Kubwajinga
JF-Expert Member
- Jan 23, 2008
- 2,193
- 299
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine. Katika pita pita yangu na kuchunguza nimegundua kuwa asilimia 65.78 ya uongozi wa Kamati Kuu ya CCM ni watu wa dini moja. Kama udini ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani, tunaweza kusema kusema kuwa Kamati Kuu ya CCM ina udini? Je kuna sababu yoyote ya msingi ya kwanini watu 25 kati ya 38 wawe ni wa dini moja? Je imeshindindikana kwa CCM kutafuta njia ya kuweza kugawa nafasi hizi kwa kuangalia uwiano wa dini?
Nikiwa mtu mwenye maslahi ya pekee kwenye CCM naona jambo hili si zuri na litazua manung'uniko yasiyo ya lazima. Kama kikundi, taasisi, au jumuiya fulani ina watu wenye sifa moja inayolingana, sifa ambayo inawatofautisha na watu wengine hasa ya vitu kama kabila, rangi, au dini basi mahali hapo ni pa kuangaliwa kwa karibu.
Katika siasa, tukitumia "Wangwe's Doctrine" kuwa endapo asilimia 50 ya watu wenye sifa hizo wakakutwa mahali pamoja ni ukabila/ukanda basi ni wazi mahali ambapo pana asilimia 65 ya watu wenye kulingana sifazao kutofautishwa na wengine basi napo patakuwa na tatizo, in this case udini (yaani idadi ya watu wa dini moja mahali pamoja ambayo haina maelezo ya kuridhisha).
wow... CCM haiguswi, au udini hauguswi?
Wakati mnaendelea na mjadala, wajumbe wenyewe ndo hawa hapa:
1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe
Mkuu MJJ,
Sijasoma article yako iliyofilisika kiuchambuzi kama hii. Kama nia ilikuwa ni ku-dilute issue ya ukabila ndani ya CHADEMA kama ulivyoiita, the "Wangwe Doctrine", basi imekufanya uchemshe zaidi.
Nilipokupongeza kwa kutimiza posting 10,000 nilikushauri ujaribu kuondoa ideologies zinazokufanya uache kufikiria sawia, lakini naona inashindikana. Chambua mambo kama unaweza, la kama haiwezekani, mwachie Mushi ku-raise unqualified issues.
Unataka kubisha kuwa hayo majina sio ya kiislam na hivyo kuifanya ccm chama cha kidini?
wow... CCM haiguswi, au udini hauguswi?
CUF ni chama cha kidini ya kiislam, CCM chama cha dini ya kiislam, chadema chama cha kikabila, NCCR mageuzi cha kikristo, DP cha kikristo, UDP cha kisukuma??!! CHAUSTA cha kipentecoste??? chagueni mnataka chama gani? cha mafisadi? cha kikabila au cha kidini?
Inaguswa sana, lakini tusiwazulie. Kasoro naona ni kwako wewe mkuu MJJ, maana naona hutaki kabisaa kuigusa CHADEMA, kunani mkuu MJJ??
kwi kwi kwi,
mimi nataka chama cha kiyahudi.... lol
Udini hapa nautafsiri kuwa ni wingi wa watu wa dini moja kwenye ngazi fulani ya uongozi ukilinganisha na ngazi nyingine.
- Tafriri yako ni finyu sana na imejaa jazba. Kwa tafsiri hii Zanzibar kuna udini kwa sababu baraza la wawakilishi lina waislamu wengi kuliko wakristu japo wakristu japo waislamu ni zaidi ya asilimia 90.
- Unaweza ukawa na hoja lakini kwa namna ulivyoiwakilisha unataka kumislead watu.
- Mbona hujatuambia hawa wajumbe wa kamati wanapatikanaje? R u sure hakuna wakristu wanawapigia kura kwenye mchakato?
UJUMBE UNAOYAKA KUTOA: wanachama wote wa CCM wawaunge mkono viongozi wa CCM kutokana na dini zao. Hii itarahisisha kuyumba zaidi kwa chama ambacho tayari kinachechemea. Naweza kukusuport kutokana na hii ideology lkn sio kutokana na hoja ulizotoa
Sasa nimeamini kabisaa kuwa ccm ni "chama cha kiislam" na kina udini baada ya kuona haya majina.......lol
Mkuu Mgaya,
Nakumbuka sana ulivyokitetea CHADEMA na ukabila wao. Kwa hiyo leo sioni ajabu mnapojaribu kugeuza mjadala ambao bado uko ndani ya CHADEMA ukichemka juu ya ukabila, mkitaka kuonyesha ummaa kuwa hata CCM nao wana u-dini. The TZ people are more inteligent than that. Chambua jinsi huo udini ulivyoingia CCM, ili tufananishe na ukabila wa CHADEMA.
Wakati mnaendelea na mjadala, wajumbe wenyewe ndo hawa hapa:
1. Ndugu Jakaya Mrisho Kikwete - Mwenyekiti
2. Ndugu Pius Msekwa - Makamu Mwenyekiti (Bara)
3. Ndugu Amani Abeid Amani Karume - Makamu Mwenyekiti(Zanzibar)
4. Ndugu Yussuf R. Makamba - Katibu Mkuu
5. Capt. (mst) George Huruma Mkuchika - Naibu Katibu Mkuu (Bara)
6. Ndugu Salehe Ramadhan Ferouz - Naibu Katibu Mkuu (Zanzibar)
7. Dr. Ali Mohamed Shein - Mjumbe
8. Ndugu Mizengo Kayanza Peter Pinda - Mjumbe
9. Ndugu Shamsi Vuai Nahodha - Mjumbe
10. Alhaj Ali Hassan Mwinyi - Mjumbe
11. Ndugu Benjamin William Mkapa - Mjumbe
12. Mzee Rashid Mfaume Kawawa - Mjumbe
13. Dr. Salmin Amour - Mjumbe
14. Ndugu John Samwel Malecela - Mjumbe
15. Capt. (mst) John Zefania Chiligati - Mjumbe
16. Ndugu Amos Gabriel Makala - Mjumbe
17. Ndugu Bernard Kamilius Membe - Mjumbe
18. Ndugu Kidawa Hamid Saleh - Mjumbe
19. Ndugu Samwel John Sitta - Mjumbe
20. Ndugu Pandu Ameir Kificho - Mjumbe
21. Ndugu Anna Abdallah - Mjumbe
22. Ndugu Rostum Aziz - Mjumbe
23. Dr. Mohamed Gharib Bilal - Mjumbe
24. Ndugu Pindi Hazara Chana - Mjumbe
25. Ndugu Andrew Chenge - Mjumbe
26. Dr. Maua Abeid Daftari - Mjumbe
27. Ndugu Samia Suluhu Hassan - Mjumbe
28. Ndugu Mohamed Seif Khatib - Mjumbe
29. Ndugu Haji Omar Kheri - Mjumbe
30. Dr. Abdallah Omari Kigoda - Mjumbe
31. Ndugu Abdurahman Kinana - Mjumbe
32. Ndugu Anne Semamba Makinda - Mjumbe
33. Ndugu Fatuma Said Ali Mchumo - Mjumbe
34. Ndugu Zakia Hamdan Meghji - Mjumbe
35. Ndugu Omar Yussuf Mzee - Mjumbe
36. Ndugu Emmanuel John Nchimbi - Mjumbe
37. Ndugu Ali Ameir Mohamed - Mjumbe
38. Ndugu Yussuf Mohd Yussuf - Mjumbe
Kuna thread ya mwanakijiji inaongelea mambo ya chadema hapa, hujaiona? mbona hujaja huko kuchangia?
Kama unaitaka nitakuwekea link hapa.
Fuata link ifuatayo:
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=15151
2008-07-02 09:46:16
Na Simon Mhina
Mengine.. nitawaandikia in private katika kulinda "heshima ya chama" chenu
Ile coalition itakayofungua kesi ya EPA...Huu ndio wakati muafaka wa kusema kitu ili wananchi waachane na hii mijadala ya udini na UKABILA!CUF ni chama cha kidini ya kiislam, CCM chama cha dini ya kiislam, chadema chama cha kikabila, NCCR mageuzi cha kikristo, DP cha kikristo, UDP cha kisukuma??!! CHAUSTA cha kipentecoste??? chagueni mnataka chama gani? cha mafisadi? cha kikabila au cha kidini?
Ndio hii aliyoandika hivi? Huku ndio unakokuita ku-criticize CHADEMA?
My Take:
- Kwanini Chadema isiwalipe viongozi wake? Hicho chama siyo taasisi ya dini au NGO, huu mtindo wa kulipa fedha za wao wenyewe na wengine kutolipwa ni mtindo mbaya. Hata mtindo wa Mbowe kutoa fedha yake mfukoni kwa ajili ya Chadema siyo mtindo mzuri kwani unamfanya aonekane kama ana maslahi zaidi ya mtu mwingine. Chama kiendeshwe kama Chama. Hata kama chama hakiwezi kuwalipa inavyopaswa ni muhimu kuwa na token payment hata kama Shs. 10,000 kwa mwezi kwa viongozi lazima walipwe, wasifanye kazi za chama bure.
- Kama Bajeti ya Chama ni ndogo kuliko mahitaji yake, ni lazima wajifunze kufanya mambo ndani ya bajeti. Kama ni kuanzisha miradi n.k wafanye hivyo lakini wasifanye vitu ambavyo hawana uwezo wa kuvigharimia. Katika hili wanaweza kuanzisha miradi ya Chama. Hili linawezekana kwa kuanzisha kampuni ya Chama (Holding Company) na wanaweza kuangalia ni jinsi gani chama kinaweza kumiliki kitega uchumi. Kama mnapata karibu milioni 66 kila mwezi na fedha zote zinaishia kwenye matumizi na hazizalishi basi kuna tatizo la kiuwekezaji.
- Uongozi mkuu wa chama ujitoe kwenye kusimamia fedha na badala yake waajiri watu ambao wana weledi wa mambo ya fedha. Mhasibu Mkuu, Mkaguzi wa ndani, watunza fedha n.k na wataalamu wa Boharia. Wanasiasa wabakie kufanya maamuzi ya kisiasa. Na watumishi hawa walipwe kwa kiwango cha fani zao, na wasiwe na uhusiano wowote ule wa karibu na kiongozi yeyote wa juu wa chama hicho. Kabila, mkoa, rangi, au dini na jinsia don't count.
- Ruzuku ya Chama isipokelewe na kiongozi wa kisiasa, period. Fedha za ruzuku au fedha nyingine yoyote inaenda moja kwa moja kwenye akaunti ya chama na hesabu zake zinaeleweka na zinasimamiwa ipasavyo. Lazima waweke mfumo mzuri wa usimamizi wa fedha ili saa ya yoyote ijulikane wana fedha kiasi gani, ziko wapi, na zimetumika vipi.
- Viongozi wa kisiasa warudi kwenye kuimarisha chama, kwa kupika makada wa kisiasa, kufungua matawi ya chama n.k. Sikumbuki mara ya mwisho kusikia Zitto, Slaa, au Mbowe amefungua tawi la Chadema mahali popote ilikuwa lini. Chama hakijengwi kwa hotuba za Bungeni, au maneno ya magazetini, bali kwa kushawishi watu kukikubali na kuzielewa sera zake. Na njia pekee ya kuonesha kuwa watu wanawakubali ni watu kujiunga na chama hicho.
Madai kuwa watu wanaelewa kuwa Chadema inapigia kelele ufisadi zaidi n.k ni madai tu lakini ushahidi wa watu kuelewa unaonekana kwa watu kujiunga. Je tangia mambo ya ufisadi yaanze na tangia sakata la Zitto Chadema imejipatia wanachama wangapi, na kiasi cha watu kujiunga kina tofauti gani na kabla ya hapo. Kama hakuna tofauti kubwa na inayoonekana basi kuna tatizo mahali fulani.