Udini Nigeria , raia 500 wapoteza maisha.

wakubwa what is exactly the source of this problems? nani mkorofi waislamu au wakristo? , kiini hasa, and what about in Tz are we safe??

Nchi haina Rais wa kutoa muelekeo when it is needed.Jamaa anaugua pole.
 
wakubwa what is exactly the source of this problems? nani mkorofi waislamu au wakristo? , kiini hasa, and what about in Tz are we safe??

Chanzo cha tatizo kiko ndani ya mioyo ya watu na siyo dini. Nilibahatika kusoma na Wanyarwandwa wawili huko nje. Mmoja alikuwa Mtutsi na mwingine Mhutu. Niliwauliza hivi: kwa nini Watutsi na Wahutu (wote Wakristo) mweze kuuana hivyo?

Wao wakanijibu hivi: Kilichotokea Rwanda hakiwezi kuelezwa kirahisi rahisi tu. Mtu asiyejua undani wa tatizo lenyewe mara nyingi atatoa hukumu ya jumla tu (blanket judgement). Lakini, fikiria hivi. A (Mtutsi) ni paroko wa parokia fulani na B (Mhutu) na yeye ni paroko wa parokia fulani.

Kwa vile, uadui ulikuwa kati ya Watutsi na Wahutu, kwa vyovyote vile Wakristo Watutsi wataenda kuomba hifadhi kwa paroko A (Mtutsi mwenzao kwa kuelewa kuwa yeye atawaelewa vizuri/hatawatilia sana mashaka kuwa ni wahalifu) na Wahutu kwa paroko B (kwa vile nao pia wataona kuwa Mhutu mwenzao atawaelwa kuwa wao siyo wahalifu).

Ikiwa walioanza kuwashambulia wengine walikuwa kutoka parokia ya A (Watutsi), si watu wengine wataona kila mtu anayetoka parokia ya A (pamoja na paroko mwenyewe) ni adui wa B?

Lakini chanzo cha uadui wenyewe bado hakijaelezwa ila itatokea tu kuwa watu wa A wataanza kupigana na watu wa B hata kama wao wenyewe hawajui kinachowapiganisha ni nini. Rafiki yangu mmoja alitoa mfano huu: kama mbwa wako akigundua kuwa una kipande cha nyama au mfupa mkononi atakunyemelea. Ukijifanya unainama na kuokota kijiti na halafu ukitupe mbele, atakimbilia hicho kijiti akidhani kuwa ni nyama au kipande cha mfupa wakati nyama au kipande umebaki nacho mkononi.

Hivyo, ni wazi kuwa mara nyingi watu wanaweza kuwa maadui na kuanza kuuawana na ikitokea ukiwakalisha chini na kuanza kuwauliza chanzo ni nini unaweza kugundua kuwa hata wao wenyewe hawajui.

Kuna mfano mwingine alinisimlia padre mmoja Mholanzi aliyefanya kazi Uganda. Alisema parokia (sehemu) alipokuwa akifanya kazi watu waliamini sana uchawi na kulikuwa na tuhuma mbalimbali. Hivyo, wakristo wake waliishi kwa woga sana.

Yeye kama padre aliona afanye utafiti ili ajue kuna nini na kwa pamoja watafute suluhisho la tatizo la uchawi. Hivyo, aliwaita viongozi na kuwaomba waanze kutafuta wachawi na waone namna gani wataweza kupata suluhisho la kudumu.

Walianza na kusema kila anayefahamu (alishaona/shuhudia) kuna uchawi na wachawi ajitokeze. Walijitokeza watu kadhaa na kuanza kuuelezea. Padre huyo akasema sasa inabidi mwenye ushahidi atoe ushirikiano ili kuondokana na tatizo lenyewe.

Walianza na wale waliojitokeza na kuwauliza, unamfahamu machawi yeyote? Aliyeulizwa alisema aliskia kutoka kwa X. Wakaenda kwa X na X akasema aliambiwa na Y na Y alipoulizwa alisema aliambiwa na Z. Mwisho siku, walishindwa kumpata mtu aliyeweza kusema alishamwona mchawi bali kila aliyeulizwa alisema: 'alisikia kwa fulani ila yeye hajawahi kumwona mchawi'.

Mambo mengi tunayoamini yanakuwa hivyo. Huwa ni mapokeo au matokeo ya kile tulichorithishwa. Ndiyo maana inafaa kufanya 'discernment' ili tusije tukaamini kitu kisicho au kama tunachoamini ndivyo kilivyo, tusije tukaamini tafsiri potofu.

Baada ya kusema haya, naweza kusema kuwa tukitaka kutoa hukumu ya jumla bila kuona tatizo ni nini tutasema Wakristo au Waislamu ndio wabaya (tutawahuku watu kutokana imani zao na siyo kutokana na ushiriki wao katika ovu husika).

Lakini tukitaka kujua ukweli au chanzo cha ugomvi ni nini tutaenda pale ugomvi ulipoanzia na kuona tatizo lilikuwa nini. Pengine lilikuwa kwamba watu wawili(Mkristo 1 na Mwislamu 1) walikuwa wanabishana kuhusu imani zao na kisha kupata washabiki na hatimaye wakaanza kugombana.

Baadaye watu wengine waliungana nao na wao bila kujua sababu wakaanza kuunga mkono mwumini wa dini yao na hatimaye kukatokea mapigano na umwagaji damu.

Unaona? Kumbe tatizo siyo dini (Mkristo au Mwislamu) bali hao watu walipokeaje kile kilichosemwa na mwenzao, kama wao wenyewe (Mkristo 1 na Mwislamu 1) na kisha wengine waliojiunga.

Nilishashuhudia tukio la namna hii. Kwenye kituo fulani cha daladala jijini Dar es Salaam, mwanamke mmoja aliibiwa simu na mtuhumiwa akakimbia. Kulikuwa na mchoma chipsi aliyemfahamu yule mama. Aliacha chipsi zake na kuanza kumfukuza yule mwizi.

Huyo kijana alikuwa na mbio sana. Yule mwizi alipoona kijana huyo anamkaribia, akatupa simu na kuendelea kulala mbele na akawa ame'save' kipigo. Yule kijana (Msamaria Mwema) akaiokota ile simu na kurudi nayo ili ampe yule mama. Yule mama lipoiona (sijui kwa furaha au nini) akapaza sauti: "Jamani! Simu yangu imepatikana! Hii hapa!

Basi watu wasiojua hili au lile wakaanza kumpa kipigo yule mkaanga chipsi (Msamaria Mwema) hadi kumwua wakidhani ndiye mtuhumiwa. Baada ya kumwua ikagundulika kuwa yeye hakuwa yule aliyekwapua simu ila alitaka amkabidhi simu yule mama yeye mwenyewe (pengine akidhani angepata asante).

Hivyo, katika 'mob justice' haiwezekani kusema nani alikuwa 'right' au 'wrong'. Ila inatokea tu kuwa watu wana'react' siyo kwa kujua bali kwa kuhisi tu kuwa fulani ndiye kafanya kosa, hivyo aadhibiwe.
 
Back
Top Bottom