‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

Magufuli kairejesha Tanzania nyumba kimawazo na fikra,.. Ung'ang'anizi wa kutaka CCM itawale milele na Uroho wa Madaraka ndio sera za Magufuli..

Kuwafunga au kuwa piga risasi wanaomkosoa

Sheria za kuwabana Watanzania wasitoe maoni yao kwenye mitandao hizi ni moja tu katika mifano ya UDIKTETA wa kuzuia uhuru wa kujieleza
 
Blogu zimejaa mitaani. Magazeti yanaanzishwa kila kukicha. TV za mitandaoni zimejaa.

Uhuru upi ambao mtu anautaka?. Wanataka waendelee na utaratibu ule ule wa kuwatukana viongozi wa nchi kadri wanavyojisikia. Uhuru huwa na mipaka yake.

Madonna aliongea maneno machafu hadharani kumhusu Trump, aliambiwa afute kauli yake na akaifuta.
 
Habari wanajamvi!

Kifo cha Mwenda zake kimeleta kizungumkuti na kwa hakika kuna mahali tunachanganya mambo. Mimi nasema ukweli lazima usemwe hata kama utakuwa mchungu kwa baadhi yetu. Nitajaribu kuweka mambo sawa.

Madikteta wote Duniani hutamani sana kupendwa. Wasipo pendwa kwa hiyari hutumia mkono wa chuma kupendwa. Hiyo ndio hulka yao ya ndani. Magufuli alitamani sana kupendwa, na kwa hakika wajinga hususan maamuma walimpenda tu kwasababu aliwatesa matajiri kwa maneno na kwa vitendo. Maamuma walitamani kuona kila mtu anakuwa masikini.

Wapi tunapishana kuelewa? Kuna watu wanadhani Magufuli hakuwa mtu mbaya kwasababu amejenga stand ya mbezi, amejenga Interchanges pale Ubungo na Tazara, amekarabati shule za zamani karibu zote, amejenga masoko ya kisasa katika mikoa 18, amejenga hospitali na vituo vya afya, ameanzisha ujenzi wa standard gauge railway n.k

Hayo yote hayaondoi ukweli kwamba MAGUFULI ALIKUWA DIKTETA KWA MANENO NA VITENDO.

Magufuli alikuwa na roho mbaya, ndio maana aliona kila mwenye nacho ni fisadi. Aliwachukuia watumishi wa umma bila sababu. Magufuli ameua watu wengi sirini na kwa wazi wazi. Magufuli alikuwa nyuma ya mpango wa kumuua Tundu Lissu, lakini Mungu akaonesha ukuu wake wa toka enzi na enzi. Azory Gwanda na Ben Saanane ni miongoni mwa wahanga wa Udikteta wa Magufuli. Matajir wengi wakubwa wamekufa awamu ya tano baada ya kubambikiziwa kodi au kuzuiliwa akaunti zao za biashara hata binafsi. Orodha ni ndefu. Magufuli hakuiheshimu KATIBA ya Jamhuri wa Muungano wa Tanzania hata kidogo. Yeye ndio alikuwa ndio kila kitu.

Tabia mbaya kabisa ya dikteta ni uuaji na kutoa ajira na teuzi mbali mbali kwa upendeleo. Alikuwa na tabia hizo zote. Alijaza watu Wa kwao kila idara bila ayibu.Alianzisha mpango wa kutawala milele. Alianza kuajiri mpaka watendaji Wa vijijini kutoka kwao.

Nini nataka kusema? Mabaya ya mtu ndio humpima na kutathimini yeye binafsi. Yakikithiri basi mzani husema huyu mtu ni mbaya sana. Akiwa kiongozi hupata sifa ya UDIKTETA. Mabaya ya Magufuli yalikithiri ndio maana anastahili kiitwa DIKTETA MAGUFULI. Truly in all terms and consideration Magufuli was a Dictator.

Id Amini alikuwa Dictator lakini kuna mambo fulani mazuri aliwafanyia Wanganda. Kufanya mambo mazuri bila kuwa moyo wa huruma kwa binadamu wenzako ni Udikteta.

Itoshe tu kumshukuru Mungu kwa kutuondolea Dikteta yule.
 
Habari wanajamvi!

Kifo cha Mwenda zake kimeleta kizungumkuti na kwa hakika kuna mahali tunachanganya mambo. Mimi nasema ukweli lazima usemwe hata kama utakuwa mchungu kwa baadhi yetu. Nitajaribu kuweka mambo sawa...
Itoshe tu kusema, Mungu ni mwema daima na ametutendea mambo makuu.

Sisi ni nani hata tusimshukuru kwa maamuzi yake?

Mama Samia anatosha, Kazi iendelee

Atakayemzingua, tutamzingua
 
na hawa wanaokwiba rasilimali za nchi waziwazi, wanaouza unga kuua nguvukazi ya taifa, wakwepa kodi, wanaodhulumu wakulima kwa kwa kupanga bei za kipigaji za masoko nk. hawa vipi?

binafsi sikuwahi kumkubali mze kwenye suala la kuminya demokrasia. lakini jinsi alivyodeal na magenge ya wapigaji niliyotaja hapo juu nadhani ni heri zaidi maana hawa ni madikteta wa uchumi wa nchi yetu yote kuliko magufuli ambae alikuwa anaonekana dikteta kwa kudeal na mtu mmoja mmoja.
 
Kwenye hili la kulazimishwa kupendwa ni kweli na hakika, Jiwe alikua anajua kwa dhati kabisa hapendwi. Roho mbaya+chuki kwa wenye nacho ilikithiri, apumzike alipojichagulia.
Sasa Mimi kila siku nikikuamsha asubuhi kwa nguvu uende ukalime viazi ili uje ule na familia yako...lazima utanichukia.....lengo ni kukusaidia ujitegemee uache kuomba omba.
 
Ukweli lazima usemwe Magufuli alikuwa kiongozi mzuri....mitanzania ukiichekea hakuna kitu utafanya....
Uzuri ulikuwa kitu kama 25% or even less kilichobakia kilkuwa shari, ubaya, chuki, uchu wa madaraka, uchu wa ukabila, kupenda kumwaga damu, kufurahia mauti ya wapinzani na wanaompinga ndani ya chama chake, kufurahia kufilisi wananchi, kuvuruga uchumi, kutukana akina mama na akina baba, kebehi, kujibu watu kunya, nk.nk.
 
na hawa wanaokwiba rasilimali za nchi waziwazi, wanaouza unga kuua nguvukazi ya taifa, wakwepa kodi, wanaodhulumu wakulima kwa kwa kupanga bei za kipigaji za masoko nk. hawa vipi?

binafsi sikuwahi kumkubali mze kwenye suala la kuminya demokrasia. lakini jinsi alivyodeal na magenge ya wapigaji niliyotaja hapo juu nadhani ni heri zaidi maana hawa ni madikteta wa uchumi wa nchi yetu yote kuliko magufuli ambae alikuwa anaonekana dikteta kwa kudeal na mtu mmoja mmoja.
Unaosema wanodhurumu wakulima.... KWANI WALE WA KOROSHO ILIKUWAJE? UNADHANI KWA NINI JESHI LILITUMIKA KWENYE KOROSHO?
 
Habari wanajamvi!

Kifo cha Mwenda zake kimeleta kizungumkuti na kwa hakika kuna mahali tunachanganya mambo. Mimi nasema ukweli lazima usemwe hata kama utakuwa mchungu kwa baadhi yetu. Nitajaribu kuweka mambo sawa....
Roho mbaya yako haitabadilisha ukweli. Rais gani alifanya mambo mengi hivi kwa muda mfupi wa miaka mitano? Wewe na wenzio mlikuwa wapigaji na wavivu, mlinenepa kwa njia haramu. Cha moto mmeonja. Msisahau kuwa maskini hafulii. Sisi maskini shida zetu alizifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kugawana mali za matajiri.
 
Back
Top Bottom