Udocta Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Udocta Tanzania

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mwanamasala, Dec 16, 2009.

 1. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #1
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Watanzania tunapenda kujikuza sana kielimu!Nafikiri kusini kwa jangwa la sahara ni sisi tu!Hata Wanaigeria wanaosifika kwa scams ,huwezi ukakuta mtu amefoji Phd maana wao elimu yao bado ni nzuri,ndio maana Ulaya na Marekani bado wao wanongoza kitaalamu kwa watu weusi.Kwa nini Slaa ajiite dr???na magazeti na vyombo vya habari vinamtambua hivyo?Hata Dr Edmond Mndolwa?ni accountant mzuri hii Phd ni ya nini.

  Sio vibaya kupata udaktari wa heshima(Honorary doctorate)!lakini kwa nini kila siku watu wakuite dr?Dr Salim Ahmed Salim?ya nini miaka yote wakati hana real Phd?????Paul McCartney(ex Beattle) ana udactari wa heshima,kama Alex Ferguson wa Man Ultd.Lakini hakuna hata mtu mmoja anathubutu kumwuita Dr Paul Mccartney au Dr Alex Ferguson.

  Mandela ,Tutu wanaheshima sana kuliko hata Nyerere wetu.Wana honorary doctors nyingi sana,lakini media ya south africa sijasikia kila siku ikimuuita Dr Mandela au Dr Tutu.haya ni bongo tu.

  Slaa ana juris doctor(though hana undergraduate degree).Fair enough .Kwanini ajihalalishe udocta?Angalia Juris doctor za Obama ,Michele Obama na Bill Clinton.Lakini hakuna hata siku moja wakajiita madoctor kama wachwala wetu bongo.Condo Rice ana Phd,lakini hakujipamba kama Dr Rice.Robert Gate wa Pentagon pia ana real Phd,lakini hata siku moja ajiiti dr Gate.
  Tukubali na tunafuuta mfumo wa Uk kielimu .Hata jamaa zetu wa SUA wanaomaliza Vet medicine hakuna sababu ya kujiita DR!!!!UK wanajiita VET kutofautisha na medical doctors.Akifanya Phd ndio anaitwa DR.

  Hata uprofesa!!!kwa nini Mwandosya na Sarungi bado wanaitwa maprofesa,ingawa hawako katika any academic institutions?Na Kapuya vilevile.?Mpaka newspaper na vyombo vikisimama kuwaita watu hawa ma dr na maprofesa meaning yake inashuka sana.

  Dr Karume,Dr Mzindakaya,Dr Nchimbi,Dr Fumbuka,Dr Chageni etc...Oh my God!
   
 2. M

  Mike 1234 JF-Expert Member

  #2
  Dec 16, 2009
  Joined: Feb 23, 2009
  Messages: 1,634
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ujiko kaka, watz tunapenda sana tuonekane tumesoma wakati si kweli,na magazeti yetu nayo ndo hayo yanayo wapandisha hawa,wakiacha kuwaita dr prof nafikiri na watu wataacha,tatizo lingingine watanzania wanajua mtu akiwa dr au pro ndo anakuwa kiongozi mzuri kitu ambacho si kweli,
   
 3. M

  Mbunge wa CCM JF-Expert Member

  #3
  Dec 16, 2009
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  we kaa sawa tu, dr makamba is arround the corner and dr. mgombea ubunge is comming soon!!!!!!!!

  unajua kuna falsafa inasema "nothing is a thing" ndio maana utasikia watu wanasema "if you dont have anything to do, dont do it here" kwa uzefu wangu hizo phd zinazoonekana kwenye media ni evidence kuwa the media has nothing in connection with those persons,

  na usilauumu media, mimi nimewahi kuona gari ya kapuya imeandikwa "mr and mrs professor juma kapuya" ubavuni, hapo huwezi kulaumu media, bali hao walioandika ambao wanaleta hadharani their "nothing" in them!
   
 4. Kang

  Kang JF-Expert Member

  #4
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 24, 2008
  Messages: 5,120
  Likes Received: 615
  Trophy Points: 280
  Nadhani Ferguson na McCartney wanna Knighthood ambayo ni Sir. siyo PhD ambayo ni Dr.
  Professa nayo inakuwa kama inakuganda kama umefundisha miaka mingi, watu wanakuwa wamesha zoea. Mengine ni ujiko tu kwa sababu TZ ukiwa na elimu kubwa unaonekana wa maana zaidi.
   
 5. M

  Mundu JF-Expert Member

  #5
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 26, 2008
  Messages: 2,719
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  kwa vinchi vyetu vidogo, mimi nadhani hakuna ubaya wa watu kutambuliwa kwa academic credentials zao! Lakini ni zile za ukweli tu. Ni mambo ya aspiration tu kwa vijana wadogo ili nao waote kuwa kama hao.

  USA na UK kuwa Dr (PhD) ni kitu cha kawaida sana. Wao wako kwenye dunia nyingine wakuu.
   
 6. Ngalikihinja

  Ngalikihinja JF-Expert Member

  #6
  Dec 16, 2009
  Joined: Sep 1, 2009
  Messages: 16,399
  Likes Received: 3,726
  Trophy Points: 280
  Sifa ndugu yangu, Watanzania tunapenda sana kuonekana tumesoma........... na njia tunazotumia kuonyesha usomi wetu ni Dr, Prof. au kuongea kiingereza kwa saaaaaaaaaanaaaaaaaaaaaaa................ hata kama kiingereza chenyewe tunakivunja.......
   
 7. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #7
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Sikujua kuwa Lawrence Gama naye ana Phd????RIP
   
 8. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #8
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Kama vile tunavyoona jinsi gani nchi masikini zinabadilishana nafasi na nchi tajiri katika mambo ya kidini, huku wahubiri kutoka nchi kama Nigeria wakienda kuwahubiria wazungu dini ambazo wazungu walikuja kuhubiri Afrika miaka 100 iliyopita, kuna kubadilishana nafasi katika nyanja za jamii pia.

  Inaonekana ile ari ya "Tanzania ni nchi isiyo matabaka" inakwisha sasa, na watu wengi waliochovya kwenye kibuyu cha asali ya ulimbwende wa kimagharibi sasa wanataka kuchonga mzinga.

  Wakati wenzetu wanaona kujiita majina ya vyeo na usomi ni ukiritimba uliobobea ulimbukeni (wengine hata wanataka watoto zao wawaite kwa majina yao ya kwanza), sie tuliojulikana kwamba hatuna matabaka, tuliokuwa tukiitana "Ndugu" (hivi hili neno bado linatumika siku hizi katika kuamkuana na kutambulishana?) sasa tumetupilia mbali ndugu, tunakumbatia "uheshimiwa", tulitaka hata kumpa rais "utukufu" na kila mtu anataka "udaktari" hata wa kuchonga.

  Na hata wahashamu wanawania ubunge, kijacho sintashangaa kuona wabunge wanataka uhashamu.

  Pengine kumaliza shida yote wengine watataka urais ubadilishwe uwe usultani au ufalme kabisa, tujue moja.

  Chonde !
   
 9. m

  mwanamasala JF-Expert Member

  #9
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 20, 2009
  Messages: 248
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kang,Alex Ferguson anayo hon. doctorate from Manchester Met University na Paul McCartney anayo toka YALE university.
  Hawa hawatajiita Drs hata media kamwe
   
 10. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #10
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Sasa wote hawa wawili ni Knights of the British Empire, wamekuwa knighted na Queen na officially wanakuwa addressed kama "Sir" which is far more prestigious than a doctorate, kwa hiyo ukiwaita doctors ni kama una wa demote.

  Ndiyo mana nasema huu ni ulimbukeni. Kwa sababu unaweza kuishia kumuita mtu Sir Dr Ambassador Chief Professor Eng Judge. So and So.

  How awkward.
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Dec 16, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Its just a prototype of utopia societies pleasing each other with fake titles, fake names and fake personalities

  Its only one minister who came out and say that he is not a doctor na wakamuelewa

  Just sad!!!
   
 12. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #12
  Dec 16, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Ulimbukeni, ulimbukeni tu hakuna lolote!
   
 13. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #13
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Halafu katika kutafuta sarakasi hizi, tunasahau mambo ya msingi kabisa.

  Kama vile, elimu haiwezi kupimwa kwa makaratasi wala miaka ya mtu aliyoenda shule.

  Walioelimika - kwa kwenda shule au la- wanalielewa hili na hata hawababaiki na mi title ya mtu, rather wanaangalia mtu anasema na kufanya nini.
   
 14. Semilong

  Semilong JF-Expert Member

  #14
  Dec 16, 2009
  Joined: Mar 5, 2009
  Messages: 1,711
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  mwanao umemvalisha joo akiwa vidudu unadhani akifika form six ataacha kujiita dokta
   
 15. Geeque

  Geeque JF-Expert Member

  #15
  Dec 16, 2009
  Joined: Aug 17, 2007
  Messages: 848
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Hon Pres.Sir.Prof.Dr.Gen.Admiral.Field Marshal Iddi Amin Dada B.A,B.Sc,M.Sc,MD,LL.B,LL.M,PhD.
   
 16. V

  Vakwavwe JF-Expert Member

  #16
  Dec 17, 2009
  Joined: May 16, 2009
  Messages: 507
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  kaazi kwelikwelii! na ndio maana wanakosea hata kwenye kujitambulisha..unakuta mtu anajidk/anajiprof/anajieng/anajichungaji na hata mamr. nao wanajimr.....
  mwalimu wangu wa lugha aliniambia kuwa ukiambiwa ujitambulishe unaanza straight na jina lako halafu unamalizia na hiyo title kama ni muhimu sana. kwa mfano....''naitwa Vakwavwe Ngogo,,mchungaji wa the ngogoz mission international....na sio kuanza kusema mimi ni mchungaji vakwavwe ngogo. vivyo hivyo kwa title zingine. now i know ilikoanzia hata ikawa common ni kwa sababu ya watu kutaka sifa, kudhani wanapandisha p kumbe kwa wanaojua wanaona ni upuuzi tu..
   
 17. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #17
  Dec 17, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,202
  Likes Received: 863
  Trophy Points: 280
  Ni tabia yetu: Angalia hapa chini:

  MRT: As you may be aware, Your Excellency, Arthur and I are very concerned about a number of outstanding issues arising out of the implementation of the Global Political Agreement.
  AGO: Point of order, Your Excellency, the Prime Minister has perhaps forgotten that I am the Deputy Prime Minister of the Republic of Zimbabwe, and his use of only my first name is an offence against my dignity as the Deputy Prime Minister of the Republic of Zimbabwe.
  MRT: The …
  AGO: The Global Political Agreement is clear on this issue. It makes it clear what my position and title shall be, and that title is clearly that of Deputy Prime Minister of the Republic of Zimbabwe.
  MRT: We have matters of substance to get through here…
  AGO: But if Zimbabwe is ever to be the Singapore of Africa, as Deputy Prime Minister of the Republic of Zimbabwe, I insist that we proceed in an orderly and strategic manner.
  RGM: Very well, very well, Deputy Prime Minister.
  AGO: … of the Republic of Zimbabwe.
  RGM: Yes, yes, Deputy Prime Minister of the Republic of Zimbabwe, what is it you want from me?
  AGO: We are highly concerned, President of the Republic of Zimbabwe.
  GC: (coughs gently) You have forgotten, perhaps, gentlemen, that he is Head of State and Government and Commander-In-Chief of the Zimbabwe Defence Forces.
  MRT: But I am the Head of Government!
  There is a burst of laughter. GC collapses into mirth, as do RGM’s security men to RGM. MRT’s security men also start laughing but are silenced by a glance from MRT.

  MRT: The Global Political Agreement says …

  He is interrupted by more laughter.
  GC: almost crying through his laughter and pointing a finger as he gasps – He believes it, he actually believes it. He believes those words are worth the paper they are printed on.
  There is another burst of laughter. One of the security guards utters “Mai vangu Gumbo imi, mai vangu Gumbo kani” through his laughter. AGO also starts to laugh, a little uncertainly at first. One of the security men laughs so violently that he has a coughing fit and leaves the room in a burst of coughs and hiccups. RGM holds up his hand and there is silence.

  RGM: You were saying?

  MRT: We are concerned about the outstanding issues, Your Excellency.
  AGO: What this intellectual midget means to say, Your Excellency, Head of State and Government and Commander-in-Chief of the Zimbabwe Defence Forces…
  GC: You forgot that he is also Chancellor of the University of Zimbabwe, Chancellor of the National University of Science and Technology, Chancellor of Africa University, Chancellor of Solusi University, Chancellor of Midlands State University, Chancellor of Chinhoyi University of Science and Technology and Chancellor of Bindura University of Science Education.
  AGO: Your Excellency, Head of State and Government and Commander-in-Chief of the Zimbabwe Defence Forces, Chancellor of the University of Zimbabwe, the National University of Science and Technology, Africa University, Solusi University, Midlands State University, Chinhoyi University of Science and Technology and the Bindura University of Science Education…
  GC: He is also the Second Husband of the Second First Lady.
  AGO: Your Excellency, Head of State and Government and Commander-in-Chief of the Zimbabwe Defence Forces, Chancellor of the University of Zimbabwe, the National University of Science and Technology, Africa University, Solusi University, Midlands State University, Chinhoyi University of Science and Technology and the Bindura University of Science Education and Second Husband of the Second First Lady, we are increasingly concerned about the apparent absence of your intellectual clarity on issues, the absence of any evidence of macro-economic management, and your consistent failure in the deployment of strategic technological apparatus.

  ...............
   
 18. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #18
  Dec 13, 2017
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,982
  Likes Received: 729
  Trophy Points: 280
  nimeikuta sehemu.
   
 19. baba swalehe

  baba swalehe JF-Expert Member

  #19
  Dec 13, 2017
  Joined: Jun 6, 2017
  Messages: 2,156
  Likes Received: 1,724
  Trophy Points: 280
  Dr maguu
   
 20. s

  salome peter JF-Expert Member

  #20
  Dec 13, 2017
  Joined: Nov 26, 2016
  Messages: 378
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 60
  Dr Philemon Ndesamburo..matehemu, Dr Reginald Mengi Post yako ni nzuri sana ina meaning ya hekima kabisa watu wamesotea kusoma hadi kupata udr wengine waiokota tu kwenye majukwaa tena wenye pesa tu ndio hujiita hivyo wakati hata wenye kipato cha chini kuna vitu vya maana kibao wanachangia kwenye jamii
   
Loading...