Naona sasa Mada zimeisha, Jamani tunaacha kuhoji UFISADI tunaanza kwenda pembeni sasa. Mgaya kuna mtu anakufadhili nini kuhamisha hisia za watu juu ya serikali?
Plz, heshima zenu wakuu, MASLAHI YA TAIFA KWANZA, Huo Uislamu wao baadae mambo yakishaenda sawa pale tutakapoona EPA, MEREMETA, DEMISE OF UFISADISM, NA MENGINEYO labda ndio tutaanza kuyafikiria hayo.
Hivi kwanza naomba kuhoji, kwa jinsi ninavyojua na kujiamini 100% na JF yangu; Ni asilimia ngapi ya watanzania wanaoishi vijijini wananufaika na haya tunayoyaandika kama habari na kuijua nchi yetu inavyokwenda ukiachilia wale wasio jua kusoma wala kuandika? na JE KAMA TUNAANZA KUANGALIA MAMBO YA DINI KWENYE CCM ITAKUWAJE WAKINA MAMA NAO WATAKAPO KUJA JUU KUHUSU IDADI SAWA? JE UKABILA? Mimi nafikiri jibu la Mwl Nyerere lilikuwa zuri sana kwa jamaa aliyeuliza swala la udini kipindi cha harakati za uhuru.
JF DONT LOSE FOCUS, Kuna wengine humu wanatumwa kupotosha maana kama Mbunge fulani aliyeweza kutetea ujinga huku akisahau kwamba watu wanahoji hata Elimu yake.(Mtanisamehe lakini ila inaudhi)
MUNGU IBARIKI JF
MUNGU IBARIKI TANZANIA