Udini, Ukanda na sasa Utanganyika na Uzanzibari; hizi mbegu zisipopigwa marufuku kwa vitendo hatutobaki wamoja

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
876
4,101
Mwenyenzi Mungu alipotupa rasilimali alitupa pia mtu wakutupatia uhuru; mtu huyo alipopewa mamlaka yakutuongoza alipewa pia mbinu sahihi za kutuleteta pamoja. Mbinu hizi zilipitwa tunu na zilipandwa kwenye nafsi za watanzania . Baadhi ya mambo yaliyotuleta pamoja yalikuwa.

1. Lugha- pamoja na lugha zetu ila kiswahili ndiyo lugha ya Taifa. Miaka yote ya mwalimu hakujawahi kutokea mamlaka iliyobeza kiswahili. Pamoja na kukishika kiswahili wasome wetu wote walikufahamu vyema kiingereza.
Leo wasomi wamekikataa kiswahil kwa sababu za kuwekeza kwenye kiingereza nacho kiingereza kimetukataa.

2. Alipiga vita dini kuingia kwenye siasa; viongozi wa dini walikaa kwenye nyumba za ibada wakiendesha ibada.
Watawala wa sasa wamechukua viongozi wa dini wanaambatana nao kila wanapokwenda. Lakini pia kila kazi ndogo wanayofanya viongozi wa dini wamekuwa wakipewa ujira wa bahasha za kaki; matokeo yake leo viongozi wa dini wamegawana majukwaa kulingana na vyama vya siasa.

3. Alipiga marufuku ubaguzi; Aliunganisha Tanganyika na Zanzibar kuzaa Tanzania
Wanasiasa wasio na maono wakakiuka miiko ya umoja huu wakaanza kutengeza na kuisimamisha Zanzibar. Kwa kuwa Mwenyenzi Mungu alimpa maono ya kupinga ubaguzi mwaasisi wetu na tukayakiuka sasa Watanganyika wanaitaka nchi yao.

Haya mambo yasipojadiliwa wazi na kuwekewa miiko si ya kutumia dola, bali maridhiano basi tunakwenda kuruhusu kuingiliwa na maadui watatu wa Dunia ya sasa nao ni

1. Uhalifu wa kimataifa ikiwemo ugaidi. Maeneo yote yasiyo na umoja ni makazi ya waasi ambao ulimwengu wa sasa unawaita magaidi.

2. Wizi mkubwa wa rasilimali kwa kutumia utengano; rasilimali zetu zinakwenda kuendelee kutumika kuwawezesha wanasiasa wabaki madarakani. Tumeshuhudia kila ikikaribia uchaguzi lazima rasilimali ziuzwe kwa miswada na mikataba ya siri na dharura.

3. Tunakwenda kuzalisha taifa lakutumikishwa, kila kitu tunaaminishwa hatuwezi. Ukikosa watu katika taifa lolote umekosa Taifa. Ukiona viongozi wanawatetea wageni means wenye nchi hawana watetezi
 
Kikubwa maliasili za nchi zisiuzwa mambo ya kutoboa au kutotoboa kwa kuonea aibu watu hayana nafasi
 
Hoja yako namba 3,

Wageni hupeleka sehemu foreign direct investment na lengo ni kuweza kutengeneza ajira huko na yeye kuzalisha na kupata faida na hii ndio nchi zilizokuwa masikini miaka ya 1950 kama Singapore zilifanikiwa kujikuza na kukua na kuwa na hali nzuri siku zote wageni wataleta vitu vigeni kama technolojia.

Fedha na skills muhimu na wazawa kunufaika chukulia mfano hali ilivyokuwa hapo mwanzo simu ikiwa ttcl na sasa kuwa na kampuni binafsi na ni kiwango gani zimekuza telecomm na pia kusaidia kukua kwa mainjinia wa sekta hiyo hapa kwetu acha waje waliotuzidi tujifunze wafundishe watu na sisi tukue ili baadae tuweze kusimama imara zaidi ya waliotufundisha.
 
Mwenyenzi Mungu alipotupa rasilimali alitupa pia mtu wakutupatia uhuru; mtu huyo alipopewa mamlaka yakutuongoza alipewa pia mbinu sahihi za kutuleteta pamoja...
Serikali ya ccm inawachekea hao Kwa kisingizio Cha kuonekana wanakandamiza Demokrasia,huu ni uhaini.
 
Back
Top Bottom