'Uchuro' waingia CHADEMA

CHADEMA kitaongozwa na watu makini wanaojua nini umuhimu wa demokrasia, Chadema kikiwa na waasisi walio komaa kwenye demokrasia na wakijua kukua kwa chama ni pamoja na kuheshimu katiba na kuilinda, kuheshimu uongozi na kuchaguana kwa kufuata misingi imara ya uhuru wa haki na usawa.

Lwakatare ni mwanachama sawa na yeyote. Na si dhani kweli Mbowe amekuwa na njozi na ya kuhakikisha kwamba mambo atayapeleka atakavyo pasipo chama, amekuwa jemedari licha ya kuandamwa na CCM na wapambe wake.

Tunajenga chama makini na si umangimeza, na kama ikijulikana yupo mangimeza basi chama kitafuata taratibu na kutokomeza hila zote za kishenzi na kipuuzi. Ni matumaini yangu kuwa Lwakatare hajaingia chadema kutuvuruga bali kutekeleza azma yake ya mapinduzi ya kisiasa na demokrasia ya kiuchumi ya mtanzania wa leo.
 
JF mnawaendekeza sana hawa ChAdEmA... Bandiko hili si lilikuwa kule kwenye habari na hoja binafsi? Limehusu nini kuwepo hapa ukumbi wa siasa?
 
Lakini Lwakatare hana hata miezi miwili kwenye Chadema hajaijua katiba na mfumo wa Chadema. kwanini asipewe KITILA MKUMBO?
mtu hamjamjua mnampa madaraka makubwa bila kupitia njia au ngazi walizopita wengine.
 
JF mnawaendekeza sana hawa ChAdEmA... Bandiko hili si lilikuwa kule kwenye habari na hoja binafsi? Limehusu nini kuwepo hapa ukumbi wa siasa?

Hata unapofanyika uchaguzi au jambo lolote ni Chadema ndio wanapewa umuhimu mkubwa hapa.hujiulizi kila kada wa Chadema anakuja hapa kuwa member hadi mzee Mtei,unafikiri inatokea kwa bahati tu?
 
Hata unapofanyika uchaguzi au jambo lolote ni Chadema ndio wanapewa umuhimu mkubwa hapa.hujiulizi kila kada wa Chadema anakuja hapa kuwa member hadi mzee Mtei,unafikiri inatokea kwa bahati tu?
Kanda,
Mbona na wewe upo? Na wewe ni CHADEMA?
 
Vipi kuhusu Kitila Mkumbo? Nafikili ni wakati wake kumake a move... there is no tomorrow!

Au arudi chama kubwa CCM
 
Kitu muhimu cha kuangalia kwenye siasa zetu, ni watu wanaohama chama kwa nia ya kupewa madaraka. Si vibaya kugombea au kuchukua form ya kugombea uongozi wowote kwenye chama unachokipenda, ila isiwe ndio chanzo cha kuhama chama kimoja kwenda kingine. Hii ni tabia mbaya na inadhoofisha sana jitahada za wengi. Mtindo wa ahadi za kupewa vyeo na uongozi hutumika CCM pale wanapotaka kudhoofisha upinzani, sidhani kama ni mchezo mzuri kwani mtindo huu haujengi misingi bali unakuza ufisadi haswa msukumo unapokuwa ni uongozi na marupurupu, hupati vichwa vinavyofikiri bali maboga yaliyoishiwa maji yanatafuta ardhi yenye rutuba.

Chama kiweke mazingira mazuri ya kupokea wanachama wapya bila kujali wanatoka wapi bila kuwaahidi chama kitawafanyia nini bali wao waseme watafanyia nini chama na wananchi.

Duniani watu wasio na misimamo wanaogopewa sana isipokuwa Tanzania. Ikumbukwe kila mahali kiongozi mahiri lazima aonyeshe uwezo wake hasa wa kupambana na matatizo na jinsi ya kuyatatua sio kuyakimbia.

Chadema kitajengwa na wanachama waaminifu na wanaoheshimu utawala wa katiba na sheria waliojiwekea wenyewe kuwaongoza na kuongoza nchi.
 
Kuna uvumi kuwa Chadema itagawika kutokana na kundi linalomuunga mkono Zitto na lile la wahafidhina ambao wanadai chama ni chao na hakuna wa kuwapangia .
 
Hawa chadema nao wameanza vizuri saivi wanatoana macho kwa vihela vya ruzuku karibu wataishia kama Mrema kama hawatotanabahi mapema.
 
Kuna uvumi kuwa Chadema itagawika kutokana na kundi linalomuunga mkono Zitto na lile la wahafidhina ambao wanadai chama ni chao na hakuna wa kuwapangia .

Si kweli huu ni uvumi na njia ya CCM kuona chadema chama makini kinayumba, hayo hayatatokea. CCM walitegemea hivyo walipomchukua Dr walid walipandikiza chuki haikufanya kazi. Vilevile walitumia kifo cha Wangwe kukigawa chama walishindwa sasa wanahaha kama mbwa koko aliyekosa chakula. CCM wanaogopa kwani Chadema wanajipanga vizuri na wanamwelekeo unaoeleweka ni chama kichanga kinachoweza kujadili mambo yake kwa uwazi na kutatua matatizo yake bila ya kishindo cha mpasuko kama huo wa wana CCM- fisadi
 
Kitila na Zitto huwezi kuwaweka pamoja (kuongoza) na Mbowe kwa muda mrefu wakaelewana bila kuliweka sawa tatizo la shule la the later. Wanamuacha mbali Mbowe kwa shule na vision.
 
Mchukia Fisadi na Junius...
Tofauti zenu ni sababu za chaguzi zenu----wote mmechagua mwanamke, lakini mmoja kachagua kwa sababu anafaa kuwa mke (marriage material), na mwingine kamchagua kwa sababu ana wowo** nzuri T*** material).
 
nahisi utakuwa mpotoshaji mzuri maana hauna uhakika na unachosema........
'Uchuro' waingia CHADEMA


lC.gif
Mwandishi Wetu​

Julai 29, 2009
rC.jpg

CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kimedaiwa kulenga kupanga safu mpya ya uongozi ikiongozwa na Freeman Mbowe na kumuingiza aliyewahi kuwa Mbunge wa Bukoba Mjini, Wilfred Lwakatare, kuwa makamu mwenyekiti, na kumn'goa Kabwe Zitto, kwenye nafasi yake ya Naibu Katibu Mkuu.
Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Mbowe, ambaye mbali na kushangazwa lakini alisisitiza kuwa wanaheshimiana sana na Zitto na kwamba binafsi wala chama hicho hakina mpango wowote wa kumng'oa kwa kuwa bado kinahitaji "Zitto" wengine wengi zaidi.
"Sijapanga safu yoyote ya uongozi, kwenye chama chetu tumekuwa na utamaduni rasmi wa kugombea na kupata uongozi. Najua kwamba kuna mbinu za kila namna kuisambaratisha CHADEMA. Mimi nitakuwa mwendawazimu kama nitakuwa sitambui mchango wa Zitto kwenye chama…huwa hatukurupuki tu kugawana vyeo, taratibu zote hufuatwa kwa hiyo si uamuzi wa mwenyekiti.
"Nasema madai hayo hayana msingi wowote na ni jungu la kitoto. Viongozi tutakuwa wendawazimu kama tutakubali CHADEMA iangamizwe kwa majungu, na Watanzania ambao matumaini yao yameelekezwa kwetu hawatatusamehe daima. Zitto ni kamanda wangu, natambua mchango wake kwenye chama na tunamhitaji," alisema Mbowe.
Lwakatare hivi karibuni alihama kutoka Chama Cha Wananchi (CUF) ambako alikuwa Naibu Katibu Mkuu Tanzania Bara, na kujiunga CHADEMA na kushiriki kampeni za chama hicho katika uchaguzi mdogo Jimbo la Biharamulo Magharibi.
Nafasi ya Makamu Mwenyekiti ambayo kwa sasa iko wazi, awali ilikuwa ikishikiliwa na aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, aliyefariki dunia kwa ajali ya gari akiwa safarini kutoka Dodoma kuelekea Dar es Salaam.
Inaelezwa kuwa katika safu hiyo mpya anayodaiwa kuipanga Mbowe, John Mnyika ndiye anayaterajiwa kuchukua nafasi ya Kabwe Zitto, ambaye kwa sasa ni Mbunge wa Kigoma Kaskazini, huku Mbunge wa Karatu, Dk. Wilbroad Slaa, akiendelea kuwa Katibu Mkuu.
Kwa mujibu wa habari zilizozagaa ndani na nje ya CHADEMA, uamuzi huo wa kumng'oa Zitto unaelezwa kuwa msingi wake ni kile kinachoelezwa kuwa ni "usumbufu" wa kiongozi huyo dhidi ya viongozi wakuu, akiwamo ya Mbowe.
"Mbowe anapanga kugombea ubunge na kuingia bungeni ikiwezekana kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni na atahakikisha anafanya kazi hiyo kwa nguvu zake zote ili umma umwamini, ataitikisa serikali na mwaka 2015 atashinda urais," inaeleza sehemu ya madai hayo ambayo yamekanushwa vikali na viongozi wote makini wa CHADEMA.
Madai hayo ambayo yameelezwa kuwakera baadhi ya viongozi hao yameelezwa kwamba mkakati mwingine unalenga kuhakikisha Zitto anapotea kwenye ramani ya siasa Tanzania "kwa gharama yoyote kwani ni tatizo."
Kwa upande wake, Zitto alipoulizwa kuhusu yeye kuwania uenyekiti alisema; "Mimi nasema sina mpango wala kufikiria kugombea uenyekiti. CHADEMA kina taratibu nzuri za kuachiana uongozi, ninaamini kama kuna mabadiliko yatakuwa ambayo yataacha chama salama. Mi bado mdogo, sitaki watu wanivurugie na kuvuruga chama. Nina imani na uongozi uliopo wa chama."
Katika hatua nyingine, akizungumzia madai ya kugombea ubunge Mbowe alisema; "Suala muhimu kwa sasa si kufikia nani anagombea ubunge au nani hagombei, jambo la msingi kufahamu kwa sasa ni kwamba CHADEMA tumejipanga kuongeza idadi ya wabunge ili kuipa nguvu zaidi za uamuzi Kambi ya Upinzani Bungeni kama unavyojua mara nyingi wabunge wa CCM wamekuwa wakitumia uchache wa wabunge wa upinzani kupitisha mambo yasiyokuwa na msingi."
Kwa upande wa madai ya kukusudia kuongoza Kambi ya Upinzani Bungeni na baadaye mwaka 2015 kugombea urais alisema; "Hivi mimi nimekuwa mpiga ramli? Na haya majungu yamepangwa kama vile mimi nina mkataba na Mwenyezi Mungu kwamba amenihakikishia kwa asilimia 100 nitakuwa hai hadi wakati huo. Nasema kila hatua ya kupata uongozi, na hasa uongozi wa umma inazo taratibu zake, mimi ni kiongozi mwanademokrasia ninayeheshimu taratibu."
Akizungumzia madai ya hivi karibuni kutoka kwa baadhi ya viongozi wa CUF kwamba CHADEMA ni CCM-B, Mbowe alisema ni utoto kuendesha siasa za kushambuliana kati ya chama kimoja cha upinzani na kingine na kwamba hayuko tayari kuingia katika malumbano ya namna hiyo.
"CHADEMA hatuwezi kuingia kwenye malumbano ya kupotezeana muda kiasi hicho, jukumu letu kubwa ni kutafakari kwa pamoja viongozi na wanachama tunakiandaaje chama chetu kuelekea Uchaguzi Mkuu 2010 kwa mafanikio makubwa katika historia yake nchini," alisema.
Historia ya vyama vya siasa vya upinzani nchini inaonyesha kuwa Chama Cha NCCR-Mageuzi ni chama kilichokuwa na nguvu kubwa za kisiasa mwaka 1995 na kufanikiwa kuwa na idadi kubwa ya wabunge, na kwa sasa chama nguvu hizo zimeshuka na chama hicho hakina mbunge hata mmoja.
Vyama vingine vilivyowahi kupoteza viti vya ubunge kutokana na sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kushuka kwa nguvu za kisiasa ni pamoja na UDP pamoja na TLP. Kwa sasa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, linaundwa na Kambi ya Upinzani kutoka vyama vitatu, ambavyo ni CUF, CHADEMA na UDP, chenye mbunge mmoja.

hs3.gif
 
Kuna uvumi kuwa Chadema itagawika kutokana na kundi linalomuunga mkono Zitto na lile la wahafidhina ambao wanadai chama ni chao na hakuna wa kuwapangia .
Uvumi! uvumi! uvumi! Basi, Lakini Jamaa wanasonga mbele na wananchi wanawaelewa na kuwakubali. Angalia uchaguzi wa Busanda na Biharamulo, hata kama CHADEMA haikushinda, mtu yeyote makini atafahamu kuwa kuna mapinduzi ya kifikra ya meshawaingia wananchi wengi katika kipindi hiki kifupi.
Ok, sawa kuna uvumi, so what?
 
Kitila na Zitto huwezi kuwaweka pamoja (kuongoza) na Mbowe kwa muda mrefu wakaelewana bila kuliweka sawa tatizo la shule la the later. Wanamuacha mbali Mbowe kwa shule na vision.

katiba ya Chadema haijasema kwamba lazima uwe na degree ndio ugombee uongozi, hilo ni juu ya wanachama wa chadema kuona ni kiongozi gani anawafaa kwa wakati gani. Wote wanahitajika kwani uongozi ni hekima na busara na shule inasaidia tu kupambana na mazingira yako, ila inaweza isikupe hekima wala busara, rejea Chenge, Dr balali, Profesa Mbilinyi, Pr. Mahalu, nk. Kweli tunahitaji wengi na wenye uchungu na nchi yao.

Zitto anaweza fanyakazi na mtu yeyeto ni kijana mahiri na hana shida kwenye maelewano na watu, misimamo yake ndio haiba yake na binadamu au kiongozi asiye na msimamo hafai. Kitila namwelewa vizuri ni kijana mwenye busara na hekima na anauwezo mkubwa wa uongozi anaweza fanya kazi na yeyeto. Na ikumbukwe hawa hawatakuwepo milele na kumfanya Mbowe kama vile Chama ni mali yake ni kumwonea, wao wenyewe Chadema ndio waliomwomba agombee uenyekiti hakung'ang'ania na hata kugombea uraisi alibembelezwa sana, haya mengine ni matokeo na dhahama za kuwa kiongozi kwani lazima ubebe dhambi za wengi.
 
Lakini Lwakatare hana hata miezi miwili kwenye Chadema hajaijua katiba na mfumo wa Chadema. kwanini asipewe KITILA MKUMBO?
mtu hamjamjua mnampa madaraka makubwa bila kupitia njia au ngazi walizopita wengine.

Watu wengine bana! APEWEJE?
 
Kuna kitu kinanishangaza hapa,hebu niambieni,nielezeni, Lwakatare anataka kuchukua nyadhafa ya juu kabisa ktk chama cha chadema,chama ambacho si kichanga ni kizoefu na cha muda mrefu,lkn je hakuna kanuni yoyote ndani ya chama inayosema mtu akiingia ndani ya chama mpaka akae muda flani na apitie kwa ngazi za wilaya mpaka afike juu, au kwa sababu Lwakatare ametoka cuf? na je mwanzo ndani ya chadema kulikuwa hakuna watu makini ambao wanaweza kuchukua nafasi za juu mpaka atoke mtu kutoka Cuf? inaonesha Cuf ina viongozi makini kwa maana hiyo?

Kule Cuf kwa sasa huwezi kutoka chama kingine au hata kujiunga tu kwa mwanachama mpya halafu ugombee uongozi,kwanza mpaka uwe mwanachama kwa muda wa miezi 6 na la pili ukianza kugombea lazima uanze kwenye matawi ya chini upitie kwa ngazi hadi ngazi. sasa hili linaonesha cuf ni makni kule chadema..
 
katiba ya Chadema haijasema kwamba lazima uwe na degree ndio ugombee uongozi, hilo ni juu ya wanachama wa chadema kuona ni kiongozi gani anawafaa kwa wakati gani. Wote wanahitajika kwani uongozi ni hekima na busara na shule inasaidia tu kupambana na mazingira yako, ila inaweza isikupe hekima wala busara, rejea Chenge, Dr balali, Profesa Mbilinyi, Pr. Mahalu, nk. Kweli tunahitaji wengi na wenye uchungu na nchi yao.

Zitto anaweza fanyakazi na mtu yeyeto ni kijana mahiri na hana shida kwenye maelewano na watu, misimamo yake ndio haiba yake na binadamu au kiongozi asiye na msimamo hafai. Kitila namwelewa vizuri ni kijana mwenye busara na hekima na anauwezo mkubwa wa uongozi anaweza fanya kazi na yeyeto. Na ikumbukwe hawa hawatakuwepo milele na kumfanya Mbowe kama vile Chama ni mali yake ni kumwonea, wao wenyewe Chadema ndio waliomwomba agombee uenyekiti hakung'ang'ania na hata kugombea uraisi alibembelezwa sana, haya mengine ni matokeo na dhahama za kuwa kiongozi kwani lazima ubebe dhambi za wengi.


angalia Lipumba bana hamna kitu!!!!!!!!
 
Pdidy, Hii ripoti inayosemekana imeandikwa na Gazeti la RAIA MWEMA, kwa maoni yangu inaizushia Chadema mgogoro ambao haupo. Hata Mwenyekiti Taifa, Mhe. Mbowe amejieleza vizuri tu kwamba Chadema (na Tanzania kwa jumla) wanahitaji vijana wengi wa aina ya Zitto. Na Zitto mwenyewe ametamka kwamba yuko tayari kuendelea na wadhifa wake wa Naibu Katibu Mkuu na ubunge.

Pamoja na kukubaliana na Mhe. Mbowe, ningeongeza kwamba Chadema inahitaji Slaa wengi na pia Mbowe wengi. Na nawapongeza kwa Operesheni Sangara ambayo inaendelea kuvutia Watanzania wengi ktk Chama ambacho kinatoa matumaini kwa Watanzania. Uzi ni huo huo. Hakuna kulala mpaka kieleweke.

Wahasimu wa Chadema wataendelea kupika majungu na kuchochea mifarakano ktk chama kinachoonyesha kwamba ni tishio kwao. Kwa hiyo jambo muhimu ni kupuuza majungu na kuendeleza mikakati ya Chadema kujiimarisha kuanzia ngazi ya chini; na kuhakikisha viongozi wanashikamana, wakitambua kwamba jukumu lao kuu ni kuleta na kuimarisha demokrasia ya kweli na uhuru wa kweli Tanzania.

Nafurahia ukweli kwamba viongozi wa Chadema wanatambua vipaji vya wenzao, na kwamba kila mmoja ana fursa ya kuchangia kwa uwezo wake wote ili kuleta mafanikio. Ushirikiano na mshikamano wa hali ya juu vinahitajika ili nembo ya USHINDI(VICTORY) ya Chadema iweze kudhihirishwa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom