikwa na Annunaki.
 
Subiri waje wakubishie kwenye hiyo nafasi ya kwanza
Bwana Ngalikihinja ni kweli watapinga ila kitu kimoja wanachotakiwa kujua ni kwamba pamoja na Udsm kushuka kwenye ranking za kimataifa, bado kwa hapa Tanzania kinashika namba moja hata kwenye references zote nilizotumia kimetokea kama chuo namba moja kwa hapa Tanzania.
 
KILE CHUO KIKUU CHA KILIMO PALE MOROGORO WANAJIONA WAKO VIZURI ILA KUMBE NAFASI YA NNE?
UKIWA NAO WANAFUNZI WANAONA WANASOMA VITU VIGUMU KUMBE NI HIVIHIVI TU,NA WAALIMU WAO VILE VILE WANADHANI WANA CHUO BORA KULIKO VYOTE TANZANIA.
SUA BANA KWA KUJITAPA WAKO NJEMA.
Egoism haiwezi kukosekana kwa wahitimu wa vyuo kila mtu huvutia kwa upande wake kwahyo hawezi kujishusha kwa kukubali uwezo wa mwenzake.

SUA wako vizuri pia, ila hawana consistency.
 
Wakati huo huo, udsm ni namba 31 kwa ubora barani Afrika. Tuendelee kujipigapiga kifua...
 
Wakati huo huo, udsm ni namba 31 kwa ubora barani Afrika. Tuendelee kujipigapiga kifua...
Bwana Eroni ubora wa elimu yetu unashuka lakini pamoja na kushuka kwake, vyuo nilivyoona at least vinajitahidi kulingana na utafiti wangu huu mdogo ni hivyo nilivyovitaja.
 
Back
Top Bottom