Udini sasa mpaka kwenye Mapenzi

Udini sasa mpaka kwenye Mapenzi

jambo1

JF-Expert Member
Joined
Jul 5, 2009
Posts
241
Reaction score
29
Jamani tunakoelekea sasa ni kubaya..
Jamaa angu muislam alikuwa na girlfriend wake mkristo mapenzi yao yalidumu kwa mwaka mmoja na nusu hiv lakin hiv karibuni ndo wakaparaganyika kwa sababu yule msichana alimwambia boy wake kuwa hawezi kuwa na yeye kwakuwa ni muislam wakati muda wote alikuwa anajua kuwa boy wake ni muislam..
Jamaa anadai siku moja wakaticwako pamoja walikuwa wanaangalia tv wakaona lile tukio la Zanzibar la kujeruhiwa kwa padri na kuchomwa moto makanisa basi yule msichana akaanza kuponda kuwa waislam ni wakatili..jamaa akamwambia sio hivyo..hayo yamepandikizwa kidiasa tu..mdada hakuelewa jamaa naye akamuuliza je na yule shekhe aliye mwagiwa tindikali kanwagiwa na wakristu.?hivyo likitokea jambo usigeneralize.
Sasa leo na mimi yamenikuta kuna dada nachat nae kwa takriban miezi miwil sasa ila leo ameniuliza dini yangu nkamwambia kuwa mimi baba angu ni muislam na mama angu ni mkristu akasema mbona jina lako ni la kiislam..akasema yaan yeye hapendi kabisa urafiki na waislam kwa kuwa ni wakorofi..nkamuuliza ukorofi wa waislam umeanza lini akasema mifano ile ile ya zanzibar..nikamuuliza mbona miaka yote haikuwa ikionekana hivyo..?hakujibu..
My Take JK na CCM wanatupeleka kubaya..ndoa za watu ziyavunjika kwa sababu ya udini..tusubiri tuone tuendako..
 
mnayataka wenyewe....dini itaendelea kuwa nafasi muhimi katika maisha ya watu.

sasa wewe mmependana alafu mnajua kabisa kuwa mkitaka kuoa lazima muende kwa wazazi....wazazi ishu ya dini kwao muhimu so hilo lazima mlifikirie.
 
Ila ndiyo tulipofika bila kutafuta wa Imani yako
ni tabu ila ukweli Serikali yetu inasababisha yote

Leo asbh kuna dada kanambia wazi kuwa wa imani yake hawajaisha hivyo hana sababu
kutafuta wa Imani nyingine

Hali ni tete sana ndugu.
 
Mwenyezi atunusuru tusifikie yale tunayosikia kule Nigeria!

Ni kweli Georgina. Viongozi wakuu wa dini wanapaswa wakae meza moja waondoe tofauti za dini wakiishirikisha serikali.
Hata hivyo huyo dada kimeo.
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK
mnayataka wenyewe....dini itaendelea kuwa nafasi muhimi katika maisha ya watu.

sasa wewe mmependana alafu mnajua kabisa kuwa mkitaka kuoa lazima muende kwa wazazi....wazazi ishu ya dini kwao muhimu so hilo lazima mlifikirie.

Huyu mleta uzi baba yake ni Mwislamu na mama yake ni Mristo: So, inabidi pia atafute mama mwingine wa Kiislamu?
Labda mleta uzi alitaka kuiga kama alivyofanya baba yake!
 
Ni kweli Georgina. Viongozi wakuu wa dini wanapaswa wakae meza moja waondoe tofauti za dini wakiishirikisha serikali.
Hata hivyo huyo dada kimeo.

Ila hli suala la vikwazo ktk ndoa kutokana na dini tofauti sio suala jipya. Suala hlo limekuwa kikwazo toka enzi. Mimi pia ni muhanga wa hlo. Ila kwa sasa chuki ndo znaongezeka.
 
Last edited by a moderator:
Jamani tunakoelekea sasa ni kubaya..
Jamaa angu muislam alikuwa na girlfriend wake mkristo mapenzi yao yalidumu kwa mwaka mmoja na nusu hiv lakin hiv karibuni ndo wakaparaganyika kwa sababu yule msichana alimwambia boy wake kuwa hawezi kuwa na yeye kwakuwa ni muislam wakati muda wote alikuwa anajua kuwa boy wake ni muislam..
Jamaa anadai siku moja wakaticwako pamoja walikuwa wanaangalia tv wakaona lile tukio la Zanzibar la kujeruhiwa kwa padri na kuchomwa moto makanisa basi yule msichana akaanza kuponda kuwa waislam ni wakatili..jamaa akamwambia sio hivyo..hayo yamepandikizwa kidiasa tu..mdada hakuelewa jamaa naye akamuuliza je na yule shekhe aliye mwagiwa tindikali kanwagiwa na wakristu.?hivyo likitokea jambo usigeneralize.
Sasa leo na mimi yamenikuta kuna dada nachat nae kwa takriban miezi miwil sasa ila leo ameniuliza dini yangu nkamwambia kuwa mimi baba angu ni muislam na mama angu ni mkristu akasema mbona jina lako ni la kiislam..akasema yaan yeye hapendi kabisa urafiki na waislam kwa kuwa ni wakorofi..nkamuuliza ukorofi wa waislam umeanza lini akasema mifano ile ile ya zanzibar..nikamuuliza mbona miaka yote haikuwa ikionekana hivyo..?hakujibu..
My Take JK na CCM wanatupeleka kubaya..ndoa za watu ziyavunjika kwa sababu ya udini..tusubiri tuone tuendako..
jambo1 acha kupandikiza chuki za kidini hapa, katika watu wasiojali udini na ukabila katika mapenzi ni wanawake na wao ndio walitokomeza udini na ukabila hapa Tanzania. Sio Nyerere, sio Mwinyi wala Mkapa, ni wanawake wa Tanzania, wanakubali kuwa na marafiki na waume wa kabila na dini yoyote ambapo imepelekea Tanzania hii tumeoleana kiasi kwamba muingiliano huo umeleta umoja wa kitaifa. HONGERENI WANAWAKE WA TANZANIA.
 
Msela wangu yeye wameachana yeye alikuwa RC mama Muislam walikuwa wamezaa mtoto alikuwa anaitwa Catherine Sasa wamemuita Sumaiya... hata simu za jamaa hapokei kabisa, ingawa Kabla ya hapo kila Mtu alikuwa na Uhuru wa kuabudu kivyake ila Hali ilibadilika baada ya vurugu za Buseresere na mwanaume kudai Waislamu wana makosa
 
Sometimes uko realistic kwa kweli.
Dini ina nafasi yake.

mnayataka wenyewe....dini itaendelea kuwa nafasi muhimi katika maisha ya watu.

sasa wewe mmependana alafu mnajua kabisa kuwa mkitaka kuoa lazima muende kwa wazazi....wazazi ishu ya dini kwao muhimu so hilo lazima mlifikirie.
 
Serikali haihusiani na Imani zenu
Kwani mkiwatafuta wanakataa? labda linapokaribia suala la kuoana
Wanasema Mwanamke hana DINI km mkipendana Mkuu wa Wilaya au Katibu Tawala wake atawapeni Cheti ambacho ndicho hichohicho kitolewacho na Padri au Sheikh
Mimi ni Mkristo lakini nimeoa Muislam na nyumba zangu ndogo zote ni Waislamu Kennedy na Jambo 1 Serikali haihusiki na kusali kwenu au kuoa nyie ni Wakristu tafuteni Waislamu watawapenda tu na mtaamua km mbadili DINI muwe Waislamu Serikali haitahusika. Bado Waislamu wapo na hata Wapagani hizi tafrani za DINI mbili zisitukwaze kwani kuna Budha nk na hakuna aliyerudi toka waliko wafu wakatuelezea kuwa huko wanasali
 
Last edited by a moderator:
Swala la dini ni muhimu sana katika maisha ya ndoa, makubaliano ni ya lazima kabla ya kuoana
Mwisho wa cku watoto ndo watakaopata shida..hawajui waelekee wapi
 
Tatizo kwangu ni chuki za kidini, lakini kuiangalia dini kama kigezo cha mpenzi kwenda katika ndoa ni swala la siku nyingi kwa watu wa dini kwa misingi ya dini zao. Bahati nzuri maridhiano kwa watu wa dini tofauti yalifikiwa bila ya kuguswa (au kuguswa sana) na hizi hisia za sasa.
 
Huyu mleta uzi baba yake ni Mwislamu na mama yake ni Mristo: So, inabidi pia atafute mama mwingine wa Kiislamu?
Labda mleta uzi alitaka kuiga kama alivyofanya baba yake!
Suala hapa ni kuangalia na kutafakari hali unavyokwenda..mi nafikir suala hili kwa sasa limekuwa serious sana kuliko wakat nwingne wowote..
Mambo yamekuwa mabaya zaidi..
 
Tatizo kwangu ni chuki za kidini, lakini kuiangalia dini kama kigezo cha mpenzi kwenda katika ndoa ni swala la siku nyingi kwa watu wa dini kwa misingi ya dini zao. Bahati nzuri maridhiano kwa watu wa dini tofauti yalifikiwa bila ya kuguswa (au kuguswa sana) na hizi hisia za sasa.
Umesema sawa kabisa mkuu..chuki za kidini zimezidi..sasa hiv kuna baadhi ya nyumba za kupanga wanaangalia sana dini yako..ni hatari sana..
 
Back
Top Bottom