Synthesizer
JF-Expert Member
- Feb 15, 2010
- 11,143
- 18,774
Nimeushangaa sana uamuzi wa Dr, Tulia Ackson kuhusu Mbunge wa CCM kuchana hotuba ya upinzani. Tulia, ambaye ni mwanasheria wa kiwango cha PhD, bila aibu ametetea uamuzi wake kwa kutoa kauli kwamba "Vuma hawezi kupelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Bunge kwa kuwa kipindi cha nyuma mbunge wa Bunda (Chadema) Ester Bulaya aliwahi kurusha vitabu bungeni na kuvichana lakini hakupelekwa katika kamati hiyo"
Hivi kweli, Dr wa sheria, anawezaje kutoa kauli kama hii? Kama uongozi wa Bunge la Tanzania umewahi kutuhumiwa kuwa dhaifu, basi kwa kauli hii ya Tulia nasema Bunge linaongozwa na maspika ambao si tu ni dhaifu, bali pia ni wameamua kwa makusudi kujifanya vipofu na mbumbumbu wa uongozi, ili kulinda maslahi ya chama chao CCM.
Kwa kiingereza ninasema kwamba "Tanzania parliament leaders are excessively biased against the opposition, to the extent that most of the time they forget to be clever or intentionally choose to be stupid". Hii ya Tulia ni typical case. Za Ndugai zipo nyingi sihitaji hata kuzitaja. Za wenyeviti wengine wa vikao vya Bunge kama kina Chenge, Zungu nk zinatia hata aibu kuzitaja.
Tulia anachodai hapa ni kwamba, Bunge linaendeshwa kwa mantiki ya jino kwa jino. Ni sawa na refa wa mpira wa miguu ambaye anainyima penati ya wazi timu moja, na ili kusawazisha kosa lake, anainyima timu pinzani penati ya wazi pia.
Well Dr. Tulia, kauli ya kwamba "two wrongs don't make it right" sio ya kitoto. Wahenga waliiweka ili kuwaelimisha watu kama wewe ambao mnasahau kutumia akili na usomi wenu kwa manufaa yenu binafsi au ya chama chenu. Kama Ester Bulaya wa Chadema alifanya kosa na hakuchukuliwa hatua, hilo lilikuwa ni kosa na udhaifu wa uongozi wa Bunge. Lakini sasa udhaifu huo unazidi kuzidishwa pale ambapo Vuma wa CCM anafanya kosa kama la Ester na unaamua kwamba basi na yeye asichukuliwe hatua kama ilivyokuwa kwa Ester Bulaya.
Huo ni udhaifu mkubwa wa uongozi wa Bunge.