nguvumali
JF-Expert Member
- Sep 3, 2009
- 4,923
- 1,325
Watu wapatao 500 wauawa nchini Nigeria
Maafisa wa serikali Nchini Nigeria, wamesema idadi ya watu waliofariki kufuatia mapigano yaliyotokea mjini Jos hapo jana, imefikia watu mia tano.
Walioshuhudia tukio hilo wanasema watu kadhaa waliojihami kwa mapanga walishambulia vijiji kadhaa karibu na mji wa Jos, kutoka maeneo ya milima. Wengi wa waliouawa ni watoto na kina mama.
Kaimu rais wa nchi hiyo Goodluck Jonathan, ameamuru wanajeshi wa nchi hiyo kuingilia kati na kuzima machufuko hayo. Vile vile rais huyo ameagiza wanajeshi hao kuhakikisha kuwa hakuna silaha zaidi zinaingizwa katika eneo hilo ili kuzuia mashambulizi zaidi.
Serikali ya Nigeria ilitangaza hali ya tahadhari katika mji huo tangu mwezi Januari mwaka huu, baada ya mapigano makali kati ya Waislamu na Wakristo, yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu mia mbili.
source........http://www.bbc.co.uk/swahili/news/story/2010/03/100308_nigeriaupdate.shtml