Udhaifu wa upinzani baada ya Uchaguzi Mkuu

econonist

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
15,756
21,748
Upinzani wa Tanzania huwa una udhaifu mmoja mkubwa hasa baada ya uchaguzi mkuu. Kugeukana na kumpa credit CCM kipindi ambacho mshikamano unahitaji.

Tuchukue mifano mitatu mikubwa.

1. Mwaka 2015, baada ya uchaguzi mkuu Zanzibar matokeo ya urais na baraza la mawakilishi yalifutwa na tarehe ya uchaguzi wa marudio kutangazwa. Mgombea urais wa CUF kipindi hicho Maalim Seif alijiondoa kwenye uchaguzi huo.

Hata hivyo wakati Maalim Seif akiendelea na harakati za kupata haki yake , akaibuka Lipumba na kundi lake na kuanza figisu mbalimbali ambazo zilififisha juhudi za CUF kupigania haki yake Zanzibar ya urais na matokeo na mwishowe Lipumba alifanya ya kwake na harakati nyingi zikatumika mahakamani bara badala ya Zanzibar mwishowe Maalim akamuachia chama Lipumba na kuhamia ACT Wazalendo.

Leo Lipumba anawaomba radhi wa Zanzibar na kuwataka warudi CUF, kipindi kile alifanya hivyo kwa aajili gani huku akijua CUF wamedhurumiwa Zanzibar. Kwanini asingepamabana haki ipatikane Halafu ndio aje kwenye Mambo mengine. Leo ndio anawakumbuka wazanzibar.

2. Pia, baada ya uchaguzi wa mwaka 2015 wakati Rais Magufuri akitoa hotuba ya kulifungua bunge, wapinzani walitoka nje ya bunge Kama njia ya kuonesha wanasimama pamoja na kupinga uonevu uliofanyika Zanzibar wa kufuta matokeo. Lakini mpinzani mmoja aitwaye Zitto kabwe wa ACT Wazalendo alibaki ndani ya bunge na kuwazodoa waliotoka nje.

Leo wale ambao Zitto aliwazodoa ndio wamekuja kuimarisha chama chake Cha ACT Wazalendo wakitokea CUF.

3. Mwisho, ni Uchaguzi Mkuu wa 2020. Baada ya madhaifu yaliyooneshwa kwenye uchaguzi mkuu wa 2020 Kama kukamatwa kwa kura bandia, vitisho, kufungiwa kufanya kampeni, kuzuia kugombea na kufungwa kwa mitandao. CHADEMA ilipinga uchaguzi huo na kuahidi kutotambua matokeo yake.

Wakati chama kikiwa katika harakati hizo , ghafla likaibuka kundi la Covid 19 na kwenda bungeni kuapishwa Kama ishara ya kukubaliana na uchaguzi mkuu. Wengi wao wakiwa wahadhirika wa madhaifu ya uchaguzi Kama kawe kwa halima mdee ambako karatasi feki zilikamatwa. Ila wakasau yote wakaenda kinyume na msimamo wa chama chao na Spika Ndugai akawaahidi kwamba atawalinda na Mwanasheria mkuu Kilangi akahidi kuwatetea dhidi ya CHADEMA. Hivyo wakawa wameua jitihada za chama kupinga matokeo ya uchaguz

Ni muda wapinzani wawe wapinzani na kusimamia misingi sio unakuja upinzani ili kuitumikia CCM hatutaki hayo.
 
Back
Top Bottom