UDINI na UZANZIBARI ndio vilimponza NYERERE? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

UDINI na UZANZIBARI ndio vilimponza NYERERE?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kibanga Ampiga Mkoloni, Jun 12, 2012.

 1. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #1
  Jun 12, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,565
  Likes Received: 1,653
  Trophy Points: 280
  Nimejaribu kutafakari ni kwanini Nyerere alimuachia nchi MWINYI na si MKAPA au SALMIN maana nikiangalia picha
  [​IMG]
  427121_1899705787730_190398420_n.jpg

  naona ni watu ambao alikuwa nao karibu sana. Nadhani alimuachia Mwinyi kwa kuogopa kuwa yeye alikuwa Mtanganyika na sasa ilibidi iwe zamu ya Mzanzibari pia ilikuwa ni zamu ya muislam kwa kuwa pia na yeye alikuwa mkristo, Je kwanini akumuachia SALMIN? Nadhani SALMIN alikuwa AOU, Kwahiyo akaona ni busara kumpa MWINYI na sio SALMIN ambaye alikuwa na majukumu makubwa zaidi huko ETHIOPIA.

  Je ni kwa nini alimpa/alishinikiza MKAPA apewe, Na amini hapa turufu ilikuwa ni UDINI kwa maana ya kwamba ilikuwa ni zamu ya Wakristo baada ya MWINYI kutoka na ndipo MKAPA alipo ukwaa Uraisi. Je na MKAPA aliendeleza lilelile kwa kumuachia KIKWETE? Ni kwanini akumuachia SALMIN? namiini ilikuwa ni zamu ya SALMIN kama Muislam na Mzanzibari.

  Ni hayo tu ndugu zangu.
  [​IMG]
  418104_1898192029887_907608624_n.jpg
   
 2. H

  Hute JF-Expert Member

  #2
  Jun 12, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 6,053
  Likes Received: 3,920
  Trophy Points: 280
  duh, mshikaji mfupii,dah, a jabu yake sasa mwinyi mfupi kuliko yeye...
   
 3. J

  JokaKuu Platinum Member

  #3
  Jun 12, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,765
  Likes Received: 4,980
  Trophy Points: 280
  Kibanga,

  ..ume-confuse kidogo ktk timeline yako.

  ..Salim Salim alikuwa waziri mkuu toka Sokoine alipofariki mpaka mwaka 1985 wakati Mwalimu anang'atuka. baada ya hapo akawa Waziri wa Ulinzi na "naibu waziri mkuu" wakati Mwinyi ameingia madarakani.

  ..Katiba ya nchi wakati huo ilikuwa inaelekeza kwamba Raisi akitoka Zanzibar, basi Waziri Mkuu atatoka Bara na ndiye atakayekuwa Makamu wa kwanza wa Raisi. Kwa msingi huo Joseph Warioba,John Malecela,na Cleopa Msuya, wote walikuwa mawaziri wakuu and 1st Vice Presidents.

  ..Salim alikwenda OAU wakati wa utawala wa Raisi Ali Hassan Mwinyi.

  ..inasemekana Mwalimu alitaka kumuachia madaraka Edward Sokoine.

  ..baada ya Sokoine kufariki chaguo la Mwalimu likawa Salim Ahmed Salim ambaye alikuwa waziri mkuu wakati huo.

  ..tatizo lililotokea ni kwamba wa-Zanzibari walimzidi "mahesabu" Mwalimu Nyerere na kumchomeka Ali Hassan Mwinyi.

  ..majina yaliyopendekezwa kumrithi Mwalimu yalikuwa ni Rashidi Kawawa,Salim Salim,na Ali Hassan Mwinyi. makubaliano ilikuwa ni Kawawa na Mwinyi waondoe majina yao na kumuacha Salim Salim akipeta. Mwinyi, kutokana na ushawishi wa wana-mapinduzi, hakuondoa jina lake, na matokeo yake ikazuka ile hoja kwamba italeta picha mbaya ikiwa Waziri Mkuu[Salim Salim] atamruka Makamu wa Raisi[Ali Mwinyi] ktk kurithi nafasi ya Raisi wa Jamhuri.

  ..again, in 1995 Mwalimu alimuomba tena Salim Salim agombee lakini akakataa kwa kuamini kwamba ilikuwa ni zamu ya Mtanganyika kwa hivyo choice ya Nyerere ikawa Benjamin Mkapa.

  ..mwisho, inasemekana[hili sina uhakika nalo] baada ya kufariki Dr.Omar Ali Juma, Raisi Mkapa alimuomba Salim Salim aje kuwa makamu wa raisi kitu ambacho kingemuweka ktk nafasi nzuri zaidi kugombea Uraisi wa muungano.

  ..baada Salim Salim kurudi Tz, Raisi Mkapa alimteua kuwa mjumbe wa kamati kuu ya CCM na kumtunukia nishani ya juu kabisa ya mlima kilimanjaro which is reserved for head of states kama wakina Samora Machel. Again that was a nod frm Mkapa kwamba Salim Salim alikuwa anafaa kuwa Raisi wa Tanzania. Salim Salim kukosa Uraisi wa nchi hii naamini is bcuz of his own political miscalculations.

  NB:

  ..picha yako imeibua watu wengi sana wa zamani.

  ..kwa mfano kuna mlinzi wa Mwalimu akiitwa Mwang'onda.

  ..hata mpambe wake jamaa wa JWTZ nimemsahau jina lakini alikuwa mtu wa Mbeya.

  ..kwenye picha ya pili kuna Joseph Warioba,Hashim Mbita,Mustafa Nyang'anyi.
   
Loading...