‘Udikteta’ wa Magufuli na uhuru wa kujieleza

Sio rahisi mijizi impende magufuli. Sema kadili uwezavyo ila yule mtu huwezi mchafua kwa maneno mabaya.

Asante mungu kutuletea chuma kilichonyoosha majizi yote.

Ila magufuli kawanyoosha mpaka hamchoki kumsema?
Mungu wabariki "wale watu walee" wanaomchukia magufuli nao uzao wao utoe rais tuone nae atanya yapi?

Tunataka vitendo sio maneno.
 
Habari wanajamvi!

Kifo cha Mwenda zake kimeleta kizungumkuti na kwa hakika kuna mahali tunachanganya mambo. Mimi nasema ukweli lazima usemwe hata kama utakuwa mchungu kwa baadhi yetu. Nitajaribu kuweka mambo sawa....

Umeweka sawa
 
Unaosema wanodhurumu wakulima.... KWANI WALE WA KOROSHO ILIKUWAJE? UNADHANI KWA NINI JESHI LILITUMIKA KWENYE KOROSHO?
kangomba walikuwa wanadhulmu wakulima. idea ya dr. magufuli ilikuwa njema tu lakini utekelezaji wake ulikuwa mgumu sana kutokana na kile alichokuwa anakiongea kila siku bila watu kukitilia maanani: 'vita ya kiuchumi ni ngumu'
 
Habari wanajamvi!

Kifo cha Mwenda zake kimeleta kizungumkuti na kwa hakika kuna mahali tunachanganya mambo. Mimi nasema ukweli lazima usemwe hata kama utakuwa mchungu kwa baadhi yetu. Nitajaribu kuweka mambo sawa....
Asante Mungu
 
na hawa wanaokwiba rasilimali za nchi waziwazi, wanaouza unga kuua nguvukazi ya taifa, wakwepa kodi, wanaodhulumu wakulima kwa kwa kupanga bei za kipigaji za masoko nk. hawa vipi?

binafsi sikuwahi kumkubali mze kwenye suala la kuminya demokrasia. lakini jinsi alivyodeal na magenge ya wapigaji niliyotaja hapo juu nadhani ni heri zaidi maana hawa ni madikteta wa uchumi wa nchi yetu yote kuliko magufuli ambae alikuwa anaonekana dikteta kwa kudeal na mtu mmoja mmoja.
Hakuna alichosaidia maana hayo makundi yote uliyo yataja bado yanaendelea kushamili tena kwa speed kubwa.


Tulikuwa tunashuhudia watu wanakamatwa na hata kilo 10 za madawa ya kuevya.

Sema mlikuwa mnahangaika na vidagaa wakati mnawafuga na kuwalinda mapapa.

Hapo ndiyo tunaendelea kuwalaumu kuwa serikali yenu ilikuwa inawaljnda mafisadi na majizi na wahalifu wakubwa.
 
Roho mbaya yako haitabadilisha ukweli. Rais gani alifanya mambo mengi hivi kwa muda mfupi wa miaka mitano? Wewe na wenzio mlikuwa wapigaji na wavivu, mlinenepa kwa njia haramu. Cha moto mmeonja. Msisahau kuwa maskini hafulii. Sisi maskini shida zetu alizifanyia kazi ikiwa ni pamoja na kugawana mali za matajiri.
Roho mbaya tu imekujaa, kwanini ufurahie kugawana mali za tajiri alizotafuta kwa juhudi zake na si kutafuta mali zako mwenyewe!!??
 
kangomba walikuwa wanadhulmu wakulima. idea ya dr. magufuli ilikuwa njema tu lakini utekelezaji wake ulikuwa mgumu sana kutokana na kile alichokuwa anakiongea kila siku bila watu kukitilia maanani: 'vita ya kiuchumi ni ngumu'
Kuna wakati tuwe wakweli... Nyie kila linalofeli mnadhani watekelezaji pekee ndo wana shida... IDEA IKFELI, NI KUANZIA MUASISI WA IDEA HADI IMPLEMENTERS WOTE WAMEFELI... Kwenu Idea ikifeli, basi watekelezaji, lakini ikifaulu, amefaulu JPM peke...

Halafu nikuulize, hivi unajuwa kuwa kuna watu bado hadi leo wanadai hela zao za korosho kwa serikali? Kwa mtindo huo, unadhani KANGOMBA INAEPUKIKAJE? Yaani mkulima hana chakula ndani (familia inaka kulala na njaa huku hawajala kutwa nzima) au ana mgonjwa hospitali, hana hela, lakini ndani ana korosho, na wakati huo anaidai serikali, unataka afanyeje? Na hapo nje tu kuna mtu ana hela CASH umpe korosho.. Wewe ungefanyeje?
 
Back
Top Bottom