Udhaifu wa Bunge ni matokeo ya Bunge kujaa wafanyabiashara tuwapunguze akina Shabiby, Nchambi, Abood, Musukuma n.k

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Bunge la Tanzania la awamu iliyopita lilikuwa dhaifu, CAG alisema, Makonda alisema, wapinzani wamesema sana. Makundi mbalimbali ya wananchi wanasema pia.

Udhaifu wa Bunge ilikuwa ni matokeo ya kupeleka bungeni wabunge wanaoangalia masilahi yao na siyo kwamba ni wabunge dhaifu.

Wabunge wafanyabiashara waliojaa bungeni siyo dhaifu hata kidogo, ukitaka kujua siyo dhaifu gusa maslahi ya biashara zao.

Hawa hawaingii bungeni kuisimamia serikali na kuishauri serikali wala kutunga sheria za kulinda mwananchi.

Nchambi anayekamatwa na silaha na risasi nyingi hawezi kutuambia ni za kujilinda lazima ana matumizi nazo haramu.

Abood anayenunua viwanda na kuvitelekeza haku wananchi wakikosa ajira hatuwezi sema ana uchungu na wananchi. Shabiby hawezi kujali wananchi zaidi ya mabasi yake, zaidi ya vituo vya mafuta, zaidi ya machimbo ya madini, zaidi ya Morena Hotel.

Wafanyabiashara wanatununua wananchi kipindi hiki cha kampeni siyo kwenda kutete Gairo ipate maji safi na salama iondokane na maji ya chumvi la hasha ni kulinda biashara zao.

Ukitaka kujua akina Nchambi, akina Msukuma si dhaifu gusa biashara zao. Wako tayari kushauri Magufuli aongezewe muda wa miaka zaidi ya 10 ilimradi wamfurahishe asiguse biashara zao.

Wako tayari kumdhuru yeyote kwa risasi kama pesa itashindwa ili mradi waendelee kulinda biashara zao.

Watatukana wasaidizi wa Rais katika majimbo yao, watawachongea kwa mamlaka za uteuzi kwa ghalama yoyote kwa lengo la kulinda maslahi yao na si maslahi ya wananchi.

Vyama vya siasa vinayo nafasi kuwapunguza watu hawa bungeni kama kweli vinauchungu na wananchi. Umaskini wetu na Serikali yetu umetufanya kupotoka tunachagua mbunge mwenye fedha binafsi na siyo mbunge wa kuisimamia Serikali.

Mbunge anaulizwa na mwananchi umetusaidia nini binafsi kama mbunge na siyo uliisimamia vipi serikali kutuletea maendeleo na hii ndiyo silaha ya wenye fedha kurudi bungeni.

Ni mwaka wa uchaguzi vyama vitusaidie, Takukuru itusaidie, Tume ya Uchaguzi itusaidie na Taasisi za kijamii. Ni wakati wa kuwajengea uwezo wananchi sifa ya kiongozi anayetufaa.

Pesa tuzile lakini isiwe silaha ya kuwapa kura zetu hata wa aina hii.
 
Back
Top Bottom