Tumpongeze Raisi wetu - MH. Jakaya Kikwete
Nahitaji maoni yenu zaidi kuhusika na uongozi wa Rais Mheshimiwa Jakaya Kikwete,kwa nionavyo mimi na baadhi ya wengi tu kuwa mheshimiwa anastahili kuongezwa nguvu ,hii ataipata ikiwa tutakuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono juu ya hatua aliyofikia katika kutatua matatizo ya wananchi.
Wengi wetu wanaona ni kazi rahisi na ya mara moja ,lala amka mambo powa kila mkoa na kijiji unapata mahitajio kamili na haya matamanio utayakuta kwa wale ambao hawawezi kupambambanua na wafinyu wa kufikiri wao kwao kila jambo ni rahisi ,hawa ndio wale waliokuwa hawaishi kumlaumu Mheshimiwa Raisi na serikali yake.
Si vibaya kumlaumu Raisi na zipo njia nyingi za kumlaumu yakiwemo maneno makali yenye kuudhi na kukatisha tamaa ila Raisi wetu ameweza kuyafahamu na kuwafahamu watu hao haraka nao pia wanauchungu wa Nchi hii na kama Raisi alitakiwa na ndivyo anavyofanya kutumia busara za hali ya juu sana ,japo wasiopenda maendeleo yake wanaona giza tu na kama hakuna linalofanyika kwa kuwa tu ile haraka wanayoitaka sivyo inavyotekelezwa na Mwenye Busara ambae ni Raisi Jakaya Kikwete,kuna watu hawapendi wakimwona anasafiri mara kwa mara ,watu hawa ni wale wasio mtakio ufanizi katika kuwajibika na majukumu ambayo kama Raisi na ambae ana uzoefu wa hali ya juu kuhusu nchi za nje kwa alivyokuwa akifanya kazi hiyo,Mheshimiwa Raisi kwa nionavyo ameona itakuwa rahisi majukumu kutekelezeka ikiwa atayavalia njuga mahitajio na kuyafuatia yeye mwenyewe.
Tumpongeze Raisi Kikwete na azidi kuwa mstari wa mbele yeye kama kiongozi Mkuu wa Watanzania.Sisi tukizidi kumpongeza na kumpa sifa anazostahili ndipo nae atakapozidi kuwa mwadilifu na kuhakikisha yale anayoyapanga yanathaminiwa na wananchi wake hivyo itakuwa rahiri kwa yeye kutekeleza amri zote ambazo zitaonekana nzito kwa wengine.
Hongera raisi Kikwete
Mimi nampongeza kwa sababu kipindi alichoingia kilikuwa kigumu na mitihani kibao.Kwanza kabisa alipambana na njaa na akahakikisha kuwa chakula kinapatikana.Hili halina mjadala.
Kutokana na matatizo makubwa ya umeme,mafisadi wakajiingiza na hakuna mtu asiyejua mambo yalivyokwenda hadi EL na mawaziri wengine wakatimuliwa.Zamani matokeo ya tume yalikuwa yakihifadhiwa kwenye kabati.period.na wananchi wanasahau.
Matatizo mengine aliyarithi kutoka awamu ya tatu,wengi wetu tumeyachanbua hapa JF na matokeo yake watuhumiwa wamefikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kesi zipo.Hukumu zitatoka.Mengine yanaendelea kushughulikiwa kwa taratibu za nchi.
JK amejikuta yuko njia panda kwa sababu ya mapambano ya kisiasa ndani ya CCM.Nia yake ni kuiongoza nchi kwa njia za kistaarabu lakini kuna wahafidhina wanamrudisha nyuma.JK bado yupo na ni matumaini kuwa atakuwa kidedea dhidi ya wapinzani wake ndani ya CCM.
Amefanya mambo ambayo wananchi wanayataka ayafanye na hii ni credit upande wake.
Uhuru wa kutoa maoni bila kushughulikiwa umetanuka(Muulize Jenerali Ulimwengu)Uhuru wa kuandamana ndiyo huo hadi anarushiwa mawe.
Watu wa Pemba walipotangaza kuwa wanajitenga alichukua hatua za kidiplomasia badala ya mabavu.Hajaua mtu yeyote anayeandamana.(Waulize kina Lipumba na Maalim Seif)
Wamemsema sana kuwa ni weak lakini matukio ya hivi karibuni yemeonesha siyo hivyo.Kule kupanda kwa hali ya maisha kunatokana na hali ya uchumi wa dunia kwa jumla.Kupanda kwa bei za mafuta kulipandisha bei za bidhaa kadhaa lakini sasa bei zinashuka na mambo yanaekea kuwa afadhali.
Kapangua baraza la mawaziri ili ku accomodate matakwa ya wananchi na juzi kapanga makatibu wakuu ili kushinikiza utendaji bora serikalini.
Tuna sababu ya kumpongeza na kumpa moyo Rais wetu.
Unapoweza kuwa na appreciation kwa madogo unampa mtu nguvu kuweza kufanya makubwa,wanadamu si rahisi kuwasatisfy ktk yote,ufupi nampongeza RAIS kwa kias chake kwa sababu zifuatazo;
1.Ametoa uhuru japo kdogo ktk vyombo vya habari,waut sasa wanaongea bila kuingiliwa sana
2.Ameweza kutoa fikra potofu za viongozi waliokuwa nazo ya kuwa wakisha pata madaraka basi wanaweza kufanya chochote bila kuingiliwa na kuulizwa abuse of power and public funds
3.
4.
5.
Tujue mazuri makubwa alofanya tumpongeze na mengine tumshauri aboreshe vip lakini sio kusema ati hakuna kitu amefanya.
Unapoweza kuwa na appreciation kwa madogo unampa mtu nguvu kuweza kufanya makubwa,wanadamu si rahisi kuwasatisfy ktk yote,ufupi nampongeza RAIS kwa kias chake kwa sababu zifuatazo;
1.Ametoa uhuru japo kdogo ktk vyombo vya habari,waut sasa wanaongea bila kuingiliwa sana
2.Ameweza kutoa fikra potofu za viongozi waliokuwa nazo ya kuwa wakisha pata madaraka basi wanaweza kufanya chochote bila kuingiliwa na kuulizwa abuse of power and public funds
3.
4.
5.
Tujue mazuri makubwa alofanya tumpongeze na mengine tumshauri aboreshe vip lakini sio kusema ati hakuna kitu amefanya.
Pongezi zangu zitakuja pindi haya yakifanyika:-
1. Watuhumiwa WOTE wakifikishwa mbele ya sheria na sheria KUACHWA kuchukua mkondo wake (na si vinginevyo).
2. Wezi wetu wote (pamoja na hawa waliofikishwa Kisutu) wakitendewa sawa na walivyolitendea Taifa bila kujali ushkaji na kulindana. Yani ikiwezekana adhabu yao iwe ni kunyongwa (kumradhi kama nahukumu vibaya as I believe ndiyo adhabu nzuri kwao). Rostam, Karamagi, Mkapa, Lowassa na wenzao ambao wamekuwa wakitajwa na tena kuoneshwa kwa vithibitisho kadha wa kadha wakifanyiwa uchunguzi wa kina na watanzania wakafahamishwa kwa ukweli na uwazi ili heshima zao ziendelee kupanda na kama ni kushuka zifikie ZERO!
3. Katiba ya nchi itafanyiwa marekebisho na kipengele kinachoweza kuwa kinamlinda rais ama kiongozi yeyote fisadi kikaondolewa na wote waliotupeleka kusiko wakahukumiwa sawa na matendo yao.
4. Rais akikubaliana nasi kuwa taifa hili ni letu sote na kufikiria kuwa na baraza dogo la mawaziri lenye 'wazalendo' wa kweli na hata kuwa na kiongozi walau mmoja ama wawili toka vyama vya upinzani.
5. Rais akiweza kudhibiti mfumko wa bei na kuangalia uwezekano wa kutimiza "Maisha bora kwa kila mtanzania" kabla ya mwaka 2010.
Tofauti na haya matano (kwa uchache) nina imani kubwa kuwa 'uzembe' wowote unaoweza kutendeka na kupelekea viongozi ambao ni wazi watanzania HAWATAKI HATA KUSIKIA MAJINA YAO wakaonekana hawakuwa na hatia kwa upindishwaji wa namna yoyote iwayo wa sheria ama kulindwa basi kutatupeleka kusiko kabisa.
Ni mawazo yangu tu
Unajua nini mkuu, kuna mjumbe humu kaandika kuwa tunapigana na watu hatari na akaomba Mungu atupe ustahimilivu. Sasa watu kama hawa njia pekee ya kuwamaliza ni kuwapa adhabu kali ya kuweza kuwafanya wengine 'wakome' mara moja michezo inayoligharimu taifa.HAAAAAAAAAAA kaka umeongea vema ila pa blue panatisha ingawa wakina China ndivyo walivyotiana adabu.
Ndio maana unajaribu kuwaambia watu tuna kazi kubwa sisi kwa sehemu yetu na viongozi.Kweli akiyafanya/kuwezesha hayo ulisema ukiacha pa blue ahahaaa,kweli tutampa pongezi sasa ni mapema mno kwa pongezi.
Unajua nini mkuu, kuna mjumbe humu kaandika kuwa tunapigana na watu hatari na akaomba Mungu atupe ustahimilivu. Sasa watu kama hawa njia pekee ya kuwamaliza ni kuwapa adhabu kali ya kuweza kuwafanya wengine 'wakome' mara moja michezo inayoligharimu taifa.
Yet, ni mawazo yangu tu
#Stupidiest comments ever seen in JF in recently days!
Hivi huyo rais anpokuja kuomb kura anwaambia atafanya kitu gani?? mnapotok nyumbani kweni siku ya kupiga kura mnataka afanye nini?
hivi mbumbumbu kama nyie msi waza japo kidogo uwezo na wajibu wa rais si ndio mnafuga ujinga, wezi n.k
Hivi Kikwete akija leo na kuwaomba vitu fulani mtampa tu......
sura inawachanganya?? mtu anafanya kazi kwa presha za donors leo mnamsifia
mpeni basi wake AU waume zenu afurahi
NYIE NDIYO MAFISADI NAMBA MOJA ZERO BRAIN IN TANZANIA, TENA NGAU MNA UWEZO WA KUSURF INTERNET MNA UWEZO MDOGO WA KUFIKIRI KAMA WA PANYA JE, WALE WASIOSOMA KABISA SI NDO WANALEWA MATAPUTAPU KWA FURAHA NA 2010 ANAINGIA TENA IKULU.
BASI TU HAMUONEKANI,NINGEWACHAPA VIBAO
NYIE NDIYO MNAJUA VIONGOZI NI MIUNGU WAKATI NI WATUMISHI WETU
YAONE VILE UJINGA TU!1
ALA!!!!!!!
Hongera raisi Kikwete
Duhhh kali hyo ni mpemba nini asiyeridhika na choote kinachofanya na SISIMNdo tatizo letu si wabongo.
Tumpongeze kwa lipi kafanya nini?Huo si ndo wajibu wake wakati anaomba kura kwa wananchi sasa tuanze kumpongeza ili iweje?Ndo maaana si ni wadanganyika siku zote tumesha danganywa na akina Mramba na Yona basi move yote inapoa.
Mkuu mwiba usiharibu mistake.
2) Endapo Baraza la Mawaziri litaona kuwa Rais hawezi kumudu kazi zake kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili, laweza kuwasilisha kwa Jaji Mkuu azimio la kumwomba Jaji
Mkuu athibitishe kwamba Rais, kwa sababu ya maradhi ya mwili au ya akili hawezi kumudu kazi zake. Baada ya kupokea azimio kama hilo, Jaji Mkuu atateua bodi ya utabibu ya watu
wasiopungua watatu atakaowateua kutoka miongoni mwa mabingwa wanaotambuliwa na sheria ya matababu ya Tanzania, na bodi hiyo itachunguza suala hilo na kumshauri Jaji Mkuu
ipasavyo, naye aweza, baada ya kutafakari ushahidi wa kitabibu kuwasilisha kwa Spika hati ya kuthibitisha kwamba Rais kutokana na maradhi ya mwili au ya akili, hamudu kazi zake; na
iwapo Jaji Mkuu hatabatilisha tamko hilo ndani ya siku saba kutokana na Rais kupata nafuu na kurejea kazini, basi itahesabiwa kwamba kiti cha Rais ki wazi, na masharti yaliyomo
katika ibara ndogo ya (3) yatatumika.
(3) Ikitokea kwamba Kiti cha Rais ki wazi kutokana na masharti yaliyomo katika ibara ndogo ya (2) au endapo kiti cha Rais kiwazi kutokana na sababu nyingine yoyote, na endapo
Rais atakuwa hayupo katika Jamhuri ya Muungano, kazi na shuhguli za Rais zitatekelezwa na mmoja wapo na wafuatao, kwa kufuata orodha kama ilivyopangwa, yaani-
(a) Makamu wa Rais au kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi.
(b) Spika wa Bunge au, kama nafasi yake iwazi au kama naye hayupo au ni mgonjwa; basi
(c) Jaji Mkuu wa Mahakama ya Rufani ya Jamhuri ya Muungano.
(4) Endapo yeyote kati ya watu waliotajwa katika aya ya (b) na (c) za ibara ndogo ya (3) atatekeleza kazi na shughuli za Rais kutokana na sababu kwamba mtu mwingine anayemtangulia katika orodha hiyo hayupo, basi mtu huyo ataacha kutekeleza
kazi na shughuli hizo mara tu mtu huyo mwingine anayemtangulia atakaporejea na akashika na kuanza kuteleza kazi na shughuli za Rais.
(5) Endapo kiti cha Rais kitakuwa wazi kutokana na Rais kufariki dunia, kujiuzulu, kupoteza sifa za uchaguzi au kutomudu kazi zake kutokana na maradhi ya mwili au kushindwa
kutekeleza kazi na shughuli za Rais, basi Makamu wa Rais ataapishwa na atakuwa Rais kwa muda uliobaki katika kipindi cha miaka mitano na kwa masharti yaliyoelezwa katika ibara ya
40, kisha baada ya kushauriana na chama cha siasa anachotoka Rais atapendekeza jina la mtu atakae kuwa Makamu wa Rais na uteuzi huo utathibitishwa na Bunge kwa kura zisizopungua
asilimia hamsini ya Wabunge wote
45.-(1) Bila ya kuathiri masharti mengineyo yaliyomo katika ibara hii, Rais anaweza kutenda lolote kati ya mambo yafuatayo:-
(a) kutoa msamaha kwa mtu yeyote aliyepatikana na hatia mbele ya mahakama kwa kosa lolote, na aweza kutoa msamaha huo ama bila ya masharti au kwa masharti, kwa mujibu wa sheria;
(b) kumwachilia kabisa au kwa muda maalum mtu yeyote aliyehukumuwa kuadhibiwa kwa ajili ya kosa lolote ili mtu huyo asitimize kabisa adhabu hiyo au asitimize adhabu hiyo wakati wa muda huo maalum;
(c) kuibadilisha adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa kosa lolote iwe adhabu tahafifu;
(d) kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu yoyote aliyopewa mtu yeyote kwa ajili ya kosa lolote au kufuta adhabu yote au sehemu ya adhabu ya kutoza, au kuhozi (au kuchukua) kitu cha mtu mwenye hatia ambacho vinginevyo kingechukuliwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano