'Uchuro' waingia CHADEMA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Uchuro' waingia CHADEMA

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pdidy, Jul 29, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,067
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  'Uchuro' waingia CHADEMA

  [​IMG]
  Mwandishi Wetu​
  Julai 29, 2009[​IMG]
  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedaiwa kulenga kupanga safu mpya ya uongozi ikiongozwa na Freeman Mbowe na kumuingiza aliyewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, kuwa makamu mwenyekiti, na kumn'goa Kabwe Zitto, kwenye nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu.
  Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Mbowe, ambaye mbali na kushangazwa lakini alisisitiza kuwa wanaheshimiana sana na Zitto na kwamba binafsi wala chama hicho hakina mpango wowote wa kumng'oa kwa kuwa bado kinahitaji "Zitto" wengine wengi zaidi.
  "Sijapanga safu yoyote ya uongozi, kwenye chama chetu tumekuwa na utamaduni rasmi wa kugombea na kupata uongozi. Najua kwamba kuna mbinu za kila namna kuisambaratisha CHADEMA. Mimi nitakuwa mwendawazimu kama nitakuwa sitambui mchango wa Zitto kwenye chamaÂ…huwa hatukurupuki tu kugawana vyeo, taratibu zote hufuatwa kwa hiyo si uamuzi wa mwenyekiti.
  "Nasema madai hayo hayana msingi wowote na ni jungu la kitoto. Viongozi tutakuwa wendawazimu kama tutakubali CHADEMA iangamizwe kwa majungu, na Watanzania ambao matumaini yao yameelekezwa kwetu hawatatusamehe daima. Zitto ni kamanda wangu, natambua mchango wake kwenye chama na tunamhitaji," alisema Mbowe.
  Lwakatare hivi karibuni alihama kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) ambako alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, na kujiunga CHADEMA na kushiriki kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo Jimbo la Biharamulo Magharibi.
  Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo kwa sasa iko wazi, awali ilikuwa ikishikiliwa na aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa safarini kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
  Inaelezwa kuwa katika safu hiyo mpya anayodaiwa kuipanga Mbowe, John Mnyika ndiye anayaterajiwa kuchukua nafasi ya Kabwe Zitto, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, huku Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, akiendelea kuwa Katibu Mkuu.
  Kwa mujibu wa habari zilizozagaa ndani na nje ya CHADEMA, uamuzi huo wa kumng'oa Zitto unaelezwa kuwa msingi wake ni kile kinachoelezwa kuwa ni "usumbufu" wa kiongozi huyo dhidi ya viongozi wakuu, akiwamo ya Mbowe.
  "Mbowe anapanga kugombea ubunge na kuingia bungeni ikiwezekana kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni na atahakikisha anafanya kazi hiyo kwa nguvu zake zote ili umma umwamini, ataitikisa serikali na mwaka 2015 atashinda urais," inaeleza sehemu ya madai hayo ambayo yamekanushwa vikali na viongozi wote makini wa CHADEMA.
  Madai hayo ambayo yameelezwa kuwakera baadhi ya viongozi hao yameelezwa kwamba mkakati mwingine unalenga kuhakikisha Zitto anapotea kwenye ramani ya siasa Tanzania "kwa gharama yoyote kwani ni tatizo."
  Kwa upande wake, Zitto alipoulizwa kuhusu yeye kuwania uenyekiti alisema; "Mimi nasema sina mpango wala kufikiria kugombea uenyekiti. CHADEMA kina taratibu nzuri za kuachiana uongozi, ninaamini kama kuna mabadiliko yatakuwa ambayo yataacha chama salama. Mi bado mdogo, sitaki watu wanivurugie na kuvuruga chama. Nina imani na uongozi uliopo wa chama."
  Katika hatua nyingine, akizungumzia madai ya kugombea ubunge Mbowe alisema; "Suala muhimu kwa sasa si kufikia nani anagombea ubunge au nani hagombei, jambo la msingi kufahamu kwa sasa ni kwamba CHADEMA tumejipanga kuongeza idadi ya wabunge ili kuipa nguvu zaidi za uamuzi Kambi ya Upinzani Bungeni kama unavyojua mara nyingi wabunge wa CCM wamekuwa wakitumia uchache wa wabunge wa upinzani kupitisha mambo yasiyokuwa na msingi."
  Kwa upande wa madai ya kukusudia kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni na baadaye mwaka 2015 kugombea urais alisema; "Hivi mimi nimekuwa mpiga ramli? Na haya majungu yamepangwa kama vile mimi nina mkataba na Mwenyezi Mungu kwamba amenihakikishia kwa asilimia 100 nitakuwa hai hadi wakati huo. Nasema kila hatua ya kupata uongozi, na hasa uongozi wa umma inazo taratibu zake, mimi ni kiongozi mwanademokrasia ninayeheshimu taratibu."
  Akizungumzia madai ya hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF kwamba CHADEMA ni CCM-B, Mbowe alisema ni utoto kuendesha siasa za kushambuliana kati ya chama kimoja cha upinzani na kingine na kwamba hayuko tayari kuingia katika malumbano ya namna hiyo.
  "CHADEMA hatuwezi kuingia kwenye malumbano ya kupotezeana muda kiasi hicho, jukumu letu kubwa ni kutafakari kwa pamoja viongozi na wanachama tunakiandaaje chama chetu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 kwa mafanikio makubwa katika historia yake nchini," alisema.
  Historia ya vyama vya siasa vya upinzani nchini inaonyesha kuwa Chama Cha NCCR-Mageuzi ni chama kilichokuwa na nguvu kubwa za kisiasa mwaka 1995 na kufanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge, na kwa sasa chama nguvu hizo zimeshuka na chama hicho hakina mbunge hata mmoja.
  Vyama vingine vilivyowahi kupoteza viti vya ubunge kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushuka kwa nguvu za kisiasa ni pamoja na UDP pamoja na TLP. Kwa sasa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaundwa na Kambi ya Upinzani kutoka vyama vitatu, ambavyo ni CUF, CHADEMA na UDP, chenye mbunge mmoja.
  [​IMG]
   
 2. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #2
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Ombi:
  Jamani mkiweka habari kama hii muwe mnaweka na Source na kama ina link basi ni vizuri ukatuwkea na link. Maana quality ya source kwa watu walio makini ni muhimu sana. Narudia tena habari katika Daily news, The Gurdian, majira, na Uwazi zinachukuliwa kwa uzito tofauti.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,067
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Raia mwema kaka...na hapo
   
 4. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #4
  Jul 29, 2009
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  analeta mambo mbofu mbofu
   
 5. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #5
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,067
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Narudia tena habari katika Daily news, The Gurdian, majira, na Uwazi zinachukuliwa kwa uzito tofauti.
  JAMANI NI GAZETI SIO MIMI MKUU ZHULE
  CHADEMA DAIMA
   
 6. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #6
  Jul 29, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,067
  Likes Received: 5,553
  Trophy Points: 280
  Hiyo taarifa ajaiweka yote...mbona raiamwema wamemwaga kila kitu kunani???pdidy
   
 7. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #7
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Mchukia Fisadi upoooo!!!!!!
  Mshapokea bunju chadema na miba yake inaanza kuwakwama, Waswahili wanasema "...akunyimae kunde......"
  Chadema wamevamia kunde wanaanza kufanya karaha sasa. haya!!!!
   
 8. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #8
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Naona hukunielewa mkuu, nilikuwa nasema ukiweka habari bila kutuambia inatoka wapi tunashindwa kuipa uzito unaostahili, na wala sikusema ni maneno yako, nilitaka jina la gazeti na tarehe (umewahi kusikia kitu kinaitwa reference)

  Pia nilikuwa nataka nikuambie kuwa Habari katika kwa mfano NY Times, The Gurdian (TZ) na Uwazi/kiu/Ijumaa zinapewa uzito tofauti. Au habari kati CNN Vs ITV Vs Abood TV (ipo morogoro) zinapewa uzito tofauti. Kwa hiyo ukiweka post hakikisha kama sio maneno yako weka umeitoa wapi ikibidi link au terehe na toleo la gazeti. Pole kama ulikwazika, tunasaidiana tu.
   
 9. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #9
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  NI RAIA Mwema pia niliisoma; ila naona imetuungwa zaidi kwa makusudi maana haina uhusiano vile kati ya heading na kilichomo
   
 10. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #10
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Junius nipo lakini sipo kwa ajili ya majungu.
  Uelewa wangu ni mkubwa mno. Nilikichaagua Chadema baada ya tafakuri kubwa. Ni chama makini chenye sera za mwelekeo ninaoutaka. Kutokomeza ufisadi na kuleta Tanzania yenye matumaini.
  Wewe ulichagua kafu kwa sababu ya d**i, na kuona mnashinda Pemba:D
  unaona tofauti yetu?
   
 11. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #11
  Jul 29, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,635
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 160
  Kheeee heeee heee... Eeh!
  Haya
   
 12. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #12
  Jul 29, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Very LOW kaka; du; mnaaibisha jamvi- puuuu!!!

  Find substance and talk; maneno ya mtaani yaache kwetu huku huku manzese; au ndio kujisahau

  Mshabiki wa Simba wakati mwingine anaweza kutulia kama amezidiwa na kujipanga kwa hoja na vitendo sio kuongea tu just kwa sababu unaongea; jitahidini kuepuka kuonyehsa level zaIQ walau tusijue sana maana inaweza kuwa aibu
   
  Last edited: Jul 29, 2009
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Jul 29, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  :D:D:D umefurahi sio? kawambie sisi m basi:D
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Jul 29, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  kwani kuna ubaya gani kama zitto ataondolewa kidemokrasia? au linatisha hilo neno 'kung'olewa'?
   
 15. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #15
  Jul 30, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Gazeti la RAIA MWEMA la wiki hii lina habari ya Uchuro ndani ya Chadema,kisa John Mnyika anafikiriwa kupewa unaibu katibu mkuu nafasi ya Zitto Kabwe,Mwenyekiti Mbowe amekanusha.

  halikadhali Gazeti hilo hilo la Raia Mwema limekiri kuchukua chanzo cha habari yake kuu hapa JF na kwa Mwanakijiji.
   
 16. Mbogela

  Mbogela JF-Expert Member

  #16
  Jul 30, 2009
  Joined: Jan 28, 2008
  Messages: 1,369
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Hii habari niitaje? Majungu? Tetesi? Udaku? Umbea?
  Kwasababu mwandishi makini hawezi akasema habari zilizoenea ndani na nje alafu akashindwa kutaja hata source moja ya waliompa habari za mipango hii. Mwandishi alipaswa japo kutoa ushahidi wa mazingira unaonyesha namna mkakati huu unavyosukwa. Yaani kama tutabaki kushabikia habari kama hizi na kuzifanya ni habari nchi hii itakosa habari.

  Sijawahi kusomea habari, lakini kutokana na kufuatilia habari mbali mbali za matukio bali kutoka kwa waandishi na mreporter mbali mbali duniani naweza kusema hii habari inaupungufu mkubwa.

  Inawezekanaje Habri ya Kubenea aliyoitoa kipindi fulani kuwa kuna fraction ndani ya SISI M walifanya mkutano Moro wa Kumng'o m/kiti wao kugombea nafasi ya Urais next yr pamoja na ushahidi wa vikao na kumbi zilipofanyika hiyo mikutano na wajumbe walioshiriki mapka magari waliyofika nayo wakaiita ni Udaku, sasa habari kama hii ambayo haitaji hata nani anapenga mpango na nani inachukuliwa kuwa ni habari?

  Nadhani munaoandika mjipange, sasa hivi wanaoadhirishwa sio wansiasa tu, kila mtu, Tanzania ya leo sio ya Jana, Watanzania wa leo tunaelewa huwezi kutununua rahisi kiasi hicho.

  Nani mmiliki wa Tanzania Daima?
   
 17. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #17
  Jul 30, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Kanda2,
  Umechelewa. Hii tumeshaletewa awali.Bukua kurasa za JF utaiona.
   
 18. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #18
  Jul 30, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Kaazi kwelikweli ngoja nitafute tundiko nyingine zenye maana..!
   
 19. S

  Sirily Mtui Member

  #19
  Jul 30, 2009
  Joined: Jul 28, 2009
  Messages: 12
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiyo ni mikakati ya maadui kukivuruga chama; ila naamini kuwa chadema ni chama cha watu makini na wala hakiongozwi na majungu bali kawa sera na kanuni, ni chama chenye dira na mwelekeo juu ya mustakabli wa taifa letu,
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Jul 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lwakatare ameshachukua fomu za kugombea kitu kwenye CHADEMA ,na alipohojiwa zaidi alisema anatumia uhuru wa Chama Chake kipya na pia ameingia hapo akiamini kuwa anawezakuongoza sehemu yeyote ile kutokana na uzoefu alionao.
   
Loading...