Picha Adimu na Kumbukumbu Zake 1980s

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,918
30,259
Picha hiyo hapo chini kaniletea ndugu yangu na kaniandikia maneno haya:
"Picha adimu hiyo nimekutunuku, iandikie habari."

Kulia ni Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dr. Salim Ahmed Salim na Rais Ali Hassan Mwinyi.
Nyuma ya Dr. Salim Ahmed Salim ni Dr. Salmin "Komando" Amour.

Kwa kuwa nimeombwa niandike nitajaribu.
Nitawaangalia watu hawa kwenye picha na nitaeleza mimi nawakumbukaje.

Komando Dr. Salmin Amour hii "Doctorate" yake ilizua mjadala mkali sana magazetini katika miaka ya 1990.
Baadhi ya watu wakihoji ithibati yake.

Nakumbuka Ali Nabwa alitoa majibu ya utetezi lakini alipata shida sana.

Nakumbuka msomaji mmoja akasema hakuna haja ya watu kubishana kwa jambo ambalo ni rahisi sana kuthibitishwa.

Akasema itakuwa vyema ijulikane chuo alichosoma, utafiti wake wa huo uzamivu unahusu nini na nani alimsimamia, yaani nani "supervisor" wake na mwisho iwekwe "dissertation" yake isomwe.

Sikumbuki baada ya hapo nini kilitokea.

Naweza pia nikaeleza mkasa wa Dr. Salmin Amour kuiingiza Tanzania katika OIC mwaka wa 1993 vipi jambo hilo lilivyomkera Mwalimu Nyerere na kumpa shida kubwa sana Rais Ali Hassan Mwinyi.

Mkasa huu ulianza mwaka wa 1989 wakati Zanzibar ilipoiomba Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitaka Zanzibar ipate "Obsever Status" katika OIC.

Waziri Mkuu Joseph Warioba alilipeleka ombi lile kwa Salim Ahmed Salim aliyekuwa Makamu Waziri Mkuu.
Salim Ahmed Salim alizuia ombi lile.

Sasa Dr. Salmin Amour alipokuja kuitumbukiza Zanzibar katika OIC Bunge likawaka moto.
Likaundwa kundi la wabunge 55 waliodai kuwepo serikali ya Tanganyika.

Rais Ali Hassan Mwinyi akapata shida kubwa sana hali kadhalika Waziri wa Nchi za Nje Ahmed Diria.

Sukwa Said Sukwa akasema Bungeni kuwa anaeweza kuweka mambo sawa ni Mwalimu Nyerere.

Nyerere akasema Zanzibar ijitoe kwanza OIC ndipo yeye ataingia kuuzima moto uliokuwa unawaka nchi nzima.

Hivyo ndivyo ilivyokuwa.

1696303533885.png

1696303595163.png

Rais Ali Hassan Mwinyi 1985
 
Back
Top Bottom