Mzee wa Gumzo
Senior Member
- Apr 21, 2008
- 197
- 6
Wakati nchi inapambana na vitendo viovu ukiwemo ufisadi na rushwa tunategemea taasisi zetu hasa za elimu ya chuo kikuu kuwa mstari wa mbele kukemea uovu huo na kuonesha mfano wa kuigwa na wanajamii wengine.
Hali inaonekana kuwa tofauti kabisa na ukweli huo.Chuo kikuu cha dar es salaam kimefunguliwa kwa muhula wa kwanza wa mwaka wa mpya wa masomo.Wanafunzi wengi wamekosa vyumba vya kulala katika mabweni ya liyopo eneo la chuo na hosteli ya mabibo.Imegundulika kuwa hali hiyo haitokani tu na uhaba wa vyumba kutokana na ongezeko la wanachuo bali kuna ufisadi wa hali ya juu.
Jana nilianza uchunguzi wangu na kufanikiwa kupata vyumba kumi na sita ambavyo vilikuwa vinauzwa na kiongozi wa DARUSO ambaye sikutajiwa jina.Nilitakiwa kulipia laki moja kwa chumba kimoja kilichopo mabibo hosteli na laki moja naishirini kwa chumba cha campus.Leo nimeendelea na uchunguzi kwa kujifanya mtafuta chumba.Nimefanikiwa kumpata mwanfunzi wa mwaka wa pili anauza vyumba viwili.vyote hivyo amepewa na kiongozi wa daruso atafute wateja wa chap chap.
Mbali na uchunguzi huu, kilio ni kikubwa sana kwa wanachuo waliokosa vyumba hasa pale wanapogundua kuwa vyumba vipo ila vimeshikiliwa na mafisadi wachache wanaoviuza kwa lengo la kujipatia fedha.
Rushwa na uchafu wa kila aina umekuwepo katika zoezi la kuwapatia vyumba wanachuo mlimani lakini siku zinavyokwenda linakuwa sugu.Haiingii akilini kama wanakuwepo viongozi wa wanafunzi wanashiriki kwenye ufisadi wa kutisha hivyo.Tuntengeneza kada ya viongozi wa namna gani kwa hapo baadae?.Jamii inayotarajiwa kuhudumiwa na watu kama hao itapona kweli?.Tuna haja gani kupambana na mafisadi wa kubwa wa EPA wakati vyuo vyetu vinatuzalishia mafisadi wenye digrii za kutungua?
Tatizo linaanzia UNIVERSITY STUDENTS ACCOMODATION BUREAU{USAB}Ni mamlaka yakusimamia suala la malazi lakini wanashindwa kuvalia njuga suala hili.Vilevile utawala wa chuo upo kimya wakati hali hii inajulikana wazi.
Tusiache kipele kikue na kugeuka donda ndugu.
Ni issue ya miaka mingi tu,kwani kwa sera ya chuo kikuu cha Dsm(kama ipo) ni kuwapa vyumba 1st year wa batch ya kwanza(Govt sponsored via loan board?) wale wa batch zifuatazo huwa hawana chao japo nao ni 1st year.Finalist wachache ambao wana network za kutosha huwa ndio 2nd priority then comes wanunuaji.Hata baadhi ya viongoz wa DARUSO hukosa vyumba sometime(mwaka jana ni mfano).Nadhan tatzo lnaanzia kwa utawala kuongeza udahili wa wanachuo bila kuhakikisha kuwa kuna mahali pa uhakika pa malazi kwa wanachuo hao,kwani elimu ni zaidi ya kukaa lecture rooms!Then USAB pia kuna tatzo kubwa kwani wanadai kuwa wana_allocate rooms using the software(zalongwa) ila ukwel ni kuwa certain rooms huwa znakuwa zmetengwa tayar kwa biashara kabla hata hiyo software haija_come into play.So zaidi ni viini macho!!!Mwenye nacho hununua ktanda(japo wenyewe huita room) na mwenzangu na mie asubiri kubebwa au apange mtaani.Hii ndo hali halisi ya suala zma la accomodatn UDSM.Naomba kuwakilisha!
Wadau, kwanza kabisa niseme wazi kuwa sina ugomvi na Wasomi wetu waliomaliza UDSM wala agenda binafsi ila ni wasiwasi mkubwa sana na UDSM ambacho ni kati ya Vyuo Vikuu vyenye sifa kubwa Afrika na Duniani. UDSM kimetoa viongozi mashuhuri Afrika miongoni mwao ni Dk John Garang, Yoweri Museveni na kadhalika.
Baada ya sera ya Taifa kutoa mikopo kwa Wanafunzi, moja ya matokeo chanya ya Srea hiyo ni ongezeko la Wanafunzi katika Vyuo vyetu Vikuu hasa UDSM. Hata hivyo kama ilivyo kawaida hakuna kitu chema ambacho hakina mapungufu lakini haya ya UDSM linatakiwa mtazamo maalumu.
Ongezeko kubwa la Wanafunzi pale UDSM limesababisha matatizo makubwa sana ya makazi kwa upande wa wanafunzi na kusabibisha wanafunzi wengi wishi mitaani kama vile Sinza, Ubungo, Msewe nk.
HAbari nilizonazo ni kuwa baadhi ya Wafanyakazi wanaohusika na kutoa nafasi za Hosteli pale UDSM wameuza kazi hiyo kuwa mradi mkubwa wa kujipatia fedha na kinachonisikitisha ni kuwa Uongozi wa UDSM umeshindwa kudhibiti tatizo la rushwa kwenye utoaji wa vyumba kwa Wanafunzi. Binti mmoja alimpigia simu mama yake akimuomba shilingi laki mbili (200,000/-) ili ahonge na kupatiwa chumba pale main campus na nilipofuatilia niliambiwa kwamba ili mwanafunzi apte upendeleo katika kupata chumba hulazimika kutoa kati ya shilingi laki mbili hadi laki tano (200,000/- to 500,000/-). Kiasi hicho inawwezeka ikankuzwa na wanafunzi wenye ili waweze kupata pesa nyingi kutok kwa wazazi lakini sua;la la rushwa katika hilo eneo lipo na limekuwepo kwa muda mrefu sasa.
Athari zake kwa Taifa
Athari kubwa kuhusiana na rushwa za makazi kwa wanafunzi pa;le UDSM ni kujenga Taifa la Viongozi wasio waadili baadaye (MAfisadi) maana kama mwanafunzi amezoezwa kutoa rushwa ili kupata huduma ni wazi kwake kutoa na kupokea rushwa haitakuwa tatizo na itakuwa ni sehemu ya maisha yake.
Wanafuzni hawa ndiyo wanokuja kuwa viongozi wetu kwenye Ofisi za Umma na Binafsi na hta kuwa viongozi wa Kisiasa- Uwaziri hata Urais! Sasa ikiwa maisha yao ya Chuo Kikuu yamezingirwa na rushwa ma jkuifanya kuwa ehemu ya maisha yao; Je; hatima yao na mustakabali kwa Taifa utakyuwaje?
Ndiposa na sema UDSM ni kitivo cha kuzalisha Viongozi Mafisadi na wasio waadilifu kitu ambacho ni hatari kubwa kwa Taifa Tanzania.
Tafadhari naomba ufafanue, hiyo Rushwa anapokea nani hapo UDSM? Ni kiongozi wa DARUSO au kiongozi wa USAB? Tafadhari liweke wazi ili ufuatiliaji wake uwe rahisi. Ikiwezekana andika na jina la mtu aliyepokea hiyo laki mbili na anayehusika na upokeaji wa hiyo hela. Naamini upo anonymous, ukimtaja, hakuna atakayejua kama wewe ndo umetaja. Kwa ajili ya kulinda heshima ya chuo pia kukomesha vitendo hivyo katika taifa, ningependa kujua undani wa jambo hili ili personally niliwasilishe kwenye vyombo husika.
hivi unadhani kwa ulkimwengu wa sasa ulivyobanjuka,matatizo yote wanayopata hawa vijana wataacha kulipiza kwa kuwa mafisadi??? hakuna wazalendo tena,serious...
Rushwa huzalishwa na UHABA (SCARCITY) full stop. Kitu chochote kinapokuwa kwenye supply ya kutosha rushwa haina nafasi.
Uhaba wa vitanda vya kulala wagonjwa Muhimbili na hospitali zingine nchini husababisha Rushwa kwa wagonjwa kuwahonga wanaodhibiti upatikatanaji wa vitanda. Uhaba wa bidhaa huko nyuma ulisababisha rushwa kubwa sana kwa waliokuwa wakifanya kazi RTC. Maafisa mauzo enzi hizo walikuwa kati ya watu wa kutafutwa sana kwani kununua bidhaa ilikuwa hadi uhonge.
Hadi leo, bidhaa fulani ikipungua, wafanyabiashara hupandisha bei (rushwa) kwa sababu bidhaa haipo ya kutosha na wanaoitafuta ili waipate inabidi kulipia zaidi.
Mifano iko lukuki ya kuthibitisha hilo.
Kama mitaani mazingira yangekuwa mazuri, nyumba za kutosha zinapatikana kwa bei zinazoeleweka (si kulipa ada ya mwaka mzima kabla ya kukaa kwenye chumba), hizo rushwa zisingekuwepo asilani.
Uhaba wa vyumba unazalishwa na watunga sera wanaposema kuwa vyuo havijihusishi na wanafunzi wanakaa wapi (kama anavyosema Waberoya hapa) wakati wanajua mazingira yetu hayajatupa jeuri ya kusema hivyo. Kupata chumba Dar si kazi nyepesi, kuna madalali (wala rushwa) ambao wamejazana mtaani hula fedha kibao za watafuta nyumba za kupanga. Hivyo wanafunzi wakikwepa balaa la wala rushwa wa vyuoni, watakutana na madalali wa mitaani; kwani hatuna mahali maalumu ambapo unaweza kwenda na ukajua nikitaka chumba maeneo gani nitakipata wapi na vipi na kwa gharama gani. Soko la nyumba ni soko la mwenda wazimu na haliko regulated na yeyote na serikali haijihusishi nalo kama vile hakuna mabilioni yanayobadilishana mikono kila mwaka kama kodi za nyumba.
Kukodisha nyumba ni biashara isiyo rasmi kwa hiyo kila mswahili anajipangia sheria na taratibu zake za upangaji. Wanafunzi wengi wanajaribu kukwepa kutotabirika kwa nyumba nyingi za mitaani na wako tayari kutoa rushwa kubwa ili kupata vyumba ndani ya maeneo ya chuo. Kuna kitu kinaitwa baraza la nyumba; kitu ambacho kinatakiwa kuregulate hili soko, lakini ukweli ni kama hakipo kabisa.
Hili soko la nyumba likianza kudhibitiwa wapangishaji wote wa nyumba wakatakiwa kusajiri nyumba zao za kupangisaha mahali fulani, wakapewa leseni kama wafanyabiashara wengine na wakapewa masharti ya biashara kama wafanyabiashara wengine; hili tatizo litaisha mara moja. Tatizo lipo kwa sababu wanafunzi wanaogopa kuingia mtaani kwani wenye nyumba hawatabiriki na sheria na taratibu za upangaji ni juu ya mwenye nyumba kuamua. Hali hii imesababisha artificial scarcity ya nyumba.
Je ni kweli kuwa serikali haiwezi kudhibiti soko la nyumba na kutunga sheria itakayowafanya wapangishaji wote wa nyumba wachukuliwe kama wafanyabiashara wengine? Uwezo upo na ni suala la kuamua tu. Serikali inapoteza mapato mengi sana kwa sababu kodi za nyumba wanazolipwa wenye nyumba hazitozwi kodi kwa sababu nyumba nyingi hazijasajiliwa kama nyumba za biashara.
Hili ni tatizo dogo tu linaloweza kumalizwa na mtu mmoja makini hapo serikalini; wala si rais. Anaweza kuwa waziri wa ardhi na makazi!!